Friday, 13 June 2008

Mpenzi apendae Familia/Rafiki zake!

Natumai unakumbuka tulipoanzia sio? Hujambo lakini mpendwa?

Nilitoa malezo ya jinsi ya kumshawishi mpenzi ampenade mpira ili atangaze ndoa mara baada ya kuwa ktk uhusino kwa zaidi ya mwaka na haonyeshi dalili yeyote ya kufanya hivyo.

Kwa kawaida sote tunapenda familia zetu kuliko kitu kingine katk maisha yetu na baadhi hupenda nakujali pia marafiki zao kama watu wao wakaribu. Ukiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu wa aina hii unatakiwa kuwa mwanaglifu sana vinginevyo utapoteza mwenza na penzi kufa kabisa.

Kwanza unachotakiwa kukumbuka ni kuwa wewe ni mtu amabe amekupenda ukubwani lakini familia na rafiki zake aliwapenda tangu anakua na upendo kati ya wewe na familia/rafiki unatofautiana japo kuwa unaweza kuhisi kuwa wanapendwa nakujaaliwa zaidi au pengine unaweza kudhani kuwa wewe ndio unapendwa/penda zaidi ya ndugu/rafiki zake kwa vile tu unachangia mambo mengi yaukubwani na yeye yalakini ktk hali halisi si hivyo.

Usisahau kuwa wewe ni mtu baki na utabaki kuwa mtu baki kwamba wakati wowote unaweza ukamtenda mwenzio au kuamua kuachana nae kwa sababu zozote zile lakini familia yako wakati wote itabaki kuwa familia yake hata wakimtenda vipi kwa vile wamechangia damu.

Sasa mpenzi mwenye kupenda watu wake (familia na marafiki zaidi) anashawishika kirahisi sana japokuwa itakuwa ngumu sana kwako kwani wakati mwingine unaweza kujihisi mpweke ndani ya uhusiano.

Unachotakiwa kufanya ni kujiandaa kupendwa na kuchukiwa (kumpendwa na yeye haina maana na ndugu zake watakupenda au wewe kuwapenda), kila mtu anahitilafu nakasoro zake hali inayotufanya tuwe tofauti hapa Duniani. Hivyo unachopaswa kufanya ni kujenga heshima kwa watu ambao ni muhimu wa mpenzi wako hilo moja.

Pili, epuka kujipendekeza na kuachia ule ushemeji-shemeji, wifi-wifi uvuke mipaka, wazazi wake waite mama na baba badala ya mama/baba'ko au jaribu kutumia mzee na Bi'mkubwa......wakatimwingine huwa wanamajina yao kama vile mama Haruna (jina la mumewe ambae ni future ba'mkwe)

Tatu, mpenzi anapokuja na malalamiko kuhusu watu wake hao (vijimambo vya kifamilia) ambao wewe unajua wazi kuwa anawazimia kinamna, msikilize kwa makini na wakati huohuo tafakari kabla hujatoa maoni yako kutokana na tukio. Hapa unatakiwa kuwa na uwezo wa kuelewa na kuchambua mambo haraka au angalau jaribu kuwa msikivu na muelewa mzuri.


Epuka kuungana, kumcheka, shangaa au kupingana nae ikiwa ataonyesha kutofurahishwa na mama au baba'ke au ndugu zake wengine na badala yake jaribu kumpa mawazo ya nini cha kufanya kwa mapenzi na upole.

Ikiwa haelewi kutokana na hasira zake basi tumia "tekiniki" za kumpunguzia "stress" au hasira(natumai unazijua) ili a-calm down, hiyo itawasaidia nyote wawili kuzungumza na kuelewana.

Siku ikipita na mpenzi hajazungumzia tukio la jana lilikomkasirisha usianzishe tena kwani huo utakuwa umbea sasa....wewe tulizana akianzisha kwa kukupa matokeo ikiwa alifanyia kazi ushauri wako hiyo bonus vinginevyo "uchubue" tu usizungumzie yaliyopita kwani hayakuhusu wewe bali yeye na wazazi wake, umetoa ushaui basi jua kazi yako imekwisha.

Haya niliyokuambia hapa ukichanganya na mengine niliyokuambia huko nyuma na bado ndoa haitangazwi? Huyo hana mpango wa kuwa na wewe kama mke......anza mbele.

Kila la kheri.

5 comments:

Savimbi said...

aminia dina naona hakuna kulala we mkali haya mama leta mambo i trust you mbayaaaaa

Anonymous said...

Dada dina mm naomba contact zako ikiwemo email na number ya simu plz.
reply by louty@hotmail.com

take care

Anonymous said...

mada ya leo, imenigusa, maan nina BF wangu ambae anaishi maisha ya kuwa na washikaji zake muda mwingii, kulala ghetto zao anapojisikia, nao wao kuja kwake wanapotaka. Sasa yupo na mie na hiyo huwa inanikera sana, ingawa tunapendana, lakini naona kama inatunyima muda wa kuwa pamoja. Nikaamua kukubali situation na kuwa nao wanapokuwepo, ila saa kosa nisicheke wakichekesha, nisipendeze, anapata wivu. Nadhani hiyo ni kama hapo uliposema dina ushemeji shemeji
Nawaza je tukiwa tumefika stage ya kuowana itabadilika ama itabakia ilivyo, maana umri ndo unaelekea huko?
kwa wanaume waliopitia maisha hayo na wameowa sasa naomba mnisaidie je mnaishi kama zamani au ilikuchukua muda gani kubadilika? Ama kwa wanawake waliopata wanaume walioishi maisha ya namna hiyo ilikuwaje walipo waowa?

Anonymous said...

Dada Dinah, kabla sijasema lolote kuhusu hii mada, ningependa kuuliza swali moja ambalo niliulizwa nikashindwa kulijibu.
Je katika hali halisi ya hisia na mapenzi, ni kweli ikifikia umri fulani wanawake wanakuwa hawana tena hisia ya kufanya mapenzi?
Kwa wanaume najua hisia haiishi, labda hupungua nguvu tu! Swali langu ni kwa wanawake.
Je hii husababishwa na `maumbile ' au uchomvu tu ,au ukosefu wa mazoezi. Na je hamna njia ya kuiendeleza hiyo hamu isiishe?
Kuhusu kuipenda familia uliyoikuta, ni vyema, na kwa ushauri wangu, wewe unapofika kwenye familia ya mume, au ya mke ni vyema ukajenga subira. Ni kweli kuna mambo mengine yanakera au huyapendi kwa sababu zako hizi au zile. Kinachotakiwa ni `kuvumiliana' na kujenga subira.
Inashangaza wengine wakifika kwenye familia `ngeni' wanataka kujionyesha wao ndio `wadhungu' au mambo waliyokuta pale ni ya `kishamba' Huenda, ikawa kweli, lakini mabadiliko yanatakiwa kwa utarataibu na kimahesabu...oh, sijui nimeenda nje ya mada?
mimi
emu-three

Anonymous said...

Nimwguswa na coment ya Annony 7:51.

Naomba nisemee hapo.... ni hatari sana kwa mwanamke kuchukia rafiki za boyfriend wake! na tena ni hatari zaidi kwake kumzuia bf wake kuwa nao!!! Kumbuka hao washkaji zake ndo walikupa wewe credit ndo jamaa akapiga step kukumaintain.Wakikuchukia blv me kwa mwanaume anayependa rafiki zake utaachika tu!
kwa hao washkaji ndo anapata dili,ndo anabadilishia kazi,ndo anapata faraja abt hard situations. "Value it" Nafasi yako iko palepale... kwa nini unaona wivu?wangekuwa wanawake kama wewe si ungewapiga? na tena wakati unamfahamu ulimkuta na hao washkaji? Nina mifano mingi ya walioachika kwa hii tabia. PD