Nampenda rafiki wa X je nimkubali?-Ushauri.

"Hello Dinah kwanza pole na kazi,
Mimi ni msicha mwenye umri wa miaka 26, mwanafunzi wa moja kati ya vyuo hapa Tanzania. Shosti nahitaji sana ushauri maana maji yamenifika shingoni. Nilikuwa na Boyfriend kwa muda mrefu lakini kwa bahati mbaya mimi nikapata shule mbali kidogo na mkoa ninaoishi.



Boyfriend wangu alifurahi lakini nahisi haikua furaha ya kweli kwani baada ya kuondoka na kukaa miezi sita hapo shuleni tabia yake ilibadilika nikimpigia simu anashindwa kuongea nikimwambia nimemiss ananijibu kana kwamba kuna mtu anamuogopa.


Baada ya mwezi mmoja baadae alinitumia message na kuniambia ana msichana mwingine kwasababu hajaweza kuvumilia, I was so frustrared baada ya kusikia hivyo kwani nilikua nampenda lakini baadae nilifikiria nakugundua hakuna umuhimu wa kuendelea nae nikamjibu kama ameamua hivyo ni sawa.


Tatizo linakuja huyo boyfriend wangu alieniacha ana rafiki yake ambaye nasoma nae chuo na anajua uhusiano tuliokua nao, ila baada ya kujua kuwa rafiki yake siko nae tena ameanza kunitaka na mimi nampenda sana na napenda awe boyfriend wangu kwani nae hana msichana kwa sasa je Dinah NIMKUBALI huyu mwanaume because I real need a boyfriend au itakua vibaya kwasabau ni rafiki wa my X boyfriend?"


Jawabu:Wanawake wa magharibi wanaamini kuwa sio vema kutoka na mwanaume kutoka kwenye mzunguuko wa rafiki zake na ni mwiko kabisa kutoka na Ex mpenzi wa rafiki yako wa kike, lakini ndio wanaongoza sio kutembea nao bali ni kuwaiba kabisa!. Sasa kuna faida gani kujiwekea miiko wakati wanashindwa kuitekeleza?



Huyu bwana hana undugu na Rafiki yake, hivyo kama mnapendana kweli na mnania moja ya kuwa kwenye uhusiano go for it!


Lakini kama huna uhakika na hisia zako za kimapenzi lakini kwa vile unahitaji kuwa nae (kama ulivyosema) "I really need a boyfriend" basi ningekushauri usimkubali kwa sasa na badala yake usubiri kwanza mpaka utakapo kuwa "in love" ili uhusiano uwe extra special n avilevile usije ukaumizwa hisia tena.




Take it slow ili kujenga hisia halisi na za kweli za kimapenzi na kumbuka tu kuwa " You can never need a boyfriend, (they come and go)....you need Education (you will have it for the rest of your life).....we only want them.

Nakutakia kila lililojema.

Comments

Anonymous said…
Lakini muuliza swali mbona jibu unalo tayari. Miondoko mlio nayo ni ya urafiki, na urafiki ni hatua nyuma ya `mpenzi' hamjawa `comited'
Well, kwa ushauri wangu, katika umri huo,ni wakati mzuri wa kujua na kuchagua rafiki wa kweli ili aje kuwa mpenzi wako, na hatimaye mambo yakienda vizuri awe mumeo.
Ngoja dada Dinah atuelimishe kwa hili
emu-three
Anonymous said…
bibiii weweeee,,kwa raha zako jiachiee na tena ikiwezekana huyo x wako ajue una uhusiano naee,,yeye si alikuona wa nini ndo ajue wenzie watakupataje....
mi naona jiachie bwana kwanza haina haja ya kuogopa kwanza nchi huru hii bwana.
Anonymous said…
Nampenda rafiki wa X je nimkubali -Ushauri
Hee pole sana dada unachotakiwa kwa sasa nikuwa makini sana isije ikafika siku mkahitimu elimu yenu na kutawanyika then ikaja ikatokea kama X bf alivokufanyia na kama kweli yuko serious bac mfanye mikakati ya kutambulishana kwa wazazi kwan dunia ya sasa ni tabu wanaume nao wamekuwa wakituhadaa kila wakati so cha muhimu ni umakini na heshima kati yenu
Anonymous said…
Pole kwa kuachwa mpenzi, yote ni mapenzi ya Mungu. Kuhusu huyo kijana mi sioni tatizo lolotwe kama anakupenda na unampenda just go on, wangekua ndugu hapo ingekua tabu, lakin angalia wasije wakawa wanapasiana mpira
Anonymous said…
Nadhani kwanza itakuwa vyema kama utasema ni muda gani tangu mmeachana na huyo BF wako.. Then kama ni less than a year, i think huyu jamaa ambae ni rafiki wa X-wako anashida nyingine kabisa na sio uhusiano.

I think tafuta mwanaume mwingine out of that cycle.
Anonymous said…
Tatizo hawa wanaume hawatabiriki, huwezi jua ni mkweli au la... ushauri wangu, Ingia tu kwenye hiyo Gamble.. kama unampenda, sio ndugu yake huyo. Jimwage mtoto kwa raha zako!
Anonymous said…
Mimi namsaporti huyu anon wa 3.16pm. Kweli dada tafuta mwingine nje kabisa ya grupu/circle ya X wako. Ndio, labda huyo rafiki wa X-wako anaweza akawa na nia nzuri lakini wanaume bwana, saa ingine huwezi jua -au ndio ukute wamepanga na X wako ili akuchukuwe na baadaye akudhalilishe. Si unaona mabinti wengine wengi wanavyopigwa picha na mpenzi - mkidhani mmependana na kuaminiana kumbe ana lake jambo la kuzipeleka online. Saa ingine wanaume wanakuwa na yao. TAFUTA MWENGINE TOFAUTI NA GROUP LA X WAKO KABISA.
Simon Kitururu said…
Tafakari swala lako nikikunukuu la ''I real need a boyfriend'' kama halichangii hisiazako za kumpenda huyo jamaa.

Inawezekana unahisi yeye ni bora kwa sababu unamjua tayari na unajisikia comfortable na fikira za kwamba anafaa, ingawa lijamaa tu jingine lingetimiza haja zako za kuwa na boyfriend.

Ukichukua muda kidogo kabla ya kuamua unaweza kutohitaji hata ushauri wa mtu katika uamuzi wako.
Anonymous said…
Ama kweli wahenga walisema"hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe"

Wewe dada tulia kwanza mbona papala hivyo?Kuwa na boy friend unafikiri ni ujasiri wowote?

Kwanza uelewe kuwa mazingira ulionayo sasa ni ya hasira nyingi zilizotokana na mpenziwo kukuacha.Kwa maana hiyo hata maamuzi yako siyo sahihi kabisa.

Jambo lingine unaonyesha kuwa unataka kumwonyesha huyo X wako kuwa nawe umo ingawa labda huvumi.Nasema hivyo hasa kutokana na kumpenda huyo rafiki wa x wako ili uanze naye mapenzi.Looo huoni kama unataka kujichomea tanuru hilo?Je, ni upendo gani hasa huo usiokuwa na macho wala fikra sahihi za maamuzi?Any way labda kwa sababu umesea una usongo wa kuwa na boyfriend!!!!!!!!!

Kwa kuwa ni mwanafunzi zingatia kwanza masomo yako ili uwe na credit nzuri za kukuwezesha kwenda juu kimasomo.Elewa kuwa wanaume wapo, watakuwepo,muhimu nu kutulia na kufanya kwanza lililo mbele yako kwanza.Najua mambo ya uanafunzi kuwa unapoona wenzio wanaenda kwenye matanuzi na vobosile vyao basi ni fahari,kumbe ni ubatili mtupu,ni sawa na kujilisha upepo tu.

Mbaya zaidi umelalia palepale, je, unafikiri kutakuwa na tofauti gani kati ya x wako na huyo rafiki yake?Huoni kama bado unajinyonga palepale?Hicho kidonda ulichokipata kwa huyo rafiki yake unafikiri kitaisha kama siyo kikabaki kwenye kumbukumbu daima(In your memories)na kukutesa daima maana kama wao marafiki bila shaka urafiki huo lazima uguse ninyi warembo wao.

Kuwa mvumilivu hayo yote yatakuja kwa wakati wake ukiisha maliza moja.Labda kama unausongo na kutombwa labda ndilo linakusumbua.

Nakutakia maamuzi mema katika hilo ukijua kuwa,kuhangaika na u-boyfriend siyo sifa sanasana ni kupotezeana muda tu.
Anonymous said…
Dada Pole kwa kuwa njia panda,
Sababu moja iliyonifanya mimi nichelewe kungonoka ni kuepukana na tatizo ambalo huyu dada anapitia.
Unakuta msichana/mvulana akiwa shule ya msingi anakuwa na mpenzi, kama itatokea akaama shule basi atakapoamia atakuwa na mpenzi mwingine 'mpya',sekondari atakuwa na mwingine,chuoni atakuwa na mwingine.
Kama shule hizi zote zitakuwa za kulala, hiyo basi ina maana wakati wa likizo nyumbani atakuwa na mpenzi mwingine, akianza kazi atakuwa na mpenzi mwingine, kama ikatokea akaamishwa kazi kama huyu dada alivyo,basi kule aendako atakuwa na mpenzi mwingine 'mpya'
Sasa mwisho wa siku unakuta amekuwa na mahusiano mengi sana, na uwezekano wa kuwa na migogoro ya kimapenzi na magonjwa ni mkubwa sana.
Unachotakiwa kufanya ni kuachana na mahusiano ya boyfriend na girlfriend na kuoa au kuolewa, kwa sababu ukiwa ndani ya nyumba inaonyesha 'committed relationship' na ni extra mile ya bf/gf. Ambacho mmoja akiamishwa kikazi,uwezekano wa ndoa kuendelea kuwepo ni mkubwa kuliko uwezekano wa mahusiano ya bf/gf kuendelea kuwepo.
Jiweke bize na masomo ukujiandaa na maisha yako ya baadae.
Sisi wanaume(baadhai yetu lakini,sio wote),sijui hasa ni kwa sababu gani,tukisikia mvulani akisema iwe kwa kujigamba au kwa kawaida tu kuwa yeye ameshangonoka na msichana fulani,basi unaanza kumtafuta na kungonoka nae.
Kuna wengine ndio wakisikia kuwa ameachana na fulani basi na yeye anataka uhusiano na huyu msichana aliyeacha, na mara nyingi uhusiano huo mpya haudumu.
Inawezekana kabisa kuwa huyo jamaa yako wa zamani ameshamfahamisha kuwa nimeshaachana na g/f wangu,na wakati mwingine inawezekana hata akawa amemuambia kuwa nimeshaachana nae 'chukua mzigo'.
Narudia tena kukushauri,kazania masomo na maisha yako ili baadae uje upate mume akuoe muishi maisha mazuri,amani na upendo.Sijakuelewa unaposema kuwa unaitaji bf,je una maana kipesa,kama kipesa bf hawezi kukuondolea shida zako za kipesa,kama kingono basi mimi naona unaingia kicha chichwa bila kufuata utaratibu,UKIMWI umetapakaa sana pamoja na wanaume wadanganyifu.
Mtanzania,
tmajaliwa@yahoo.com
Anonymous said…
TMAJALIWA KAMALIZA KILA KITU NIMEPENDA PRESENTATION YAKE, DADA UNAYE HANGAIKA TULIA FATA USHAURI HUU, UTAKUJA UKUMBUKA BAADAE SOMA KWANZA, WANAUME WAPO TU KWAAJILI YAKO, NOW UNA RUSH UTAPATA VIMEO VITATOMBA NA KUKIMBIA,MM NIMEPITIA HAYO MAISHA YA CHUO NAYAJUA SANA ASILIMIA 80 NI UDANGANYIFU,UTAKUJA CHUO HAPO UKIWA AT LEAST NA MNATO HATIMAYE KAMA HUPO MAKINI UTATOKA UMETEPETA SIKUTANII HUO NDIO UKWELI WENYEWE KAMA HUYO JAMAA ANAKUTAKA EXTEND MUDA UONE KAMA HAJATAFUTA MWINGINE..., TULIA SOMA DADA MIMI HUWA NAPENDA KUWA SHAURI SANA WADADA KUHUSIANA NA HILI WALIONIFUATA WAME WIN WALIO ONA MM SINA MAANA KWA USHAURI WENGINE WANALIA LIA TU, NA WENGINE NIKIONANA NAO WANANIKIMBIA KWA AIBU MAANA WAMEISHIA KUAIBISHWA, UKIACHANA MPENZI TULIA KWANZA MUDA MREFU AKILI ITULIE, NOW UNAWEZA ONA HUYO MZURI KWANI UNA HARAKA LKN BAADAE UTAONA KAMA NI WRONG CHOICE, SO TULIA KWANZA VINGINEVYO WATAPOKEZANA MPAKA UCHOKE NA UTASHINDWA HATA KUSOMA HAPO CHUO.HENCE UNAWEZA ANZA TAFUTA NANI KAKUROGA MAY BE BCOZ HUPENDWI USHAKUWA 'USED' SORRY NIPO SERIOUS KTK HILI, SO TAKE CARE KWA MAISHA YA CHUO UKIONA HUNA MARKET KINCHOFUATA NI KUJIUZA MTAANI MAANA CHUO HUTAKUWA NA DILI TENA, SO TULIA DADA UTAPATA MUME AMBAYE WEWE UKIWA NA ELIMU YAKO MNA ENJOY, USIPENDE KU ENJOY KIIVYO WAKATI UAN MIPANGO YA KUSOMA UTAKOSA YOTE UTASHINDWA WA KUMLAUMU, HAPA SISI TUNAKUSHAURI TU UKIONA USHAURI HAUFAI IT IS YOU NA ROHO YAKO! ILA MM PAMOJA NA KWAMBA NI MWANAUME HUWA SIJISKII VIZURI WANAUME WENGINE WANAVYO WACHEZEA DADA ZETU MWINGINE UKUTE ANAKUTEGA TU UKIKUBALI TU UNALO HILO BOO, NA MIBOO MINGINE NI YA KIHARIBIFU, BORA ULIPATE NDIO UMEOLEWA MAANA ITAKUWA NGUMU MWENYE MEDIUM SIZE KUKUCHUKUA/KUOA COZ ATAONA KAMA USED SANA SO KINCHOFUATA HAPO NI KUACHWA KUACHWA, PIA HAPA SINA MAANA KUWA WANAUME WASICHUKUE DADA ZETU, NO MAANA YANGU NIKUWA NA WASICHANA WENGI KWA MAKUSUDI AU KUCHEAT, SO AKILI KICHWANI.
LAJK@YMAIL.COM