Sikujua kuwa mpenzi ni Kaka,Nifanyeje-Ushauri

" Habari dada dinah mimi ni msomaji wako wa kila siku naitaji sana ushauri wako ili ni niweze kufikia hapo ninapotaka na naitaji sana ushauri wa wasomaji wenzangu.

Mimi ni msichana 24, kutoka ndani ya Tanzania tatizo nililonalo ni kwamba mimi nilikutanana na kijana mmoja ktk chuo kimoja basi tukatokea kupendana sana lakini siku moja tulijikuta wote kwenye msiba wa Binamu wa mama yangu ambaye kwa upande mwingine ni mjomba wangu ambae ikatokea kuwa ni baba yake mdogo Mpenzi wangu.

Sikuamini da Dinah lakini swali linakuja bado tunapendana sana na Je undugu uluopo unaweza kuwa kikwazo mpaka sasa bado hatujaachana na nilimuuliza Bibi yangu akaniambia kuwa uwezo wa kuishi mume na mke upo ila mpaka mama yangu akubali naogopa kumwambia mama nifanyaje?

Nimekuja kugundua kuwa huyo mpenzi wangu ni mtoto wa marehemu Binamu yake mama yangu mzazi je dada dinah mama akikataa mi nitakuwa kwenye hali gani? nampenda sana na yeye ananipenda mno naombeni ushauri wenu jamani jamaa yupo tayari kunioa.

Wazazi wetu ni Binamu wa damu. Kibaya zaidi nampenda sana na yeye ananipenda na tumeshangonoana. Hatutaki mapenzi yetu yawe ya siri tena, je dada dinah kama mama yangu akikataa nitafanya nini? Nimuache au niusikilize moyo wangu au jamii itanichukulia mimi ni maLaya?

Najiuliza maswali mengi sana kiasi kwamba nilimuuliza mchungaji akaniambia kuwa hilo swala halina tatizo kwa kuwa sisi ni mabinamu wa pili. Najiuliza tayari sisi tushafanya ngono sioni sababu ya wawo kunizuia?

Dada dinah mi sielewi nini hatma ya penzi letu, siunajua moyo ukishapenda, Natamani kumueleza mama lakini naogopa akisema hapana! mi nitaumia zaidi, naitaji ushauri wako na
wasomaji wenzangu"

Jawabu: Shukurani kwa ushirikiano wako, pole sana kwa kuwa katika utata wa kimapenzi na undugu. Kwa Makabila mengi Tanzania kuolewa na huyo kijana sio tatizo kwani undugu wenu sio that "strong".

Kwetu (pande zote mbili) ni ruska kabisa kuolewa na binamu yako yaani mtoto wa Mjomba (upande wa kike) sio Binamu mtoto wa Shangazi (upande wa kiume), nafikiri hii ni kutokana na Imani kuwa mtoto akizaliwa anabeba damu ya baba yake zaidi kuliko ya mama yake.(Kisayansi sijui, kimila ndio hivyo tena).

Napenda nikufafanulie hapa kabla sijakuambia nini ufanye. Mama yako na Baba wa Mpenzi wako ni mtu na Binamu yake kwa maana kuwa mmoja wao ni mtoto wa Shangazi/Mjomba(kuna damu za pande mbili tofauti hapo) kwa vile mmoja wa wazazi wao alioa au kuolewa na mtu tofauti ambae sio ndugu.

Huyo binamu mwenye damu 2 tofauti amekwenda kuoa mtu mwenye damu tofauti na sio ndugu na kuzaa mtoto ambae atakuwa na damu 3 tofauti ambazo zinafanya undugu uwe wa mbali kimtindo.

Watoto hao ndio wewe na Mpenzi wako mna damu za watu 3 tofauti kwa maana kuwa mama wa baba yako(bibi anadamu 2 tofauti), baba wa baba yako(babu anadamu 2 tofauti) na baba yako anadamu 2 tofauti.

Hali kadhalika mama wa mama yake mpenzi wako(Bi'mkwe anadamu 2 tofauti), baba wa mama yake mpenzi wako (babu'kwe anadamu 2 tofauti) na mama yake mpenzi wako (mam'mkwe anadamu 2 tofauti)....hivyo Technically ninyi sio ndugu wa damu.

Hakuna haja ya wewe kumuambia mama moja kwa moja bali mtumie bibi (hawa watu wanambinu zao za kizamani za kufikisha ujumbe bila kusababisha mshituko), itachukua muda lakini hatimae mama atajua nini kinaendela kati yako wewe na huyo mpenzi wako hasa kama mnakenda kufunga ndoa.

Lakini kama unahisi kuwa mama atakuwa mgumu kuelewa na unauhakika kuwa mnapendana sana na mnania moja ya kuishi maisha yenu yote pamoja milele na milele basi ni vema kufunga ndoa kwanza kisha ndio kumwaambia nini kimefanyika, hapo hatokuwa na namna ya kuweka kigingi au kukataa kwa kisingizio cha undugu ambao upo kati ya wazazi wake na wazazi wa baba wa Mpenzi wako.

Kila la lililojema.

Comments

Anonymous said…
Dada Dinah, naomba huyo dada atuambie pia kama ameishangonoka/tombona naye ili wachangiaji tuweze kukwepa kuwa bias katika ushauri wetu.nangoja kwa hamu kusoma ufafanuzi wake.
Anonymous said…
pole sana dada,kwa yaliokufika, ushauri wangu ni kwamba tuende kwenye dini kidogo,kwa sisi waislam mtu ambae hawezi kukuoa ni yule mlie zaliwa tumbo moja ninamaanisha baba mmoja mama mmoja huyo hawezi kukuoa lakni waliobaki wote unaoa au unaolewa hata ikiwa mama yako mdogo au baba yako mdogo kiumri mnaendana manaeza kuoana, lakni kibinadam na tunavoishi maisha ya leo mengi hayawezekani kutokana na familia zilivo, ila binam inawezekana mtoto wa mamdogo inwezekana.
kwa mtazamo wangu mimi hapo hujakosea na tena kwa mambo ya sikuhizi watu hustiriana weneywe kwa wenywe.
Anonymous said…
you go on, nasaba hiyo hiko mbali sana, other wise utaja gunduabaadae kuwa kwa kuchambua kiasi hicho karibu 1/4 ya kabila moja ni ndugu. mweleze mama ataelewa tu. na kama wewe imani yako ni ya uislamu, huyo haina nasaba naye kabisa na ruksa kutoa au kupewa kipondo - kugonoka
Anonymous said…
Mtoto wa binamu wa mama yake? Mbona huyo yupo mbali tu, unaweza ukamuo bila wasiwasi,lakini ni kweli kama mama ataona haina `noma'
Nakumbuka, zamani walikuwa wanaoa binamuu ili kuhakikisha kizazi cha familia hakiendi mbali, lakini siku zilivyoenda hali hiyo ikafifia.
Kitaalamu,wansema sio vyema,kwasababu inaweza ikawa inaendeleza `uzaifu' fulani wa kurithiana.
Jambo jema nikukutana na familia zenu mliweke sawa, nafikiri watawaruhusu tu
emu-three
Anonymous said…
Mdogo wangu! Mimi nahisi huyo ni ndugu yako kabisaa Mama yako akisikia hawezi kukubali hata kidogo. Hujui kuwa penzi la ndugu ndio huwa linanoga kuliko.
"si unajua familia zetu za kibongo, mnaweza itana ndugu kumbe hata DNA hailingani".....lol nimependa hiyo sentensi yako ya mwisho imeonyesha nikiasi gani uko in love na huyo mpenzio

kwa maoni yangu mie naona inawezekana kuoana mfano sijui niseme waarab kama si waislam inaruhusiwa ndoa kati ya mtu na binamu yake..."Binamu nyama ya hamu ndipo msemo huo ulipotokea" sasa sijui we wa dini gani.

sembuse huyo binamuwa mama ako...na ulizia wakuu wa ukoo lakini hapo nimeona bibi kakwambia inawezekana inamaanisha kiukoo imepita sasa tume wakubwa waongee na mama mfunge mjadala

kila la kheri ...picha za harusi uniforwadie tu mie...lol
Anonymous said…
Huyo ni mtoto wa mjomba ambaye katika jamii nyingi na hata baadhi ya dini, kama dini ya Kiislamu, mnaweza kuoana kisheria. Hakuna matatitizo. Wasioweza kuona na mama yako na ndugu yake mwenyewe, awe halisa -yaani mama mmoja baba mmoja- au ndubu kwa baba tu au kwa mama tu. Wao wenyewe kwa wenyewe hawawezi kuoana, lakikni watoto wao wanaweza kuoana; yaani mtoto wa mwanamke anaweza kuolewa na mtoto wa mwanamume- ambaye atakuwa mjomba wa mtoto wa mwanamke na haloo kwa mtoto wa mwanamume. Hao wanaitwa mabinamu: kama ulivyo wewe na mtoto wa mjomba wako.

Ila, kiafya, si vyema kufanya hivyo kwa kuchelea kwamba kama kuna ugonjwa wa kifamilia - yaani ugonjwa wa kuritihiwa kifamilia, basi kuna uwezekano mkubwa wa kuwarithisha watoto wenu kwa urahisi zaidi, kuliko lau kama mngekuwa mnatoka familia mbili tofauti, au zenye uhusiano mdogo wa damu. Hivyo, ni vyema kwenda kupima kwa madakitari, kwanza, ili kujua kama hakuna tatizo la maradhi ya kifamilia. Mfano wa maradhi hayo ni Kisukari, Moyo; Shinikizo la damu; Safura; Vichembe-chembe vya damu (sickle cell) na kadhalika.

Kila la heri.
Anonymous said…
HIYO NI RUKSA KABISA TENA KMA NI MTOTO WA KISLAMU WALA HAINA TABU,SEMA TU SASA MAMA AKO ATALICHUKULIAJE KUNA UWEZEKANO AKALIONA KMA NI JAMABO LA AJABU ILA KMA NI MSHIKA DINI NA DINI YAKE NI ISLM BASI NADHANI HAPO KUTAKUWA HAMNA TATIZO KABISA.PIA OMBA MUNGU SANA ALIWEKE HILI LIWE RAHISI KWAKO MHH NAKUMBUKA NILISHGONONANA NA MTOTO WA SHNGAZI YANGU KABISA DUHH ILIKUWA TAMU MNO USIOMBEE YANI KWELI BINAMU NI MTAMU
NAWAKILISHA
Anonymous said…
Nashindwa kutoa ushauri kwa sababu huyo dada hajatoa ufafanuzi wa yale dada Dina ameshauri yatolewe ufafanuzi.Inaonyesha hajaenda internet kuangalia kilichijiri hapo.tafadhali fanya hima kufafanua jambo lako ili litolewe ushauri wa kukusaidia.
Kila la heri
KKMie said…
Anony@8:42PM, muuliza swali katoa ufafanuzi, hebu some vizuri kwenye ufafanuzi.