Familia haimtaki, Kasaliti penzi letu,nimfanye nini?

"Unajua mapenzi ya ndoa ni kitu tofauti na mapenzi kwenye uhusiano wa kawaida. Linapotokea jambo ndani ya ndoa mnaweza mkasameheana yakaisha, lakini lipo jambo likitokea inakuwa kama kisu kimekata nyama pande mbili, kuziunganisha inakuwa sio rahisi inahitajika nguvu ya ziada.

Sijui wenzangu mtasemaje mkisikia kisa hiki `live' ambacho mhusika ndiye aliyeniletea na hatua aliyoichukua sijui wewe au mimi ungeweza kufanya hivyo.


'Rafiki yangu, hapa nilipo nimechanganyikiwa sina mbele wala nyuma. Wewe ndiye wa kwanza kukuhadithia kisa hiki kilichonikuta. Uliniuliza kuhusu hali ya shemeji yako, ukasema mbona hana raha, na unaona kama ananyong'onyea. Ni kweli, hana raha, na mimi mwenyewe namuone huruma kwa namna fulani, lakini hata hivyo nahisi adhabu anayoipata sasa bado haimtoshi kwa kitendo alichonifanyia.


Shemaji yako tumeoana kwa shida, wazazi wetu hawakukubali ndoa yetu, kwasababu hasa za utofauti wahali za kiuchumi. Mimi ni malalahoi, mwenzangu ametoke upande wa geti kali, lakini tukawa tumependana kupita kiasi. Hii ni habari ndefu kidogo.



Mapenzi yetu yalifikia kuposana, lakini posa ikagonga mwamba, sio tu kwa upande wa kikeni hata kwetu wazazi wangu walikataa wakisema familia hiyo ina nyodo, wanaijua sana. Lakini sisi hatukujali na kwakuwa tulishapendana tukasema mbele kwa mbele.


Visa vingi vilitokea, mpaka nikawekwa ndani kwa visingizio vya ajabu, siunajua tena hawa wenzetu wenye hela, wanaweza wakakusingizia kitu, ukajikuta umefungwa. Nilifungwa miezi kadha nikatoka jela, nabado mapenzi yetu yalikuwa pale pale, mwenzangu akawa amenisubiri na hatimaye wazee walisalimu amri, tukafunga ndoa.


Maisha yetu yalianza kwa shida, kwani jela iliharibu ajira yangu, na kupata kazi ikawa shida ajabu. Nikawa nabangaiza hapa na pale, na mungu akajalia nikajenga kibanda ambacho tunaishi na make wangu had sasa.



Mara nikaona mabadiliko ya ajabu kutoka kwa mke wangu, ile adabu na upendo nikaona kama vinafifia siku baada ya siku, lakini sikujali, kwasababu ya shughuli zangu. Ila, nikahisi kuna kitu, mbona safari za matembezi zimekuwa nyingi kulikoni, mara naenda kumuona shangazi mara mjomba nk. Lakini hata hivyo sikujali sana.


`Mwezi uliopita, … ' alipofika hapa aligeuza kichwa upande mwingine, nakahisi kuna msiba au vipi. Lakini nikahisi ni kitu fulani cha ajabu ambacho kimemkumba rafiki yangu.
'Mwezi uliopita siku kama ya leo nilirejea nyumbani mapema, sio kawaida yangu, huwa nashinda kwenye biashara zangu hadi usiku, na kama nitaamua kurejea nyumbani huwa namuarifu mke wangu mapema ili kama katoka aniachie ufungua mahali fulani.



Siku hii mbaya nilirejea ghafla, kwani nilihitaji pesa nikagomboe mzigo wangu wa pesa nzuri tu. Nilifika nyumbani, na kwa vile ni kwangu nilipitiliza ndani hadi chumbani , la haula, sikuamini macho yangu. Najuta kwanini nilirejea, nikaiona hiyo hali. Ogopa likukute lililonikuta.


Rafiki yangu mpendwa, ambaye tumeshibana, ambaye ndiye aliyenidhamini kwenye kesi yangu na ambaye ndiye aliyenisaidia mtaji wa biashara alikuwa …..sikuamini, `live' anafanya ufusuka na mke wangu…



Nilishikwa na butwaa, nikawa kama mtu aliyemwagiwa maji, nguvu iliniisha, na …' alipofika hapo niliona machozi yakimtoka.

Sijui kanini nilishindwa kufanya lolote, niliwaangalia weee, na wenyewe wakawa wameduwaa, wakisubiri nifanye la kufanya, lakini cha ajabu, niligeuka nakurejea kwenye biashara zangu, hadi jioni. Jioni nilifanya kitu cha ajabu ambacho sijawahi kukifanya, nilikunya kupita kiasi. Niliporejea nililala kama gogo, naikawa ndio tabia yangu hadi leo.



Unajua mpaka leo sijampiga mke wangu na wala sijasema chochote na huyo rafiki yangu, ila ndio wananiogopa kama nyoka. Rafiki yangu ananikwepa na kila akiniona anashituka kama kaona kitu gani sijui, mpaka watu wameshaanza kuhisi kitu.


Mke wangu ameisha/konda kwa mawazo, sijamsema, sijamfanya lolote na ninajifanya kama vile hakuna kitu kilichotokea.


Sasa rafiki yangu, sio kwamba nimepanga iwe hivyo, sio kwamba sikutaka kuchukua hatua yoyote, lakini nichukue hatua gani? nimuache?au nimfanyeje? ukumbuke kwao ni kama walimtelekeza, baada ya kung'ang'ania kuolewa na mimi.

Nimeshindwa la kufanya na siku zinaenda, na hata hamu ya kufanya mapenzi naye sina kabisa…nina mwezi sijui ladha ya mapenzi. SIJUI NIFANYEJE…


Dada Dinah, hata mimi nilishikwa na kigugumizi na sikumshauri chochote kwani mke wangu alifika na mazungumzo yaliishia hapo. Nikaona niliwasilishe hili swala kwako ili kama unaushauri, au kama wanakijiwe chako wanaweza wakashauri, ili nikikutana naye niweze kumpa hayo maoni.


Hayo ni mapenzi ya kusalitiana, je msamaha unaweza ukasaidia? Kifanyike kitu gani ili hali irejee, je upendo utaendelea kuwepo
emu-three"

Comments

Anonymous said…
Dada Dinah, sijawahi kuchangia mada humu hata siku moja ingawaje ni mpitiaji mzuri wa kona hii kuona kinachojiri.
Huyu jamaa ni mwanaume wa shoka na hutokea kwa mwanaume 1 katika wanaume 1000 wanaoweza kuchukua maamuzi kama aliyoweza kuchukua huyu jamaa, ngumu, na ni vigumu kuamini na kukubali hatua aliyochukua huyu jamaa.
Mimi nnaeandika hapa ni mwanaume lakini sina hakika nini kingetokea kama ningemkuta mke wangu anafanya kama alivyofanya mke wa huyo muungwana chumbani kwake na kitandani kwake.
Duh! nilikua nasoma huku mwili unanisisimka, huyu mshikaji kiboko na namkubali kwa maamuzi aliyochukua, ushauri wangu mkuu uamuzi wako uwe huo huo usipunguze chumvi wala usiongeze sukari kuwa hivyo hivyo, ila sasa, result yake usije kushangaa siku utaporudi kwenye mitkas kumkuta wife kakauka chumbani kwa pressure au kujinyonga.
Maamuzi uliyochukua wakati mwingine hiyo ndio huwa matokeo yake.
Nakupa respect mkuu kwa sababu ni wanaume wachache wanaoweza kuamua ulichoamua wewe.
Duh!
Anonymous said…
Dada D mambo?mmmh hiyo kesi ni ngumu sana.Ningekuwa mimi ningefanya kama alivyofanya huyo jamaa nisingefanya chochote sana sana ningewambia kuna kitu nimekuja kuchukua samahani kwa kuwaingilia.Nisingelewa sababu sio suluhisho.Nisingemuuliza wala nini kama alivyofanya ili ajiadhibu mwenyewe mpaka aniombe msamaha ambapo hapo sasa angeyakoga ya kwangu.Inauma sana simlaumu huyo jamaa kwa lolote lile.
Anonymous said…
Huyo ni malaya na hivyo hawezi kuacha. Mimi ningeachana nae. Mke wangu akitenda kuso hilo (wakati minaheshimu ndoa yangu kama mboni ya jicho langu), maamuzi yangu ni kumuacha tu. Hakutakuwa na simili hata kidogo. Hakuna cha shehe, padri, wazazi, watu wa busara wala nini. Aende zake akaendeleze umalaya wake mbele kwa mbele.
Anonymous said…
Awali ya yote, nimpe pole sana kwa hayo yalimtokea rafiki yako.Pili pole sana kwako mwenyewe kwa mshituko ulioupata kutoka kwa rafiki yako hata ukashindwa kumpa mssada uliohitajika.Na umefanya vizuri kulipeleka jambo hilo kwa dada Dina ili lipate maoni ya wengi juu ya kisa hicho cha kusikitisha.

Ndugu mpendwa, kwanza kabisa niseme kwamba amefanya vizuri sana kutochukua hatua yeyote ya kumpiga mkewe au huyo rafiki yake.Si jambo rahisi kwa wengi katika hali hiyo kutochukua hatu yoyote.Huyu bwana anafaa kuwa mcha Mungu kweli maana ameitwala hasira ambayo haitawaliki kirahisi.
natoa ushauri wangu kuwa amwambie mkewe kuwa pamoja na yote yaliyotokea amemsamehe na aonyeshe upendo ambao yamkini hajawahi kuuonyesha kwa mkewe hapo awali.

Jambo lingine ajue kuwa ndoa yao ilipatikana kwa shida sana,hivyo kuushinda mpango wa kishetani uliokuwepo wa tofauti za familia zao,ni muhimu huyu ndugu agharimie maisha yao ya ndoa.Gharama hizo ni kama hiyo iliyotokea ambayo ameishinda kwa kutawala haeira na kuendelea kuvumilia.NAMPONGEZA SANA!!
Nina imani kubwa kwamba,mpaka katika hatua hiyo huyo mkewe ameishajifunza jambo,hivyo nina imani kuwa atajirekebisha kabisa,lakini lazima ajue yalioko moyoni mwa mumewe baada ya kumfumania ni nini,yaani amwambie kabisa kuwa alitenda kosa kubwa ambalo lilimsikitisha na kwamba amemsamehe na anampenda.

kama ana wasiwasi kuwa labda ameambukizwa mijigonjwa, ajaribu kumshawishi mkewe ili wakapime, maana amesema ni mwezi hajamwingia kimwili. Asije akakimbilia nje naye akasababisha kituko kingine.

Ujue kuwa kusamehe ndiyo jambo pekee tu linaloweza kumaliza kisa cha namna hiyo.Asamehe na asahau.

Pia namshauri huyo rafikiyo, akutane na huyo rafiki yake aliyekuwa anangonoka na mkewe ili asawazishe naye mambo.Amwambie tu wazi kuwa yeye bado ni rafiki yake na anamsamehe kabisa kwa yale yote aliyomtendea.Amwambie kila mtu aweza kufanya kosa,lakini kurudia kosa ni kosa kubwa mno.Kwa kuwa wamekuwa marafiki muda mrefu katika shida na kusaidiana,mimi naona amsamehe tu na wanendelee kuheshimiana.hakuna njia nyingine ni hiyo tu itampa amani daima.Unajua inawezekana mkewe ndiye aliyekwenda kumchikonyoa huyo jamaa.Sisis wanaume tuna kaudhaifu fulani ukioona ngono inakusogelea kwa karibu hatupati nafasi kubwa kuchekecha mambo hasa kwa wale wanaofahamiana jambo hilo linapojitokeza wanakuwa wepesi zaidi kutegeka katika mtego.

Nakutakia kila la heri katika kuendelea kumtia moyo huyo rafiki yako ili asije kupata madhara kwa mawazo mengi.
mchangiaji na mdau wa blog hii nipo USA.asante dada Dinah.
Anonymous said…
Pole sana Kaka yangu,Aliyesema ubinadamu kazi hakukosea kabisa.baada ya kusoma mkasa wako kweli nimeumia sana.napenda kutoa ushauri wangu kidogo juu ya hilo ingawaje mapenzi huwa haya ushauri maana moyo wako ndio ujuao unampenda vipi.Ni ngumu sana kutoa maamuzi kwa papala hapo ,ukitazama kuwa familia ilimtenga kwa ajili yako,ma wewe ushatupwa mpaka jela kwa ajiliyake,mimi naomba uache kunywa pombe kwanza maana kunywa sio suluhisho,uwende kanisani ukatubu na umrudie Mungu wako,Mungu ndiye alikupa mke huyo yeye atajua airekebishe vipi ndoa yako ,na kama hayakuwa mapenzi yake Mungu anajua atakupa nini au atakupa hekima ufanye nini.Pia ukumbuke wapo binadamu wameubwa kuudhi na kukera wenzao,mkeo alilubunika tu,kaa pia utazama upande wako labda ulikuwa humpi nafasi ya kuwa na wewe sana uko Busy kwenye biashara ukamsahau? Inawezekana ulikuwa humtoshelezi kitandani kwa ajili ya uchovu wako?
Lakini yuko Mungu ambaye atakusaidia.Kuwa hekima katika hiloo.Nakuombea sana Mungu akupe Faraja
Anonymous said…
Kwa upande wa rafiki yako,Msamehe ili umpalie makaa ya moto juu ya kichwa chake,usimuulize muache samehe na kusahau ndipo utakapo shuhudia atalipia maumivu aliyopata kwa gharama kubwa sana.
Wewe punguza ulevi,Tumia busara kumsamehe mkeo,mmepita katika mambo makubwa sana,maumivu aliyopata ya kufumaniwa si kidogo,maana usipo samehe unaweza kusababisha hata kifo kwa mwenzi wako.
Anonymous said…
Hi all!
Kwa kweli hiyo iliwahi kunikuta hata mimi niliwahi kurudi nyumbani na kumkuta mume wangu "akipiga push-ups" na mwanamke mwingine. Ni ngumu mno! Maumivu ni makali sana! Sikuwasemesha kitu wala sijawahi kumsemesha kitu huyo bwana.
Kwangu mimi mapenzi yaliisha palepale!!!
Ninachoweza kusema, msamaha unaweza kusaidia, lkn sidhani kama mapenzi na upendo utakuwa kama mwanzo.
Hata hivyo,according to their story which is very touching, they can sit down and talk things out.
Let them try for the best!
Anonymous said…
Hi all!
Kwa kweli hiyo iliwahi kunikuta hata mimi niliwahi kurudi nyumbani na kumkuta mume wangu "akipiga push-ups" na mwanamke mwingine. Ni ngumu mno! Maumivu ni makali sana! Sikuwasemesha kitu wala sijawahi kumsemesha kitu huyo bwana.
Kwangu mimi mapenzi yaliisha palepale!!!
Ninachoweza kusema, msamaha unaweza kusaidia, lkn sidhani kama mapenzi na upendo utakuwa kama mwanzo.
Hata hivyo,according to their story which is very touching, they can sit down and talk things out.
Let them try for the best!
Anonymous said…
Inasikitisha sana mtu unaweza kuwa mwendawazimu hivihivi. Jamaa anamapenzi ya kweli kwa mke wake asiemwaminifu na wakati huohuo anamuonea huruma. Lakini watatesana mpaka lini? ni bora kumtaliki na kuanza moja huyo mke sio rizki yake.
Anonymous said…
Kwa sababu hawaja kuomba msamaha sio vizuri,basi
wewe endelea kuomba Mungu atakusaidia utapata
mke mwingine mzuri atakaye kuheshimu zaidi.
Maoni yangu mpe huyo mkeo talaka.
Hapo Bongo kuna wanawake wengi wazuri na wenye
heshima nzuri. Mungu akujalie !!!
Anonymous said…
WEWE BWANA MKUBWA KWANZA POLE SANA NA SKENDO HIYO KWA KWELI INAUMA KWELI.LAKINI NAOMBA NIKASHAURI KITU JAPOKUWA UNAKUUMA SANA LAKINI JARIBU KUSAMEHE MARA MOJA RUDISHA MAPENZI KWA MKEO TENA HAPO UTASHANGAA ATAKUPENDA KUFA,KUMBUKA YAKUWA HAPA DUNIANI TUNAPITA TU NA KUTOMBEWA SI MWISHO WA MAISHA EMBU FIKIRIA INGEKUWA NI WEWE NDIO UMEFUMANIWA NA MKEO NADHANI UNGEFURAHI NAKUONA KUWA KWELI NIMEKOSA NA KAMA ILIVYO TABIA ZETU SISI WNAUME HUWA TUNAONA AKIKOSA MWNAMKE NDIO KOSA HASWAAA HASTAHILI KUSAMEHEWA LAKINI MBONA SISI TUNATOMBA NJE MARA NGAPI ? NAKUMBUKA KUWA NI KWA SABABU TU ULIMFUMANIA NDIO MAANA IMEKUWA HIVYO LAKINI SIDHANI KAMA USINGEMFUMANIA NADHANI MAISHA YANGEKUWA YANAENDELEA TU NA KUTOMBWA ANGEENDELEA KUTOMBWA AU SIO NDUGU YANGU? SASA CHA MSINGI MSAMEHE MKEO TENA MRUDISHIE IMANI YAKE YAKUWA WEWE NI MUME WAKE NA KAMWE HUTOKUBALI KUMKOSA YEYE EMBU FIKIRIA NDUGU YANGU USIPOMSEMESHA HADI LEO AKIFA ITAKUSAIDIA NINI NDUGU YANGU? ni kweli inakuuma na NINI LAKINI TUJARIBU KUSAMEHE TU NA TURUDISHE MAPENZI UPYA SAWA BROTHER HAYO NI YANGU MACHACHE TU
PRINCELEE
Anonymous said…
kWANZA KABISA NAPENDA TOA PONGEZI ZANGU KWA DADA dINNA KWA KULETA MADA NZURI ZINAZOTOA FUNDISHO KATIKA JAMII.

PILI NAPENDA KUMPA POLE SANA KAKA KWA YALIYO MPATA NI MAMBO YA DUNIA NA YANAWEZA KUMTOKEA MTU YEYOTE

NASEMA HILI SABABU YAMENIKUTA NA MBAYA ZAIDI WAMEKUWA WAKIENDELEZA UHUSIANO WAO JAPO KWA SIRI.

BINADAMU TUNA MAJARIBU MENGI SANA HAPA DUNIANI.

KWA USHAURI KAKA AMUA NINI NIA YAKO KATIKA MAISHA KAMA UNAUWEZO WA KUSAMEHE NA KUSAHAU NA KUMPENDA MKE WAKO KWA DHATI BASI FANYA HIVYO SAMEHE NA ANZA UPYA ILA NI VIZURI UKAE NA MKEO MJADILI HILI SUALA MAANA UNAWEZA SAMEHE KUMBE MWENZI WAKO BADO ANA MAPENZI NA YULE RAFIKI YAKO. JAMANI HII IPO NA NASEMA HIVI SABABU IMESHANITOKEA.

KAKA KAMA UNAONA UNAWEZA KUSAMEHE ILA PENZI KWA MKEO LIMEKUFA BASI NAOMBA MUACHANE( INGAWA WATU WENGI WATAPINGA) KWA MAANA MOJA TU HAKUNA MATESO MAKALI DUNIANI KAMA YA KUISHI NA MTU USIYEMPENDA SABABU UTAJIKUTA UNATENDA DHAMBI TU NA KUJIONGEZEA HESABU ZAKO KWA MWENYEZI MUNGU NI BORA UTENDE ZAMBI MOJA YA KUACHANA KULIKO KUJA KUTENDA NYINGI ZAIDI NAANA KUNA UWEZEKANO MKUBWA SANA WA WEWE KUMLIPIZIA MKEO KWA NAONA YEYOTE ILE MBAYA ZAIDI AMBAPO NI DHAMBI NA PIA KUTOONYESHA UPENDO KWAKE UTAJIKUTA UMRESPECT NA UNAPUUZIA JAMBO LOLOTE TOKA KWAKE NA MENGINE MENGI ZAIDI YA HAYA MWISHO KUIKUTA HAMPATI MAENDELEO KATIKA FAMILIA YENU SABABU HAMSHAURIANI MAANA HAKUNA MAPENZI TENA..

NI HAYO YANGU MACHACHE POLE SANA ILA TUPO WENGI YALIYOTUKUTA NA MPAKA SASA HAPA NILIPO SINA RAHA YA MAISHA INGAWA YAMENIKUTA MIAKA 2 ILIYOPITA KISU CHAKE BADO NAKIFEEL MPAKA SASA. ASIKUAMBIE MTU JAMANI MPAKA YAKUKUTE NDIO UTAJUA.
Anonymous said…
Hata cjui nianzaje?inahuzunisha,lakini magumu,shida zote,zimeumbiwa sie binadaamu,kaka,wasamehe,ingwa ni ngumu,jitahidi na mola wetu,atakua pamoja nawe,kidini yoyte ile hiyo ni automatiki talaka haina mjadala,lakini kama keshatengwa na ndugu hio ni issue nyingine,lakini mie nashauri msamehe,hata kama utamuacha msamehe pia,maana end up yake yaweza kua mbaya,kuhusu pombe kipindi hiki kwako sio nzuri,inakupa ujasiri ambao huna,ikiwezekana acha kabisaaa!
MARTHA said…
JAMANI MIMI NAHISI MACHOZI YANANITOKA SABABU NAJUA MSHIKAJI INGAWA KAFANYA UAMUZI HUO LKN BADO ANA MAUMIVU MAKALI USHAURI MWANGU KAKA YANGU MWITE KAA NAE CHINI UONGEE NAE AKIKUTAKA RADHI MSAMEHE. KUMBUKA HUYO NI BINADAMU ALIJIKWAA ATAJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA,INGAWA HUNA UHAKIKAKAMA WANATEENDELEA AMA LAAH! MAANA NI KAZI NGUMU SANA KUVUNJA PENZI.
Anonymous said…
pole sana kaka yangu ni mungu amekupa ujasili na swala lililokutokea ni majaribu tu, nakupongeza kwa kuhimili jambo zito kama hilo ambalo linaupa moyo maumivu makali.
ushauri wangu ni hivi,mkeo ameshajifunza jambo kama ni mtu mwerevu sasa basi mwombe utoke naye kwenda sehemu yoyote even for two days mkae mbali na home umwelezee jambo alilofanya umelichukuliaje na kama kunakitu anakosa kutoka kwako pia awe muwazi kwa hilo after that umsamehe na umweleze kuwa umemsamehe mwendelee na maisha kama mwanzo kwani maisha ya sasa ni magumu na nivigumu kupata mwenyetabia nzuri na isitoshe kila binadamau anamapungufu yake tujaribu kusameheana na kuoneana huruma, pole kaka mungu yupo nawe.
Anonymous said…
Shure amepitia machungu sana kwa upande wangu naona huyo mkewe bado ana matatizo maana alichotakiwa kufanya ni kukaa n mumewe na kumwomba msamaha hata huyo rafiki yake angekuwa na akili angemwomba msamaha naamini angewaseme na upendo ungerudi kama mwanzo bila hivyo ataendelea kuteseka. ila sasa mtihani kwa mkewe ajirudi na kuomba msamaha
Anonymous said…
Hi all,
Ukweli inauma sana kusikia habari ya kusalitiana, nimesoma maoni ya wengi hapo juu na kuona juu ya maana ya Ukristo kwa kuwa wote ni wapendwa katika kristo cha kufanya ni kukaa chini kuongea na kumshirikisha Mungu maana katika kuamini Mungu ndio suluhisho la yote, huyu kaka amesema amefikia mahali anakunywa sana pombe wala sio suluhusho lakini ninaweza kumuelewa kuwa ni stress ni ngumu sana mie niliwahi kuwa kwenye hali hiyo lakini nilimwomba sana Mungu na baadaye nilipata suluhisho hivyo nakushauri kaka yangu sali sana na Mungu wetu atakupata jibu within seven day!! All the best.
Anonymous said…
Mimi nakubaliana na ANONYMOUS wa saa 3:37:00 kwanza nampa pole huyu KAKA na kwa ujasiri alionao, kwa nyongeza na jinsi nilivyosoma hii habari nzima mimi nimefikiria kwamba; wakati uko jela huyu mkeo alikuwa na uhusiano na huyo unayemuita best friend wako ambae alikuwekea dhamana ya wewe kutoka kifungoni na ndio maana ilikuwa ni ngumu kuachana hata wakati wewe umetoka kifungoni na ndio maana walikuwa wanatumia muda wa mchana kungonoka na ndio maana uliona mabadiliko ya mkeo sababu tayari alikuwa na mtu anayemgonosha zaidi yako na itakuwa ngumu sana hata ukimsamehe na kuendelea nae bado mapenzi hayatarudi. Ushauri aliokupa ANONYMOUS wa saa 3:37:00 ndio haswaaaaaa fanya maamuzi kuliko kuendelea kuishi na maumivu unayoyapata, wazazi wake hawakutaka muoane ila kutokana na mapenzi mliyokuwa nayo wakati huo hamkutana hali ya kuachana iwepo na kama walimtenga kwa ajili yako, huu ndio wakati wa kufanya maamuzi na hao wazazi/ndugu zake watamrudisha kundini mwao.

Ciao
Mh hii ngumu kumeza aisee nadhan iyo style uliyoichagua ndiyo yenyewe we endelea tu na maisha ye akitaka aombe msamaha na akielndelea kujikausha itakuwa ana kiburi....hiyo ni adhamu tosha japokuwa ni ngumu kuipractice
Anonymous said…
Mimi nataka kuuliza swali hata kwa wachangiaji na sana sana huyu kaka. Kama kweli mkikaa kitako na mkeo ukamsamehe, utakuwa na uhakika kweli kuwa ameacha(na siyo na rafiki yako tu bali na mwanaume yeyote), japokuwa(mke)anaonekana mwenye uzuni sana nakadhalika, lakini mimi naona - kusameheana ni sawa LAKINI KWELI HUYU KAKA(MUME)ataweza kumwamini tena mkewe, na hapo ukifikiria labda siku mume apate safari, na mama yupo nyumbani, mawazo yake (huyu kaka) yatakuwa ...'jamani sijui mke wangu ananisaliti tena??" kweli kusamehe na kuendelea na maisha ya kawaida kama mke na mume baada ya kusalitiwa na haswa akachagua pakufanyia uchafu huo ni nyumbani kwenu, in your matrimonial bed - AISE!!! , kweli msamaha huu unabidi usali sana ili Mwenyezi Mungu akupe nguvu ya KUSAMEHE KUTOKA KINA CHA ROHO YAKO NA KUSAHAU - Lakini kama sivyo utakuwa unabeba mzigo wa mawazo siku kucha.