Kwanini "romance" hufa baada ya kipindi fulani ktk ndoa?


Samahani mi nataka nitoke nje ya mada,naomba ruksa yako dinah na wadau kwa jumla. Mimi leo na kitu kimoja nataka nimuulize dada yetu,kama vp na washika dau karibuni,kwa lengo la mahala hapa ni kuelimishana na kuwekana sawa kuhusu maisha yetu ya kila siku.

Issu dada iko hivi,mwanamume anapompenda na kumtaka mwanamke huenda kwa nguvu zote na baada ya makubaliano mahusiano hukua na mapenzi hushika hatamu, zawadi kibao,out usiseme kila siku,ahadi za kila aina ili mradi tu kuonyesha ni jinsi gani mwanamme amempenda huyo mwanamke.

Mwisho wa siku wanavalishana pete za uchumba na hayawi hayawi mwisho yanakua wanaoana. Kama mungu anapenda huwa na familia kwa maana ya kuzaa watoto, hudumu ktk mapenzi kama yale ya mwanzo kwa muda na baadae taratibu huanza kuporomoka.

Suala la mume kutoka na mkewe kwa ajili ya matembezi na burudani huwa halipo tena,badala yake ni kuona mume anakwenda na wanawake wengine kwenye kumbi za starehe.

Hapo mimi ndipo nakuwa sipati jibu,najiuliza kwani yale mapenzi ya awali yamekwenda wapi?na ni nini kinasababisha na kupelekea hali hii kutokea? Usinitupe kapuni dinah naomba mtizamo wako(wenu )wadau.

Jawabu: Nashukuru kwa ushirikiano wako. Hili swala la kifo cha "romance" baada ya muda fulani wa uhusiano hasa baada ya watoto kuzaliwa husababishwa na mambo mbali mbali ambayo nitajitahidi kuyaelezea kwa kifupi na kukusaidia ama kuepuka au kuyaangalia kwa karibu ili "romance" indelee kuwepo siku hadi siku mpaka mwisho wenu.
Kujisahau kwa wapenzi mara tu baada ya kufahamu kuwa wamefunga ndoa na hakuna sababu ya kujaribu au kujitahidi kum-wow ili akuone kuwa wewe ni mpenzi bora kuliko wengine aliowahikuwa nao (hapa ukishangaa unamkosa mpenzi na ndio maana unajituma) hilo moja.
Pili, ni ile hali au kasumba ya mwanamke kujitoa/badili kutoka mpenzi na kuwa mama/mke mara tu baada ya kujifungua watoto fulani. Hii inatokana na shindikizo kubwa kutoka kwa jamii inayotuzunguka(yaani ukizaa mtoto wewe ni mtu tofauti, yaani hujichanganyi na kuongea na watu ambao hawajazaa hata kama ni umri mmoja), kitu kinachomfanya mwanamke ahisikuwa amekuwa mama na hivyo hapaswi kuwa kama alivyokuwa kabla hajazaa.
Tatu ni mwanamke kwa namna moja au nyingine ajione mpweke kutokana na kutopata usaidizi/ushirikiano kutoka kwa mume wake hivyo "comfort" aipatayo ni ile ya mtoto/watoto wake.
Mama hukaza zaidi ile-bond kati yake na mtoto hali inayomfanya awe karibu zaidi na mtoto/watoto na kumsahau mume/mpenzi (atamuona kuwa ni baba watoto na sio Mpenzi kama ambavyo yeye mume anamuona). Hili likitokea mume ataisi kuwa hapendwi/hajaliwi tena na hivyokwenda tafuta penzi nje.
Nne ni kupoteza ile hali ya kujiamini na hivyo anaamua kutojijali na kujipenda na hivyo anakuwa havutii tena kama mwanamke na anabaki kuwa hana habari na muonekano wake, kitu kitakachomfanya mpenzi/mume kuona mkewe havutii (kuona aibu kutoka nae) hapa kama ni mtu wa mikutano-mikutano, kuoka kwa kinywaji nakadhalika hakika ataibua kimwana mwingine anaevutia kwa "kampani" mkutanoni.
Yote kwa yote, ni vema jamii (hasa wanaume)watambue kuwa mwanamke anapokuwa mjamzito na kujifungua huwa anakabiliana na mabadiliko makubwa sana kiakili, kimwili na kiroho.
Mwanamke huitaji ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa mume wake, anahitaji kusaidiwa, anahitaji kukubushwa, anahitaji kupewa matumaini n.k ili arudi kama alivyokuwa awali.
Wanawake unafofautiana na kila uzazi unatofautina hivyo kila mtu na kila uzazi huwa na mabadiliko yake kivyake hivyo yanapaswa kushughulikiwa kitofauti ili mwanamke kurudia hali yake ya awali na hivyo kubaki mpenzi na sio mama Ashura!
Asante.

Comments

Anonymous said…
Mimi sipingi hoja yako, ila ninachotaka kusema hapa ni ile hali halisi ilivyo. Wewe kama mwanamke una haki ya kuwalalamikia wanaume hivyo kuwa wao wanabadilika punde tu pale mnapoishi kwa muda fulani au baada ya kuvikana pete. Hiyo ni kweli lakini huenda wote wawili nikiwa na maana mwanamke na mwanaume tunachangia hilo.
Swali la kujiuliza je, wewe mwenyewe jinsi ulivyokuwa awali, kimaumbile na vitendo ndivyo ulivyo sasa, je ulivyokuwa ukijiweka mwanzoni ndivyo ulivyoendelea hivyohivyo? Je mahaba yako, tabasamu lako, ulimbwende wako nakadhalika vimeendelea kuwa hivyohivyo? Kama utajibu kweli na sahihi, utakuta kuna mabadiliko yanakuwepo kwa wote wawili. Hii ni kuona kuwa, ‘kile kitu nilichokuwa nikikitafuta kwa udi na uvumba sasa kipo, nimekipata, sasa udi na uvumba wa nini tena’. Tunajisahau wote kuwa kila kitu kinahitaji maboresho. Hata shamba ukililima, linachoka, linahitaji mbolea kila siku ili litoe mavuno mengi na bora! Je sisi tunajiboresha? Huenda tukawa tunajilaumu huku tukijiimbia nyimbo za taarabu za kimapenzi lakini kile tunachokiimba hatukifanyi. Hayo yatakuwa mapenzi ya taarabu. Tunachotaka ni mapenzi ya kivitendo.
Upo pia usemi kuwa kitu kikiwepo huwa moyo haudundi, ‘sikipo bwana, nikitaka nitakipata’ lakini kitu kikiwa mbali moyo na mshawashwa huwa mkali, na unatamani ukionje ili uone tofauti yake au sio?. Lakini kama wote tutakuwa wabunifu, kiasi kwamba kila mmoja akiwa kazini anajiuliza `sijui leo mwenzangu atatoa jipi jipya, mmh yale mapenzi ya jana, sijawahi kufanyiwa’ Mbona tukifanya hivi mapenzi yatakuwa motomoto kila siku. Siri kubwa na vishawishi vipo mikononi mwetu!
Ni kweli siku zinavyozidi kwenda mbele, na mishughulisho ya kimaisha na sisi wenyewe kujisahau, tunajikuta hata ule muda wa kuonyeshana `maraha’ unapungua, na inafika hali ambayo mmoja anaona `ampe mwenzake tu’ kwasababu anataka. Na huenda anatamani kutoka nje na wewe, lakini anakuona upo busy na mihangaiko ya nyumbani, au ulivyojiachia haipendezi tena na vitu kama hivyo. Inafikia hata tendo lenyewe la ndoa linakuwa halina raha kama awali, kinahofanyika ni kupitisha muda, na ukizingatia kwamba ule muonekano wa awali na ule urembaji haupo tena basi ni kama kutwanga mchele uliokobolewa!
Mimi nahisi romance ni wewe mwenyewe na jinsi mlivyojiweka toka awali. Kosa kubwa ni ile hali ya kusubiri kila kitu aanze mwanaume. Wewe katika hali hiyo una haki sawa kama yeye, buni, toa ushauri, na elekeza ikibidi. Lakini hata hivyo ninakubali kuwa wapo wanaume sugu, hawaelezeki hawaambiwi, na pia vilevile wapo wanawake wasiojua majukumu yao, hawajifunzi na hawabuniki, wapowapo tu. Hivi ndivyo ilivyo kuwa wote tuwapungufu na wote tunahitajiwa kujifunza.
mimi emu-three
Anonymous said…
habari zenu wote mliojumuika na mada hi ya leo.mi leo ndo siku ya kwanza kuingi aktk blogg hii. ni nzuri.

kuhusu mada hii ya leo.
kuhusu romance kupungua katika mahusiano jamani mi sidhani kama kuna formula yoyote ila ndio nakubaliana na wengine waliosema,kuwa sometime ni mwanamke anaweza kuchangia na pia kuna wanaume wasiofugika hata umfanyie nini basi tu yaani yeye hatosheki na mmoja.sasa mi naona ni mtu tu mwenyewe eidha mwanamme anaweza akawaanmwambia mwenzie watoke hata baada ya kuzaa ila mwanamke hataki kwa madai kwamba"aah nishazaa mie naenda wapi sasamie ni wanyumbani tu au ooh mtoto nimuachie nani" na kuna wakati mwnamke anataka kutoka na mumewe ila mume hataki.
Na romance si lazima mtoke mnaweza mkawa mnaenjoy pamoja nyumbani starehe ziko za aina nyingi as long as wote wawili mna have fun.
ila wanawake wenzangu msikubali kushundwa kiurahisi hata siku moja hata kama umeona dalili si mnuri kotoka kwa mpenzi wako.

grace.
Anonymous said…
Mimi jamani naomba nitoe muono wangu katika mada hii. Kweli jinsi mwanaume anavyomfuatia mwanamke kabla hawajamuoana onaona ni tofauti na wakati wakiwa wameshafungua ndoa na zaidi wakiwa wamebarikiwa watoto.

i) Kwanza kunakuwa na mabadiliko kwa upande wa mwanamke, kimwili, hasa wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua. Na hapa kuumbuka mlipokuwa mnatoka matembezi wakati wa uchumba, sasa inakuwa tofauti - (huu ni muono wangu) i.e. mama labda ni miezi saba au karibu kujifungua au tuseme tu labda mimba changa na mchafuko/feeling nausea(kichefuchefu) unatokea mara kwa mara, na kama Mume akimwambia, vipi twende kwenye cocktail/party kazini au tukajifurahishe kwenye pub unakuta mama anaona wacha tu abakie nyumbani na mwenzake aende.
Ndio saa nyingine hata kwenye madisco unakuta kina mama na mimba wanajivinjari na mumewe, ni vizuri ikiwezekana lakini si kina mama wote wanaweza kufuatana na mumewe wakati wanalea mimba.

ii) Kumbuka mtoto akizaliwa, unakuta inabidi mtoto atunzwe na wazazi wote wawili, lakini mtakubaliana na mimi - mtoto mchanga/mdogo anamhitaji mama zaidi i.e. kunyonya etc. Na unakuta watoto wengine wakiwa wachanga hawalali usiku mzima, mara nyingi inabidi mama anahangaika nae usiku kucha, na labda siku inayofuata mzee anamwomba mama watoke kuburudika, hapa mara nyingi mama atakuwa bado amechoka kutokana na tutolala usiku, unakuta anamwomba mumewe aende mwenyewe yeye abaki na mtoto ili apate kupumzika.

Mabadiliko ya kimwili

i)Kama familia imebarikiwa kuongezeka (kupata mtoto) - kwa upande wa mama kuna mabadiliko ya kimwili, unakuta mara nyingi tumbo la chini ninashindikana kurudi kabisa na hata kama likirudi sii 100% kama zamani, mistari mistari(strech marks) ya tumbo na hips au pia maziwa (matiti) kuwa malaini zaidi na kidogo kulala (inategemea kama mama amenyonyesha na ni watoto wangapi), na pia kina mama wengine wanapata mabadiliko ya umbo, wakati wa kubeba mimba mwili unaongezeka na unakuta kujirudi kabisa unahitaji muda na mazoezi makali, ili yake mafuta (ule unene wa mimba)uishe - kwa hivyo unakuta kina mama wanakuwa hawajioni ni wazuri tena kama zamani, hawajisikii wanavutia, kwa hiyo hii inawafanya kujitenga kidogo katika maneno ya mapenzi na sio kujisikia free kama zamani, e.g. zamani labda mtu ulikuwa unapenda kidogo kufanya miondoko flani flani au hata kutembea uchi chumbani mbele ya mpenzi wako, lakini sana unakuta kina mama wengine(sio wote) hawajisikii free kama zamani (wana withdraw), na hapa inahitaji saaaanaa mume mwelewa, "wakumhakikishia kuwa mke wangu wewe ni mzuri tu, nimekuchagua wewe" la sivyo huu kweli niwakati mume anaanza kuruka na vimwana wengine na mara nyingi wadogo kiumri.

ii) katika jamii zetu utakubaliana na mimi kuwa wanaume wetu kidogo hawaelimishwa vya kutosha kuhusu mabadiliko ya kimwili ya mwanamke aliyebarikiwa watoto, kwa hivyo unakuta wanaume wengi wanashindwa wanashindwa kuhandle na wengine waona aibu kuonekana na wake zao hasa sehemu za kujivinjari kama disco ambambo asilimia kubwa ni kinadada wenye umri mdogo au single. Na unakuta wanatoa sababu hambazo zinaficha tatizo sahihi, kama mke wangu hajui kupika vizuri, au hanihesimu siku hizi, ili mradi tu awe na sababu ya kujivinjari mwenyewe.

iii) Na zaidi ya yote, kwa mwoneko wangu asilimia kubwa ya wanaume ni watu wanaochoka haraka saaaannaaaa "lose interest or get bored very easily"(sio wote lakini asilimia kubwa), wanata
tofauti za mpenzi, na unakuta hapa ndio maana hata wanaiba wake za wenzao (japokuwa wanakimbia tofauti za mwili nilizoongelea hapo juu na pia hata kama wanatoka na mwanamke ambaye bado hajajaliwa watoto- hii ni ukiangalia wanaume walio single.)

Lakini tusisahau kuwa kuna wanaume walio wapenzi wa dhati kwa wake zao na wanatunza familia zao vizuri sana, na ukiangalia vizuri hizi ndoa ambazo mume ameridhika na mke wake na verse versa mara nyingi sana unakuta Mke anajitwaa 110% kuendeleza penzi hilo.

Ni hayo tu na ni mwoneko wangu.
Anonymous said…
Mi labda kimtazamo nitaonekana tofauti but wanaume wetu walio wengi wana hulka ya kufanya ngono mbali na mwanamke mmoja hata kama utamuonyesha staili tofauti na michejo ya kila namna kama bado hulka yake ipo nje atatoka tu cha msingi ni kumalizika kwa hamu wakati wa tendo la ndoa.
Mwingine anakuwa na kinyaa awezi hata kulamba chumvi lakini yeye anataka ule pipi kijiti yake kwa iyo hii inaweza kuwa pboblem ya kutoridhika na mapenzi mfano before ulishakuwa na wanaume tofauti ambao yeye kila sehemu ya mwili anaifanyia kazi na kukulainisha ipasavyo ukampa huyu ambaye hajui hata kitu ndio maana mtu anaamua atafute mwingine wa kukpa raha. Naomba kuwasilisha
Anonymous said…
Dinah pole sana na majukumu, ni muda mrefu sana m2 wangu...mi mzima kabisa...
any way nakuja na mawazo yangu kuhusu hii mada...
" binafsi mtizamo wangu unajaa sana kwa kina mama, especially wa kiafrica, malengo yao makubwa huwa ni ndoa, na wakishapata ndoa na watoto basi hujiachia...na kuna wengine huwa na vitambi japo ni wanawake...
sasa kwa mwanaume kuona yale mabadiliko hurudisha nyuma hamu ya kutoka nae tena...
ila ni ukweli kwamba...." kwa kila penzi likiwa kama lilivyoanza basi hudumu kila siku"

sina mengi sana kwa leo....

ni yule yule m2 wako....
Anonymous said…
Nakubaliana na wewe na mimi ni kijana niliyeoa kama miaka 6 ilopita.
Kuna kubwa nililojifunza wanawake wengi wakishaolewa wanabadilika sana na uota mapembe mambo mengi wanafanya kwa kubweteka na kulewa Ndoa. na kutotimiza wajibu wao kama wake nakubaliana na wewe kuwa hata wanaume kwa upande wetu tunapaswa kuonyesha upendo ila lililopo mara nyingi naona wanwake wanabweteka sana na kumea pembe.
Anonymous said…
Dooo,hapo umenena,lakini na mimi nitaongezea kidogo kama yalivyo mapungufu ktk mapenzi.
Kuna magomvi au kupishana ndani ya nyumba kwa wapendanao nayo pia inachangia kwa kiasi kikubwa kuligawa penzi ndani ya nyumba.
pia kwa upande mwingine ni kujaribu kutafuta kitu kingine ambacho kitakuwa kinawaunganisha wote wawili tofauti na tendo la ndoa.mnaweza kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi pamoja kila jioni na kuhufanya huo kuwa ni utaratibu wenu ktk maisha si lazima kwenda gym.ni vizuri kama mnanafasi nyumbani ni bora zaidi.
Anonymous said…
Pole sana kwa hayo lakini huwa kuna pande mbili.1)Wanaume wasio na msimamao ndiyo huwa wako hivyo.2)Wanawake wasio jiuliza kama je wao hufanya sehemu yao ktk mapenzi au huwa wana ridhika baada ya kuolewa na kuona hawa na tena jukumu.Mwenzio ame hangaika kuku tongoza na wakati mwingine ulim sotesha sana .Lakini baada ya kuolewa huoni umuhimu wa kujitahidi kumwonyesha mapenzi unataka uhudumiwe wewe tu.Kubembelezwa ubembelezwe we kila siku je mwenzio huwa unambembeleza na kujiuliza bidii yake unailipa vipi.Ni kama kitega uchumi ambacho unawekeza lakini hakibadiliki(yaani kununa kila siku).
Anonymous said…
Dada dinna hongera kwa ushauri wako mzuri,mimi naomba kuuliza mnaposema romance hufa kutokana na mwanamke kupoteza mvuto baada ya kujifungua au kuwa na watoto, mbona unakuta mwanaume anatoka nje ya ndoa na ankuwa na uhusiano na mke wa mtu ambaye tayari naye ameshazaa na ana watoto je hiyo imekaaje?