Nimefiwa na baba, Mpenzi kaniacha pia-Ushauri!

"Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka thelathini na tano niimeachana na mpenzi wangu karibu miezi miwili sasa, kilichopelekea tuachane ni mimi kutokuwa karibu nae pia kutofanya nae mapenzi kwa vile sikuwa najisikia kufanya hivyo na nilikuwa naona kama Dunia imenilemea kutokana na kuondokewa na Baba yangu Mzazi. Tatizo nililonalo hivi sasa ni kwamba bado nampenda na ninataka turudiane nifanye nini?"

Jawabu: Pole sana kaka yangu ka hilo lililopelekea wewe kuniandikia mimi. Nimefurahishwa na uwazi wako ktk hili. Niliposoma maelezo yako nikahisi kwamba ulikuwa unasumbuliwa na mawazo mengi kutokana na kuondokewa na mmoja kati ya watu muhimu sana ktk maisha yako, hali hiyo ilipelekea wewe kuwa na aina yua "Depression".

Sasa kabla sijakushauri nini cha kufanya ningependa ufahamu kuwa hali hiyo sasa imekwisha yaani umebadilika au niseme umepona na umekuwa wewe kama hapo awali na ndio maana swala la kutaka kutafuta suluhisho au njia ya kurudioana na mpenzi wako limekujia na umetambua kuwa wewe ndio ulikuwa sababu ya yeye kuondoka!

Ni wazi kuwa mpenzi wako hakujua kuwa wewe ulikuwa unasumbuliwa na "Depression" na kwa mawazo ya mwanamke wa kawaida ndani ya Bongo alihisi labda humpendi tena na ndio maana akaamua kujitoa kitu ambacho ktk hali halisi hakupaswa kukifanya na badala yake alipaswa kuwa mvumilivu, kukupa ushirikiano kwenye "nyanja" nyingine na sio ile ya kimwili tu.

Unajua watu tunapokea na kuchukulia matatizo kitofauti sana, kuna wale ambao wakikumbwa na tatizo kama lako huwa haliwapigi/shitua kama ilivyokutokea wewe, na hiyo inategemea zaidi na ukaribu/uhusiano kati yako na mpendwa wako ambae ni Mzee (baba'ko).

Ushauri wangu kwa kuanzia ni kujenga hali ya kujiamini tena kwa kuanza kujichanganya na marafiki (outing), jiunge "gym" au anza kufanya mazoezi ya viungo mepesi (kukimbia, push-ups n.k), soma sana vitabu vya "challenges", angalia funny movies (usiguse zinazohusu mapenzi au huzuni) au jishughulishe na mambo ya shamba, bustani hata kama ni ya maua, usafi n.k (kuwa-busy) na kamwe usipende kukaa peke yako ama kumtembelea mama yako kila wakati (atakurudisha nyuma yaani utakuwa na uzuni zaidi).

Ikitokea uko peke yako basi jitahidi kusikiliza muziki uliochangamka Mf ule wa Mr blue na Chillah wa "Nipo, nilikuwepo na nitakuwepo" au Fiesta wa Ray C au hata ule wa Ngoma zetu sijui kaimba nani au za Mr Ebbo kwanizitakuchekesha kimtindo......those kind of songs na kwa sauti ya juu (usisumbue majirani lakini).

Wakati unaendelea na utaratibu huo anza kwa kuwasiliana na mpenzi wako mara moja/mbili kwa siku (ni salamu najisni gani unamkosa na kumpenda, tafadhali usithubutu ukagusia tatizo lako) Kisha mambo yakiwa "swafi"(baada ya wiki mbili mpaka tatu utakuwa umerudisha kujiamini kwako) na hapo ongeza "gia".

Pendekeza kuwa ungependa kuonana nae kwa ajili ya kinywaji mahala fulani (sio nyumbani kwako/kwake) ikiwa ni mpenzi wa maua basi si vibaya "kuibuka" na "bunch" la maua tafadhali yasiwe ya "plastic" (wanawake wengi tunapenda maua lakini si wote tunathamini maua), ili ushinde basi nunua hereni nzuri kwa ajili yake.

Natambua kuwa mkikutana utapenda kumwambia "nakupenda sana na ninataka turudiane na tupendane kama zamani" ni maneno mazuri lakini sio mwanzo mzuri, nakushauri uzungumzie mambo ya kawaida tu kama siasa, movie, muziki, jamii n.k, mtegee aanze yeye.

Mpenzi wako akijaribu kugusia mambo fulani mliyokuwa mnafanya pamoja kama wapenzi, hapo ujue umeshinda na ndio atakuwa amefungua mlango wa wewe kuomba msamaha na kumueleza ni nini haswa kilikuwa kinakufanya uwe mbali na yeye hasa pale kunako uhondo (kitandani)!

Nakutakia kila la kheri na mafanikio katika safari hiyo ya kurudiana na Mpenzi wako umpendae

Comments

Anonymous said…
Pole sana ndugu kwa kufiwa na Baba yako,sote ni wa mungu na kwake tutalejea. Kuhusu mpenzi wako mi nadhani ni suala la kumtafuta mkae mzungumze na huenda mambo yakawa kama yalilivyokua mwanzo.japo huwezi jua huyo gf wako nae kwa sasa ana mawazo gani kuhusu ww.usife moyo kuna watu ktk site hii,watasema zaidi nn ufanye kwa wakati huu,kuhakikisha unakua pamoja na gf wako. Rama
Anonymous said…
`Kupendana..' ina maana tata, inagwaje kuielezea ni rahisi. Mara nyingi utasikia mtu anamwambia mpenzi wake, `mimi nakupenda sana' na anaitamuka mdomoni kirahisi,kwa mahaba na hisia za kiukweli, lakini inapofika kwenye vitendo, hasa kwenye mitihani ya maisha, msemo huo huyeyuka kama barafu.
Ndugu yangu pole sana na mshukuru Mungu wako kwa hilo. Nasema umshukuru Mungu wako kwa hilo, kwani kuna usemi wa busara unaosema `kila jambo hutokea kwa taaswira ya kitu fulani'.
Hatua ya kwanza unayotakiwa kufanya ni kumuita huyo mpenzi wako na kumueleza hadithi yote, na kumpa muda fulani ili naye afikirie.
Hatua ya pili kama kweli mlishaujenga upendo wa kutambulika, tumia rafiki unaowaamini,au wazee wa busara, mkae muwekane sawa.
Sielewi wewe ni upande gani, yaani umwanaume au umwanamke, kwani katika maelezo yako umegusia tu kuwa wewe ni kijana. Na maana ya kijana nahisi upo kwenye 20's, na mara nyingi hapo ndipo kwenye mitihani mingi. Kwahiyi ushauri nitakaoutoa mimi utakuwa wa kijumlajumla tu.
Hebu jaribu kukumbuka, `upendo' wenu ulisheheni kwa vitu gani hasa kabla ya tukio hilo, kama ulilalaia kwenye starehe zaidi, basi alikaneni hukohuko kwenye starehe. Na kama ulilalia kwenye muonekano basi jaribi kujirudi nakujiweka katika hali inayovutia. Kama ndio kwenye ngono, basi hivyohivyo....
Lakini yote hayo yanategemea `upendo wenu', na upendo hutakikana na nyote wawili, kama kweli anakupenda, basi atakurejea. Kwasababu kilichokupata kinampata kila mtu. Na kama jamaa ameamua kukuacha katika hali kama hiyo sidhani kama `ana upendo wa kweli'
Upendo wa kweli hupimwa kipindi cha matatizo. Ukiona jamaa anakukuacha kwasababu ya `mitihani' ya kipato, misiba , magonjwa basi ujue huyo hana upendo wa kweli. Lakini huu sio ushauri wa moja kwa moja, kwani hatujui kipindi hicho mlichokuwa hamuivani, ulimfanyia nini zaidi.
Kama nilivyotangulia kusema awali, kila jambo huja kwa ishara yake, huenda huo ndio mwanzo wa kupata penzi la kweli, unachotakiwa ni kujenga subira. Unachotakiwa ni kuwa mkweli kwa mwenza wako, na kupata jibu la uhakika, kuwa kweli `unanipenda au ulikuwa wa kupass time'
Mengineyo tusubiri dada Dinah, atusaidie
mimi
emu-three
Anonymous said…
pole sana kaka,yani kwa kweli inasikitisha sana, huyo mpenzi wako hana mapenzi ya dhati ndo maana kakufanyia hivyo a good woman is always there to support her partner in good times and bad times pia. yani story yako inanigusa kweli, mimi nina mchumba wangu ambaye ilikuwa tuoane hivi karibuni lkn amepata family problems ambazo zinamfanya aamue kuahirisha kufunga ndoa mwaka huu, na mimi kweli nampenda sana nimeamua kumsubiri tu asolve matatizo ya familia yake kwanza then tutaoana mwakani, kaka yangu kusema kweli imekuwa kama gumzo sasa kwa baadhi ya ndg na rafik wakiona kama jamaa anazingua lkn si kweli ana matatizo ambayo ni sensitive.wengine wanadiriki hata kusema kuna wanaume wapo wanatafuta wachumba wa kuoa waniunganishe lkn mimi nimekataa maana nampenda sana mpenzi wangu na tumetoka mbali sana ntasubiri tu. kwaiyo naweza kusema huyo mpenzi wako si ajabu amepata ushawishi toka kwa marafik au ndg zake ndo maana kaamua kufanya hivyo. jaribu kumwita uombe uzungumze nae umweleshe kwamba wewe si kusudio lako lkn ni kutokana na uchungu wa kufiwa imepelekea kutokuwa nae karibu. kama ataendelea kukataa hakutaki basi itakuwa huyo Mungu hakupanga awe wako kaza moyo utapata mwingine tu,kila la heri kaka yangu.
linah
Anonymous said…
kaka pole sana jamani.. ndio mambo ya dunia hayo,kufa kuliumbwa kwa ajili yetu sisi wanadamu,na hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kila jambo,ila kinacho nishangaza hapo ni huyo mpenzi wako.. jee? unauhakika amekuacha kwa sababu hizo ulizosema na si nyingine!!wakati wa shida ndo mzuri wa kumjua mpenzi na rafiki wa kweli nadhani huyo alikuwa hana mapenzi ya kweli kwako.dont rush things jaribu kutulia kwanza..lily.Arusha.
Anonymous said…
Kama huyu msichana alishindwa kumliwaza mwenzie akijua amefikwa na tatizo kubwa then sio mzuri maana kila mwanaadamu anaumia kwa namna yake sasa na mpenzi wako anapaswa kuwa wakwanza kukuliwaza na akijua unamhitaji sasa sijui ilikuaje lakini yeye ndio anaeweza kupima na akaona lipi ni bora hapo......