Wednesday, 26 November 2008

Miaka 5 na mume wa mtu, Familia hamtaki-Ushauri.

"Habari yako da Dinah !!!!

Mi msichana mwenye umri wa miaka 29, sasa nimekuwa na uhusiano na mwanaume wa mtu takriban miaka mitano sasa na kipindi chote tulichowahi kukaa ananijali sana na kunitimizia mahitaji yote ninayohitaji ikiwa ni pamoja na mapenzi ya dhati mpaka ikafika kipindi mkewe akajua lakini baadae mwenyewe akasalimu amri na kutuacha tuendelee na penzi letu.


Sasa dada yangu kinachoniumiza kichwa familia yangu haitaki kumsikia kabisa huyu kaka na tumeshapanga mipango mingi ya kimaisha so niko kwenye "dilema" najiuliza nianzie wapi kwani nilishawahi kumgusia hiyo ishu tukagombana sana na akaishia kusema atakuwa mgeni wa nani kwa sababu mkewe ashamtenga hawajagongonoka miaka yote 5 wala kulala kitanda kimoja toka alipogungua mumewe ana uhusiano nje.


Na mimi pia kwa sasa naona ni mda wangu wa kumpata mume awe wangu peke yangu naomba ushauri wako dada nifanyeje na wadau wa blog hii nisaidieni kwasababu toka nimekuwa na huyu jamaa hajawahi kujitokeza mtu hata kusema nakupenda ya unafiki.


Kazi njema dada Dinah tunashukuru sana kutuelimisha kupita hii blog yako Mungu akubariki."

Jawabu: Aisee nimeshituka lakini nimefurahishwa na uwazi wako, ndio nia na madhumuni ya D'hicious watu kuwa wazi kwani sote tunajua haya mambo yapo na ya natokea, hapa tunasaidiana na kujifunza namna ya kukabiliana nayo kama sio kuyazuia yasitokee kabisa. Safi sana dada.

Unajua kuna mambo mengine unatakiwa kujigeuzia kibao kwanza upate picha ya itakavyokuwa kabla hujaamua kutenda......ingekuwa wewe ndio mkewe na akaamua kutoka na mwanamke mwingine ungefanya nini? ungejisikiaje?


Alafu mwenyewe hapo mwisho umesema kuwa unadhani kuwa sasa ni muda wako wa kuwa na mume wako peke yako, kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa unaamini kuwa kila mke anapaswa kuwa na mume wake peke yake.


Lakini umesahau kuwa huyo mpenzi wako sio wako peke yako na hata akikuoa hatokuwa wako peke yako, hajawahi kuwa wako peke yako na basi hivyo hatokuwa wako peke yako.


Kutembea na Mume wa mtu ni kosa, hata siku moja usijaribu kulala na mume wa mwenzio ukijua kuwa ana mke wake nyumbani. Kumuiba mume wa mtu sio tu kwamba ulimuumiza mwanamke mwenzio na watoto ambao wamezaliwa ndani ndoa yake bali unachangia kwa kiasi kikubwa kufanya watu wasiheshimu ndoa tena.


Familia yako haitaki kumsikia kabisa Mpenzi wako kwa vile wanajua kuwa ni mume wa mtu mwingine, wanakupenda na wasingependa na wewe kwenda kupata matatizo ambayo mke wa huyo jamaa anayapata kwa sababu yako. Yaani wanahofia kuwa Jamaa akikuoa atakuacha na kwenda kutafuta mwanamke mwingine kama alivyokuja kwako.


Huyu bwana ni mnafiki na muongo, kama mkewe kamtenga kwa miaka yote Mitano jiulize kwa nini basi hakumpa Talaka? Hiyo pekee inakuambia kuwa jamaa anampenda mke wake na hayuko tayari kumuacha kwa ajili yako. Hilo moja.


Kitu kingine cha wewe kuzingatia ili kugundua kuwa huyu bwana hana mpango na wewe kama mkewe ni kuwa, kwa kawaida mwanaume aliyetulia kiakili, kimaisha (sio mwanafunzi) hawezi kukaa na wewe kwa muda wa miaka mitano bila kutangaza ndoa.....mwisho ni mwaka mmoja tu....anataliki na kukuoa wewe(kama anamke) na ikiwa hakuwahi kuoa basi inakuwa kama vile kutereza mahali pakavu....pili.


Tatu, inakuwaje awe ametengwa na wanalale vitanda tofauti lakini kila siku anakwenda kulala kwa mkewe? Oh well, anaweza kuzuga tu ili jamii isigundue uchafu wake au wasihisi kuwa yeye na mkwewe wanauhusiano wa ajabu (huenda wameelewana hivyo kwa vile mkewe hawezi kumpa ngono ya kutosha mumewe).


Kama nilivyogusia hapo juu, kuna uwezekano mkubwa kabisa wameelewana kuwa Mume akutumie wewe tu(asibadili wanawake kila leo) kwa ngono kwa vile yeye mkewe hawezi kumpa ngono mumewe kama ambavyo anahitaji.


Sasa ili kukufanya usimuache na kuwa na mwanaume mwingine (kutokana na maelewano na mkewe) hali inayoweza kuwaweka kwenye hatari ya kuambukizwa VVU......anajitahidi kukupa huduma zote unazohitaji.......usijiamini nakusema alisalim amri kumbe wawili hao wanajua walifanyalo.


Usikute wanapendana sana na wanafanya mapenzi kila wanapohitajiana lakini kwa vile anajua wazi kabisa akikuambia wewe hivyo hutofurahi hivyo ni heri kukuambia kile unachotaka kusikia.....(wanaume wengi husema kile wanawake wanapenda kusikia ili kuepuka mizozo au kuachwa).


Hakuna wakati wa kuwa na mume wala muda wa kuolewa unless unataka kufunda ndoa kwa sababu nyingine na sio mapenzi. Umri wako ni mdogo sana kuhofia muda wa kuolewa (hiyo kuolewa b4 hujafikisha miaka 30 waachieni wenye kuamini kuolewa ni bahati).


Lakini wewe Olewa unapokuwa na mpenzi mmoja (sio mpenzi wa mtu) mnapendana kwa dhati,wote mnania moja ya kuishi maisha yenu yote pamoja na mko tayari kwa wakati huo. Vinginevyo furahia maisha yako kama yanavyokuja.


Nini cha kufanya-Maliza uhusiano na mume huyo wa mwenzio, kufanya hivyo sio mwisho wa maisha yako bali ni mwanzo mpya wa maisha yako. Bado kijana na ninauhakika kabisa utapata mpenzi mpya ambae atakuwa mume wako peke yako.


Tangu umekuwa na uhusiano na mume wa mtu umedai kuwa hakutokea hata mwanaume mmoja aliyekutamkia kuwa anakupenda hata kwa kinafiki, ni kwa vile walikuwa wanakuiba hivyo hakukuwa na sababu ya wao kuji-commite kwako wakati wanajua kwamwe huwezi kuwa wao peke yako........wanaume hawapendi kuchangia, wanapenda kumiliki mwanamke wake peke yake.


Hivyo ukiachana na huyo Mume wa watu, utaona watakavyo miminika. Jitahidi tu kubadilisha mtindo wa maisha yako (soma makala hapo chini).

Kila la kheri.

23 comments:

Anonymous said...

sikusemi vibaya, lkn mimi cpendi tabia uliyo fanya,let me put it this way.u may get married bt kumbuka wat goes around comes around. so nadhani itakuwa vizuri uachane nae na utafute mwingine. but i think ou should turn to GOD.

belle said...

wewe ulitaka mke aachwe basi na ww ukiolewa na ww utaacha.just put yurself in the other lady's shoes for a minute.
na nani atakuambia anakupenda while yur stuck to the married guy.kunamsemo wa kizungu unasema THERE IS NO A FOOL LIKE A FOOL IN LOVE. so sikulaumu sana.
gudluck

Anonymous said...

shosti eee pole sana kwa yaliyokukuta,,mimi naona endelea nae huyohuyo kwa sababu mke wake keshamtenga n awala hana habari nae,,basi mwambie akuoe muishi nae kama mnapendana kwa dhati nyumbani haijalishi kwa sababu mnaoenda kuishi ni nyinyi wawili..na ukimwacha tena huyu unaweza kumpata mwingine kimeo kupita kawaida...ulishalikoroga toka mwanzo wewe linywe tuuu ndugu

Anonymous said...

I'm a guy and huu ni ushauri wangu. Dada yangu i think ulichofanya ni kibaya, you need to acknowledge that. I don't condem the activities ya kuwa na huyo bwana, but dhuluma ambayo umeifanyia familia yake.

However, that is past and i don't think it will make any difference talk about it now.

Ukiamua kuendelea na huyo bwana ni sawa na kucheza kamari. You take a gamble, you may win or loose. Kumbuka jamaa ana familia ambayo haitimizii sababu yako, na pili jamaa anakuja kwako sababu at the end of the day anajua haja jicommit. Things will look different ukiwa mke wake.

I think ni bora umwambia, "Dear i think i like you so much, however after look the prons and cons of this relationship i think it is wise to cut it off. Najua itakuuma and believe na mimi inaniuma but this is for the best interest us."

So, dada yangu end that staff au utakuwa guilty maisha yako yote.

Anonymous said...

Wewe shosti... hebu achana na waume za watu. Unafikiri alivyomfanyia mkewe ni sahihi? tena kabisa unadiriki kusema eti mkewe alipogundua mahusiano yenu ikabidi asalimu amri!!! Hivi unajua kuibiwa mume kunaumaje?? Aliwezaje kutoka nje ya ndoa yake na kukufata wewe,tena akawekeza kabisa!!! Atashindwaje kufanya hivyo kwako ukiwa mkewe? Omba mungu akusamehe hiyo dhambi na utubu kabisa, na umuache huyo mume arudi kwa mkewe. Malipo hapa hapa duniani. Utalipwa vibaya wewe, tena na hivi ulikuwa unafanya uhusiano wenu wazi, huku ukijua fika mkewe anatambua uhusiano wenu, na wewe ukawa unafurahia tu!! mh sina mengi ya kuongeza. Ilala ndugu yangu subiri malipo yako yaja!

Anonymous said...

Belle na Anonymous mmeongea kiukweli kabisa ujue kama alikuwa anakwambia mabay ya Mkewe basi na ww atakutenda hivyo Ila Malipo ni hapahapa Duniani Mind youu kwani Wat Comes Around Goes Around.Hawabebeki wanaume ni Mizigo ya Mavi,Mimi nawaita Mikunguru Ya Zanzibar maana hayatosheki ujue kama mpaka aliamua kumwoa Mkewe ujue anampendaa wewe alikutamani tuu

Anonymous said...

pole sana dada yangu amimi kwamba ipo siku atakuchoka nawe pia kuwa makini sana my dia mwombe Mungu atakusaidia,mume mwema hutoka kwa Mungu

mama sarah said...

Mh, mh, shost nawe ulizidi, ukachukue Mmewawatu ahadi nae ajisahau kama anamke, Penzi lote akahamishia kwako. Mie nakupa tahadhari. Kama aliowa kwa ridhaa yake na alipokupata wewe akamswaga mkewe. Jiulize wewe una lipi lililo zidi sana? hivyo basi, akishakuweka ndani, atatafuta Kimada kingine. Vinyumba vidogo wanasemaga ni vitamu!! take care. Mara nyengine hivo vihuduma unavovipata kwa sababu ni nyumba ndogo hutavipata tena atapewa nyumbandogo yako basi nawe utaanza kupunguza mapenzi na malalamiako yataanzia hapo. Ninauzowefu, mie nilinyang'anywa kama wewe ulivyo nyang'anya. nilipoona mh, nikasarenda kama huyo mke wa jamaa kwa kua namudu maishayangu, nilihama kwake najitegemea. Kweli jamaa kafunga ndoa na huyo mwanamke, Lakini hivi nikwambiavyo huko kwao hakuna amani, kwani jamaa baada ya kuondoka mie katafuta kinyumba kidogo pia kwa hivyo anavinjari nacho nae yuko nyumbani anapika ugali. Take care, na kama familia yako haitaki akianza hivyo vituko utamweleza nani?

Anonymous said...

Kwa kweli wewe dada ni wa ajuabu sana yaan una guts za kujieleza kuwa ulikuwa na uhusiano na mume wa mtu for 5 yrs.kweli is not fear sasa unatakaje??? amuache mkewe aje kwako??? basi ujue na wewe atakuja achwa vile vile thats means huyo mwanaume na yeye pia ni kiheche na sio uko peke yako basi kuna wengine wapo naye find your own husband na sio waume wa wenzio . habari ndio hiyo!!!!!!!!!

Anonymous said...

Wachangiaji wengi wanaonekana kuegemea katika upande wa usemi "what goes around,comes around". Lakini tuangalie, upande mwingine, siyo watu wote wanao oa au olewa wanajiuta compatible baada yamuda. Inawezekana kabisa kuna sababu za msingi zilizofanya huy jamaa akaamua kutafuta kimada nje, na inawezekana ni tamaa tu za kimwili. Ushauri wangu kwanza thibitisha kama sababu zilizosababisha akamuacha mke wake ni kweli. Nasema thibitisha kwa sababu bajua mtakuwa mmeshaongelea na atakuwa amekueleza sababu zilizosababisha kumuacha mke wake. Ukishathibitisha kuwa hizo sababu ni kweli na za msingi, then angalia kama, je hizo sababu zaweza kutokea tena katika uhusiano wenu kama mke na mme? Ukisha jiridhisha kama haziwezi kutokea waweza kuendelea na huyo jamaa.

Anonymous said...

Yaani wewe dada nakuonea huruma. Uliingia kwenye huo mtego wakati mbaya sana kwako na pia ulishindwa kungatuka. Ulitegwa ukategeka halafu ukafikiri ume-win, but you need help both spiritually and psychologically.

I have two friends of mine caught in same situation as you na ni kweli wapo frustrated, you have to be strong and walk out of that now. Then utubu na kumuomba Mungu akusameha na kukuondolea adhabu kwa dhami uliyoitenda.

Another thing ni kwamba one day utatamani ungefuta hicho kitu kisiwe kwenye historia yako kabisaaa. Maana unawezaq pata mtu mwingine ambaye mmependana na kuelewana ila akajua uliwahi kuwa na such form ya relationship na ikawa imeharibu kabisa form ya mahusiano yenu.

Pole sana, uliharibu but from now on work on rectifying i5

Anonymous said...

Yaani wewe dada nakuonea huruma. Uliingia kwenye huo mtego wakati mbaya sana kwako na pia ulishindwa kungatuka. Ulitegwa ukategeka halafu ukafikiri ume-win, but you need help both spiritually and psychologically.

I have two friends of mine caught in same situation as you na ni kweli wapo frustrated, you have to be strong and walk out of that now. Then utubu na kumuomba Mungu akusameha na kukuondolea adhabu kwa dhami uliyoitenda.

Another thing ni kwamba one day utatamani ungefuta hicho kitu kisiwe kwenye historia yako kabisaaa. Maana unawezaq pata mtu mwingine ambaye mmependana na kuelewana ila akajua uliwahi kuwa na such form ya relationship na ikawa imeharibu kabisa form ya mahusiano yenu.

Pole sana, uliharibu but from now on work on rectifying i5

Anonymous said...

Weweeee! achana na hiyo kitu unataka kufanya. Mume wa mtu ni sumu tena mbaya. Kilichounganishwa na Mungu mwanadamu hakitenganishi, trust me, utakaanae muda kidogo tu atarudi kwa mkewe. Wanaume waliooa hawaachagi wake zao kwa taarifa yako. Na ukiolewa machozi ya familia yake yatakutesa, ni laana hiyo dada, fungua akili. Wanaume hawakufuati manake umejifungia milango mwenyewe. achana nae na fungua mlango wako wa ndoa, utapata tu wako, wapo kibao na wazuri.

Anonymous said...

Unajua ndugu yetu, nikuulize swali moja tu. Mfano wewe umepata mume, huyu au mwingine, na ghafula ukagundua kuwa ana mahusiano na mtu mwingine utafanyaje?
Nikuambie ukweli ulivyo, katika hali yoyote `kuibiwa mume au mke' ni kitu kinachouma saana moyoni, ni rahisi kuona ni jambo la kawaida kama hakijakutokea, lakini ukifunga ndoa na kikakutoke kitu kama hicho, utaona jaza yake,kwasababu mnapooana mumeshakuwa kitu kimoja, kwahiyo mtu akija kuwabambanua ili mtengane, lazima kutabakia majeraha.
Kwa ushauri wangu, sijui mpo katika imani gani. Kama imani yako mnaruhusiwa kuishi mitala,basi wewe kama muungwana, nenda kwa huyu mke uliyemuibia, umwangukie na kumomba msamaha, na kama atakukubalia muombe uolewe na mume wake ili muishi uke wenza.
Kama kuna ugumu,basi ndio uone jinsi gani mahusiano ya namna hivyo yalivyo tete.
Ukimwibia mwenzako ili usamehewe, inabidi kwanza utubu kwa kukiri kuwa ulichokifanya sio jambo jema, pili umrejeshee mwenyewe ulichokiiba, na tatu umombe msamaha kuwa umekosa na ya kwamba hutarejea tena kufanya kosa hilo. Ukikubaliwa basi huna dhambi. Je unaweza hilo?
Mimi
emu-three

Anonymous said...

shosti kama unakumbuka misemo ya kiswahili mla kuku wa mwenzie .......utamaliza, fikiria wewe kama ni mwanamke kama mumeo ndio anayafanya hayo isitoshe kama ndio unawatoto wadogo na mumeo huyafanya kama uliomfanyia mwenzio ungependa hayo sio mambo ya kujisifu wala kuomba ushauri kwani jibu unalo mwenyewe wewe ni mwanamke mfikirie mwanamke mwenzio

Anonymous said...

we dada hata haujanibamba! tabia mbaya sana hio kulala na mume wa mwenzio ni dalili kuwa huna heshima! mwanamke kujihshimu bwana..kwakweli umetudhalilisha sana wanawake! anyway no need ya kukulaumu kwakuwa yashatendeka cha msingi since mshaharibu na yeye kaharibu mahusiano na mumewe then hamna budi kuendelea..wat he has to do ni ku grant divorce aachane na mkewe ili muishi pamoja ila kumbuka mwanaume anaye dirik kutembea nje ya ndoa ndio yuko ivo always! na wewe anakutokea nje tu na akishakuweka ndani atakutokea nje tu! upo hapo??

Anonymous said...

Wewe dada nakupa pole sana kwa hilo maana mpaka umejitokeza hapa kweupe ina maana jambo hilo limechukua nafasi nzuri ya kuona kosa.Basi dada kukosa si kosa bali kurudia kosa ni kosa kubwa sana.

Wengi wamekushambulia hapo juu,lakini mimi naamini kuwa kila binadamu anafanya kosa lililo tofauti na la mwingine,wewe lako hilo na wengine wanayo ya kwao hata waliokusema sana hapo juu.

La muhimu ni lile tu ambalo wengi wakushauri kuwa achana na huyo bwana ili arejee kwa mkewe na wewe utafute wa kwako.

Umesema kwamba hakuna mtu amewahi kusema nakupenda,hivyo umejenga aina fulani ya wasiwasi kama unaweza kupata mume.nadhani hilo si jukumu lako sasa bali jukumu lako ni kuninasua katika huo mtego kwanza ambao mimi nadhani ndiyo UNAKULETEA NUKSI.

JAMBO LINGINE KUMBUKA KUWA UMESEMA NDUGU ZAKO HATAKI KABISA UNAENDELEA NA UHUSIANO NA HUYO JAMAA,BASI HATA UKIOLEWA NAYE ATAKUW NDUGU WA NANI?? Na anaposema yeye atakuwa mgeni wa nani?kwani mkewe hayuko?wewe mwenyewe hamjaoana kisheria iweje aseme atakuwa mgeni wa nani?

Umesema kwamba hajatombana na mkewe miaka mitano,Je, una uhakika gani?au una ushahidi gani?Mimi ni mwanume ninayekuandikia,nataka nikutahadharishe kuwa wanaume waogope kama ugonjwa wa ukoma kwani wanajua kughiribu ile mbaya.Achana naye tafadhali kabla ya hatari.Utachelewa kupata mumeo uking'ang'ana hapo.

Wachangiaji tafadhali jaribu kutumia lugha ya kiswahili mnapotoa maoni yenu kwani si wote wanaotuma masuala yao hapa wanajua hicho kiingereza chenu cha makengeza tu kwani mnachanganya mno lugha hata hakieleweki mnaongea nini kwa sis tunaojua lugha hiyo.Hapa ni mahali pa kujifunza na kupata msaada kwa matatizo mengi yanayowasibu watu.usomi si kujua kiingereza!!!!!

Dada nakutakia maamuzi mema haraka.

Anonymous said...

anoy wa 7:31:00, nakataa ulivyosema kufanya kosa si kosa hilo mi sikubaliani nalo, kufanya kosa ni kosa na kurudia kosa ni uzoefu wa makosa kwa hio simpe fursa huyu dada akajiona hajafanya kosa amefanya kosa tena kubwa anachotakiwa ni kujifunza na alilofanya na kama atarejea basi atakuwa ni mzoefu hayo makosa

Anonymous said...

kuibiwa boyfriend inauma sikwambii uibiwe mume uliebarikiwa nae hembu jiulize wewe dada au hujawahi kuibiwa boyfriend, sembuse mume khaaaaaaaaa

Anonymous said...

kawaida mwanamme mwenye mke au girlfriend tu, akitaka kufanya affair na mwanamke mwengine na kama wewe unajua kama yeye hayuko single hata siku moja mwanamme hawezi kumsifia mawanamke wake au mke wake kwako always atakwambia mke wangu mmbaya, hatulali pamoja, hatufanyi mapenzi au hajui akivaa hapendezi na mengi ya kupwa na kujaa, na atakusifu wewe na wewe kama huna akili utajiona ndio unapendwa, lakni siku zikizidi mke wake hamuachi juu ya kuwa mabaya yote aliokuwambia kuhusu yeye na weweutajiona siku miaka inakatika hakuoi na mkewe anaendelea nae, wewe ukimuambia suala la kumuacha mkewe hakupi jibu kamili na ukimuambia akuoe hakupi jibu kamili wewe jiulize kwanini.hao ndio wanaume shoga wakitaka kufanya affair hamsifu wake ili umkubalie kwani akimsifu mwanamke mwenzio kkwako hutopenda sindio , kwahi fanya uondoke tafuta wako wa peke yako naamini siku utakayopata wako hutopenda kuchangia na mtu na ukisikia kuna nyumba ndogo hutopenda lakni ujue yatakurudi yote uliofanya.

Anonymous said...

doo yamenigusa na mie niko kwenye mtego wa huyo huyo dada...nalia kila kukicha najitahidi kujinasua kwenye huu mtego...mungu anisaidie

Anonymous said...

Nashukuru sana kwa ushauri wako Da dinah na wachangiaji wote mlioniponda na kunishauri vizuri ila kila mtu aelewe ana makosa yake bora na mie niliyejiweka wazi kwan tatizo hili limekuwa gumu kwangu kujinasua.

Nimeyasikia yote na nitayatendea kazi nachowaomba tena ndugu zangu mnishauri nitumie mbinu gani katika kuachana na huyu bwana na niwakati gani muafaka unastahili kumweleza ili 2fikie mwisho kwan kila nikimtamkia kuachana inakuwa ugomvi hauishi kila siku na ndo inakuwa kama vile nimemweleza abaki kwangu.

Kwakwel nahitaji msaada na ushauri wenu wa dhati ili unisaidie na sio kuniponda. Asanten na siku njema wote

Dinah said...

Asante kwa ufafanuzi. Nimeweka maelezo yako yaliyowazi kama topic inayojitegemea na itatoka kesho.

Kumbuka kuwa kutokuwa wazi ndio kumesababisha watu kupatwa na hasira, kwani kutoka na mume wa mtu ni kitu ambacho wengi tusingependa kukitenda au hata kitutokee.

Pole sana kwa kukwazika. Lakini Hongera kwa kuwa wazi.