Mume wangu kaoa M'ke mwingine,kumtaliki ni sahihi?-Ushauri.

"Hi Dinah habari za leo?
Nashukuru kwa maelekezo yako , ni mimi nilieuliza jinsi ja kupost mada. Jina langu kapuni.

Dinah nimekua mpenzi na msomaji wa blog yako, kwa kweli inamambo mengi kwa upande wangu nahisi inatoa elimu, na mara nyengine kuburudisha. Hua nasoma blog nyingi ila ni chache zimekua zikinivutia mada zake. Udumu mdogo wangu katika hili.

Mimi nijiite ni mama mzee tu nina umri wa miaka 40,nilianza mahusiano ya kimapenzi nikiwa na umri wa miaka 22,nikiwa katika mazingira ya kishule nikimaanisha chuo kikuu nje ya nchi, kabla ya hapo sikua nataka kusikia hayo mambo kwa kutegemea tutakae anza ngono ndio awe Mume wangu.

Nili bahatika kukutana na huyo kijana kwa bahati sijui niite mbaya , tulikua ni dini tofauti (mie muislamu yeye mkristo)kabla ya kuanza ngono, nilimueleza kuwa mie niko serious, sasa ikifikia hatua tukaona ni bora tuoane utakua tayari kubadili dini alikubali.

Hapo sikusita tukaendeleza kungonoka kwa miaka kadhaa tukiwa masomoni. Baadae tulirudi TZ , tukabahatika kupata mtoto, binti nzuri kabisa na tulifunga ndoa ya kiisilamu, kwa maana kua aligeresha wazee ili tupate ridhaa yao tuwe pamoja.

Baada ya muda mfupi tu wa hiyo ndoa , alinitaka nami niende kanisani tukafunge tena, nimi nilimshauri kama ni hivyo tuende bomani itakua ndio neutral, lakini aligoma kwa wakati huo, tulikua tunaishi kwenye nyumba ambayo ilikua chini ya mamlaka yangu, alihama na kuniambia huko aendako, nitaenda pale nitakapokubali kufunga ndoa ya kanisani.

Niliacha aende kwa wakati huo. Siku moja nilienda kumtembelea huko alikohamia, wakati nagonga nikasikia redio inalia mara redio ikawa kimya, baadae nilipofungua nikakuta mwanamke ametoka humo ndani. Mie niliamua kuondoka nikarudi kwangu.

Baadae jioni mume wangu alikuja kwangu na nikamuomba msamaha kwa kua sikumwambia kua naenda na kwa kuwa ameamua kuwa na yule labda nae atakua ameondoka, baadae yeye aliomba msamaha na kuniambia anataka kuwa nami ili tumlee mtoto.

Na aliniahidi anamuacha huyo msichana, na akaniruhusu kuhamia kwake, mie bila kusita nilihamia. Baada ya miezi mitatu akaenda shule ya miaka minne nje ya mkoa wa DSM. Alikua anakuja kila mwisho wa mwezi lakini kadiri miaka ilikua ikienda nikawa nahisi upendo wake kwangu ulikua unapungua, kwa maana kua alikua akija ingawa ni siku mbili lakini hashindi nyumbani kwa kutumia visingizio niko na huyu na yule (marafiki).

Hatimae alimaliza akarudi nyumbani,nikaanza kubaini simu za usiku hata saa tano,sita anapigiwa , MSG, baada ya uchunguzi niligungua ni yule mwanamke wa miaka ile na kwa MSg tayari wakawa wanaitana mke/mme. Kwa wakati huo yule mwamamke hakua nchini.

Nilipomuuliza mume wangu hii ni heshima gani ya ndoa, yeye alisema eti yule mwanamke hayupo nchini ninaogopa nini, na baadae nikabaini kadi ya benki ya yule mwanamke anayo huyu baba (mume wangu). nikamwambia hongera kwa kuaminiwa.

Kwa kweli nyumba nilizidi kuiona mbaya, nikimlaumu kwa hilo, mara nyengine aliniambia nikamshitaki kwa wakubwa. Siku moja nilichukua hatua ya kushitaki kwa kaka yake, lakini kaka yake alichonijibu sikuamini,ila nikahisi,hawanifurahii kwenye ukoo wao kwa sababu ya dini.

Shemeji aliniambia eti mimi nitafute watu wengine, ukweli sikutafuta mtu na hapo nilimwambia huyu baba (mume wangu) kama mie ninatafuta nyumba nikipata nitahama kwake kwani inaonekana ameshanichoka nahata heshima hana na ametegesha ili nijifukuze mwenyewe ili yeye asipate lawama.

Nilikua namuambia kua wanaume waliowengi wenye heshima hua wanamahusiano nje lakini wanaficha kwa wake zao, alinyamaza. Baadae akanitangazia kuanzia mwezi fulani nitaanza kulala mitara, na kweli ulipofika huo mwezi akaanza kulala huko siku nyengine.

Nilikata tamaa na hiyo ndoa Niliamua kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja , kutafuta shule, na kutafuta nyumba, kwa bahati mungu alijibu sala zangu zote, nilibahatika kupata shule nje ya nchi na nikapata nyumba.

Nilipomuambia nimepata nyumba , nitaondoka kwako hakuleta hata ile lugha ya kusema usiondoke mke wangu, nilihama mwaka juzi mwishoni na baada ya muda mfupi nikaenda shule nje ya nchi ambapo niko hadi sasa. Mwaka jana wakati nikiwa likizo nimekuta ndio anafunga ndoa ya kanisani, na hakuniambia kama ameamua kuoa ilihali tunandoa ya kiisilamu.

Nilichoamua dada ni kua nikiaenda likizo hii nimtake tuende mahakamani ili tuvunje hio ndoa na nibadilishe document, Naomba ushauri kwa hilo, niko right????

Pamoja na hayo, jambo jengine ni kua , mtoto nilienae ni mmoja, ningetamani nipate mwengine, umri ni 40kuna jibaba moja lilionesha interest ya kuzaa nami, ila hofu yangu ni mume wa mtu ana watoto wawili anasema ananipenda ila ndio hinyo, kusubiri hadi nipate asie na mke pia kwa umri wangu sio rahisi sana (inachukua muda) naogopa kuingia kwenye menopolse kabla sijajaribu tena kuzaa.

Naomba mnishauri mwenzenu, niamuaje hapo? ili nikija huo mwezi wa 12 niwe na maamuzi kama nijaribu na huyo mume wa mtu au nifanyeje?

Nawakilisha

Pole kwa maelezo mengi unajua hua ninatension ya maisha yangu ndio maana nikianza kuyaeleza hua naeka mdorongo huo, sikutegemea kua na ndoa ya aina hio

Kila la kheri".

Jawabu: Asante kwa ku-share sehemu ya maisha yako ya kimapenzi na ndoa mahai hapa. Shukurani za dhati kabisa kwa wote waliotoa michango juu ya hili.

Nisingependa kuegemea sana kwenye kitu amabacho kimepita lakini hata hivyo nitagusia kidogo tu kuwa kosa kubwa lililofanyika ni kufunga ndoa kwa "kuzuga" ndugu na jamaa wako kitu ambacho Mumeo pia alikitaka kwa kufunga ndoa ya "kuzuga" kanisani.

Unajua kila mtu huwa anazingatia vitu fulani muhimu ktk maisha yake ya kimapenzi na hatimae ndoa, na hujitahidi kwa kila wawezalo ili kuhakikisha vile vitu muhimu vinakuwepo kabla hawajaamua kuendelea mbele na masuala mengine kwenye uhusiano husika.

Kwako wewe na mume wako (kutokana na maelezo yako) pamoja na mambo mengine Dini na kuridhisha familia zenu vilikuwa ni vitu muhimu zaidi hivyo basi hilo lingezingatia yote yaliyotokea yasingetokea ( hatuwezi kubadilisha kilichokwisha fanyika)......


Uamuzi wako wa kumtaliki mumeo ni sahihi kabisa ila fanya hivyo kisheria ili kutopoteza haki zako kama mke. Jaribu kutembelea Mahaka yako ya Wilaya ya mahali ulipo na omba kuonana na Hakimu, mara nyingi inachukua wiki moja mpaka miezi 3 inategemea na uzito wa Kesi yenu.


Mahakama kupitia Hakimu ndio itatoa "samansi" ili mume wako aende mahakamani, usimfuate wewe kama wewe (nje ya sheria) kwani inaweza ikakusumbua na vilevile kufanya kesi kuwa ndefu, zingatia kuwa utakuwa nyumbani kwa likizo tu sio kwamba unaishi huko hivyo muda ni muhimu.


Hilo la wewe kutamani/taka kuzaa tena kabla hujafikia "kikomo cha hedhi" limetulia lakini usijifikirie wewe zaidi bali yule mtoto atakae zaliwa na yule ulienae hivi sasa. Fikiria maisha yao ya baadae na mahusiano yao na baba zao.


Hilo baba lenye kuonyesha "interest" kuzaa na wewe wakati tayari anamke na watoto halija kaa vema kwani atakuwa anacheza nje ya ndoa yake kitu ambacho wewe machungu yake unayajua, sasa kwa kujali hisia za mwanamke mwenzio na kuepuka huyo mwanamke mwenzio kutopata maumivu uliyopitia wewe (mume wako alipoibiwa na mwanamke mwingine na hatimae kufunga ndoa) jiepushe na huyo jamaa.


Miaka 40 sio uzee (uzee ni muonekano wa ngozi yako na unavyojiweka wewe sio namba), nina hakika kabisa kuna vijana wengi tu ambao hawajaoa au wale "Wajane" (wanaume wanaitwaje vile?...)na wako huru kabisa kuanzisha uhusiano mzuri na wewe na hatimae kujizalia mtoto au watoto zaidi.

Kila la kheri dada....

Comments

Anonymous said…
Kuna `mchango wangu' niliutoa kuhusu mada ya dini na mahusiano, katika kuchangia nilielezea kuwa mnapoingia katika mahusiano, msijiangalie wenyewe tu, mjue kuwa mtakuwa na familia ambayo nayo itategemea misingi mliyoiweka.
Tukirudi kwako mtaka ushauri, kwanza kabisa nikupe pole, kwani wahenga walisema siri ya mtungi aijuaye ni kata. Usiombe unapomuamini mtu kimapenzi akaja kukusaliti hasa anapofanya hivyo katika umri wa utu uzima. Miaka arubani ilitakiwa muwe katika mahusiano mengine kabisa siyo ya `kutalikiana’.
Katika hali ilivyo kwa vile kila mmoja wenu ameshikilia imani yake kama msingi mkuu wa mahusiano yenu na kila mmoja anataka mwenzake awe ndani ya dini anayoitaka yeye hapo hakukaliki. Na mapenzi yenu yajayo yangetegemea kabisa mapenzi yenu mliyoanza nayo. Na kama mngekuwa mumeshibana ilivyo, hakuna angeweza kuwaachanisha. Lakini kwa maeleze yako, mapenzi yenu ni ya kutegeana, sio ya `kushirikana.
Mwenzako yeye kashaamua kuoa,na dini ya mwenzako haihitaji `mitaala' kwahiyo kwa vvyovyote atakavyokueleza kuwa `anakupenda' itakuwa ni `danganya toto'. Hilo lipo dhahiri.
Uamuzi wa busara, ni mkae tena wakiwemo wazee (au watu wazima wenye hekima), ingawaje kwa upande wa mwezako sidhani kama wanakuhitaji tena (inavyoonyesha), kwani walichokitaka kwa mtoto wao wamekipata-mtoto wao kuoa ndani ya dini yake, na hilo ndilo wazazi wengi wanataka. Hii sio siri.
Nasema mkae na watu wazima ili mjue hatima ya ndoa tata yenu. Hiyo ni ndoa tata kwani mwenzako kama kesharudu kwenye dini yake, sidhani kama ndoa hiyo inatambulika tena kidini(mashehe watusaidie)! Ndoa ya Kiislamu inaweza ikavunjika kwa matendo yenu bila kujua, na bila hata ya kumhusisha shehe. Mtafute shehe akuelimishe kwa hilo.
Pili ili mjue msimamo wa mtoto wenu, hili ni muhimu, na sidhani baba mtu atamkataa mwanae, na sijui imani ya mtoto wenu ni ipi! Hili linahitaji hekima zaidi. Msiliache hivihivi mkampa mtoto wakati mgumu wa kuamua la mama au la baba. Lifanya hili mapema kabla hujampata mwenza mwingine.
Kwa upande wa pili wa kumtafuta mtu wa kuzaa naye. Ningekushauri usifanye kosa mara mbili. Wewe ulishaona uchungu wa `kuibiwa mumeo' sidhani uliona raha kufanyiwa hivyo. Kwahiyo na wewe usiibe vya wenzako. Kama umempata mume muislamu, yeye anaruhusiwa kuoa zaidi ya mke mmoja mwambie `mimi najua machungu ya kuibiwa' naomba tufunge ndoa halali.
Kwa umri wako huo kama ulikuwa unajiweka vizuri bado wamo na unaweza ukapata mtoto, ila ninalokushauri usizae ilimradi kuzaa, yaani `nje ya ndoa' hili athari zake sio kwako ila kwa watoto. Nazungumza hili kwa `ushahidi wa hali halisi'. Watoto wa namana hii kuna `kuathirika kia kili kwa namna fulani' ingawaje sisi wazazi tunajifanya hatuoni.
Ombi langu usijifikirie wewe mwenyewe tu katika maamuzi ya kuzaa, jaribu kwenda mbali na kumfikiria na huyo utakaye mzaa. Sidhani kama utafurahia na yeye apitie maisha uliyopitia, sidhani kama utafurahia, mtoto awe anakuja kukuimbia wimbo wa `baba yangu yupo wapi'. Haya kwetu tunayaona madogo lakini yanajenga shinikizo la moyo hasa katika umri wa juu.
Huo ndio ushauri wangu
emu-three
Anonymous said…
pole kwa yakiotokea pia kabisa unatakiwa kuwa na msimamo wa dini yako,kuzaa utazaa tu hakuna neno ila usurudue makosa kwa ndoa isio sahihi kwako na usifanye kwa kumkomoa mtu fata taratibu zote uwe na maisha ya heri na salma
Anonymous said…
Pole mdada kwa yote nafikiri kosa ni sahihi kabisa kumtaliki mumeo kwa kuoitia mahakamani ili uweze kuendelea na maisha yako. Kutaka kuzaa tena sio baya lakini huoni kuwa utakuwa ubinafsi zaidi yaani unajali zaidi mahitaji yako na sio nini kitatokea kwenye maisha ya mtoto na uhusiano wake na baba yake ambae ni mume wa mtu mwingine. Jaribu kutafuta wanaume ambao ni wajane au ambao hawajaoa alafu mkubaliane kuzaa tena kama uko nje ya Tanzania ndio rahisi kwani wako wengi wanachelewa kuoa kuliko walioko nyumbani.
Anonymous said…
Mimi naona mlifunga ndoa kabla mmoja wenu hajawa tayari.Mume wako hakuwa akijua anachokifanya na hakuwa na mapenzi ya kweli kwako na ndio maana akatafuta penzi kwingine, Maisha yana mambo jamani.
Anonymous said…
mm pole sana mwezanga yani ata mimi nilikuwa natatizo kama lako ndoa niliona chungu bahada ya mume wangu kupata nyumba ndogo nilicho fanya nilibeba watoto wangu na kutoka bahada ya mwezi1 ninasikia hameamia kwa mwanamke bahada ya mwezi mwingine nikasikia uyo dada ana mimba,mimba imefika miezi8 mtoto akafia tumboni sasa toka tuwachane ni 1na nimepatamwingine hila dini ya kiislam ndio ninapofikiria hapo hapo mimi na baba watoto wangu wala mawasiliano atuna wala kuwajulia waotot wake ali akuna hila ninapiga moyo konde na kuomba mungu atupe uzima na sasa mambo yangu sio mabaya kwani ninakwangu,na nipo njia panda x mume wangu akukutana na rafikizangu ama dada yangu anasema mimi yule mwanamke (mimi) basi tena hapo hapo baba yake anasema anataka turudiane,,so ninachokushauri mimi mume wa mtu wala usizae nae la wala usijisikie vibaya x wako kuowa mwanamke mwingine hayo yote ni maisha
Anonymous said…
Pole dada,

Mie naomba nikufahamishe kuwa,kawaida katika ndoa ya kidini (iwe kiislam au kikritu) mmoja wa wanandoa atakapo badili dini ndoa hiyo huwa batili,kwa hiyo mahakama labda ikusaidie kupata haki zako na mwanao.
Anonymous said…
Mpendwa dada, nadhani Emu 3 amefafanua vyema. Wazo la kuzaa na mume wa mtu lifute kabisa akilini mwako. Kwanini umuibie mwanamke mwenzio mumewe wakati wewe mwenyewe umekuja kuomba ushauri hapa kwa kesi ile ile? Halafu jambo jingine, kuzaa na mume wa mtu ni kujiongezea stress mpyaaa... Manake usitegemee huyo mume wa mtu utakuwa naye, baada ya muda mfupi tu atakukimbia kwa sababu sio wako! sasa hiyo stress ya kuhangaika na mtoto peke yako unaitaka? Nadhani miaka 40 ni umri wa mtu mzima kufanya maamuzi sahihi ukizingatia umeshapitia mengi katika maisha yako. ACHANA NA MAMBO YA KUZAA NA WAUME ZA WATU, HATA MUNGU HAPENDI.
Anonymous said…
dina natumaini u mzima ,ningependa niwasiliane na wewe,ila nimeshindwa kupata email address yako,asante nitakuwa nachungulia hapa kila wakati leo ,asante.
Anonymous said…
Most of us have been in religion we have now cause was the parents's religion. Been Islamic or Christian to me doesn't matter cause all of them insists on loving @ other (the most thing I care when we talk of main responsibility to all people believing in God) Your own family with the one you got married to is very important than your wishes of getting divorsed. Been in marriage sometimes needs tolerance just to save it. But to people who really know and believe in God, who counts on basic important things haihitaji kufikiri kiasi hicho. To me God is not of religions, is for people wanaotenda mema no matter is Islam or Christian. Sometimes I feels religious as just different kinds of cultures on how to worship God. Ukiacha zile dini za kishetani, wanaofanya dini zionekane mbaya ni wanadam na si biblia au kurhani. I advise u, uwe wa kwanza kutafuta amani nyumbani mwako fuata dini ya mmeo, ingawa ametumia mbinu isiyoonesha ukomavu wala Ukristo wenyewe, USICHUKUE MME WA MTU.Rashid.
Anonymous said…
Ni mimi Rashid, hiyo namba huwa naitumia @siku jion saa 12 hadi saa 1 jion unaweza call au kutuma sms mida hiyo kama sipo we sms tu ntaikuta. Doing this just for Dinah. Kuna matokeo makubwa na mazuri sana kwa relationship nyingi kutokana kazi ya huyu dada, acha tusaidiane kadri iwezekanavyo. Much Big up 2 Dinah.
Anonymous said…
Hi Dina mdogo wangu, napenda nipitishie shukurani zangu za dhati kwenye hii blog yetu kwako wewe binafi kwa kupost hii mada na kwa wale wote waliotoa michango na ushauri wao kwa kweli kwa kiasi kikubwa imenisaidia hasa katika masula ya kuzaa na yule baba. atleast kutokana na ushauri wenu nimepata maauzi ambayo sikuanayo kabla ya hapo.na nahisi ni mazuri na yatanisaidia kutokujichanganya tena. Nawashukuruni sana na mungu awabariki.
Mdogo wangu nimeona kuna Jibaba limejigonga hapo kama nimemuelewa vizuri. sasa niko makini na nahisi nawezakua na maamuzi sahihi na kukabili challenge, kama linataka kuleta mambo fulani au huenda akawa nae yamemchanganya. if he is serious mpe hio Emai address: mohamed.saumu@yahoo.com tuone analeta utani gani?