Mume wangu amebadilika sana,nifanye nini?

"Dada Dinah nakupa hongera sana kwa kazi unayoifanya kwa ajili yetu. Baada ya kuwa mpitiaji wa blog yako na kujifunza mambo mbali mbali kuhusu ngono na kukusoma jinsi unavyowaelezea watu kwa upeo wa hali ya juu nimeamua kuchangia tatizo langu ili nipate malezo kutoka kwako.

Nimekuwa kwenye ndoa na mume wangu kwa muda wa miaka 15 na tumejaaliwa kuzaa watoto watatu. Nilivyofunga nae ndoa mimi nilikuwa sio mtu wa kujishughulisha sana kutokana na kutokuwa na Elimu ya awali kama wewe na matokeo yake nimejifunza mambo mengi hapa na kwenda kuyafanyia kazi kla ninapofanya mapenzi na mume wangu.

Tumekuwa tukifurahia zaidi maisha yetu kitandani kuliko ilivyokuwa hapo zamani na cha kushangaza mume wangu hajawahi kuniuliza kuhusiana na kubadilika kwangu kitandani lakini amekuwa akiwahi kurudi nyumbani lakini kinachonikera ni tabia yake ya kunichunga kwa kunipigia simu kila wakati na kuuliza nilipo, sio kawaida yake.

Je ananichunga kwa vile yeye ndo mtokaji au imekuwaje? Naombeni ushauri wenu ili nisije kuwa nachezwa shere. Ashura"

Jawabu: Shukurani Ashura nafikiri mpenzi wako anajitahidi kukuonyesha kuwa anakujali na kukupenda. Huenda kabla ya hapo (haikuwa kawaida yake) hakuwa na hofu ya "kuibiwa" kwa vile ulikuwa hujamuonyesha uwezo wako wa kufanya "mambo fulani", katika hali halisi alijua kabisa kuwa "kingono" hujiamini kama ulivyosema wewe kuwa hukuwa mtu wa kujituma mlipofunga ndoa.

Lakini baada ya kujifunza na kufanyia kazi yale uliyojifunza kupitia hapa amegundua kuwa mambo yako ni makubwa na akishangaa-shangaa iwe kutokukuridhisha kingono au kutokukuonyesha anakujali na kukupenda basi mtu mwingine anaweza "kupata mambo" anayopata hivi sasa.

Mume wako anastahili pongezi kwa kutokukushutumu au kukuhoji umejifunza/julia wapi na badala yake anafurahia na wewe na kujitahidi kukuonyesha yuko pale kwa ajili yako(najua ni tabia mpya na hakika inakera kwa vile hukuzoea) lakini hana jinsi zaidi ya kuhakikisha Mke wake yuko salama popote alipo na hakuna mtu atakaethubutu "kutaifisha mali zake".

Kwa kawaida wanaume wengi huishiwa hali ya kujiamini ikiwa wapenzi wao ni wakali/watundu na hapo utaona "ulinzi" unaongezeka.

Hongera sana na kila lililojema kwenye maisha yano ya ndoa na familia.

Comments

Anonymous said…
Dada Hongera sana kwa kujifunza na kuyafanyia kazi mafundisho ya Dina.
Dina Hongera sana kwa maana kazi unayoifanya sio bure, majibu unayapata kama haya ya kutoka kwa huyu dada.
Mimi ninafikiri kwamba anarudi nyumbani kutokana na wewe ulivyobadilika na kuanza kumridhisha, pili kutokana na wewe ulivyobadilika na yeye kuridhika upendo umeanza kurudi na wivu umekuja.
Hivyo usione ajabu ni jambo la kawaida hilo.Kutokuuliza mtafutie wakati mzuri/mazingira mazuri na kwa upendo umuulize na kumfahamisha kuwa umebadilika kutokana na Dina, na umshauri nae apatapo nafasi apitie.
Mapenzi ni sanaa ambayo tunajifunza kama tunavyojifunza mambo mengine, hakuna mtu aliyezaliwa akijua kupenda, kufanya mapenzi, n.k. Vitu vyote tunavikuta hapa Duniani na kujifunza,
Kila la kheri na hongera sana,
Mtanzania,
tmajaliwa@yahoo.com.
Anonymous said…
Mapenzi yalipungua na kutokana na juhudi zako kupitia mafundisho ya Dinah umefanyikia kuyarudisha mapenzi ya mume wako nyumbani.
Mume wako amekuwa na wivu baada ya kumuonyesha mambo hadimu na anaogopa wengine wasije kumuibia na kufaidi zaidi.Tumpe hongera dada dinah wetu kwa kubuni kitu kama hiki.
Anonymous said…
Mumeo anahisi kuma watu wamekufundisha hayo manjonjo, either shoga zako au umepata jamaa la pembeni lililokufundisha hayo manjonjo. Kwa sababu mumeo ana busara ndo maana hakurupuki kuuliza na kudadisi kuhusu hayo madiliko. anachofanya ni kujaribu kutafuta mtu ambaye amesababisha wewe ubadilike kihivyo, so ana monitor nyendo zako kujua unapita wapi na wapi na kina nani unakutana nao.

Ushauri wangu ni kufanya jitahada za haraka kumuambia umepata wapi huo ujuzi ili kumuondoa duku duku, kabla kibao hakijakugeukia.

Njia unayoweza kutumia ni hii hapa: Baada ya manjonjo akiwa hoi muulize ki swali cha uzushi, kuhusu manjonjo yako mapya, then angalia atakavyokujibu, then muulize unajua ni nani aliyekufundisha, akaionyesha interest ya kujua kama mna internet nyumbani mfungulie hii page, kama hakuna mpe URL kwenye karatasi na umwambie akaangalie. Hiyo blog.

Akirudi atajua reaction yake. Ni ngekuwa mimi ninaiangalia.

Ataelewa na kupunguza wasi wasi