Friday, 7 November 2008

Unataka kuolewa in 2 yrs time? Hii ndio nafasi yako.


Kwa kawaida D'hicious huwa sifanyi haya mambo ya kutangaza lakini kutokana na maelezo ya huyu bwana kuna mawili matatu ambayo tutajifunza (ndio lengo la D'hicious) na ningependa kuyazungumzia siku zijazo, kwa sasa msome na kamilisha ndoto yake kwa kuwasiliana nae.
Tangazo hili litakuwa hapa kwa masaa machache tu kisha nitalipeleka kwa Mwakilanga ambae ana-deal na matangazo ya uchumba zaidi. Asante kwa ushirikiano.

"Hi dada Dinah! Kwanza kabisa nakusalimu sana na pole kwa kazi yako ngumu na yenye msaada mkubwa kwa jamii.Dada mimi nina ombi kwako. Naomba niitumie site/blog yako kuweka tangazo langu ambalo nadhani labda litakuwa tofauti na matakwa ya wengi kama ilivyokawaida yake.

Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 34 na niko Marekani kwa miaka 7 nikifakamia elimu na kuandaa maisha yangu vilivyo. Natafuta rafiki msichana ambaye natarajia kuweka uchumba baada ya kufahamiana na kuelewana vizuri na kuoana ndani ya miaka si zaidi ya miwili ijayo.

Nimekaa hapa US muda wote nikila shule na nimekutana na wasichana wengi wa kibongo,lakini bahati mbaya sijaridhika na yeyote kutokana na sababu mbalimbali. Na ieleweke hapa kwamba sijafanya urafiki na yeyote kwa kuogopa mambo kadhaa ambayo sitayataja hapa, yaani sijaona mwenye sifa ya kuwa mke wangu.

Hivyo nimeamua kurudi nyumbani.Mambo yafuatayo ni muhimu kuyazingatia kwa yeyote atakayekuwa tayari kuanza mawasiliano nami:a. Awe mkristo mwaminifu ambaye nafasi yake ya kwanza amempa Mungu katika yote mema ayafanyayo.

a)-Haidhuru ni dini gani ya kikristo anatoka, bali awe tayari kubadili dini yake mara tutakapoivana kuwa Mlutheri kwani mimi ni muumini wa Lutheran.

b)- Awe na Elimu kuanzia kidato cha nne hadi juu na mwenye nia ya kuendelezwa ili afikie kiwango kizuri cha elimu inayokubalika kitaifa na kimataifa(Digrri ya kwanza) na mimi niko tayari kumgharimia.

c)-Awe tayari kwenda nami shambani kwani nina shamba kule Chanika ambalo nataka kuwekeza mifugo mara nitakaporudi huko baada ya miaka mitatu ijayo.Hivyo nikimleta US asipende kubaki hapa, kwani mimi nategemea kufundisha pale mlimani au Mzumbe ili kuijenga nchi yangu.

d)-Awe na heshima, na mwenye kusikiliza memngi lakini yeye aseme machache yenye maana.Sijali kabila, mimi natokea Mbeya.

e)-Awe mtu wa mawasiliano sana na muwazi katika mambo mengi.

f)-Asiwe na umri zaidi ya miaka 34. Pia awe hajawahi kuolewa au kuzaa kabla ya ndoa.

Dada Dinah hayo ndiyo yenye umuhimu kwangu. Naomba kwa yeyote atakayekuwa tayri kuwasiliana nami atume barua pepe kwa anwani hii : abosili@yahoo.com.

Nitashukuru sana iwapo utanikubalia kuniwekea ombi langu kwenye blog yako hii muhimu.Unisamehe kama nitakuwa kwa aina yeyote nime-abuse the proper use of your blog.

Please bear in your mind that I am serious with this issue, so take care of me!! Mungu akubariki sana kuendelea kutoa ushauri wako nasaha kwa jamii yenye dharura na nyufa nyingi za kimaisha."

Tafadhali kuwa mstaarabu kwa kaka Abosili. Asante.

4 comments:

Anonymous said...

dada dinah eh usiruhusu kupostsuch issues watu km wanatafuta wachumba waende kwa braza tk ye ndo anahusika huko..sie huku tunataka mafunzo tu! ukiruhusu kila mtu ataanza kuleta tangazo lake hapa...ni maoni tu mpnz!
shaister

Anonymous said...

Naamini wanawake wote wanakuja kujifunza kwa Dinah wanawapenzi wao tayari.Mungu akujaalie upate wa kumua.

Anonymous said...

JAmani mbona mnaanza nakumpaka kaka wa wau kaja kwan nia njema kama muna waume zenu si nyie wapo wengine hawajaolewa na wanatafutaw achumba kutoa tangazo kwa Dinah isiwe issue mbona Dinah mwenyewe hajasema iweje mseme nyie MNAHILA YA KWAPA.

Anonymous said...

ur ryte anony wa juu i waz about kusema same thing! wengi tunaojifuna humu tuna waume/wapenzi wetu!
shaister