Wednesday, 29 October 2008

Hili ni Buti au Posa?-Ushauri

Dada Dinah naomba niwasilishe shida yangu kwa njia ya kunukuuu.

"Stella! Najua kuwa unanipenda sana. Lakini tangu nimekuwa na wewe roho yangu inaniuma sana kila ninapoenda kanisani kuwa nafanya mapenzi kabla ya ndoa. Kwasababu nampenda Mungu wangu na natamani kuishi kwa mapenzi ya sheria zake naomba tuache kutenda dhambi hii.

Nisamehe sana kwa uamuzi huu mgumu. Nakuombea nawe ufuate mapenzi yake. Usiku mwema na mungu akubariki."

Je hapo nifanyaje? maana mpaka sasa sijamjibu kitu chochote hivyo naomba unipe jibu la kumjibu. Na pia nimemuomba kuonana nae na amekubali, je nikimuona nimwambie maneno gani?asante sana wako Stella.

Jawabu: Asante Stella kwa mail na pole kwa mshituko. Mpenzi wako ni mmoja kati ya wanaume wachache sana wenyewe uwezo wa kuwa wazi. Huyu bwana kutokana na Imani yake ya Dini amegundua kua mlichokuwa mkikifanya ni makosa/linyume na Imani yake na hakuwa na amani kila mlipokuwa mkifanya, hivyo unapaswa kuheshimu hilo.

Hayo maelezo yake hakika yanachanganya kidogo na huenda kuna mawili matatu ambayo mpenzi wako anawakilisha kutokana na ujumbe huo, kama nilivyoweka kichwa cha habari hapo, inawezekana kabisa akawa anakutaka wewe uamini kule anako amini, yaani muwe na Imani moja ili mfunge ndoa na kufanya mapenzi ndani ya ndoa.

Mpenzi wako huyu (kutokana na upande mmoja wa maelezo yake)hajakuacha wewe kama mpenzi bali ameacha kufanya ngono na wewe kabla ya ndoa na kama alivyosema anakuombea ili ufuate mapenzi yake Mungu. Inaonyesha huyu bwana anakujali na hata ulipoomba kukutana nae alikubali moja kwa moja bila kukuzunguusha.

Lakini pia kwenye maelezo yake hayo kasema kuwa "najua unanipenda" hakuna mahali amesema kuhusu hisia zake juu yako,hiyo inaonyesha kuwa wewe ndio ulikuwa unampenda zaidi kuliko yeye alivyokuwa akikupenda, natambua ulipokuwa ukifanya nae ngono uliamini kuwa anakupenda lakini haikuwa hivyo.

Unajua mwanaume ni kiumbe wa ajabu sana linapokuja suala la ngono, huwa hajui kumtosa mwanamke japokuwa hafurahishwi na anachokifanya au anajua kabisa kuwa ni kosa lakini bado ataendelea kukifanya ili kukuridhisha na kutokuumiza hisia zako.....hata akiamua kukutosa bila kukungonoa hutotambua, atafanya hivyo bila wewe kujua kirahisi. (kuna mbinu zao za kufanya hivyo nitazielezea ktk siku zijazo).

Sasa kwa vile tayari mmepanga kukutana inabidi iwe hivyo, ila mimi ningekushauri kuepuka kuzungumzia kilichotokea kwani hakuna litakalobadilika hasa kama wewe wataka ngono tu ndani ya uhusiano mliokuwa nao, ni wazi kuwa haitopatikana.

Ikiwa uhusiano wenu ulikuwa zaidi ya ngono basi unaweza kumjibu kwa SMS/Barua pepe kwa kumwambia "Samahani sitoweza kukutana na wewe kama tulivyopanga. Naheshimu uamuzi wako wa busara, pamoja na kuwa nakupenda nilikuwa nakosa amani kabisa kila tulipokuwa tukifanya mapenzi lakini nilikuwa nafanya hivyo kwa ajili yako nikidhani ulikuwa unapenda.

Ni jambo jema mimi na wewe kuacha dhambi hii na kufanya tendo hili takatifu kisheria na kwa mapenzi yake Mungu". Hapo utamuacha njia panda kama alivyokuacha wewe......uchune!

Kama anakupenda na ilikuwa posa basi atakutafuta iwe kwa simu/sms au barua pepe na kujaribu kukushawishi ili ufuate imani yake na hatimae kufunga ndoa au kukuuliza maswali au kuomba m-baki marafiki n.k.

Akiuchuna ujue buti.....usipoteze muda bali endelea na maisha yako kwani penzi halilazimishwi.

Natambua buti linauma haijalishi kama umepigwa la kwenye meno au ummempiga mwenzio kwenye ugoko, yote yanauma the same lakini siku zinapita na unajikuta umesahau. Ni sehemu ya maisha na hatunabudi kukabiliana na kila linalotujia liwe zuri au baya.

Endelea kuwepo hapa na kila la kheri.

8 comments:

Anonymous said...

Dada Stella,
Kwanza NALIPONGEZA SANA MCH na KANISA ambalo mpenzi wako anasali.Kwa nini nalipongeza, ni kwa sababu ni makanisa machache ambayo ibada zao zinaweza kumbadilisha mtu, kama ambavyo mpenzi wako alivyobadilishwa. Ibada za makanisa mengi zimepoa,watu wanaenda makanisani kama mazoea,huku wakitenda dhambi na kutokana na mahubiri yalivyopoa, hawabadiliki.
Kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa ni DHAMBI KWA MUNGU.Kwa kuwa umemuomba muonane nae amekubali, basi ana mipango ya ndoa huyo, na sio rahisi mtu kukupa sababu za MUNGU kama angekuwa anataka kukupiga kibuti.
Mkionana mueleze wasiwasi wako, kwamba unahisi atakupiga kibuti, nae kwa upendo atakuelezea vizuri na kwa undani jinsi alivyofikia maamuzi yake.
Nawe nakushauri umueleze kuwa ungependa uende ukajiunge na kanisa analosali ili iwe rahisi kufunga ndoa, na iwe rahisi kuweza kusimama na kuvumulia vishawishi vya kuja kurudia kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa.
Pia mjiepushe na kukaa wawili9peke yenu) tu sehemu ya giza au kificho ili kujiepusha na hisia za kurudia kufanya tendo la ndoa.
Watu wengi wanapinga kuwa mtu anaweza kuishi bila ya kufanya tendo la ndoa,lakini ukweli ni kwamba teno la ndoa linaendeshwa na hisia hivyo kama utaweka hisia zako huko,basi unaweza kufanya na kufikia kuwa mtumwa wa mapenzi, lakini kama hisia zako utazifanya kwamba unaweza kuishi bila ya tendo la ndoa, na ukamuomba MUNGU akuwezeshe,basi ATAKUWEZESHA.
Mimi niliwahi kufanya tendo la ndoa mara kadhaa,baadae dhamira ikawa inanisuta kuwa wasichana wote niliofanya nao sikuweza kudumu nao, basi nikasutwa kwamba nafanya kinyume na MPANGO WA MUNGU, nikaacha hivi sasa naelekea miaka mitatu ya kukaa bila ya kufanya mapenzi na nina mchumba ambaye tunatarajia kufunga ndoa mwakani.
Hapo juu ulivyoandika, kwamba dina akushauri ili ujue utaenda kumuambia huyo rafiki yako utakapokutana nae,nakushauri kuwa uwe na maamuzi yako mwenyewe,usitegee sana mawazo ya mtu mwingine ndio uyaingize katika uhusiano wako,hiyo si busara.Uwe unapokea ushauri halafu kabla ya kuinginza katika uhusiano,jaribu kuchuja kwanza,hata huu wa kwangu,jaribu kuuchuja kwanza.
MUNGU akupiganie ili uweze kusimama na mpange mipango ya kufunga ndoa takatifu.
MUNGU AKUBARIKI SANA,
Mtanzania,
tmajaliwa@yahoo.com.

Ckie said...

kweli ulivyoweka hii ni buti au posa?? it could be both, buti amepata mtu mwingine na pengine si posa na si buti, ameamua tu kujirudi na kurudia imani yake,
wewe mwenyewe akili kichwani, mara ya kwanza ilikuwaje kwani? who proposed ngono between the 2 of you, did he seem to regret the act after doing it? kama ndivyo basi alikuwa anafanya with a guilty conscious, kama sivyo basi alikuwa na yeye anaenjoy kama wewe, nadhani heshimu maamuzi yake na muendelee na urafiki wa kawaida, usimuache, kwani uko naye kwa mengi na hicho kikiwa kimojawapo, ila kama na urafiki hataki tena... salalaaa huyo kapata mtu......ila usikonde kama bado kijana tulia usimuoneshe uko desparate all the best !!

Anonymous said...

Pole sana nafikiri nikisema mdogo wangu Stella nitakuwa sijakosea sana. Hii ni mojawapo ya dalili za mwanaume kukata kona, yaani amekosa ujasiri wa kusema anataka kuachana na wewe hivyo anatumia vigezo ambavyo vitamuweka mbali na wewe, na ukifuatilia kwa karibu usikute ameshapata replacement yako. Sasa hapo wala sikushauri umlazimishe au ung'ang'anie kwa sababu ni hatari sana kupenda usipopendwa na utapoteza muda wako bure. Wewe mshukuru kwa kuliona hilo leo wakati huko nyuma alikuwa akifurahia hayo anayoyakataa leo, na usonge mbele kwa kuanza kutafuta atakayekufaa taratibu. Huyu utamsikia tu ripoti zake baada ya muda. I am sure kama wewe ni mzuri na unajiamini utapata mtu wa maana.

Anonymous said...

Mimi napenda kumpogeza sana huyu jamaa yako kwa kuamua kuachana na uzinzi! Hakuna asiyejua kuwa kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa ni uzinzi, ndiyo maana linaitwa tendo la ndoa!!

Uamuzi wake ni wa busara sana na inapasa hata wewe ndugu yangu Stella ukampongeza na kuungana naye ili msiendelee kumkosea Mungu kwa kutenda maovu.

Umeomba kukutana naye, nakushauri siku hiyo mtie moyo kwa uamuzi wa busara aliouamua, hakuna uamuzi bora kuliko huo wa kumkumbuka muumba wako kwani siku moja utarudi kwake na kutoa hesabu za maisha yako.

Dada yangu Stella, naomba ufahamu hivi, kama maamuzi haya ni kwa sababu ana mtu mwingine, basi ni bora sana ameamua kukuacha kuliko angeendelea na wewe huku ana mwingine, maana mwisho wake ni kifo. Lakini kwa maelezo aliyoyatoa, mimi siamini kama sababu ni hiyo, bali inaonekana ameamua kuacha dhambi.

Kuna wale waliosema kuwa kama zamani alikuwa akifurahia au nani alianzisha hoja hiyo, mawazo haya hayana uzito wowote kwani hata kama ni yeye, na kama sasa ameona vema aache uzinzi, basi anahitaji kupongezwa huyo. Kama mtu akiacha ulevi tunampongeza, akiacha wizi tunampongeza kwa nini asipongezwe akiacha uzinzi? Uzinzi ni mbaya sana na madhara yake ni makubwa ingawa watu wengi wanachukulia rahisi rahisi.

Mwisho nakushauri na wewe Stella uache uzinzi, huyo ndugu amekuonyesha njia, ni vema ukaacha kabisa ili nawe utafute njia ya kumpendeza Mungu. Mungu atakubariki. Ushauri wangu ni kuwa yatoe maisha yako kwa Yesu ili awe Bwana na Mwokozi wako, yaani uokoke, na huyo ndugu yako mwambie naye aokoke, ili ajikabidhi kwa Mungu na ndipo mtakapouona wema wa Mungu.

Nakutakia mema

JayJay said...

Kumbe hata walokole huwa wanapita kwa Dinah kujifunza mambo. Stella wewe na mpenzi wako mlikuwa mnafanya ngono kabla ya ndoa na sio nje ya ndoa ambayo mimi ndio najua kuwa ni uzinzi.
Mpenzi wako anataka mfunge ndoa kutokana na imani yake kwa kukuomba ufuate mapenzi yake. Yaani mfuate huko anako amini mkafunge ndoa.

Anonymous said...

Dada pole sana kwa mawazo. kumbuka tu kuwa wanaume wana staili tofauti za kutuacha, kuwa makini na endelea kumchunguza kama kweli anayo yaongea yanaendana na anachomaanisha. kama sivyo utamuona tu anavyotapatapa hata mda wa kukaa na kupanga misingi ya maisha yenu atakuwa hana kila siku ana dharura. hivyo utajua kama muongo na achana nae kwani sio chaguguo lako na Mungu atakupa ambae mtaishi milele
asnte
super!

Anonymous said...

Eheeeee!! Stella una bahati ya hali ya juu sana kama umeweza kushuhudiwa na mtu mliemkosea Mungu pamoja basi shika hilo, na wala usishughulike na kuwaza kuwa amepata mtu mwingine.

Mtu huyo nampongeza sana, kila jambo lina mwisho wake, na kila jambo lina mwanzao wake, hivyo huo ni mwisho wa kuvunja amri ya Mungu na pia ni mwanzo wa ninyi kumrudia Mungu wenu na kumpendeza sana.

Nimeona wasichana waliotoa maoni yao hapo juu wameegemea zaidi kudai kuwa ni njia tu ya kukuacha, la hasha, mawazo kama hayo ndiyo yanayowaponza sana wasichana wengi kuwa wepesi tu wa kuwaza kirahisi na kuanza kurubuniwa kutombwa na mtu asiyekuwa na mzigo naye wa kujenga unyumba na maisha ya kifamilia.
Tafadhali Stella elewa kuwa kwa kupata ujumbe huo kutoka kwa rafiki yako huyo umepona!!!

Je, ulipomwomba mkutane unataka uendelee kumbembeleza ili muendelee kutombana kabla ya ndoa au unataka vipi>hapo hakuna ushauri zaidi ya kukusihi kumshukuru mwenzio kwa alert hiyo kuwa kumbe amekuokoa katika jinamizi hilo la uzinzi.tena amekuambia tu kwamba amemkosea Mungu kwa kuzini nawe, hivyo kumbe mna nafasi ya kutengeneza mahusiano yenu vizuri ili mpange mpango wa kuoana.

Hatari yenu wasichana ni hiyo kwamba mkishawapa penzi wanaume huwa mnapoteza sana msimamo, kwa sababu mwanaume anakuwa ameisha kukuonja na wewe unaona umeishahadharika tayari hivyo kunga'ng'ana naye. Mungu ambariki huyo kijana na wewe Stella, Please. please change your behavior right away for it is not safe and it sounds so crazy to continue intending having sex with guys.Please try to think out of your box. This world is full of diseases! what do you think dear sister? Is it sex part and parcel of your daily life?Please make a difference from now onwards in your community.Stay thinkable and macusudical patinowery.Good luck baby

Anonymous said...

asanteni sana ndugu wachangiaji, dada dinah kwa maoni yenu, mawazo yenu na mitazamo yenu.

na pia naheshimu sana mchango wa kila mtu naahidi kuyafanyia kazi kila moja kwa muda wake.

na pia napenda nikujibu ndugu mchangiaji wa hapo juu yangu kuwa nia yangu haikuwa kwenda kumbebembeleza tuendelee kutombana. ila ilikuwa ni kutaka kujua ni sababu gani nyingine ambazo zimemfanya kutuma sms hiyo. maana ikiwa ni swala la mungu tuko mimi na yeye almost 2yrs na kwanini asiniambie live anitumie sms. ndio lengo langu kuu.

na pia dada dinah ushauri wako ninaufanyia kazi leo hii nitamsendia hiyo sms muda na wakati kama ule alionisendia yeye yaani saa 7 usiku. na majibu yake nitakurudishia.

asanteni sana
Stella