Mimi ni mzuri, nifanye nini kuwa nae?-Ushauri

"Dada dinah naomba msaada wako kuna Kaka fulani nampenda sana na najua mimi ni mzuri hawezi kunikataa ila sitaki kumuambia kwamba nampenda sijui nifanye nini ili niweze kuwa naye naomba msaada wako dada"

Jawabu: Asante kwa barua pepe,kutokana na maelezo yako mafupi ni kuwa "umefika bei" lakini unahofia kukataliwa ndio maana hutaki kumwamabia kuwa unavyojisikia juu yake. Suala la uoga wa kukataliwa (kutokuwa na uhakika kama utakubaliwa) pia huwakumba wanaume lakini kwa vile wanaume wameumbwa na ujasili wanayo namana ya ku-deal na "rejection" kitu ambacho sisi wanawake hatuna.

Mwanaume ukimkatalia atajitahidi kukushawishi na mwishoni unajikuta unaanza kudondokea kidogo kidogo, mwanamke ukikatataliwa inakupunguzia ile hali ya kujiamini, aibu mbele ya mwanaume huyo na ukimfuatilia ili kujaribu kumshawishi utaonekana unawalakini kwa vile mwanamke sio muwinaji bali anawindwa.

Kitu muhimu unachopaswa kutambua ni kuwa hakuna uhusiano kati ya uzuri wa mtu na mapenzi kwa vile uzuri wa mtu uko machoni mwa mtu(mtazamaji) huenda wewe ukajiona umzuri sana na pengine rafiki na jamaa wa karibu wanakuona na kukusifia kama vile Mungu alitumia muda wake vizuri sana alipokuwa akikuumba wewe. Hiyo sio tiketi ya yeye kukupenda au kutaka kuwa na wewe kwa vile mimi na wewe hatujui kama anakuona mzuri kama unavyojifikirua/jijua.


Kwa vile huna uhakika kama na yeye anahisia juu yako(hujagusia kwenye maelezo yako kana na yeye anaonyesha "interest") kumwambia moja kwa moja haitokuwa sahihi hivyo unahitaji kuwa karibu nae kwa kurafikiana kwanza, kama mwanaume atajua wazi kuwa "unamzimia" na hakika atakutokea lakini kama hana hisia za kimapenzi juu yako basi hatofanya hivyo namtabaki marafiki tu.

Njia rahisi ni kutafuta mawasiliano yake kama anuani ya barua pepe au nambari yake ya simu kisha anzisha mazungumzo nae lakini hakikisha unabaki na ahiba yako kama mwanamke. Kama jamaa hana mpango na wewe utatambua na ikiwa jamaa anampango na wewe pia utafahamu.

Akionyesha kuwa na mpango na wewe basi unaweza kumualikwa kwa ajili ya kinywaji pale dukani kwa Mangi (popote patulivu) au kwenda kwenye tamasha/mkutano/kanisani n.k. vilevile kama kuna sherehe basi jaribu kumpa taarifa mapema ili aweze kuhudhulia hali itakayokufanya uwe karibu nae zaidi kwani kati ya wageni/watu wote watakao kuwepo mahali hapo ni wewe tu ndio atake kuwa anakujua hali itakayo mfanya asicheze mbali.

Wanaume ni wepesi kutambua ikiwa wanapendwa bla hata kuambiwa hivyo baada ya muda fulani atajua tu kuwa unamtaka na atakutokea/tongoza au vyovyote itakavyokuwa ilimradi tu lengo lifikiwe ambalo ni kuwa nae kama mpenzi wako.

Kama huna namna ya kupata nambari yake ya simu njoo nikupe mbinu moja rahisi sana ya kufanikisha hilo.

Kila la kheri.

Comments

Anonymous said…
Dada very simple nenda msalimie then muambia can we have coffe tea or lunch ? or just propose going out together kucheki move hukohuko muambi direct makupenda basi hehehehe sasa ni zamu yako kusema msisubiri jamaniw anaume tu nao wanapendaga kuonyeshwa wanapendwa. Na kingine sio uzuri tu dada ni tabia na mangineyo huwezi jua na uzuri wako asikupende kwa mambo mengineeeeeeeeeee
Anonymous said…
Kimazoea wanaume ndio wanaotafuta/tongoza wanawake. Hii ni taratibu zilizozoeleka na kujijenga, ikizingatia kuwa wanawake wameumbwa ha `aibu'. Lakini siku zinavyokwenda, wanawake wanakuja juu, ile aibu inayeyuka machoni, na hutaamini wanaume wanazidiwa na `kujiamini' na wanawake.
Sasa, sio rahisi sana kwa baaadhi ya wasichana kuwaambia wanaume kile kilichomo moyoni mwao, na hata kama `amempenda aliyemtaka, hawezi kusema hapohapo nimekubali'
Hulka hii inaumiza, hasa ukimpata ambaye naye anaaibu kama zako, au naye hana uhakika kweli `upendo upo'. Je utampateje mtu kama huyo?
Wasomi na wale walioosha macho huko majuu, kwao ni `easy' tu. Anaweza akamualika mwenzake kwenye `dina' au `lanchi' na mambo yakaanzia hapo. Kwetu sisi bado ni ngumu, na kama utafanya hivyo, huenda hata huyo mume `kaweka walakini. Sasa kwanini sisi au wewe ushindwe kumwambia ukweli mwenzako kuwa `nakupenda'?
Zipo njia nyingi za kujitambulisha kwa mwenzako kuwa ninahisi kuwa nimekupenda, mojawapo ya njia hizi ni ile ya `kujipendekeza/kujipitishapitisha' ambayo inazalilisha kwa kiasi fulani. Ipo njia ya barua na mawasiliano ya mbali. Lakini ipo njia nzuri ya kutumia rafiki, shangazi nk. Hii ukimpata ambaye anaaminika inasaidia sana kumwambia mwenzako `nakupenda'.
Na kama ulivyosema `wewe u mzuri' basi huenda nayeye `amezimia' kwako, ila huenda ndio wale `wasiojiamini' au wanaogopa kuachwa solemba. Unajua tena wasichana wazuri mnatafutwa na wengi, na wavulana wengine hawataki ushindani.
Ushauri wangu mtumie shangazi yako, au rafiki yako unayemuamini akufikishie ujumbe, lakini sijui una umri gani. Maswala haya ya mahusiano siyakukimbilia, kwani unaweza ukakwaa kisiki, na kuwa mtu wa kuhangaika.
Kumbuka usemi wa chema chajiuza na kibaya kinajitembeza, wewe kama umzuri vuta subira. Wanasema upendo ni kama sumaku, umpendaye anavutika kwako kama chuma kinavyovutika kuliko na sumaku.
emu-three
Anonymous said…
to make it simple jitahidi upate atention yake..kama mdau alivyosema hapo juu jipitishe ila usizidishe...ongea naye muonyesha kwamba unampenda kama nayeye anakufeel sweet utaona tu haya mambo huwa hayafichiki .ukiona hana time hata baada ya kujitahidi achana naye usije ukajiona mjinga bure siunajua unaweza kuwa mzuri lakini mtu hata asikuangalie au anamzuri zaidi yako...nenda kwa step dada.