Tuesday, 25 November 2008

Nimejikuta nampenda, kumbe anawake 2!-Ushauri

"Hi, Dada dinah hujambo mpenzi wangu?
Mie naomba nitafute ushauri kupitia kwa watuma comments nisikie watu na we Dinah unaishaurije hii Kesi?


Nina miaka 38, sina Mume kwa sasa(nimeachika). Kuna mwanamme amenichanganya sana.Tulipokuwawadogo tuliwahi kusoma pamoja na ilitokea tukapendana sana, lakini sikutaka kuwa na mahusiano ya ngono na shukuru hilo lilifanikwa kwani hatuwahi kutombana.


Mwenzangu huyo alibahatika kwenda Masomoni na mimi huku nikaolewa kwani kwa kipindi hicho kwa mila zetu huku hatukuwa tukichaguwa waume bali wazazi ndio waliokuwa wakipanga. Niliishi na Mume wangu vizuri na nilibahatika kupata kazi ya kuajiriwa. Kwa kuwa nilikua mtu wake wa karibu(huyo mwanaume)aliheshimu ndoa yangu.


Kwa bahati mbaya baada ya kurudi kutoka masomoni hakupata Kibarua kwa ulaini hivyo maisha yalimuwia magumu. Mie nikaamua kumsaidia kwakumpatia pesa mpaka pale alipopata kazi.


Akaamua kutafuta mke kitu ambacho aliniarifu na nikampongeza kwa hilo. Akabahatika kwenda masomoni tena kwa muda usiopungua miaka mitano. Akiwa masomoni huku nyuma ndoa yangu ikapata mtihani na kuharibika hivyo nikaachika. Huyu jamaa aliposikia nimeachika , akaanza kurejesha zile za nyuma (uhusiano wa kimapenzi) ingawa bado yuko masomoni.


Kwa kua tulipendana miaka hio na Dini ya kiisilamu inaruhusu kuoa zaidi ya mke mmoja haikua shida kwangu kumrudisha moyoni kwangu. Sikumpa jibu la moja kwa moja ,lakini, nikajikuta nimerudisha penzi na nimempenda sana, mawasiliano yalikuwa mzuri na hazikupita siku mbili bila Simu, Email, Chat za maneno matamu, I love you N.K ndio usiseme Dada Dinah.


Kwa hivyo nimeingia kikweli kweli na nilikua nasubiri arudi tu nimpe jibu la ndio. Kilichotokea dinah mpenzi, juzi nilikua naongea na rafiki yake wa karibu, natulikuwa tukiongea mambo ya kawaida tu. Yule rafiki yake ndio kuniambia kuwa jamaa (yule mwanaume nimpendae yuko masomoni) ana wake wawili tayari na kila mwanamke anamtoto mmoja.


Nikauliza kaoa lini? Nikaambiwa alienda conference nchi jirani ndio akakutana na huyo mke wa pili na kuoa. Kumpenda nampenda lakini ninamasuala mengi kichwani kuhusu huyu mtu kiasi cha kunichangaya na naomba wanablog wenzangu mnishauri nawe da Dinah.


Kwa nini mwazo wa mazungumzo yetu hakuniambia ana wake wawili? Kama ana moyo wa kuoa wake watau anatamaa huyu, ataongeza na 4 na 5 na hatimae atatupa ukimwi wote.


Nilimuomba dada yangu amuulize jamaa kijanja kama kweli ana wake wawili lakini hakumpa jibu na tokea siku hiyo kakata mawasiliano nami, hapigi simu, wala hachat tena. Mimi nimeamua nisiwasiliane nae, nijitahidi ili niweze kumtoa mawazoni mwangu.


Kwa kweli kipindi hiki nina hali ngumu kimawazo, naomba ushauri kwa yeyote, pale ambapo nimefanya sivyo pia mnikosowe ili nisirudie tena kosa.
Nashukuru sana"

Jawabu: Pole sana rafiki kwa kuumizwa hisia zako, hivi kuna nini kati ya uwazi na wanaume? Hali hii inatisha sana jamani. Wachangiaji wangu wengi hawakuelewa unataka ushauri juu ya nini? Kutokana na majibu yao nimegundua kuwa hawakukuelewa nilivyokuelewa mimi. Sasa nitaweka sawa hapa kidogo ili tuwe kwenye mstari alafu nitakupa ushauri wangu.

Huyu mdada sio kwamba anataka ushauri wa nini cha kufanya baada ya kugundua mpenzi wake alieyempenda kuwa ana mke zaidi ya moja tayari(Hawasiliani nae na anajitahidi kumuondoa moyoni mwake ili amsahau).


Yeye anaomba ushauri kwa kile alichokikosea (wapi kakosea), kama basi alikosea mkosoe na umwambie nini cha kufanya ili asirudie kosa (kama kuna mahali amekosea)......nadhani tuko kwenye mstari mmoja sasa.

Dada yangu mpendwa, kutokana na maelezo yako nimegundua kitu kimoja ambacho kwa mpenzi wako hakikuwa mapenzi bali huruma na "guilt" kutokana na msaada mkubwa uliompatia alipokuwa hana kazi.


Wapi ulikosea-Baada ya ndoa yako kuharibika yeye kama rafiki yako wa karibu alihisi kuwa anajukumu kubwa kukusaidia kwa namna yeyote ile kama ambavyo wewe ulifanya hapo awali.


Baada ya kuachana na mumeo ni wazi kuwa ulifanya uamuzi wa haraka kujiingiza kwenye ushusiano mpya (ni kosa kubwa hilo) kwa vile unapotoka kwenye uhusiano "serious" na wa muda mrefu mara zote unakuwa "Emotionaly vanurable" hivyo mtu akijitokeza na kuonyesha kukutaka/tamani au kukupa "attention" unaanza kujisikia poa na kuanza kujiamini tena kama mwanamke hali inayoweza kusababisha kuanzisha uhusiano na anae kutaka/kupa-attention na kuamini kuwa anakupenda, lakini katika hali halisi sio hivyo.


Sasa kutokana na historia yenu kama wapenzi mlipokuwa wadogo na kubaki marafiki wazuri kwa muda mrefu, ilikuwa rahisi kwako wewe kushawishika na kuamini kuwa kweli unapendwa......ulipaswa kujiuliza hili swali, "nimetoka kwenye ndoa na nilikuwa peke yangu (bila mke mwenza), je ilikuwa sahihi kuingia kwenye ndoa nyingine na kuwa mke wa pili? Kilichosababisha ndoa yangu kufa je hakitokea tena ikiwa nitafunga ndoa tena? Ni muda gani nahitaji kuwa tayari kuingia kwenye uhusiano mpya"?.......bikakabla hujauachia moyo na hisia zako juu ya huyu bwana.


Unapotoka kwenye ndoa au siku zote haishauriwi kuingilia ndoa ya mtu mwingine hata kama unampenda huyo mume au Imani ya Dini yako inaruhusu, hakikisha unajiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi ambao auhusishi mwanamke mwingine.


Kuna vijana wengi tu ambao hawana wapenzi, kuna wanaume wengi ambao wameachwa au kufiwa na wake zao na huwa wanatafuta kupenda tena na kufunga ndoa kwa mara ya pili. Hata kama walizaa na wake zao bado utakuwa hujaingilia uhusiano wa mwanamke mwenzio kwa vile mwanamke huyo hayupo kwenye maisha ya mwanaume husika.


Sio vema kumhukumu kuwa huyu jamaa ni Malaya kwani hatuna uhakika kama analala ovyo na wanawake tofauti kila kukicha na badala yake akipenda anafuata sheria ya Dini yake na kuoa. Ila kwako wewe dada yetu hakuwa na nia hiyo, alikuwa anajaribu kukuliwaza ki-emotionaly kupitia mawasiliano yenu ya Simu, Chat na Emails mara kwa mara na kama nilivyosema alikuwa akihisi "guilt" kutokana na msaada uliompa.


Hakutaka kuliweka wazi kwako kuwa tayari anawake wawili kwa vile hakutaka kukuumiza zaidi hisia zako za kimapenzi juu yake ambazo alikuwa na uhakika kuwa zimejengeka, kutokana na unavyozungumza nae mara kwa mara. Hilo ndio limemfanya aamue kuuchuna kwa vile hana mpango na wewe kama mke wake wa tatu au hata Kimada.


Nini cha kufanya-Chukulia yote yaliyotokea ni ya kawaida na ni mwanzo mzuri wa maisha yako mapya kama mwanamke. Ulikuwa binti wa Baba yako, ukawa mke wa mume wako huu ni wakati wa kuwa wewe kama wewe hivyo basi badili yote uliyokuwa ukiyafanya ulipokuwa mke wa.....na sasa ibua mikakati mipya ya maisha yako.


Kama unaweza basi, hama mahali ulipokuwa ukiishi au badilisha mpangilio wa vitu ndani ya nyumba yako, badili mtindo wa maisha yako kwa kuanza kufanya mazoezi.....hii itakusaidia sana kuondokana na mawazo na wakati huohuo kukufanya uwe "fit".


Badilisha mtindo wa mavazi yako uliyokuwa ukiyavaa ulipokuwa mke wa.....na sasa vaa kama mwanamke yeyote ambae ni kijana, "single", anajua anataka nini maishani na anaejiamini (kama unataka msaada kwenye hili nitafute).


Ibua "hobbie", anza kujichanganya na rafiki zako, ndugu na jamaa kila mwisho wa wiki. Epuka marafiki au ndugu ambao watakuwa na waume/wapenzi wao, hakikisha unasisitiza kuwa unataka mfurahie mwisho wa wiki mkiwa wanawake tu.


Kwa kufanya hayo machache niliyokueleza yatakusaidia sana kuvuka siku hadi siku na hatimae utajikuta mwaka umepita, huna mawazo tena na Ex mume wako wala rafiki, hutojilaumu tena kwa kosa ulilofanya na kubwa kabisa ni kuwa tayari kwa uhusiano mpya.

Kila la kheri.

6 comments:

Anonymous said...

Jamani Dadaangu, hivi na hili kweli ni la kuomba ushauri? Ina maana hadi sasa hujui tu cha kufanya? ahh mimi naona unatania tu, hivyo sitakupa ushauri

Anonymous said...

Antie,
Again mimi sio mchangiaji hapa mara kwa mara, but every now and then nikipata time nasimama na kuangalia nini kinaendelea.

Mimi kwa experience yangu, na pili kama mwanaume,ushauri wa bure ni kuachana na huyu bwana. Kwanza kabisa utaona kabisa huyu bwana ana tamaa na si jingine. Pili, hao wake wawili ni wale ambao amewao kisheria, jee vimada unadhani anavyo vingapi?

Nadhani kwa ushauri tuu ni bora ukaomba mungu akujalie mume ambae ata kurespect wewe kama wewe and nothing else.

GoodLuck antie

Anonymous said...

Ninampenda japo ana mke - Ushauri

Habari za kazi dadinah! nilituma mada yangu wiki iliyopita lakini mpk sasa cjapata majibu nahitaj msaada wako na wanablog hii.
Nimekuwa kwenye mahusiano na mume wa mtu takriban miaka 5 sasa na kadri cku zinavyozid kwenda mapenz ya2 yanazid kuchepuka ila linalonisibu moyoni ni kwamba wazaz wangu, ndugu wananishaur niachane na huyu jamaa coz ameoa sasa 2napendana sn nashindwa kumwacha Je nifanyeje kwan ashanitambulisha kwao ndugu wazaz wake wananitambua na wamenikubal ila kwangu mtihan Je ni2mie njia gan ili 2achane bila mmoja we2 kuumia roho.

Nitashukuru sn kwa ushauri wenu

Dinah said...

Anony hapo Juu kuwa mvumilivu. Huwa naweka maswali kwa kufuata lini yametumwa au lini nimeyapokea. Yote huwa nayahariri na kuyaweka ili yajitoe yenyewe Automaticaly.

Huwa sitoi kipaumbele kwa yeyote na vilevile huwa siweki kapuni maswali ya watu. Yanatokea hapa kulingana na tarehe au saa. Asante kwa uelewa wako.

Anonymous said...

Mimi kwa ushauri wangu, ni kuwa wewe unaweza ukaolewa kuwa mke wa tatu au wa nne kutegemeana na imani ya dini yako ilivyo,lakini kuna mambo mengi unatakiwa uyatizame kiundani.
-Je kweli mume huyo anakupenda na wewe unampenda kwa dhati
-Je wenzako wapo radhi na wewe? Kwani ujue hawo watakuwa sehemu ya maisha yako, kwahiyo upendo wa kama dada unatakiwa ili pendo lenu lidumu.
-Je huyo mume unauhakika kweli anaoa kwa tamaa,au upendo, na je ana uwezo wa kuwatosheleza wote kwa hali zote, kwani asije akawaoa kama picha, wakati wapo watu wengine wanakutaka. Wakati ukimwi upo njenje, kwani hatuji wote mnasubira kiasi gani.
Swala la uke wenza kwa karne hii ni gumu na nyeti kwa kuzingatia imani zetu zilivyo. Imani za dini kwa sasa hazipo kwa wengi wetu,tunaimani zakujionyesha kwa watu sio kwa kumuogopa Mungu. Kwahiyo kuishi uke wenza ni mtihani na `very risk' Sijui waliojaliwa kuishi hivyo wanafanyaje,lakini hali hiyo inawezekana kama wote mpo radhi na mna upendo na mume wenu ana upendo wa kweli na sio tamaa.

Mimi ndio niliyo nayo
emu-three

Anonymous said...

Mdada wewe fikiria kwa haraka kabla ya kutaka ushauri .tambua kabisa huyo mkaka ni malaya tu mwisho aje akuletee ukimwi bure anakutamani tula ila hakupendi kama angekuwa anakupenda angekwambia ukweli .achana naye utapata anayekupenda kiukweli ukweli