Friday, 15 August 2008

Kwanini W'wake pesa mbele mapenzi nyuma?

Imefikia wakati sasa nimekata tamaa, Dinah na wadau wengine mnajua kuwa ndani ya miaka saba kila mwanamke niliempenda na kuanzisha nae uhusiano anaonyesha kuipa pesa kipaumbele kuliko hisia za kimapenzi.

Awali nilidhani ni ugumu wa maisha kwa baadhi yao lakini nikaja kugundua hata wale mabanti waliotoka kwenye Familia zinazojiweza bado wanakuwa na hii kasoro ya kuthamini pesa zaidi kwenye uhusiano kuliko mapenzi yenu.

Je ni kasumba kuwa ukiwa na mwanaume ni lazima pia uwe mchimbaji wa dhahabu au ni nini hasa?

Imefikia wakati sasa naogopa kuanzisha uhusiano kwa vile nahisi hakuna atakae nipenda na kunipa penzi la kweli kama nifanyavyo mimi bali atakuwa na mimi ili kupata kile kidogo nilicho nilichonacho.

Jawabu: Shukurani kwa kuleta mchango wako hapa ulio katika mfumo wa swali. Hili suala nimekuwa nilisikia sana tangu nakua mpaka leo nimekomaa. Tena ni juzi tu nimetoka kuongea na Rafiki mmja akawa anasikitika kuhusu hili, hali inayofanya nitambue kuwa limekuwa tatizo kubwa kwenye jamii.


Inawezekana kabisa ikawa ni sehemu ya Asili ya mwanaadamu kuwa Mwanaume mtafutaji/mwindaji na Mwanamke mzazi na mlezi, lakini kutokana na maendeleo tuliyonayo hali imebadilika na sasa tunashrikiana na kusaidiana ktk kila jambo.

Kasumba ambayo imejengeka/zoeleka kuokana na mfumo dume inaweza kuchangia tabia hii kwa baadhi ya wanawake, vilevile kuna uwezekano kuwa ni mazoea yaliyobadilika na kuwa tabia na sasa imekuwa kama sehemu ya "Utamaduni" au niseme maisha ya baadhi ya wanawake kwa kisingizio cha "ugumu wa maisha".


Pia baadhi ya wanaume wanachangia hii tabia kuota mizizi na kuwa kasumba na hatimae "Utamaduni" (kama nilivyosema hapo juu) wa wanawake wengi kutokana na kitendo cha kutumia pesa kama "fimbo" au nyenzo ya kupata mwanamke.

Wapo baadhi ya wanaume ambao hujiona "Baba" kwa wapenzi wako (hasa kama ni wakubwa kiumri), kila ukikutana nae lazima akuachie "kitu kidogo" akisema nauli au kanunune soda.

Hii tabia wanayo akina baba wazazi (well baba'ngu miaka ile) mkipanga mihadi na kukutana lazima atakushikisha senti kabla hamjaachan akisema nunua kitu utakacho huko njiani.

Sasa Binti aliyezoea shikishwa Laki moja ya "nauli" na Mpenzi ajionae "baba" mara uhusiano huo ukiisha itakuwa ngumu sana kwake kuvumilia uhushiano mwingine bila kupewa pesa ya "nauli" kwa hiyari, na matokeo yake ama atahisi hapendwi (Kisaikolojia atakuwa akidhani kupendwa na mwanume ni kupewa pesa) au ataanza kukuomba kila mkikutana.


Kinachosikitisha zaidi kwenye hili suala ni kuwa Wanaume wengi wanapenda kujionyesha na "kujisigizia" mali ambazo hawana ilihali "kum-wow" mwanamke ili kushawishika kirahisi na akifanikiwa kumpata mwanamke husika Bwana atajitahidi kwa hali na mali ili aweze kuendeleza aina ya maisha fulani ambayo ameyaanzisha sambamba na uhusiano wake.

Hapo ni wazi kuwa uhusiano utaegemea kwenye ulichotumia kumshawishi (pesa/mali) na sio penzi kwani kilichomvuta kwako ni "misifa" na sio penzi au mvuto wao kwake japo kuwa wewe ulimpenda kimapenzi.


Kitu kingine ningependa kuongezea kwenye kujibu swali lako ni kuwa wanawake wengi wanapenda kusingizia ugumu wa maisha kama fimbo ya kupata senti kutoka kwa wanaume, na wanasahau kuwa ugumu wa maisha ni kwa kila mtu na sio Jinsia moja tu.


Mwanaume pia anakabiliwa na ugumu huohuo wa maisha lakini inakuwaje yeye anapata hata hicho kidogo chakukugawia wewe wanamke na wewe usipate ili mchange na kuwa na mahela ya kutosha kuendesha maisha kwa pamoja kama wapenzi?

Natambua pesa ni muhimu sana ktk maisha yetu ya kila siku na ni vema kuwa kwenye husiano ambao unajua kabisa utakuwa umelindwa kiuchumi, kihisia, kimwili n.k. incase of anything kama Mimba, kuugua namenginemengi ya kibinaadamu.

Pamoja na kusema hivyo ukubali ukweli kuwa unapoingia kwenye uhusiano unaingia kwa vile unampenda huyo mtu na unataka uchangie maisha yako na yake kwa ukaribu zaidi, mshirikiane kwa kila jambo.

Kidokezo

Penzi ni hisia na sio pesa au chochote kinachohusisha pesa. Kwa kumalizia tu napenda kusema kuwa ni vema unapomtokea mtu umtokee kwa kumueleza hisia zako za kimapenzi juu yake.

Ule mchezo/tabia ya kutongoza mabinti kwa kuwaahidi maisha mazuri, kuwapeleka popote watakako, kuwanunulia watakacho muiache. Wakati umefika kwa wanaume kuwa wazi na kuachakutumia pesa/uwezo wenu wa kimaisha ili kumshawishi mwanamke.

Just be yourself au a bit humble kama mambo yako safi na utakumbana na penzi la kweli lisilojali ulichonacho bali hisia zako tu.

****Samahani kwa kiswahili changu cha ovyo....Asante.

10 comments:

Anonymous said...

habari dada dinah,
mimi naomba uliza kama hili ni tatizo ama la. nimekua na bf kwa muda wa miaka 5 sasa lakini kila nikifanya naye mapenzi shahawa hua zinakua nyepesi sana hadi hua nahisikama nimelowa sana na wakati mwingine hadi twachafua godoro.
tatizo hilo nimekutana nalo kwake lakini kwa bf niliekua naye kabla mambo hayakua hivyo.naomba msaada ili nijue ni tatizo au nini hasa otherwise he is good n make me feel happy n gud after the game.

Anonymous said...

Tabia hii ya wanawake wengi kuamini kuwa na mpenzi ni kupewa pesa hata mimi inaniudhi na ilinikatisha tamaa nikaa mua nikaoe nje yaani mke wangu ni Mtanzania lakini anamtazamo mwingine na anathamini penzi na utu wa wangu na sio kilichoko mfukoni.

Anonymous said...

Sio wanawake wote wanaothamini pesa katika uhusiano, Binafsi boyfriend wangu an hatimaye mume wangu alikuwa na kipato kidogo kuliko mimi na mimi ndo niliyekuwa nampa yeye pesa za kulisha familia yake ambayo ilikuwa inamtegemea yeye kama first born. Baada ya miaka tisa ya ndoa na kuhangaika sana hatimaye nayeye sasa ana kipato kikubwa cha kueleweka cha ajabu anataka kuoa mke mwingine, mimi tena sina maana............hapa inaonyesha hakuwa na upendo wa dhati zaidi ya kunifanya mimi ATM maana baada ya kupata mapesa ya kuzidi, kisomo cha kueleweka kwa mgongo wangu anaoa mwanamke wa hadhi yake. YANGU MACHO!!
Kwa maana hiyo hii issue iko kwa jinsia zzote ila kwa wanawake imezidi.....na hii ni kwasababu tumeshajijengea kwamba katika uhusiano mwanaume ndo wa kutoa na mwanamke ni wa kupokea tu kitu ambacho sio sahihi.

Anonymous said...

Ni kweli wanawake wengi, naweza kusema 8 kati ya 10, kama si zaidi, wanaweka mbele pesa kuliko penzi. Penzi lao linafungana na pesa. ukiwa na chako basi kila mmoja atakutaka. Ukiwa huna chake basi hakuna akutakaye. Wanawake wengi ni waathirika (victims) wa matangazo ya biashara: vipodozi, mavazi, manukato na kadhalika. Vile vile niwaathirika wa mitazamo na matarajio ya jamii zetu ambazo, kwa kiwango kikubwa, nazo ni waathirika wa matangazo ya kibiashara kwenye vyombo vyetu vya habari, runinga, redio na magazeti.

Anonymous said...

Mimi nawaungeni mkono kwenye mada ya kwamba wanawake wengi hutumia ishu ya hela kumkagua mme kama anaweza kuwa bf au mme wao (potential mate). Hebu niwapeeni mfano ulio hai. Tangu 2005 nilibahatika kuwa na mpenz toka Tanzania. Niliwahi mwaka huo kufika pale mlimani kama msahihishai mitihani wa nje (external examiner). Kwa kuwa nilikuwa mgeni, simu nayo ikaamua kunipatia aibu. Ikaisha chaji kati kati ya siku kazi huku zikiwa zimenibana kishenzi. Nikaamua kuenda hadi hapo kituo cha vipanya niende zangu Ubungo au Mwenge ninunue chaji. Nje tu ya ofisi za idara nikakutana na msichana mzuri tuu, mweupe, mzigula etc etc. Akanieleza ana chaji ya nokia ofisini mwake. Yeye sekretari huko chuoni. Alipendezwa sana kufahamiana nami na nikamuamini. Ukweli alichaji simu na baadaye nikaipokea na kumshukuru na pia kumdhamini kwa ukarimu wake. Ghafla bin huu mapenzi si yakanoga! Tumekuwa pamoja hadi niliposafiri nikaenda ng'ambo kwa madhumuni ya kuongeza masomo. Imagine wenzangu nilikuwa nikiwa Nairobi ananipigia simu anasema hana dola naenda western union natuma. Anapiga simu anasema nanihii mgonjwa, sijui matanga, sijui nani kakimbizwa Muhimbili minatuma hela kadri ya uwezo. Akisema anataka nishuke dar wikendi fulani, mi nafanya mpango hata saa zingine naiba offu naja dar. Ukweli ni kwamba tulipendana sana. Wazazi wake wakanifahamu na familia yao pia. Ila nilipopata nafasi ya kuenda masomoni, hakupenda niende na mda sio mrefu nikaambiwa anatembea na wengine. Sikukubali. Lakini miezi mitatu iliopita akanipigia simu na akanitangazia ana mimba na anaomba ruhusa tuachane.Ni kweli nilimsaidia kifedha. Na ni kweli pengine singekuwa na fedha hangenipenda. lakini lililo muhimu ni kwamba tuliheshimiana siku zote. Ukweli iliniuma ila kwa upande wangu najilaumu pia. Pengine ningemsikiza nije dar tupange tuishi na tusahau masomo ya juu. Nimekuisha kuwa kama Mtanzania sasa. Hivi sijui kama itawezekana kwangu kuishi na mke wa kikenya tena. Nilipata mapenzi mazuri tuu tena sana tuu Dar. Kwa hio nawashinikiza wakiume kama mimi msife roho. Tanzania kubwa sana. Sio wote akina dada wanapenda hela. Wanachotaka ni sekiuriti maishani. Yaani hela iwe kama kizingiti cha kutengeza releshenship au ndoa. Tuwape masista zetu sappot. Na tutafanikiwa. Laiti ningekua mimi bf wa huyo dada alietangulia hapo juu. yule yule ambaye alimsapot bf wake kisha bf alipofanikiwa akamtupa na antaka sasa kuoa mwengine. Ningekupenda siku zote kwa ufukara au ukwasi. pengine nitumie email: tunaweza kuwasiliana kama marafiki, ya mungu ni mengi. makokha@zedat.fu-berlin.de

Tusijimulishe wanawake wote. Wengi wazurii tuu kama akina Dinah.

Egidio Ndabagoye said...

Dah! pole sana 8:32:00 nikisia simulizi kama zako basi naona bora niendelee kukamata Foster's tu mambo hayo nayapa kisogo.

Kusema ukweli dada zetu ni kawaida yao kupima uwezo wako kabla hamja date.Na sio wabongo tu hata wa nje nao vile vile sema wabongo kwa kiasi fulani wamezidi,hata ile cost sharing wengi wao huwa hawana inakuwa taabu kwa wachumi kama mimi.Kwanza lazima ifahamike kuwa mapenzi sio pesa haitakiwi kuwekwa mbele sana.

Wakina dada wanaweza kujibu why kwanini? inakuwa namna gani sisi ATM?

Richard said...

dinnah pole na kazi umenifurahisha kwenye kidokezo chako,ukweli ni kwamba ukimfuata mtoto na ukajionyesha kuwa wewe ni maskini haki ya nani hupati kitu,nakuhakikishia utaishia kupewa namba ya simu kila ukipiga yupo bize,hivi nani anataka shida na matatizo???hahahah!!

Anonymous said...

hapa mimi nakataa kabisa, sio kweli kwamba wanawake wote wanapenda pesa ni baathi yao tu. Lakini siku hizi wanaume wanapenda sana kulelewa labda ndo maana wanawake wamestuka.

Jamani maisha sasa ni magumu ni bora tukawa tunasaidiana na sio kubaki kulaumu wanawake peke yao.Mimi nina mifano mingi sana ya wanaume tegemezi.

Anonymous said...

Hali halisi ya kimaisha ndiyo inayosababisha yote hayo, sidhani enzi za mababu zetu watu walijali sana mali katika kupendana. Ndio walikuwepo matajiri wa ngombe, shamba nk. Lakini vitu kama hivyo havikuwekewa manani sana, kama siku hizi pesa ilivyokuwa ibilisi.
Jinsi maisha yanavyokuwa magumu na hali ya kiduniani inavyokwenda kasi ndiyo matapeli wanavyokuwa wengi wakiwemo matapeli wa mapenzi.
Tukubali kuwa wanawake ni wengi na wingi wao unawatia hofu kwao kuwa huenda nisipofanya hivi mapema, atawahi mwenzangu. Hapo ndipo wale wajanja wanaojulia wanapochungulia chunguni kuwa kuna nini, ili kilichopo nikiwahi kabla ya mwenzangu. Wengine ndio hawo wameamua kabisa kujianika mabarabarani wakijiuza...`angalia mimi matiti yamesimama, mimi haina maji'...aibu tupu
Mapenzi ki kawaida hayahitaji pesa, ila pesa inayafanya mapenzi yang'ae na ya pendeze zaidi. Kiukweli mfano huna pesa na mwanamke anahitaji kujiremba, atapata wapi vipodozi, labda wa kijijini ambaye anaweza kupaka `maparachichi' lakini hapa mjini kulipata tu hilo parachichi ni kazi kwelikweli. Hayo machicha ya nazi yenyewe yanahitaji gharama ya kuinunua hiyo nazi. Kwahiyo hali yenyewe inawatumbukiza dada zetu pamoja na tamaa kuwahitaji wanaume wenye pesa. Na hapo ndipo penzi linapogeuka kuwa ni la pesa.
Sio wote lakini ipo asilimia inayoangukia huko.
Hayo ndiyo yangu
emu-three

Anonymous said...

MIMI NINGEPENDA KUUNGA MKONO HILI SUALA!!KUA WANAWAKE WENGI WAMEKUA NA TABIA HII CHAFU!!
MIMI NI MMOJA WAWA ATHIRIKA NA HILI JAMBO!!NILIKUA NA MSICHANA MMOJA TULIETOKEA KUPENDANA KWA MIAKA 8,TULIANZA KUPENDANA YEYE AKIWA FORM1 NA MIMI FORM2!!
HUYU BINTI YEYE ALIKUA AMENIZIDI KIPATO!!KWAKUA ALITOKEA KUNIPENDA KWAKUA NILIKUA HANDSOME NA NILIKUA NAJUA KUMFIKISHA KUNAKO YANI KUMCHEZESHA SEGERE NA VANGA!!NILIKUA MJUZI WA KUMLA BATA VILIVYO!!HIVYO ILIMFANYA AZIDI KUPAGA JUU YANGU!!NA ISTOSHE NI MIMI NDIE NILIE MFUNDISHA MAPENZI!!
INGAWA ALIKUA AKINIPENDA KUKAWA NA KIKWAZO CHA KIPATO!!WADOGO ZAKE WA KIKE WAKAWA WAKIMPIGIA KELELE KWANINI ATEMBEE NA MWANAUME KAMA MIMI!!
MARA KADHAA NIKAANZA KUMKUTA NA WAVULANA WENGINE AMBAO NAO WALIKUA NA KIPATO KIZURI MAKWAO!!NIKIMULIZA ANANIAMBIA NI MARAFIKI TU!!
BONTI HUYU TULIKUA TUNAPENDA MNO NA ALIJIVUNIA KUA NAMI!!HATA MBELE YA RAFIKI ZAKE KUA MIMI NDIO CHAGUO LAKE INGAWA DINI NI TOFAUTI.
IKAENDA HIVYO MPAKA TULIPOANZA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM,TULIKUA WOTE MABIBO HOSTEL!!HAPO MIGOGORO IKAANZA!!ALIANZA KUA NA URAFIKI NA MVULANA MMOJA WALIE KUA WANASOMA NAE KWANI YEYE ALIKUA AKISOMEA UCHUMI NA MIMI NILIKUA NASOMA POLITICAL SCIENCE AND PUBLIC ADMINISTRATION!!MIMI SIKUPENDEZEWA NA UKARIBU WAO!!NIKAMWAMBIA MWENZANGU MWANZONIIKAWA UGOMVI BUT BAADAE AKANIELEWA TUKAENDELEA KUPENDA ZAIDI,HUYO MVULANA NI MTOTO WA MFANYABIASHARA MMOJA WA MADINI MWA?ZA.
IKAJA KUTOKEA NIKAPATA SCHOLAR SHIP¨YA KWENDA KUSOMA NJE YA NCHI.MWENZANGU ALIUMIA MNO NAKUMBUKA ALIKUA AKILI SIKU ZOTE.NIKAONDOKA TUKIWA NAAHADI YAKUJA KUFUNGA NDOA NIKIMALIZA MASOMO.
BAADA YA MWAKA MWENZANGU AKAINGIA KATIKA ULE MTEGO WA YULE KIJANA KWA KUA ALIKUA NA KIPATO KIKUBWA WKT HUO ME MAMBO YANGU BADO HAYAJAKAA SAWA!!
AKAACHANA NAMI KWA NYODO!!NA KUNIKANA,ILINIUMA SANA!!IKAWA SIMUAMINI TENA MSICHANA NIKAWA PLAYER WA AJABU!!KWA KUA NIMVULANA NA NINAMVUTO WASICHANA WENGI WALIOKUA NA KIPATO NAWASIO NAKIPATO WALIKUA WAKINIBABAIKIA!!MIMI NILIHITI NAKURAN!!IKAWA MPAKA WASICHANA WENGINE WAKINIHONGA ILINITULIE LAKINI NILIKUA SINA IMANI NAO!!
MWAKA 2006 MWISHONI NIKAKUTANA NA BINTI WAKIBONGO NIKATOKEA KUMPENDA NA YEYE AKANIPENDA AKANIVUMILIA SANA NAYE PIA ANAKIPATO BUT ANANIPENDA KWA DHATI NAMI NAMPENDA KANIBADILISHA TABIA!!NAKUNIFANYA NIAMINI KUNA MAPENZI DUNIANI!!SASA NIMETULIA NAE MAMBO YETU YAMENYOKAA SANA!!NANINA MPANGO WA KUFUNGA NATE NDO TUKIRUDI TANZANIA