Monday, 22 September 2008

Aliniambia ananipenda, sasa ananikwepa-Ushauri!

Habari dada Dinah, pole na majukumu yanayokuzonga kila siku, mimi ni msomaji na ni mpenzi wa blog yako kiasi ya kwamba siwezi kupitisha siku bila kufika hapo nikaangalie kipi kipya.

Tuyaache hayo leo nami kwa mara ya kwanza nimekuja na tatizo langu ambalo linanizonga na kunisumbua sana kichwa changu na jibu si lijui.

Mimi ni msichana mwenye miaka 24, kuna kijana mmoja niliwahi kukutana nae mwaka mmoja uliopita yaani 2007, kipindi hicho hakuwai kuniambia kitu chochote zaidi ya salamu kutokana na kukosa muda wa kuwa karibu, kwani hatujawi kukutana kwa ukaribu hata siku moja yaani mita 20.

Sasa mimi nikaondoka eneo lile tulilokuwa tunakutana kwa umbali nikaamia sehemu nyingine, ndio juzi tutakutana tena na tukapata muda hata wa kupeana mikono na kuongea mawili matatu, na tukapeana namba za simu.

Ikapita kama siku mbili akanipigia na kunikaribisha kwake,nami nikaenda tutakaa na akaniambia kuwa amevutiwa nami na anapenda awe nami, ki ukweli dada Dinah ni hata mimi nilivutiwa nae ingawa sikuweza kumjibu pale pale kwa kuona soo.

Baada ya kuachana siku hiyo yule kijana akawa amesafiri akakaa kama wiki moja, toka amesafiri ni mimi ndie niliyekuwa nampigia simu, mwishowe nikiwa nampigia akawa ananiambia nikate then anipigie.

Sasa kweli huyu jamaa ananipenda kweli au alikuwa ananibeep maana hata sijawahi kufanya nae kitu lakini ananikatisha tamaa kabisaa, maana hata alivyorudi hii ni wiki hatujaonana kwa kisingizio kuwa anakazi nyingi.

Wakati mwingine huwa namuona kabisa akipita kutoka kazini nikimpigia simu ananiambia kuwa bado hajatoka sasa je huyu kijana anamapenzi ya kweli au alikuwa anataka kuonja na kuondoka, please naomba unisaidie dada yangu maana ki ukweli huyu kijana nampenda but nahisi kama nitaingia kusikofaa.

Sara"

Jawabu: Asante sana Sara kwa ku-share suala hili mahali hapa. Mwanaume anapokuambia kuwa anakazi nyingi (busy) harudishi simu zako au anakiongea basi inakuwa kwa kifupi/haraka fahamu kuwa hilo ni buti la kistaarabu.

Unapaswa kumshukuru Mungu kuwa huyo jamaa anakukwepa hasa kama unaamini kuwa kila kitu hutokea kwa sababu zake. Huyo bwana lazima kuna kitu kinamsumbua ambacho mimi na wewe hatukijui. Inawezekana kabisa jamaa anamatatizo ya kiafya na anahofia kukuumiza ikiwa atakuambukiza, huenda alikuwa anajaribu zali ili apate nafasi ya kukungonoa lakini baada ya kutopata "kidude" akahisi humfai kwa vile umembania, labda alidhani anataka kuwa na wewe kama mpenzi lakini baada ya kusafiri akagundua kuwa hisia alizokuwa nazo juu yako zimekwisha kwa maana hazikuwa za kweli.


Ni heri mwanuame anae epuka kukupotezea muda kwa kuepuka kuwa karibu au kuonana na wewe kuliko yule anaeijifanya anakupenda na unakuwa nae kila siku lakini anajua wazi uhusiano wenu hauna maisha marefu yaani anakuchukulia wewe wa "kupita tu".

Mimi nakushauri uache kupoteza muda wako kuwaza na kuumia kihisia na badala yake mdharau na uendelee na maisha yako, Mungu atajaalia siku moja utakutana na kijana atakaekupenda kwa dhati na kuwa pale kwa ajili yako.

Kila lililojema.

4 comments:

Anonymous said...

Wanasema wengine kuwa `hisia ya kupenda ni katika jicho la kwanza' ile kuangaliana tu kunajenga hisia fulani ya kupenda. Lakini hii sio sahihi kwa watu wote. Unaweza ukadanganyika na tamaa ya macho.
Tunapokutana kwa mara ya kwanza, tunaweza tukahisi kuwa tunapendana, lakini uhakika wa `kupendana' unatokana na mambo mengi sio hilo tu la kukutana au kuvutiwa na sura. Mapenzi ya kweli yanahitaji mambo mengi ikiwemo kujuana tabia, historia na imani zetu, na mambo mengine kadha wa kadha.
Kwahiyo jamaa uliyekutana naye, huenda bado unachunguza, au kakutana na mwingine ambaye naye amemteka mawazo yake na vitu kama hivyo.
Jambo jema ni kuweka malengo ya muda maalumu. Mpe muda, na kama mkionana na kwa vile mlishazoeana kiasi fulani, umweleze ukweli lengo na nia yako, ili asikupotezee muda. Pia na wewe unatakiwa umchunguze, sio lazima wewe mwenyewe, lakini jaribu kudadisi kupitia kwa watu wanaomfahamu ili umjue `kulikoni'
Yupo jamaa mmoja kaniambia `mapenzi ' ya siku hizi ya barabarani itafikia siku watu wataoa majini. Akiwa na maana, vijana wengi wanapupia `tamaa' na kushindwa kujua `mpenzi' ni mtu muhimu katika maisha, na kabla hujamkaribisha moyoni mwako unatakiwa `umjue' vilivyo.
Mambo mema hayaji kwa haraka, likiwemo hili la mapenzi, huenda hilo linalotokea sasa ni kwa manufaa yako. Mungu huepushia watu balaa bila wao kujua. Vuta subira na mpe muda muafaka. Kama ni wako utampata tu.
emu-three

Anonymous said...

Pole sana sana kwa hali uliyonayo kimapenzi!! Mapenzi ni pamoja na uvumilivu, sasa basi kwa kuanzia hapo naweza sema kwa wewe pia imetokea kumpenda huyu kija kuwa mvumilivu kwa kipindi furani then kwa wakati huo huo ambao unaendelea kuvumilia ujue unapaswa kuwa nae kwa karibu nikiwa na maana ya kwamba, uwe tayari kumueleza ukweli wako na wewe kujua ukweli wake yeye.

Kwani kwa namna moja au nyingine anaeza akawa labda kweli ni busy but pia anaweza akawa yuko na mtu mwingine sasa inapotokea kuwa hivyo wewe unapswa kujua mapema na kujua hatua ya kuchukua kuliko kuwapo mahali na ukapoteza muda wako na hata Gharama.

Kwakuwa hata ulishawahi fika kwake pia ni vema kwenda kwake tena kwa kipindi au wakati yeye yuko frii ilikuweza kujua mustakabali wa mapenzi yenu kwani jinsi ulivyoeleza ni mapema mno kujua kuwa anakupenda kweli au la!!!

Sina zaidi miss Sara nakutakia kila kheri.

Malo

Anonymous said...

jamani nashukuru sana kwa mawazo yenu, nawaahidi kuyafanyia kazi, na uku nikingojea maoni ya watu wengine.

mimi na sara.

Anonymous said...

DUH HICHO NIKIBUTI CHA KISTAARABU UKIONA MPENZI WAKO ANAJIFANYA YUKO BUSY UJUE TAYARI HAKUTAKI HUYO AU ANAPEWA NAFASI MWENZIO.