Friday, 14 November 2008

Kumbe mpenzi ni Kaka...nimerudi tena-Ushauri!


"Habari dada dinah mimi niyule dada ambaye sikujua kuwa mpenzi wangu ni kaka tatizo lingine limejitokeza, nilikuwa naenda kuoga na simu yangu niliiacha kitandani mara baada ya kutoka kuoga nikakuta dada yangu ameshikilia simu yangu.Dada akaniambia/uliza "yaani we unatembea na Kaka" (tumuite Beka) akaanza kunitukana kwa kuniita "malaya mkubwa wewe hata baba yako mzazi utatembea nae na kuanzia sasa hivi nitakuwa na mchunga hata mume wangu".
Dada dinah nifanyaje? naumia kwa kutukanwa na dada yangu hasa kuniita hivyo, nisaidieni jamani? je nimuache huyo mtoto wa binamu wa mama yangu ambae ni mpenzi wanfu au nifanyaje? "


Jawabu: Pole sana kwa tatizo lingine lililojotokeza hivi sasa, Kuitwa Malaya mbona ni kawaida tu, wala huna haja ya kumia au kuwa na huzuni kutokana na kitu kidogo namna hiyo.Lakini jamani, inakuwaje mtu mwingine achukue simu yako ya mkononi na kusoma msg au hata kupokea simu bila ruhusa yako? Hicho ni kitu binfasi na kinaweza kuwa na mambo mengi binafsi ambayo hayapaswi kuonwa, sikiwa, somwa na mtu mwingine unless ni mpenzi wako.Baada ya ushauri uliotolewa hapa umeufanyia kazi au unaendelea kuufanyia kazi? Kama ungeufanyia kazi mapema hili suala la dada'ko kukutukana lisingekuwepo au lisingejitokeza. Mpenzi "Kaka" anasema nini kuhusu uhusiano wenu?Wakati mwingine mwanadamu unapaswa kuwa a little bit selfish na kutojali kwa sana hawa ndugu ambao hivi sasa kila mtu anaendesha maisha yake kivyake. Dada yako anamaisha yake na mume wake na anapaswa ku-focus huko, Mama yako anamaisha yake na mume wake ambae ni baba'ko na anapaswa ku-focus huko na wewe una maisha yako kama binti mdogo lakini unataka kuwa na maisha yako kama wao kwa kuungana na mtu mwingine ambae mnapendana na atakuwa baba wa watoto wako na unapaswa ku-focus huko.Pamoja na kusema hivyo sina maana kuwa uwadharau, hapana. Endelea kuwaheshimu, sikiliza ushauri wao na fanya maamuzi ya kuyafanyia kazi au kuyaacha pale pale kama yalivyowakilishwa kwako.Ulisema kuwa wewe na mpenzi wako mnakwenda kufunga ndoa(Ikiwa nakumbuka vema, nitaangalia). Kama kweli mnapendana na mnania moja na huyo Ndugu yako wa jina (sio wa damu) basi kuweni "serious" na fungeni ndoa (sio lazima iwe kubwa na kushirikisha kila mtu, mnaweza kufanya ya kiserikali ili wewe na yeye kuishi pamoja na kihalali kama mke na mume) ili kumaliza kesi.
Fanya uamuzi wa busara kwa kuzingatia nani ni muhimu kwenye maisha yako kama mwanamke, mama ambae anamaisha yake? dada ambae anamaisha yake? au Mume wako ambae mnapendana na mnakwenda kuwa na maisha yenu pamoja?Vinginevyo matatizo yatazidi kujitokeza juu ya matatizo mengine ambayo ukiyafuatilia kwa karibu utagundua ni kupotezeana mida tu.


Kila lililo jema!

6 comments:

Anonymous said...

Pole dada yangu!

Kwanza nimepata swali juu yako, Je, kule kuacha simu, na dada yako kuichukua kuna maana alikuta message inayozungumzia mapenzi yenu na yule kijana au yule kijana alipiga simu na huyo dadayo akapokea na kuzungumza na huyo jamaa yako?Sijaelewa kwa kweli ni vipi simu ilizua kasheshe na dad yako?

pamoja na hayo nini maamuzi yako baada ya kupata ushauri pale mwanzoni,Je, uliamua kuendelea naye na kuoana au umezidi kuwa katika mahusiano ya kuibiana?Kwa nini dada yako akuite malaya?Je, amewahi kukufuma na wengine?au anajua una mtu mwingine?
Samahani kwa maswali hayo kwani inanipa ugumu kuchangia katika swala lako ninapokuwa bado sijaelewa mambo yanayozunguka hapo.

Anonymous said...

jamani dada TUMEKUCHOKA! dada dinah topic nyingine plz..

Anonymous said...

halow pole sana dadaangu
najua jinsi mapenzi yanavyotesa hasa mkifikia point fulani mnakua kama vichaa,then mje muachane mmmmh ngumu sana....
sasa mi ushauri wangu we achana na huyo nduguyo kwa kweli kwa sababu we mwenyyewe utakuwa unajistukia mara nyingine kuwa huyo ni nduguyo???
ila jaribu kukaa nae then umwambie kwa kirefu najua itakuwa ngumu sana lakini sasa kuepusha yote bora nusu shari kuliko shari kamili...
wee mweleze mkubaliane.....
poleee saaana-

Anonymous said...

Nakumbuka wengi tulikupa ushauri kutegemeana na `hisia, au imani zetu' nafikiri uliamua kitu kutokana na ushauri huo. Hapo nikakumbuka usemi usemao `unalo hilo'
`Unalo hilo' sina maana mbaya kulitumia hapa, ila nina maana kuwa asilimia kubwa inategemea `uamuzi wako' binafsi, sisi ni washauri tu.
Nasema hivyo nikiwa na maana kuwa `mapenzi' hasa yale ya kweli ni kati ya `wawili wapendanao' wengine ni washabiki tu,na wengi wa washabiki nia yao ni `kuharibu ili wapate kila wanachozani watakipata.
Mfano mzuri ni dada zetu wanapomuandama wifi yao, wengi wanadhani kuwa huyo wifi akiondoka wao watafaidi kile alicho nacho kaka yao. Na vitu kama hivyo.
Lakini,narudia tena LAKINI' kama nyie wawili mnapendana na mna msimamo wa kweli na penzi lenu washabiki hawataona ndani.
Wewe kama umeamua kuwa dada-binamu is ok,kama mimi ninavyoona,basi usijali hayo maneno wanayosema, kwani nyie sio mlio-anza hilo. Ila ukiona vipi wazuri, na wanaofaa kuwa nawe wapo,usikate tamaa.
mimi
emu-three

mgm said...

Habary waungwana!! Pole sana Mdadaa!! Ni mtazamo wangu, kuwa wewe hivi sasa umekosa kwa kuangalia hasa kwa kuwa binadamu huwa tunakasumba ya kuhamaki na wewe ndiko uliko.

Sasa basi baada ya kusema hivyo nataka nikurudishe nyuma kabisa kwani kila watu na jamii wa mila na Desturi zao, natumaini pia wewe na huyo mwenzio na ndugu zako pia mna desturi zenu nikiwa namaana tufuate "ITIFAKI" izingatiwe japo mnapendana, kwani kuachana mngali mnapendana ninyi si wakwanza na haitawaumiza milele kwani itakuwa ya muda tu then mtazoea na badae mtapa kila mmoja wake wa maishaishani.

Kwani jambo jingine hata kibaologia kunaweza kukawa na matatizo juu ya familia yenu i mean watoto mtakao kuwa mkiwazaa.

Na la mwisho ni kuwa ni kweli mwaweza pendana wenyewe kiukweli lakini mapenzi yenu hayatakuwa na furaha na amani hasa pale mtakapokuwa mnakutana na wanandugu kwani mnakuwa moja kwa moja mmewasaliti kati suala zima la mila na desturi, kwani kwa upande huu wa mila mimi siioni sababu ya ninyi kung'ang'ania kuwa pamoja kwani kama ni hivyo basi ni weli kama alivyokuambia Dada yako kuwa waweza pia kumchukua hata baba yako nikiwa namaanisha baba yako mdogo, mkubwa na hata wajombazako pia kitu ambacho katika jamii yetu ya kitanzania ni tofauti..

Huo ndio ushauri wangu kwa leo..

ur's
Mgm

Anonymous said...

Kwako Mgm, huyu dada na huyo kaka yake hawana undugu wa damu na tulimuambia hivyo baada ya kuja hapa mwanzo.

Angekuwa ndugu wa karibu kidamu ambae anaweza kusababisha matatizo ya kibailojia wangekuwa wakijuana tangu awali sio mpaka baada ya msiba wa fulani ambapo kwa kawaida ndugu wengi hujitokeza hata wale ambao ubinamu ni wa kukaa jirani kule kijijini.

Kibaolojia, ukizaa na binamu yako watoto wanatoka bomba bila matatizo ya kiafya kwa vile wote wawili mmechanganya damu za watu wengine na zinawafanya msiwe ndugu. Makabila mengi wanaona na binamu zao kabisa ndio itakuwa mtoto wa mtoto wa binamu wa mama?
Ebu kafungeni ndoa na mzaliane bwanaaa.