Tuesday, 11 November 2008

Kubemenda mtoto ni Imani tu au kuna Ukweli?

Ni matumaini yangu kuwa unakumbuka ile somo kuhusu kufanya ngono baada ya kuzaa/jifungua kiasili, nilipokea maswali mengi kuhusu Kubemenda mtoto ambayo niliayajibu kwa kirefu kupitia Kipindi changu Radioni. Lakini kwa faida ya wale ambao hawakubahatik akunisikia basi karibus ana.

Unaweza kunipa maana ghalisi ya neno Kubemenda?

Nijuavyo mimi au nisema kama nilivyokuwa nikisikia, kubembenda mtoto ni kitendo cha baba na mama wa mtoto huyo kufanya mapenzi/ngono na watu tofauti kabla mtoto hajakua vya kutosha au hajatoka Arobaini. Inasemekama ktk kipindi hicho mama akifanya mapenzi basi mtoto anapata matatizo kiafya.

Matatizo yenyewe hujitokeza mtoto anapofikia umri wa kuanz akuropoka maneno, kutembea, kujaribu kusimama n.k. kwa kawaida ni kati ya miezi 6 na nane kwa watoto wengi lakini wengine huwahi au kuchelewa zaidi.

Matatizo hayo ambayo kama vile kuchelewa kufanya/anza hatu ahizo za mwanzo za ukuaji wake, mtoto anakuwa kama vile anautindio wa akili, anatokwa na udenda ovyo....yaani anakuwa mlemavu.

Endelea kuwepo basi........pia nitakupa maelezo muhimu yahusuyo ngono ya mdomo. Una nyege mpaka kwenye kope na mume anataka mpaka anatetemeka kama sio kulia lakini uke ndio uko"sore" unaamu kumpa mdomo na yeye akupe mdomo......si ndio? Nini kinafuata baada ya hapo basi?

Naja.....

7 comments:

Anonymous said...

Samahani Dina bora kuuliza kuliko kujiuliza! mie ni msomaji mzuri wa hii blog yako, lakini sikujua kama una kipinda cha radio..unatangaziaa radio gani? kipindi chako kinaitwaje? muda gani? au wewe ndio Dina Marios wa Leo tena ya Clouds?

Dinah said...

Mimi sio Dina Marios.

Kipindi changu kipo kila siku ya J'2 saa tatu za usiku kwa masaa ya Tz. Kipindi kinaitwa Dinahicious live.

Radio inapatikana online upande wa kulia ukibonyeza nembo ya Bongo radio.

Karibu sana.

Anonymous said...

Kubemenda maana yek sijui lakini wanasema eti mwanamke akifanya ngono alafu amnyonyeshe mtoto bila kuoga mtoto anadhurika na kushindwa kukua vizuri au anachelewa kuongea na kutembea.

Anonymous said...

Hamna ushaidi wa kisayansi unaosapoti hiyo mada ya kubemenda,ni imani za kiasili tu,ni bora kufanya tafiti zaidi za maendeleo ya mtoto na ukuaji,kuna magonjwa mengi ya watoto kama Down syndrome n.k,au ya kihormone ambayo yanaweza kumfanya mtoto akachelewa kutembea n.k.Nchi kama Tanzania inakosa sana utafiti wa mambo mbalimbali kama magonjwa ya watoto na ukuaji,kwa hiyo vitu vya kitaalamu vinaongewa na watu wasio wataalamu.Tunukuu vitabu vya kisayansi na sayansi ya magonjwa sio kuongea pasipo na vyanzo vya kueleweka kama mambo ya vijiweni.
Mdau wa magonjwa ya watoto Sweden

Anonymous said...

Dada Dina nashukuru kwa blog yako inaelimisha sana,nakupongeza.
Nasubiri mada ya ngono ya mdomo,vp inakuja lini?plse tupe mambo dada.

Anonymous said...

Dada dinah mimi naomba kujua zaidi ktk suala hili la kufanya mapenzi baada ya mtu kujifungua,kuna watu wana imani ukifanya mapenzi wakati una mtoto unamtesa mtoto mpaka utosi unaweza kugawanyika je hii ni kweli?

Anonymous said...

mambo dina mi ni msomaji sana wahii blog yako iko poa sana na inatuelimisha sna wapendwa wako.tuje kwenye hii mada ya kubemenda na fikiri watu wanaongea vitu vingi kwamba ukiwa na mtoto kisha ufanye nje na mpenzi mwengine mtoto anaweza kuwa na afya mbaya hapana kwasababu mfano ni mimi nilikuwa na wangu aliyenipa mimba ila alikuwa mbali ushaona sasa nilikuwa na wangu mwengine wa pembeni baada ya mtoto kuzaliwa nilisubiri kama mwezi miwili kabla ya kufanya yale mambo matamu sababu ye ndo aliyebaki wakaribu kunimalizia hamu so nikawa nafanya nae kitendo kile vizuri tuu ingawa watu walikuwa wanasema kubemenda '' ila amna kitu kama hiko '' mi nafikiri niimani tuu .sababu mtoto wangu sasa nimkubwa tuu na alikuwavizuri ,aliwahi kuongea, kutembea bila matatizo yoyote. mina fikiri hayo mambo ya kitaalamu zaidi kama alivyosema mdau hapo juu kuhusu magojwa ya watoto down-syndrome [ndo mtoto anaweza kuwa vigumu kuongea ,kutembea haraka ila anakuwa ni mtoto kama watoto wengene ila yeye ukuaji wake ni tofauti .ni hayo tuu wadau wenzangu wa blog ya kujidai [dinahicious.]