Nifuate Moyo wangu au Imani ya Dini?-Ushauri

"Dear Dinah Naomba ushauri wako na wadau wenzangu wa blog yetu hii Mimi ni binti mwenye umri wa miaka 25 sasa niko Australia, ila ninatokea Mombasa na nimekulia Arusha.

Katika kipindi cha nyuma nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu tofauti kila nikipata mpenzi hanifai either hatuko sawa kidini au kifikra .Kwa kuwa nilikuwa disappointed na mimi mwenyewe na mahusiano yangu nikaamua kutafuta mvulana mwenyewe bila kutafutwa .

Nikafanikiwa kumpata kijana ambaye tumekua pamoja tunajuana vizuri tu (tumuite JP) .Mahusiano yetu yalikuwa ya kirafiki , baada ya muda akaniambia anahisi ananipenda tukawa na mahusiano ya mapenzi kwa mwaka mmoja. LAKINI mahusiano yetu kipindi chote yalikuwa kwa simu.

Kwa sababu mimi niko huku nje na yeye yuko Arusha. Tumewasiliana kwa kipindi kirefu tukafikia hatua ya kukubaliana kama Mungu akipenda tunaweza tufunge ndoa. Hivi karibuni mwezi mmoja umepita alikuja kunitembelea rafiki yangu wa kiume (rafiki wa kawaida tu) kutoka nchi jirani(tumuite LUCKY).


Tumekaa pamoja kwa muda wa siku kumi kipindi chote tulichokaa tulizoeana sana kupita mazoea ya mwanzo hisia za mapenzi zikajitengeneza ndani yetu na tukagundua tunapendana sana tu .


Tatizo linakuja nimempenda huyu rafiki yangu LUCKY sana ila yeye tunatofautiana kimila kitamaduni na kidini japokuwa kifikra tuko sawa sana na tunaendana kwa mambo mengi. Wakati JP tuna Dini moja japokuwa tamaduni tofauti na yeye hajachacha sana kielimu na kifikra yuko sawa vya kutosha japo kuna tofauti kidogo ambazo hazistui sana .

Ukweli ni kwamba JP naye nilihisi kumpenda, ila kwa sababu siajonana naye kwa muda mrefu mapenzi si strong sana na pia mapenzi yetu yalianza kufifia haswa kipindi LUCKY alipokuja huku kwangu.

Hivi karibuni nikaamua kuchukua uamuzi wa kumuacha JP kwasababu nilihisi ntampotezea muda. Kwasasa nahisi kama nilifanya uamuzi usio wa busara. Kwa sababu Wazazi wangu hawata kubali nioane na mtu wa dini tofauti na mimi mwenyewe roho inanisuta nahisi kama nitaikosea Imani yangu.

Ninashindwa kuelewa je nampenda LUCKY kweli au ilikuwa mapenzi ya muda. Je ni kweli simpendi JP au ni kwa sababu yalikwa mapenzi ya mbali na pia sababu hatujaonana kwa muda mrefu??

Au nimuache pia LUCKY nisubirie nyota yangu inimulikie mtu mpya? Yaani sina raha wala amani kwa sasa. Nakaribia kurudi nyumbani Rafiki zangu wote wanaolewa na najua swali litakalo fuata kwangu ni nitaolewa lini.

Kujieleza nampenda mtu Dini tofauti sitaweza. Sijui nifanye nini? Naomba ushauri je nibaki na LUCKY kwasababu nampenda niachane na Imani za kidini nifuate moyo.

Au nikapendane na JP kwa sababu ninamjua vizuri na ni Dini moja kuhusu mapenzi tutazoeana huko huko baaada ya ndoa? Au nisubiri labda nitapata bahati nyingine??

Ni mimi R"

Jawabu:Asante R kwa ushirikiano, kutokana na maelezo yako inaonyesha wazi kuwa kuna vitu 3 muhimu sana kwenye uhusiano wako wa kimapenzi, Mosi ni Imani yako ya Dini, Pili Uwezo wa kiakili wa mhusika na Tatu ni Tamaduni.

Nasikitika kusema kuwa yote hayo hayahusiani kabisa na mapenzi, unapompenda mtu huangalii wala kujali ananini? aina ya maisha yake, Dini, Umri,muonekano n.k.

Penzi linajitokeza popote, kwa yeyote na wakati wowote, huwezi kupanga kumpenda mtu hata siku moja jampokuwa kama wanadamu huwa tunapenda kujiwekea viwango fulani vya aina ya wanaume/wanawake tunaotaka kuwa nao kama wapenzi lakini ukweli ni kuwa sio lazima utakuja mpenda mwenye "viwango" vyote utakavyo ama atakuwa na tatu kati ya kumi au ukiwa na bahati basi itakuwa tano kati ya kumi.

Kutokana na umri wako bado unakua kiakili hivyo ni mapema sana kusema kuwa umekuwa "disappointed", katika kipindi ulichonancho wanawake wengi ndio wanaanza kuijua miili yao na pia kuharakisha maisha wakitaka kuwa wamefunga ndoa by the time wanaumri wa miaka 30 hali inayosababisha wengi kuhisi hawana "bahati" kwa kuacha au kuachwa kwa vile wanaharakisha mambo ambayo wapenzi hawako tayari kuyafanya (wanataka ku-enjoy life kwanza) hali inayosababisha kutokuwa na amani ndani ya uhusiano.

Nilichokigundua hapa ni kuwa upweke ulichangia kwako kutokuwa na msimamo juu ya penzi la PJ na wewe na ni sababu kuu ya wewe kujihusisha kimapenzi na rafiki yako Lucky.

Kwa kawaida mwanamke anapofanya mapenzi huwa anahisi kujiamini "sexually" na kupendwa, hapo ndio tatizo lilipojitokeza na kukufanya um-buti PJ lakini ukweli unaujua moyoni mwako unajua wazi kabisa kuwa unampenda PJ(maelezo yako yananieleza hivyo).

Ili kufupisha hadithi (usije hisi "nakudongoa" bure hehehehe), Kwa vile PJ ana vitu muhimu unavyovitaka mwanaume awe navyo Imani, Tamaduni na Uwezo wa kiakili ukiachilia mbali kuwa anakupenda (kajtolea kaka wa watu kukupa moyo wake japo ukombali na kukusubiri ni wazi kuwa mabegi kayashusha juu yako).

Mimi nakushauri urudi kwa PJ na kumuomba msamaha na kueleza kitu gani kilikufanya umtose (usiseme ulikuwa na Lucky kwani utamuumiza), Sio rahisi kumpata mtu ambae ana "viwango" 3 muhimu kati ya vitano utakavyo kutoka kwa mwanaume......PJ anavyo.

Unaweza kutumia sehemu ya maelezo yangu haya "Akili yangu ilikuwa haijatulia na nilikuwa sijui nataka nini, nilipagawa na nidhani kuwa nahitaji muda kidogo kujua nataka nini na ili kufanikisha hilo sikutaka kukupotezea muda kwa sababu sikujua nitaamua nini na ndio maana nikampa nafasi (kibuti) ili uwe huru incase ungeamua kupenda mwanadada mwingine badala yangu."

Tuombe Mungu PJ hajaamua kuendelea na maisha yake na alikuwa anakusubiri urudi (wanaume wakipenda kweli huwa wanasubiri urudi).

Nenda taratibu na maisha, hata siku moja usiharakishe na pia unapoamua kufunga ndoa fanya hivyo kwa kujua kuwa uko tayari na pia una mapenzi ya kweli kwa mwenza wako kwani ndoa ni milele.

Ndoa ni Muhimu na ni sehemu ya pili ya maisha yetu baada ya kuzaliwa lakini usilazimishe ndoa kwa vile tu rafiki zako wamefunga ndoa au kulazimishwa/songwa na familia ufunge ndoa haraka kabla hawajaondoka Duniani n.k.

Furahia kila siku kama inavyokujia na umshukuru Mungu kwa kukuwezesha angalau kuiona siku mpya kuliko kujaribu kufanya mambo haraka kuridhisha jamii na marafiki.

Kila la kheri!


Comments

Anonymous said…
MAPENZI NA IMANI ZA DINI.
Hii dada Dinah, tuuite `mapenzi na imani za dini. Natumai katika maelezo yako mengi dada Dinah, umekuwa ukijaribu kutokuingilia imani za dini, kwani wapenzi wa blog yako wana imani zao tofauti, lakini yapo maswala kama haya ambayo yanahitaji kuingia upande huo kwa ujumla wake, bila kubagua huku au kule.
Kipindi hiki kama alivyowahi kusema rafiki yangu Jerumani, ni `nyakati tofauti’ na nyakati nyingine, na mambo yake huja kwa mabadiliko. Ingawaje mabadiliko haya tunayaleta sisi wenyewe `wanadamu’, kuwa hiki sasa kimepitwa na wakati au hiki sasa ndiyo kinafaa. Na mabdiliko makubwa yanaletwa kutoka nchi tajiri na kuziathiri nchi masikini kama za Afrika. Ingawaje yapo maswala kama ya imani za dini mabadiliko yake ni madogo na hayahitaji mjadala. Na kiukweli siku zinavyokwenda mbele maswala ya kiimani za dini yanazidi kupungua, ingawaje misingi ya imani ipo palepale.
Katika maisha ya kimapenzi, pale yanapooanza mara nyingi hatuangalii tofauti za kiitikadi. Kwani mapenzi wakati mwingine yanakuja `ghafula’ na wakati mwingine yanaweza yakakugeuza kiziwi au kipofu ilihali macho na masikio unayo. Unapopenda bwana chongo unaliita kengeza,na kengeza ni sehemu ya mahaba kama kukonyeza vile.
Ndugu muumbo ushauri, kitu kikubwa katika maisha ya `kimapenzi’ hasa mnapojiingiza katika ndoa, ni WEWE MWENYEWE kujiuliza unatakaje maisha yako yawe? Je wewe mwenyewe imani yako ya dini ikoje? Je wewe ungelitakaje watoto wako wawe? Wakulie katika imani za dini au wayumbeyumbe huko na huko na kujiamulia wao wenyewe? Kwani kwa mfano mkioana katika imani tofauti, ina maana mnawapa watoto wenu kazi ya kuamua imani ipi BORA, ya baba au ya mama?
Katika mapenzi kuna nyanja mbili, mwanzoni ni nyanja yako wewe na mwenzako, mtapendana, mtashibana nk. lakini ujue kuwa ipo nyanja kubwa ya pili ya familia yenu mtayaoijenga. Msingi wa familia yenu utategemea nyie wawili. Kama mtayumba mjue familia yenu itakuwa katika maisha ya kuyumbayumba vilevile.
Sasa basi,nionavyo mimi, imani ya dini ina umuhimu wake katika maisha yenu, kama kweli wewe mwenyewe unaamini imani ya dini yako. Kwani elewa dini ni imani, na imani hujegwa na hisia zako, kuwa najiandaa kwa maisha fulani baadaye ambayo mwanzo wake huanzia hapa duniani. Kwahiyo kama imani hiyo unayo, nakushauri umatafute mwenye imani yako. Wapo wengi na utawapenda kulikoni. Lakini kama imani yako ina mashaka, na `mapenzi’ kwako ni vyovyote basi uamuzi ni wako. Lakini kumbuka sana swali la familia yako unataka iweje, usilalie sana kwako peko yako? Sidhani kwamba huhitaji kupata matunda ya mapenzi yenu (familia)!
Hayo ndiyo yangu
emu-three
Anonymous said…
Huwezi kujua unampenda mtu kwa dhati mpaka uishi nae au kuwa nae ana kwa ana kwa kipindi fulani.

Huo uhusiano wako wa simu nafikii ulikomaa kwa vile ulihisi hakuna mwanaume mwingine atakae kufaa na kwa vile jamaa huko mbali basi huwezi kuona mapungufu yake kama yule ulienae karibu. Dini ni Imani ni muhimu lakini je inakupa raha na amani moyoni kama mapenzi ya huyo mtu? Kuna mahali Dada Dinah kamwambia mtu afuate moyo wake lakini asisahau akili yake.
Anonymous said…
nimefurahishwa sana na comment ya emu - three. labda mimi niongeze kidogo au nitoe mawazo binafsi kuhusu swala zima la mapenzi na dini.

mimi naona uko in a fix JD unamjua muda mrefu but distant imewagawa na ni ngumu kidogo kuweza tambua kama anafaa kuwa mwenza wako wa maisha unatakiwa kuwa nae karibu ili uweze kutambua mapungufu yake na uhimara wake .

kuhusu LUCKY kutokana na maandishi yako ni haraka sana kusema kwamba anafaa kuwa mwenza wako wa maisha naama mapenzi yenu yamedevelop kwa kipindi cha muda mfupi sana.

kwa ushauri wangu bila kuingilia masuala ya dini maana dini inaambatana na imani na sijui imani yako ikoje.naona unaharaka sana ya kuolewa na ndio maana umechanganyikiwa kidogo. Sitaki kuku laumu kwamba umerush kutembea na LUCKY wakati tayari ulikuwa na mahusiano na JD ila kwa mtazamo wangu binafsi hujampa JD time ya wewe na yeye kudevelop mahusiano yenu vizuri . nikimaanisha ungesubiri ukarudi Bongo then ukaangalia mwenendo wa JD then ukadecide kama anafaa kuwa mwenza wako au la.

ninachotaka kukuambia ni kwamba kuna msemo usemao usiache ambachao kwa msala upitao maana yake usije ukawa umemwacha JD ukadhani LUCKY ni bora zaidi kuliko JD kumbe ilikuwa ni lust.

Asante sana na nakutakia kila la kheri utekeleze yote unayoshauriwa na pia nakuombea upate mume aliye bora ambaye mtapendana na kuheshimiana katika maisha yenu yote. hilo ni muhimu zaidi.
BRAYAN said…
Imani zilikuja duniani ili kutufanya binadamu tuwe na hofu katika maamuzi na matendo yetu ya kila siku,kwani bila kuja kwa imani basi tungekuwa tunaishi kama wanyama kuuwa na kuowa dada yako au mtoto wako ingekuwa swala la kawaida sana chukulia mfano wa wanyama kwani scientific sisi pia ni wanyama ila wenye akili na akili imejazwa na hofu ya imani.

kwahiyo mdogo wangu swala la maamuzi ya wewe uwe na nani ni juu yako imani isiwe kigezo kama kweli umependa na unauhakika unapedwa kweli,Maana kaa ukijua kuwa uamuzi utakao ufanya hapo na kama kweli ikatokea mkaja kuwa mume na mke basi jua katika maisha yako huyo ulie mchagua utakuwa nae milele kwa shida na raha na utalala nae kitanda kimoja hata kama amekuudhi,sasa ni vema ukakaa chini na kuamua ni nini wewe unapenda na jaribu kupata free time ukiwa peke yako na hakikisha akili imetulia huna stress kaa na kufikiri je nini moyo wako unapenda waweke wawili hao kichwani kwako wakati huo bila kuweka swala la imani zao na fikiri kwa muda huo ukiwa mwenyewe je ni vigezo gani wewe ulikuwa unapenda na ni kwanini unapenda je ni yupi kwako amevuka vigezo vyako ingawa huwezi kupata mtu mkamilifu 100%,na je kama anavigezo vyako je ni kweli anakupenda kwa dhati na je unajiskiaje ukiwa nae au ukiwa unaongea nae,je ni aina ile ya wale wanaume uliyokuwa ukitamani siku zote kuwa nae??Maana yangu kubwa ya kukwambia hili ni ili wewe upate muda wa kuusikiliza moyo wako zaidi kuliko kitu kingine.
Nafikiri baada ya hapo utakuwa umepata a good breath na utaweza kuamua ni nini cha kufanya,wapo ambao wameowana kwa imani tofauti lakini ndio wenye maisha mazuri sana na wanapendana kwa dhati kuliko wale walio katika imani moja,Duniani kuna majaribu mengi sana huwezi kujua hili ni moja kati ya majaribu yako so take it as a challenge to u make it,

MAN FOLLOW IN LOVE THROUGH SEX,WOMEN FOLLOW IN SEX THROUGH LOVE.
Tchao.
Anonymous said…
Asante sana Dinah.
Nilikuwa kila siku nasubiri kuona usahuri wako utakuwa vipi. Nashukuru kwa ushauri wa Busara. Na nikirudi nyumbani ntaufanyia kazi nione kama kweli mapenz yatawezekana kati yengu na JP.
Nawashukukuru wachangiaji wote kwa ushauri wao mzuri.
Nahisi iliyobaki ni mimi kujua nifanye nini.
Asanteni sana

Ni mimi R.
Anonymous said…
Dinah mimi nakupenda yaani Mungu anajua,unavyojieleza mimi nasikia raha ya ajabu utafikiri nakuona na kukusikia. Naomba tuonane tafadhali au nikuone kwenye Luninga tu niridhike.