Ushuhuda!

"Dinah mambo vipi? pole na kazi sijui utakuwa unanikumbuka mimi......(Dinah kaifadhi jina kulinda utu wako) nilishawahi kuomba ushauri kwako na nimefanikiwa nashukuru sana. .DINAH nashukuru sana yani ilikuwa kama kumsukuma mlevi juu ya daraja nitakualika kwenye wedding yangu.kila la kheri kazi njema"


Nimefurahi sana kwa kuwa umefanikiwa kupitia D'hicious na ukachukua wasaa kuja kunipa "ze auti kam", lakini nasikitika sitoweza kufanya vile ulivyo omba (nime-edit kulinda utu wako) kwasababau watu wengine wenye tatizo kama hilo wanaweza kujifunza mbinu-mbili tatu ili kufanikisha mambo yao fulani sio, sasa nitakachofanya ni kurekebisha kidogo tu, lakini sio kuiondoa topic nzima.

Nakuhakikishia kuwa wanawake "tukishafika bei" hasa baada ya urafiki ku-turn romance huwa inakuwa ngumu san akushawishika, hivyo hata wakijaribu vipi hakuna atakae weza kumuondoa Sisy duu wako ubavuni mwako.

Focus on your love relationship and have fun......wengine achana nao, wala wasikupunguzie kujiamini kwenu kwenye uhusiano wenu.

Unajua, unapo-share tatizo unapaswa kutambua kuwa sio wewe tu unaekabiliana nalo, wapo wengi ila wewe ndio umekuwa na moyo wa kuwa wazi na kujiamini nakuja kuliweka hapa. nakuhakikishia kuna wengi ambao walifaidika na maelezo yako na pia watakuwa wamefaidika namajibu yaliyotolewa hapa.

Comments

Anonymous said…
Hongera sana kwa kufanikiwa dada Dinah ni kiboko na wengi wanafanikiwa sema huwa hawarudi kusema kama walifanikiwa ila mimi namkubali sana huyu dada.
Poa sana.Unajua kuna ile mameni tunasema kupigwa mabuti ni kawaida kwa wanaume.Wengine hapa tumeshapigwa mabuti mpaka nimeona kawaida.

Sijui nizoee vibuti au? na mpaka lini?
Anonymous said…
Egidio, kwanini upigwe `vibuti' wakati dada Dinah, yupo, mwaga sera zako upate ushauri, na dada Dinah, hakudai chochote zaidi ya `ushuhuda' kama ukipenda, huenda nasi tukaneemeka na hilo.
Unajua kila mtu anatatizo lake, lakini unaweza usilikumbuke kulisema, au unasita kulisema lakini akiuliza huyu au yule ndipo unagundua kuwa `kumbe' na mimi nina tatizo hilo....
emu-three