M3-Faida/Hasara na umuhimu wa ndoa!

M3 michango yako inanifurahisha sana kaka. Shukurani!

"NDOA ni muhimu na ina faida na hasara zake `Je ni vyema tukasubiri hadi tufunge ndoa ndipo tungonoane au ni vyema `tukapimana’ kwanza ili baadaye tukifunga ndoa tuwe tumejuana vyema? Na kama ni hivyo ina maana gani ya kufanya `fungate’.

Nini hasa FUNGATE, Ina umuhimu katika ndoa? Naomba utusaidie zaidi katika haya. N.B Hapa wengi tunashindana tunaposikia hoja ya kuwa `ndoa’ na ngono ni vitu viwili tofauti naya kuwa Ndoa ni mjumuiko wa vitu vingi ikiwemo ndoa.

Ni sawa kutegemeana na imani zetu, lakini zipo imani zingine `ngono’ hairuhusiwi mpaka ndoa, kwahiyo ngono ni kipengele muhimu kuliko mambo mengine. Hapa napo unasemaje?

Na kama ulivyosema ni vyema kuishi kimaadili na kiimani. Kimaadili na kiimani nijuavyo mimi, nikukwepa kabisa swala la ngono hadi ndoa itimie kama sikosei, sasa katika hoja tulizoshauriana hasa zile zinazowahusu `wapenzi’ kuwa mfanye hivi na vile.

Hawa je siwanafanya ngono nje ya ndoa, je kipindi hicho wakiwa wanafanya hivyo nje ya ndoa , kuna tofauti gani waliyoiona baada ya kuoana?

Hili lilikuwa swali la awali na nafikiri majibu tumeyapata. Basi katika mada zako zijazo pia utusaidie kutuelezea umuhimu wa `imani’ katika `ndoa’ au mapenzi kwa ujumla. "

Ahsante tena emu-three

Comments

BRAYAN said…
Na hasa kwa wale tuu ambao wanaamini maandiko ya vitabu vya dini na kuamini kuwa kuna mungu basi,
maana maandiko yanasema hakuna ngono mpaka ndoa na ndoa yenyewe iwe ile ya kutambulika kidini pia sio umvute mwenzi wako njoo tukae style halafu useme umeowa big No.sasa sijui ni wangapi tumefanikiwa mpaka sasa.
Tchao
Anonymous said…
Ndoa ni kufanya ngono kihalali.
Anonymous said…
Wewe kaka umeongea mambo ya msingi sana tusuburi dada yetu ataongezea nini.
KKMie said…
Asante Brayn na wachangiaji wengine, hakika nitakuja nanyongeza juu ya swala hili muhimu sana ktk maisha ya kila mwanadamu.
Anonymous said…
nafikili imani zinatofautiana sana,hivyo unapojibu please uwe kati kwani imani zinatofautiana sana
Anonymous said…
Naomba na mimi nismeme dada Dinah!
Sidhani kama kuna imani inayoruhu ngono kabla ya ndoa. Labda za mashetani ambazo zinaruhusu kunywa hata damu za watu. Pili, hata mila na desturi zetu za Kiafrika, maana hapa tunasema Kiswahili na hivyo sote tu Waafrika na waTz zaidi,hazituruhusu kungonoka kabla ya ndoa. Hata busu na Romansi zimeanza siku hizi. Please, subiri ndoa tu kama hujaolewa.
Gumegume