Ignorant kwenye Hasara,Faida,umuhimu wa ndoa.


Ignorant, mchango wako umenifurahisha sana.

"Kwanza kabisa, pamoja na sababu ya mada hii kupata... Kwanza kabisa, pamoja na sababu ya mada hii kupata wachangiaji wachache kama ilivyotolewa na M3, nadhani urefu wa maelezo ya DL nayo pia ni inachangia kupata wachangiaji wachache.


Sidhani kama watu wengi wanaoingia hapa wamesoma post yote, na kama ndiyo, wachache wanaweza pata wazo la kuchangia baada ya kusoma post ndefu kama hii. Ok, nirudi katika mada yenyewe.Kwa mtazamo wangu, maelezo ya wachingiaji hapo juu yana-reflect jinsi tulivyokuzwa kuamini ngono ni mbaya.


Mbali na hilo, maelezo mengi yanachanganya madhumuni ya ngono na ndoa kuwa kitu kimoja. Nitaeleza haya.Tukiweka imani za kidini pembeni, (kwani mambo mengi ya kidini huwa hayajadiliki kutokana na kuwepo kitu utakatifu na hivyo kutompa binadamu yeyote uwezo wa kukosoa au kujadili uhalali wake).


Kwa mtazamo wangu, ngono ni kitu tofauti kabisa na ndoa. Ngono ni tendo la kukutanisha sehemu kike na kiume ilhali ndoa ni makubaliano ya watu wawili kuishi pamoja na inatarajiwa watu hawa kua jinsia tofauti (ingawa siku hizi kumeingia aina mpya ya ndoa). Kwa mtazamo huu, hailazimishi vitu hivi viwili kuendana kwa pamoja au kuuliza kipi kianze na kingine kifuate ingawa inajulikana kua katika ndoa kutakua na ngono.


Kutokana na makuzi yetu, mambo haya mawili yamewekwa pamoja na hivyo kuzua utata katika kutambua kila kimoja wapo. Kuchanganya kwa madhumuni ya kingono na ndoa ndiyo yanasababisha wanawake wengi kudhani wamedanganywa na wanaume pindi wanaposhindwa kuolewa ilhali wameshangonoana na hao wanaume (same men).


Kwa upande mwingine, wanaume nao wanakua waongo kwa kuahidi ndoa kwa wanawake/wapenzi wao ili wapate ngono. Kama ngono na ndoa vingeeleweka kua ni vitu viwili tofauti, maumivu na uongo huu usingetokea. Suala la kudhalilisha utu/ubinadamu kwa kuonyesha uchi/utupu linahitaji mjadala zaidi.


Suala la kudhalilika kwa kuonyesha utupu linategemea sana jinsi mtu alivyokuzwa kama sio utamaduni. Napenda nipingane na maelezo kua ngono hudhalilisha mtu kwa kua anaifanya akiwa mtupu, tunaweza kusema nini kwa wale madaktari walio na mwanya wa kuona utupu wa wagonjwa wao? Vp udaktari nao unadhalilisha utu?Kwa kumalizia, naomba tusome alama za nyakati.

Tuangalie ni nini kinawezekana kwa nyakati hizi na pengine kutambua mabaya na mazuri yake na jinsi ya kupunguza athari za hayo mabaya. Suala la kujadili ngono kabla ya ndoa ni bora au la ni la msingi, hata hivyo kwa kuangalia kinachoendelea katika jamii, ni vizuri tukafikiri zaidi ya swali hili. Sidhani kama watu wanaofanya ngono kabla ya ngono hawafahamu faida na hasara zake.

Tujadili yale tunayoweza kuyafanyia kazi."

Comments

Anonymous said…
Nafikiri mjadala unaanza, kinyume na nilivyotarajia, na naona Dada Dinah, kaamua kutupa nafasi wachangiaji, hasa kuhusu hii maada ya Ngono kabla ya Ndoa.
Mchangiaji Jeremia ameanza na kujihami kuwa anaiweka imani ya dini pembeni, sio mbaya lakini kwa vyovyote utakavyoeleza utajikuta unarejea palepale. Hii ni kwasababu kila tunachokifanya kwa utashi wetu kinakuja kuleta ulakini na madhara makubwa kinyume na kama tungeamua kufuta jinsi imani za dini zinavyotuelekeza.
Nia yangu sio kuhubiri imani ya dini, ila kwa uoni wangu mdogo hasa katika maswala ya mahusiano na maumbile ya kibinadamu imani za dini zingesaidia sana kuokoa `maisha na matatizo yanamkabili mwanadamu’ Na hapa nikimaanisha kuwa `ndoa’ ipewe kipaumbele kabla ya `ngono’ na yakuwa hivi vitu viwili viende sambamba.
Tuache imani ya kidini ina wenyewe, turudi kwenye mada inayokwepa imani za dini. Kuna baadhi ya hoja uliyoitoa Jeremia kuwa tusichanganye `ngono’ na `ndoa’. Hili kwangu linaleta utata, naomba ufafanuzi. Hebu tujaribu kujiuliza baadhi ya maswali ya uhalisia kwa kuvitenganisha hivi viwili kama kweli hayana mahusiano kwa kuangali faida na hasara zake.
Jeremia yeye kwa maelezo yake, kama sikosei anataka kusema `ndoa’ haina umuhimu, kwahiyo inaweza ikajitenga na ngono? Ya kwamba watu wanaweza wakaoana na wasifanye ngono au sio? Na halikadhalika watu wanaweza wakafanya ngono bila kuoana? Na je kwa haya mawili faida zake na hasara zake zikoje?
Ndio nakubaliana na wewe kuwa nyakati zinabadilika na kwahiyo wanadamu wanataka wajiendeshe jinsi nyakati hizo zinavyokweda, lakini tunatakiwa tuwe makini na nyakati, kwani sio vyote vinafaa kutegemeana na nyakati. Kama wanadamu wenye `utashi’ wa kufikiri tunatakiwa tuchambue jema na baya, na ukifanya hivyo utakuwa unarejea katika `imani’. Kwa mfano imefikia watu wa jinsia moja wanaoana, hii sio `ndoa’ lakini nyakati inataka ilazimishe iwe ndoa. Imefikia wakati watu wanafanya ngono na wanyama, hii huwezi ukaiweka katika ngono inayoeleweka, ngono inayoeleweka ni ile iliyohalalishwa ndani ya ndoa, lakini nyakati na huko tunakokwenda utasiki hilo limehalalishwa. Tuwe makini na nyakati.
Nia kubwa ya ndoa na (ndoa ninayoizungumzia hapa ni ile ndoa halali, sio ndoa za nyakati hizi)
-Ni kutaka tendo hili lifanyike kwa faida na sio kwa hasara, ili kukwepa magonywa nk
-Ni ili kukwepa migongano ya kijamii kwa kuwepo na mizania inayohakikiwa na wahusika au kwa kufuata imani za dini.
-Ni kuleta mahusiano mema, katika jamii.
Zipo faida nyingi, ile tukirejea kimfano kama watu wengeachiwa kujifanyia ovyo, watoto watazaliwa ovyo, haki zitakosekana , hili lipo wazi. Yapo madhara ya magonywa kuelezea hapa ni kupoteza nafasi.
Kwa uoni wangu, ngono inatakiwa ifungamane na ndoa. Yaani hivi vitu viende sambamba. Kwani ngono ikifanyika kivyakevyake `madhara’ yake ni makubwa kuliko kama ingefanyika ndani ya ndoa.
Ngoja nifikiri kidogo
Kuonwa uchi na daktari ni katika hali isiyozuilika. Kwani kwa hali kama hiyo hata mkwe ambaye ni dakitari anaweza akamuona mkwe-mwana wake. Lakini katika hali ya kawaida sio ya dharura tunaweza kulinda utu wa binadamu kwa kutokujidhalilisha, nikiwa na maana kufanya ngono kiholela, na kumvulia nguo kila mtu, hata kama utaifanya ukiwa umevaa nguo lakini tendo lenyewe likiwa nje ya ndoa linadhalilisha! Tusihalalishe hili tendo lifanyike kiholela, kwa kusingizia nyakati. Nyakati zipo na zina mazuri yake lakini mabaya yapo, mojawapo ni hili.
Naomba tuwaonee huruma wanetu na kizazi kijacho, kwani nionavyo mimi, hali njema tuliyoishi katika mambo haya tunakuwa wachoyo kuwahusia wanetu na kizazi kijacho. Tunafurahia hali inayoendea kuiangamiza jamii. Tuwe na huruma kwa kuwahusia na kuwaelekeza wenetu pale inapowezekana hata kama ni vigumu lakini wapo watakaoitikia na kwahiyo hawo wachache wanaweza wakawa wakala wazuri wa wenzao.
emu-three
KKMie said…
Shukurani sana Jeremai, maelezo yako yatasaidia kufungua watu macho kama ya DL na M£...keep them coming.

Nami nakuja kuongezea ili kuwekana sawa, naona wanawake wameamua kuegesha kwenye swala hili.
Anonymous said…
Ahsante sana Dinah kwa shukrani ya mchango wangu. Napenda nitoe rekebisho kidogo, jina langu hapa ni Ignorant na kwa sasa niko Ujerumani (jeremani) ingawa siku si nyingi nitakua nchi nyingine kabla ya kurudi Tanzania.

Kurudi katika mada, si nia yangu kuendeleza malumbano na M3, ila napenda nitoe maelezo machache kwa sehemu ninazodhani sikueleweka.
Kwanza kabisa, niliepuka kujadili dini kwa makusudi kabisa na napenda nisieleweke kutokuona mchango wa dini katika kuleta tabia nzuri kwa binadamu. Kama nilivyoeleza mwanzo, niliepuka dini kwa kua majadiliano yake ni mapana sana na yanavizingiti vingi ikitiliwa maanani mambo mengi ya dini hayapaswi kujadili. Dini ikishasema hiki au kile ndo mwisho hakuna kuangalia upande mwingine. Hivyo kwa kua dini nyingi zimeshasema ngono ni baada ya ndoa, sikuona maana ya kujadili hapa kwani kwa mfuata dini yeyote ana paswa kufahamu hilo na kufuata pasi kujadili (kama dini zinavyotaka).

Pili, niliposema ndoa isichanganywe na ndoa sikumaanisha kua ngono haina thamani katika ndoa. Ni sawa kujadili viungo vinavyofanya chai - kwa mfano sukari, maji na majani ya chai vinaweza kutumika kutengeneza chai, lakini haimaanishi kua unapotaka kuifahamu sukari lazima uijadili katika mfumo wa kuunda chai.

Tatu, suala la kusoma nyakati halimaanishi kuhalalisha maovu kama M3 anavyotaka kunielewa (M3 ni kiwakilishi tu maana natumai kuna wengi wenye mawazo kama yake). Kwangu mimi usomaji wa nyakati ni jinsi ya kuangalia jinsi tamaduni zinavyobadilika na kujaribu kubuni mbinu zinazoweza kuwa na mienendo bora pale inapoonekana mienendo mipya inakinzana na mazoea au mambo tuliyozoea kuyafanya. Nitatoa mfano katika hili.

Naomba nitoe mfano wa mabadiliko yanayofanywa katika baadhi ya dini/madhehebu ili kuendana na miendeno au tabia za nyakati hizi. Kwa bahati nzuri, mfano wangu unaendana kabisa na suala tunalolizungumza leo. Kuna mambo yamelegezwa katika suala la kufunga ndoa hasa katika dini ya kikristo, kwa mfano suala la kufunga ndoa na mtu wa dhehebu tofauti au pengine dini tofauti. Hapo zamani ilikua haiwezi kubalika kabisa kwa mkatoliki afunge ndoa na muumini wa dhehebu lingine au dini nyingine.

Suala la ngono kabla ya ndoa nalo ni kama mchezo wa kuigiza katika baadhi ya dini zetu. Hebu na tujiulize ni watu wangapi leo hii wanafunga ndoa huku bibi harusi akiwa mjamzito, na wakati mwingine siku chache tu kabla ya kujifungua. Hivi hao wanaofungisha hawaelewi au kutambua kua huo ujauzito ulipatikana kwa hao wawili kungonoana?

Kukatiza maelezo haya marefu, napenda ieleweke kua lile suala tu la kujadili kama ngono kabla ya ndoa ni bora au la tayari linatuweka nje ya dini kwani dini haziruhusu, kutambua au kukubali majadiliano hayo kwani kwayo ngono ni baada ya ndoa.... period!!!

Ignorant,
Jeremani
Anonymous said…
Ahsante sana Jeremani,,nami sipendi kuendeleza mjadala huu, kwani umeshaniweka katika kundi fulani, ambalo mimi ni kiwakilishi. Sio kwamba sina la kukujibu, lakini tutakuwa tunazunguka pale pale, na matoke yake tutajikuta tunajadili mambo ya dini, ambayo hapa sio mahali pake.
Nisalimi huko uliko, na nimefurahi kuwa pamoja nawe katika mjadala huu, i wish tungepata nafasi ya kujadiliana zaidi, kwani ningejua mengi upande wako, nami ninekupa mengi ya `uwakilishi' wangu. Na ahsante sana dada Dinah, tunasubiri utoe vitu vyako kuhusiana na hili
emu-three
Anonymous said…
Naombeni kusaidiwa jamani, Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 28 nimeolewa kwa bahati mbaya sijabahatika kupata mtoto. Tatizo linalonisibu licha ya kuchelewa kupata mtoto ni kuwashwa sana sehemu za siri. Nimeshakunywa sana dawa na kuweka vidonge ukeni bila mafanikio. Nimeshachukuliwa vipimo na mara zote ugonjwa hauonekani ila naambiwa labda itakuwa fungus ninapewa dawa sioni nafuu. Ninafuata taratibu zote za afya na ninazoshauriwa na madaktari kama usafi ukeni na kunyoosha nguo ikiwemo na nguo za ndani. Kama kuna mtu mwenye ushauri mwingineo naomba mnisaidie maana inafika wakati nakata tamaa hadi ya maisha kutokana na adha ninayoipata, Asanteni, Juliana, Iringa