Tuesday, 8 July 2008

Ningependa kufunga Ndoa lakini anaharaka sana-Ushauri!

"Mambo vipi Dinah, Sorry nimejaribu kutafuta e-mail yako bila mafanikio lakini katika kuangalia huku na kule finaly nikaipata.

Mimi nina swali moja ambalo linanitatiza sana kuhusu mpenzi wangu ambae ninataka kumuoa lakini nasita kutokana na vitabia vyake. Hivi wewe binafsi unamchukuliaje mwanamke ambaye yuko very anxious for marriage kiasi kwamba akiona rafiki yake anaolewa basi ujue siku hiyo na wewe utakuwa na kesi.

Pia anakuwa na hasira zisizo na msingi. Yaani kila mara unapokuwa nae basi hakosi kukasirika(sio muda wote) but still anainsist marriage. Mimi natishika na matendo yake kiasi kwamba kila mara najiuliza...hivi nikioa si ndio itakuwa balaa kama kipindi hiki cha mapenzi bila ndoa hakuna kuelewana? bcoz naona hata adabu amepunguza but still anasema ananipenda sana.

In short she is soo aggressive and wants to control me such that anataka anachotaka yeye ndio kifanyike lakini mimi nikitaka jambo hakosi kuweka pingamizi. Nimemwambia nataka kumuoa mwakani (2009) lakini yeye hataki alikuwa anataka this year.

Zamani alikuwa mpole sana kwangu kiasi nikimwambia kitu ananisikiliza lakini siku hizi akinisikiliza basi ni kwa muda. Pia anatabia ya ku-revenge eg. Kama nilisave namba ya mwanamke kwenye simu yangu ambaye yeye hamjui basi ujue na yeye ipo siku atasave namba ya mwanaume na kumchokoza ili ampigie mida ya usiku mimi nikiwa nae, na nikiuliza basi najibiwa "IS MY FRIEND, I THOUGHT IT WILL BE OK WITH YOU BCOZ NA WEWE UNACHUKUA NAMBA ZA WANAWAKE"Naomba ushauri wako Dinah. David"

Jawabu:Asante David, mimi binafsi nitamchukulia mwanamke huyo hajiamini, hajakomaa/kua kiakili na anawivu wa kizembe.

Unajua, Mtu yeyote ambae hajiamini mara nyingi huvaa "wasifu" wa mtu mwingine pale anapoanza uhusiano mpya, kama ujuavyo siku hizi kabla hatujajikita kwenye uhusiano wa kimapenzi huwa tunaanza na kaurafiki fulani hivi kabla ya "date" ili kufahamiana vema sio?, sasa wakati unauliza maswali labda na kuelezea nini unapenda/taka kutoka kwa mwenza, huyo "date" anachukua yale unayopenda zaidi na kujitahidi kuwa hivyo hasa kama anahisi kakupenda au kunakitu anadhani atapata kutoka kwako.

Mfano unaposema "sipendi mwanamke/mwanume mlalamishi, mkaidi, mvivu n,k....napenda kuwa na mwanamke/mwanaume mwelevu, mpole, msafi nje na ndani, asie penda ulevi" n.k basi ujue huyo mwanamke/mwanaume atafanya vile upendavyo ili asikukose.

Mara nyingi hii sehemu ndogo ya jamii hufanikiwa kuwa na huo uhusiano lakini baada ya muda fulani mhusika (mwanamke/mwanaume) anachoka kule ku-"pretend/act" au kuvaa wasifu ambao sio yeye na badala yake anakuwa yeye kama yeye na hapo ndio utakapoanza kuona mabadiliko makubwa sana kama ulivyoshuhuida kwa mpenzi wako huyu.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa mpenzi wako anataka kufunga ndoa kwa vile rafiki zake tayari wamefungandoa yaani anafuata mkumbo kwa kujiona kuwa anaachwa nyuma, mtu kama huyo hafai kwani baadae atakusumbua sana, pili huenda anahisi kapoteza sana muda kuwa na wewe na hivyo anahofia ukimuacha hatopata tena mtu wa kuji-"commite" kwake kama wewe (ndio maana nikasema hajiamini) hivyo anatumia nguvu (ukali, ujeuri, kisirani, visasi n.k.)

Mimi naamini kuwa swala la ndoa ni maamuzi ya watu wawili hasa ukizingatia maisha tunayoendsha hivi sasa, ofcoz kimila na kidesturi mwanaume ndio anachumbia lakini baada ya hapo ninyi wote wawili ndio mnapanga,shirikiana na kuelewana lini mfunge ndoa na hiyo inategemeana na aina ya maisha mnayoishi/endesha na aina ya ndoa (sherehe) mnayoitaka.

Kuna wale wanaopenda "simple" lakini bab-Kubwa (hapa unahitaji kipato cha maana na miezi kama mitatu mpaka sita hivi kujiandaa) alafu kuna wale wanapenda kubwa na bab-Kubwa(utahitaji zaidi ya miezi sita inategemeana na kipato), wengine hutaka ndogo na ya kawaida (hii inachukua siku saba tu kitu na box).

David ulivyotoa maelezo yako hakuna mahali umegusia wewe kumpenda yeye, sito kulaumu kama ile hali ya kumpenda inapungua kutokana na matendo yake ambayo ni ya aibu sana kama mwanamke (mambo ya usawa hayo), hata hivyo kitendo chako cha kutunza namba za wanawake wengine bila kumshirikisha yeye sio kitu kizuri (wewe hapo ulikosea pia).

Lakini kama unampenda na nia yako ni kufunga nae ndoa basi nakushauri mfanye maswasiliano....zungumzeni na mwambie wazi kuwa anahitaji kubadili mwenendo wake vinginevyo uhusiano wenu utakuwa hadithi, mwambie wazi tu kuwa unampenda lakini vitendo vyake vinakukatisha tamaa na unahofia kuwa ukifunga nae ndoa bado utakwenda kutafuta amani nje....Mikwara yenye ukweli ndani yake huwa inafanya kazi.

Kisha msikilizie, kama anakupenda kwa dhati ataomba radhi na kujitahidi kubadili tabia yake mbaya, maana ya kuomba radhi ni kubadilika, kama hubadili matendo basi hakuna sababu ya kuomba msamaha.

Kila la kheri!

16 comments:

Anonymous said...

She is just too much for you. Achana naye mapema. Ukimuoa atakusumbua sana. Yaani huyo anachezea shilingi chooni. PIGA A CHINI as soon as possible.

Anonymous said...

Nikuambie ukweli rafiki. Swala la
`wife to be, or husband to be ni mchakato mrefu na wenye vikwazo mbalimbali. Wapo waliobahatika wakapita `short-cut na wakawin' na wapo wanajijutia hadi leo kwanini walioa/waliolewa, na wapo pia ambao wame
gonga ukuta.
Lakini kati ya hao unaweza ukawasikia wengine
wakisema `afadhali bwana, sikujua, kumbe nk. yote hii ni kuonyesha kuwa `kuoana na kuivana sio jambo rahisi' na maandalizi ya kumpata `mweza sio jambo rahisi.
Kitu muhimu katika kila jambo ni `subira' huyu rafiki yetu `subira' anapatikana bure, lakini tunamuogopa,wachache sana wanampenda wengi tunampapatika bwana `Pupa au papara'.
Kipindi cha wazee wetu wao walikuwa na hekima, kwani wakitaka kuoa, au kuoza huanzia kuchunguza familia historia zake, kwani tabia za watu huwa mara nyingi zinarithiana. Lakini sasa hivi ni vigumu. Kinachotakiwa ni `kuelezana ukweli', kuaminiana na kupeana muda. Kusomeshana nini maana hasa ya `ndoa', nini maana ya upendo, nini maana ya mahusiano mema. Shule zipo, vitabu vipo, na watu wapo, akina dada Dinah, watakusaidia vyema kabisa.
Wengi tulio-oa, tumepitia vikwazo hivyohivyo, na hutaamini yule ambaye ulimuoana hatafaa, baada ya kuolewa hubadilika kabisa, na wengine ambao walikuwa wanaonekana wanafaa wanageuka wanakuwa nyoka. Hiki ndio kitendawili cha ndoa, mteguaji na mwanandoa mwenyewe.
Kwa uoni wangu, kaa naye mueleze mustakabali wa maisha yako. Kubali kukosolewa, na wakati mwingine huenda yeye yupo `right' lakini wewe huelewi kwasababu ya kujiwekea vizingiti, na huenda yupo `wrong' lakini yeye haelewi, peaneni muda wa kuchuja yale mnayoelezana. Mifano dhahiri ipo, iangalieni.
Jaribu kumwambia jinsi gani unataka maisha yako yawe, naye pia atakuelezea na kama ulivyosema anapenda `kurivengi' basi naye atakutolea kubwa kuliko. Lakini usikate tamaa, msomeshe, na hatimaye atanyooka, ikishindikana `akili kichwani mwako, kwani `ndoa ni ndoana bwana na makali ya maisha yanahitaji maelewano makubwa ili muweze kujenga familia iliyotulia.
Hayo ndiyo mawazo yangu
emu-three

Anonymous said...

Mhhh yaani unaulizwa swali wakati jibu unalo david mtu mpaka anakuonyesha hivyo vitendo sasa wewe unategemea nini hapo??Yaani anataka kukuteka akili na bado hata haujamuowa sio vizuri kabisa yaani huyo hakufai kabisa maana itafikia kipindi atakuambia kwamba kanifulie chupi sasa si itakuwa mchezo huo cha muhimu kama vipi piga chini achana nae huyo hana mpango wala nini ila pia tusiseme kwamba achana nae na wewe unajua nini anakupa na nini anakulidhisha kama mimi naona achana nae hana mpango wala nini mbona mabinti wengi tu wapo wa kuoa watoto wa mafisaidi kibao wapo angaisha kichwa DAVID utafanikiwa ila hapo mimi siwezi kukushauri kabisa hakutakii mema huyo dada yangu ni hayo tu labda tumsubiri DINAH na yeye atuambie uzoefu wake....

Anonymous said...

Mkuu pole sana....!

Mimi naona huyo ni mjeuri by nature. cha kufanya wewe jifanye mkorofi sana kwa muda wa miezi 3 tu utapata majibu yako yote. Give her Harsh answers,be rude unnecesarily,act drankardness sometime and talk sencelessly. Pangilia maneno then yaongee kilevi hata km umeonja tu jifanye unalewa ila km hunywi ni tabu kidogo.Talk happily with other women in her presence...ila usifanye kweli; akikuuliza jibu hovyo.

I promise you...ukifanya hivo na yeye atadisplay habit zake to the fullest.... then u will decide "kunyoa ...hakuna kusuka hapo"

Kinyume chake kwa mwanamke mwenye akili na mapenzi ya dhati...yeye ndo ataongeza mapenzi na kuwa mpole kuliko maelezo ,kujaribu kukuhandle with care. If u miss this...give her a DAMN Drop OFF.

PD

Anonymous said...

David,
Kuachana pole,ila jaribu kuangalia kwa nini amebadilika,inawezekana anarekebishika,lakini kama ukishindwa nawa mikono,maisha ya ugomvi na kisasi hayafai..........

be careful

Anonymous said...

Kuna mtu mmoja kachangia hapo mwanzo,huyo jamaa mkali kinoma,mkali mpaka kwenye mitandao.lakini yupo right kutokana na yule mwanamke anavyomsumbua jamaa yake(mchumba wake)si ndivyo alivyosema mwenyewe. Mi pia naweza kusema the same kuwa hakufai,huo ni mwanzo tu,mwenyewe unaona,ukioa utafanyiwa mambo mpaka utajilaumu kwa nini ulioa.kuoana ni jambo kubwa na la mwisho kufanywa,likifanywa bila umakini waweza kualika msiba cku za usoni za maisha yako.tizama uoe mtu wa aina unayoona mtaenda nae sawa,kazima ajulikane wanamme nani na mwanamke nani.lakini kama anakuta namba ya cm tu na yeye anaweka namba ya mwanamme kwenye cm yake huyo c size yako.kuna siku mzee utapandwa na hasira uje upige bure.tizama cha maana cha kufanya,kama vp mwache,ila isiwe kwa kukurupuka. "Rama"

Anonymous said...

David, hapo utachemka.

Anonymous said...

ana njaa ya kuolewa tu hiyto huwa inatupata sisi wakina dada ikifika kipindi ambapo unaona unahitaji kuolewa. Kusave number za wanaume wengien ni kukubeep tu kukupa wivu ili ujiweke sawa. Ila kama unampenda unasubiria nini kuoa, kwani ukioa mwaka huu kuna tatizo gani hadi umepanga mwakani. Inawezekana alinyeneykea wee ameona mhh husemi chochote sasa imebakia mabavu ingawa sio poa.

Anonymous said...

WASICHANA WENGI TOWN WANAPENDA NDOA SABABU YA KUWAONA WENZAO WAMEOLEWA,BUT ANAKUPENDA SANA NA ATAKUJA KUJUTA,RAHA YA NDOA MWANAUME NDIO AITAKE SANA BWANA,WANAWAKE UWA TUNAJIFICHA KAMA HATUMIND SANA,ENDELEA KUMWAMBIA KWAMBA UR NOT READY YET,N IF U DONT TRUST HER,USIFUNGE NAYE NDOA,UTAKUWAUNAMLAUMU BADAE KUWA YEYE NDIO ALILAZIMISHA,KAMA ANAKUPENDA ATAKUSUBURI,NA SASA KUTOKUKUHESHIMU KAMA MWANZANO,NI SABABU AMEKUZOEA NA MAKUCHA YAKE YAMETOKA SO NI KAZI KWAKO KUNYOA AMA KUSUKA,ZAIDI YA YOTE SI NZURI KUMSHAURI MTU KUMUACHA MWENZI WAKE,BUT NYIE NDIO MPIME KAMA MTAFAA KUWA PAMOJA FOR THE REST OF YA LIFE KAMA NI WAKRISTU,KAMA NI WAISLAM HAKUNA NOMA NI TALAKA INAKUBALIKA,LAKINI KAMA UNASITA SANA USIMPOTEZEE MUDA MUAMBIANE UKWELI,NI HAYO TUU

Anonymous said...

Mimi Mkereketwa tu kaka,
Habari hii kama ni ya kweli inatisha sana!
Umefanya vyema kuliweka jambo hii wazi mapema. Wengi huwa wanadanganyika kwa kuficha na baadae wanaambulia aibu ya kuachana wakati walishaoana na kuzaa watoto.
Nivumilie nikupe stori moja ya kweli. Kuna kaka mmoja pia alikuwa na mahusiano na mwanadada, wakawa na uhusiano wa jinsi hii. Mwanaume akaamua tu kumuoa. Wakaishi kwa miaka 6. Wakazaa watoto 2. Lakini kwa kipindi hiki chote ndo yao ilikuwa inawaka moto. Mwanamke alikuwa na vurugu kibao. Mara amsingizie mmewe anatembea na watu kazini kwake. Jamaa naye akaboreka akafanya kweli, kwa sasa unaweza usielewe, inakera sana kubughudhiwa ukitoka kazini na umechoka. Nilitaka nikupatie hata mstari wa maandiko unavyosema kuhusu mke mgomvi. Basi bwana, baadae mwanamke alipogundua kikweli naye akaanza kulipiza kisasi kwa kutembea na mwanamme mwingine. Kasheshe lake ni hivi, hapa ninapoandika wameshaachana. Hwaishi pamoja tena. Watoto wamewapeleka kwa ndugu kwa vile mwanaume yuko busy. Hebu jiulize, kwanini uoane na mtu halafu mje mmpate watoto/viumbe watakatifu wa Mungu halafu mje muwafanye waishi maisha ya shida?
Kwa ujmla mimi nakushauri uachane naye. Unavyofikiria ni sahihi kabisa. Mkioana bwana watu mnazoeana sana. Unamjibu mtu bila wasiwasi. Sasa kama ameanza mapema hivyo, una hatari sana baadae. Usije ukadhani nakkutisha, ndio ukweli huo. Utalia bila kupigwa. Inauma sana kuachana. Inauma sana kuishi bila amani. Zaidi sana inauma ukigundua mke wako anachezewa na mwanamme mwingine. Usilazimishe.
Naomba niishie hapa.
Mkereketwa tu.

SIMON KITURURU said...

Katika watu wote naowajua ambao walikuwa na machale kama wewe kabla ya ndoa, HAKUNA hata mmoja ndoa yao ILIDUMU baada ya HARUSI!Baadhi walifanikiwa mpaka kuwa na mtoto halafu ikawa full VIMADA na kukwepa kurudi NYUMBANI kabla ya DIVOSI.

LAKINI hapa Sisemi kuwa wewe na mpenzi wako ndoa haitadumu.Ila usipuuzie machale yako haya.Jaribu kuangalia kama kunauwezo wakurudisha mahusiano pale ambapo wewe na mpenzi wako mko UKURASA mmoja. Moja ya njia ni KUJADILI naye nini unafikiria kuhusu swala zima hili ligusavyo uhusiano wenu. IKISHINDIKANA usilazimishe NDOA ambayo hautaifurahia, mpenzi mpya yupo tu INGAWA hujamstukia au atapatikana tu pale HUYU mpenzi wako wa sasa atakapo kukutoka akilini.

Anonymous said...

Achana nae..anahitaji mtu wa kumcontrol kwahiyo ajua wewe ndie unafaa lkn tatizo anaharaka sasa...pasua kichwa siku zote ni wa kupigwa chini...majina yenu eidha herufi zinafatana namaanisha ab au ef nk au zinatouti ya namba moja yani kama wewe ni 5 nae ni 6 ujue kimeo icho kuhusu nyota siwezi kuelezea saana ila huyo anaonekana hakufai bro.

Anonymous said...

ushauri wangu sikiliza matakwa yake na mweleze yako ili muishi na maelewano,kama unaona hakufai jua cha kufanya,watoto na mama wa kambo baadae is too bad

Anonymous said...

NIMEJARIBU KUSOMA COMMENTS ZOTE NA KITU NILICHOGUNDUA MOST OF THE BACHELORS(MEN) WAMESHAURI DAVID AMUACHE HUYO BINTI ILA WALIO KWENYE NDOA KWELI NAWAKUBALI KWA USHAURI WAO. MAANA THEY KNOW THE MEANING OF LOVE LIFE.SIKU ZOTE KATIKA MAPENZI KUKIMBIA TATIZO SIO KUSOLVE TATIZO.DAVID KAMA KWELI UNAMPENDA HUYO DADA KAA NAYE CHINI MUELIMISHE MAANA HUYO NDIO MPENZI WAKO.MUELEKEZE KIUPOLE TU AM SURE ATAKUELEWA TU.INAWEZEKANA YEYE ANA PRESSURE AMBAZO ZINAMFANYA AWE HIVYO.MUELEWESHE TU JAMAN ATAKUELEWA TU. NA PIA MSISAHAU KUOMBA MUNGU.THATS ALL
GOOD LUCKY DAVID.

Anonymous said...

Dear all,
Nawashukuru sana kwa ushauri wenu. Nimekuwa kimya kwa muda nikifuatilia ushauri wa dada Dinah na watu mbalimbali hapa kwenye blog. Kwa kweli nimeona wengi wenu mmenishauri nimwache.

Kwa kweli mimi binafsi nilikuwa njia panda kwa muda mrefu huku nikiangalia kama ataweza kubadilika lakini kadri siku zinavyokwenda basi mambo hayanyooki. Nimeshakaa nae chini mara nyingi na kumueleza kuhusu kubadilika kwake lakini amekuwa anaitikia kwa wiki moja au siku chache then anarudi palepale. Sasa this time nimejaribu kutumia ushauri wa dinah usemao "...zungumzeni na mwambie wazi kuwa anahitaji kubadili mwenendo wake vinginevyo uhusiano wenu utakuwa hadithi, mwambie wazi tu kuwa unampenda lakini vitendo vyake vinakukatisha tamaa na unahofia kuwa ukifunga nae ndoa bado utakwenda kutafuta amani nje...". I hope this time atabadilika maana tokea nimemwambia hivyo amekuwa mpole fulani. Sasa sijui ananichora au vipi. Kitu kingine ambacho anafanya ni unywaji wa pombe kali. Mimi sipendi kabisa yeye anywe pombe kali. Zamani alinitii but later on akarudia tabia yake. Lakini tokea nimeongea nae mara ya mwisho naona hajanywa tena. Mimi nakunywa bia tu.

Kuhusu mimi kumkosea yeye, nimeshamkosea mara kadhaa "magomvi ya wenyewe kwa wenyewe" na nilishamuomba msamaha lakini tatizo anasema amenisamehe then siku zijazo anakuja kuchimbua kesi na kuianza upya. Pia ameniambia kama nikimwacha sitapata mtu ambaye atanipenda sana kama yeye alivyonipenda. Sijui kwa nini anajaribu kunitisha kwa style ya kitoto hivyo.

Let me try my best may be she will change. Si unajua tena kukimbia tatizo sio kusolve tatizo. Na mimi huyu ndie msichana niliyempenda sana. She is just 26 years old.

Thank you all for your valuable advice.

Regards,

David.

Anonymous said...

Habari ndunguz,

NAjua nimechelewa kutoa ushauri ila haya mambo yanatugusa kidogo.

the same case ilinikuta, mi ni mtu mwenye hasira sana, hivyo baada ya kuona mabadiliko pamoja na dharau kwa wingi, na mie niliamua kuwa kiburi.
Na baada ya miezi kadhaa aliweza kubadilika.

Kwa hiyo Mr David naomba utambue dawa ya jeuri ni kiburi. Sio kubembeleza, atakupanda kichwani huyo ohooo.

Najua huwa tunawapenda sana hawa madem ila sometimes inakubidi uwe strong kwa kumuonesha kuwa unaweza kuwa na mwengine anytime. Nakuhakikishia atatulia mwenyewe huyo mtoto na utoto wake.

Ni hayo tu