Saturday, 19 July 2008

Nitumie nini kuondoa michirizi ya Uzazi?

"Dinah dada nakukubali! Mimi nina shida naomba ushauri ikibidi kutatua tatizo langu. Mimi nina tatizo la michirizi iliyotokana na uzazi nina kitoto kimoja ila mwili wangu matakoni na hipsi kama kenge.

Sasa nilikuwa nauliza je hii michirizi itatoka? na ninunue kitu gani itoke maana nimeshakwenda maduka mbali mbali (jina kapuni) hamna kitu.Naomba ushauri wako/wenu nifanyeje ndoa yangu ipo mashakani? Nisaidie naomba saaaaana?"

Jawabu: Asante sana kwa kunikubali na pia kwa kuchangia swali lako mahali hapa. Nasikitika kusema kuwa michirizi (stretch marks) haitoki bali inapungua tu kwa kutumia bidhaa zilizotengenezwa maalumu kabisa kwa ajili hiyo.

Pamoja na kusema hivyo inasemekana kuwa kuna dawa za kuzuia na kuondioa kabisa alama hizo juu ya ngozi ambazo baadhi ya wanaume huziita "mistari ya utamu" lakini dawa hizo hazijathibitishwa kisayansi kitu kitakachonifanya niseme kuwa hakuna dawa ya uhakika ya kuzuia na kuondoa kabisha michirizi.

Michirizi hiyo hujitokeza kwa mwanamke yeyote (wengi wetu tunayo) sehemu mbali mbali za miili yetu kama vile kwenye matiti, matakoni, sehemu ya kwapa/chini ya mkono, mapajani, sehemu ya nyumba ya miguu na kinachosababisha hili kutokea na kutanuka kwa ngozi yako sehemu husika (mahali ilipo).

Michirizi hii pia huwapata zaidi mama wajawazito au wazazi na hilo hutokana na kutanuka kwa ngozi yako sehemu hiyo ya tumbo na meneo ya karibu kama vile kiunoni, n.k.

Natambua hofu ya ndoa yako kuwa hatarini kwa sababu ya mabadiliko ya mwili wako baada ya kujifungua kwa vile mistari hiyo (mabadiliko ya mwili wako) inaweza au inakusababishia ujisikie huvutii tena kama zamani au "ukajishitukia" kuwa mumeo havutiwi na wewe tena hali itakayokufanya umkimbie au uanze "vijitabia vya ajabu" kamavile kufanya mapenzi gizani, kwenda kubadilishai nguo mahali ambapo yeye hayupo, kulala na nguo zako, kufanya mapenzi ukiwa "full dressed" nakadhalika yaani kwa kifupi inakupunguzia ile hali ya kujiamini ukiwa mtupu(uchi) mbele ya mpenzi wako.

Mimi nauhakika kabisa kuwa mumeo hatosumbuliwa au kuwa "put off" na hizo alama ikiwa wewe bado ni yuleyule na unafanya mambo yako fulani kama awalia au ukaongeza ujuzi kidogo ili kufurahia zaidi.

Unachotakiwa kufanya ni kujirudishia tena ile hali ya kujiamini kwa kufanya mazoezi ili ku-shape up, kula na kunywa vizuri ili ngozi inawiri, badili mtindo wa mavazi......kwamba, kama ulikuwa mtu wa khanga mbili sasa pia moja, kama ulikuwa mtu wa khanga moja sasa piga gauni bila khanga au sketi na blauzi nakama ulikuwa mtu wa magauni basi sasa wewe anza kupiga suruali na kaptura, hali kadhalika unaweza kupia mini.


Yaani badili muonekano wako kwa ujumla na usijisahau ukawa mama nanihii, bali kuwa wewe na wakati huohuo mama wa mtoto wako sio MAMA FULANI( hili linaathiri wanawake kisaikolojia na kimwili pia).

Ikiwa unashindwa kuwa huru mbele ya mume wako hata baada ya kufanya nilivyokuambia basi ni wakati wa kuifanyia kazi Nguzo ya tano ya uhusiano bora ambayo ni mawasiliano, weka wazi hofu yako. Muulize mabadiliko gani anayaona juu ya ngozi yako tangu umejifungua? Akisema machirizi muulize je michirizi yako inamkera?

Asipo gusia michirizi kama sehemu ya mabadiliko juu ya ngozi yako basi ujue jamaa hana habari na anakupenda pia anafurahia kama ilivyokuwa awali.

Kila la kheri mdada!

14 comments:

Mamdogo said...

Pole, ndoa yako iko mashakani kwasababu una michirizi ya uzazi?? lol.
Mi nilidhani michirizi ya uzazi hutokea tumboni tu kumbe hata mahipsi na matako hupata athari za mimba?
Nasubiri kwa hamu sana jibu la Dinah na wachangiaji wengine

Anonymous said...

dada Dina na wachangiaji<

Labda niweke vizuri, pamoja na uzazi mwili ulitanuka pamoja na sehemu ya makalio, Ila yote ni baada ya kujifungua yaani michirizi ya kutisha sio mchezo na tumboni pia, Hata sielewi nahitaji msaada wenu

Nawaomba saana

Anonymous said...

tumia HOLLYWOOD COCOA BUTTER CREME. Ile ambayo ndani ni km mafuta (ina kifuniko cha blue). sio ile ambayo ni kma lotion (yenye kifuniko chekundu). Manake zipo aina mbili. haitaondoa kabisa ila itapunguza kwa kiasi kikubwa! na uwe unapaka kila cku sehemu zote za mapaja na makalio. Ni nzuri sana!

Anonymous said...

ni ngumu sana kutoka ila itapungua kuilinda ndoa yakoni wewe wanaoachwa sio wote wenye michirizi,jitahidi mpe mambo na usihofie hiyo kitu kama alivyosema dada dinnah usiwe na wasiwasi

Anonymous said...

Mhhh hapo swali lako ni rahisi sana lakini inabii ufanye kitu chenye uwakika maana usije ndio ukaongeza baada kupunguza.... ushauri sana ila labda tumsubiri DINAH anaweza kutueleza zaidi....Na mhh mdau wa kwanza kutoa maoni wewe umeachwa kwa ajili hiyo nini???

Anonymous said...

Pole mum,
Mie ilinitesa sana, nilitumia Hollywood kama alivyosema mdau juu, ilipungua,kwa hio natumia palmers cocoa butter cream asubuhi na jioni Hollywood cream tumbo na matako talikuwa kama nilipigwa michilizi(strech marks) Zimeisha zote yani kwa mbali sana na ni mwaka mmoja tu.try hard anza na hollywood then after three month changanya u will be ok.

Ushauri
Hollywood usinunue kwa SH AMON,
Nunua kwa mary rose au agiza Nairobi kama unamjua mtu hakikisha ina karatasi la nylon ambalo so feki.

ziko feki kibao mjini.

Anonymous said...

Tumia pia mafuta ya itwayo BIO-OIL sijui kama yako huko dar as niliyaona huku nilipo(uk). But nimazuri mie yalinisaida.

Kamili

Anonymous said...

Jaribu pia "Bio Oil" km upo Dar au nje ya nchi hii hupatikana. Nenda Marry Rose Cosmetics wanayo inauzwa ghali kiasi lakini nayo husaidia sana kupunguza michirizi hiyo mimi nimeitumia na imepunguza. Ukipata mtu anaweza kukuletea toka South Africa ni bei rahisi ni nusu ya bei kwa hapa. Huwa pia inapatikana katika maduka makubwa ya dawa

Mamdogo said...

http://www.stretch-mark-cream.net/reviews/index.php?a=4225&gclid=CMHjv-mh1pQCFQyD1QodoSgDkQ

Click hiyo linki na utapata products za stretch marks, kama uko bongo na una credit card waweza kuoda online.
All the best

fatma said...

Salaam kwa wote na Dina. Ahsante sana kwa blog hii, M/mungu akubariki. Kuondoa alama hizi pia unaweza kutumia olive oil. Jipake ukae kwa muda mrefu kama kuroweka halafu nenda kuoga,tumia maji ya uvuguvuu na kitambaa safi kujisugua hasa sehemu zenye alama.

Anonymous said...

Asante saana dada Dinah pia asanteni saaana wadau.

Nitafuata kama mlivyoniagiza pia dada dina yupo right na yote aliyosema kujihisi ni tatizo kubwa sana.

Cha msingi ni kujiamini, sure

thnks.

Anonymous said...

Jaman hizo hollywood na palmer cocoa butter creme zinauzwa bei gan?pliz anon 12:15pm help?

Anonymous said...

Jaman bei ya hizo hollywood na palmer cocoa creme ?am.soo desperate kujua

Boniventure Mchomvu said...

Cjaelewa mchanganyo huo mdau now nimeanza na hollywood je after 3months nachanganya vp???