Saturday, 13 September 2008

Tunaposingiziwa kila kitu.....

Ni matumaini yangu Mfungo unakwenda vema kabisa na senti ya "kurekebisha" Futari ipo kwani sote tunajua kuwa kipindi hiki ni ghali miongoni mwetu, mbaya zaida unaishi nyumba ya kupanga ambapo nijuavo mimi (kule bara) ni sharti kufuturu pamoja sio familia bali majirani pia, na kila aliyefunga hupenda kuchangia kile alichopika na wenzake, lakini M'Mungu anaangalia kilicho moyoni na matendo yako hivyo hata kama ukifuturu supu ya dagaa poua tu......tuachane na hayo.


Unajua kwenye mahusiano yetu ya kimapenzi iwe ni ndoa au wale "bado wapo wapo" lakini wanawapenzi huwa hakukosi mikwaruzano na mtu akikuambia kuwa kwenye uhusiano wao hawajawahi kutofautia na kusababisha mabishano, mzozo ambao unaweza kusababisha kununiana (mara nyingi sisi wanawake)basi ujue mmoja wao ni muoga kuachwa yaani anakuwa mtumwa wa uhusiano a.k.a "ndio bwana" au uhusiano wao bado mchanga.


Kuzozana kwenye uhusiano ni afya kwani inadhihirisha kuwa ninyi wapenzi na mnapendana sana tu lakini hamko sawa kiakili, kimwili,kimtazamo, kifikra, kidamu(ndugu)na bila kusahau kijinsia. Natambua kuwa kuna wakati mnaelewana vema kabisa na kujihisi kama vile mungu alikushushia yule uliyemtaka, mwanamke habishi wala kuuliza maswali au mwanaume hakutumikishi wala kukutawala (si mwajua wanaume wa kibongo kwa ku-control??? hehehehe).


Ninachojaribu kusema hapa ni hivi, wanaume ni walalamishi pia kwenye mahusiano mengi ya kimapenzi lakini sisi wanawake ama huwa hatuoni au hatujali kwa kufikiria kuwa mwanaume kila wakati yeye yuko sahihi(well most of the time huwa wanakuwa sahihi kuliko sisi wanawake lakini hiyo haifanyi kila wasemalo/kufanya ni sahihi).


Kinachosikitisha au kunisikitisha ni kuwa sisi wanawake tumekuwa tukisingiziwa na hatimae kujulikana kuwa ni walalamishi au tunapenda kulalama kila wakati. Lakini ukweli ni kuwa wanaume ndio wanaongoza kama sio wako mstari wa mbele kulalama kwenye mahusiano kuliko sisi wanawake, kwa vile mfumo dume bado uko miongoni mwetu basi huwa tunadhani kuwa mwanaume anahaki ya kulalama au kujaribu kukumiliki kimtindo.


Mume/mpenzi akichelewa kurudi nyumbani au asipokujulisha/julia hali katikati ya siku (kutokana na maendeleo ya Tekinolojia)ni wajibu wake kujieleza kwanini kachelewa na asipofanya hivyo basi wewe kama mkewe/mwenza wake una haki zote za kuuliza aliko kuwa na alikuwa akifanya nini na yeye ni wajibu wake kutoa majibu mpaka utakaporidhika.......lakini tunachokosea hapo ni namna ya kuuliza, wengi wetu huwa tunauliza kwa hasira kwa vile huwa tunafikiria mabaya zaidi(yuko na nani) kuliko mapenzi yetu na ile hali ya kujali juu ya mpenzi.


Hali kadhalika wewe mwanamke ni wajibu wako kum-alifu mume/mpenzi wako mahali uliko au hata mipango yako ya siku nzima na kuwa "intouch" na ikitokea umechelewa basi unapaswa kutoa maelezo ya kutosha na kuridhisha......lakini kwa bahati mbaya hili likitokea mwanaume huwa mkali na kutoa shutuma ambazo hujawahi hata kuzifikiria. Kwanini anafanya hivyo basi? kwasababu bado anaile "nakumiliki" anakuwa "controling".....unakuwa binti mbele yake na sio mpenzi tena.

Kuuliza kwake mwanume kwa ukali na konyesha umiliki dhidi yako ni kwasababu (kama nilivyosema hapo awali) anakuwa na mawazo mabaya/machafu zaidi kuliko kujali na mapenzi juu yako.

Katika hali halisi sote kwenye uhusiano (wake kwa waume) tunapaswa kujifunza namna ya kuzungumza na wapenzi wetu, badala ya kuuliza maswali katika mtindo wa "talking to you" iwe "talking with you", onyesha uaminifu wako kwa kumuamini mwenza wako, hata kama meudhika au kwazika na kuchelewa kwake basi jitahidi kuuliza maswali kwa mapenzi, kwa upendo katika hali ya kujali na mambo yatakuwa bomba.

Mida mida basi mpendwa.....

6 comments:

Anonymous said...

Hi Dina hujambo?
Asante kwa blog yako tunayoihitaji sana watanzani, Mimi ni mmama mkubwa tuu, sasa nina yangu nataka kuwakilisha ila sijui tunatumaje hizo post, leo nimeteza mda mwingi kutafuta ni jinsigani naweza tuma. hebu nieleweshe nduguyangu.kwani nina yanayonikuna nahitaji kushare nanyi.
Asante na mfungo mwema

Dinah said...

Asante sana kwa ushirikiano wako, unaweza kutuma yote yalioujaza Moyo wako kama ulivyotuma hii au unaweza kunitumia Email ambayo inapatikana kwenye Profile yangu.

Mara baada ya Comment kunifikia au Email nitaihariri alafu nitaiweka hapa kama topic.

Kila la kheri.

Mswahilina said...

Dada Dinahicious
Naomba kuuliza
Kulikoni blog ya Dada Chiku?
mbona tangu septemba mwaka jana haonekani kabisa?
Asante.

Anonymous said...

Hii mada naona isinipite bila kutoa hoja, ingawaje wenzangu wameipiga chenga. Hapa wanaume wanatakiwa wakijitetee kwanini wanapenda kuwasingizia wanawake kila kukitokea makosa, au inaweza isiwe makosa, lakini kila kukiwa na walakini tunatoa lawama(visingizio vingi).
Dada Dinah, labda mimi niulize swali moja, mfano `kila ukifanya kosa mumeo hakuulizi, kila ukichelewa harusini, au kazini au kokote ulikoenda, mumeo hakuulizi au hasemi jambo, wewe huoni kwamba itakukwaza kwa namna fulani.
Nasema hivi kuonyesha kuwa sisi wanaume tuna `wivu' na wivu ni dalili mojawapo ya `kupenda'. Wewe unakitu chako unakipenda, sidhani utaona furaha kiharibike. Kwahiyo tunapouliza, tunapolalamika, au tunapowatupia lawama ni ile element ya `wivu' ambayo inaonyesha kuwa tunawapenda na tunawajali, lakini, wengine wanatumia `amri' badala ya `busara' na hapo ndipo tunaposigishana.
Mfano `mke wangu vipi kulikoni, mbona umenitia kitumbo joto, kurudi saa hizi...
Lakini unakutana na rijamaa ambalo halina simile utasikia;
`Wewe urikuwa wapi unarudi saa hizi, unajiona ridume sio...'
Mifano hii inaonyesha utofauti wa hekima ndani ya ndoa, lakini nia yao kubwa ni kulinda `chao' ili kisiharibike.
Naona niishie hapo, nisije nikaenda mbali zaidi.
emu-three

Dinah said...

Mswalihina nasikitika kusema kuwa sina habari yeyote kuhusu Blog ya Da' Chiku.

Anonymous said...

dada dina hongera sana na mambo unayotupatia