Tuesday, 3 June 2008

Anatosa wengi, Je atanikubali mimi?....ushauri!

"DINAH MIMI NAKUKUBALI KULIKO HATA MAELEZO NA NIME... DINAH MIMI NAKUKUBALI KULIKO HATA MAELEZO NA NIMEKUWA nikifuatilia blog yakO 4 long time lakini nimeona niombe msaada wako na naamini Utanisaidia, sasa dada yangu mimi nasoma chuo kikuu ughaibuni.lakini kuna mtoto nampenda sana, tuna miaka miwili tangu tujiunge na chuo ,lakini sasa huyu mtoto mimi sijawahi kunwambia kwamba nampenda ila mara nyingi nimekuwa namtembelea na kuongea naye mambo ya kawaida ila yeye ashajua kuwa namtaka .sasa dada yangu naogopa kumwambia manake ameshawa tosa watu kama watatu lakini hawa wote ni wa mwaka wa kwanza ambao walimkuta sasa DINNAH naomba ushauri wako manake watu wa nchi nyingine wanaweza kumbeba.NITASHUKURU KAMA UTANISAIDIA,KAZI NJEMA!!"

Jawabu:Acha uoga, hao aliowatosa huenda hawamvutii au yeye hawapendi, sote tuko hivyo kwamba ukitokewa na mtu hakuvutii,hana viwango (hehehehehe) au huna hisia hata za kirafiki unamtosa tu mpaka utakapotokewa na yule roho inapenda au kemikali zake zinakubaliana na zako.

Pia inawezekana huyu binti ana-focus kwenye masomo zaidi na urafiki wa kawaida tu sio wa "kimalavidavi" na inawezekana kabisa unapomsemesha kimapenzi anapoteza ile hali ya kukuthamini kama rafiki. Hata hivyo hayo ni mawazo yangu tu, swala muhimu hapa ni wewe kuchukua "risk" kisha mtokee kama ifuatavyo.

M-alike kwa ajili ya kinywaji au mlo wa mchana, pia unaweza ukam-alika/alika kwa ajili ya kwenda kuangalia sinema (mtokee kiughaibuni-ughaibuni) ukimtokea kibongo-bongo mambo utakosa mtoto na maji ya moto......ila kama kweli unadhani binti anakupenda (anahisia na wewe) basi toka nae kwaajili ya "movie" mwisho wa wiki hii alafu jaribu kumbusu kikawaida tu (sio denda unless ajilegeze) bila kumtongoza.

Baada ya hapo usionyeshe kuwa uko-too needy na badala yake tumia muda mwingi na marafiki zako wa kiume au kupiga kitabu, kwa vile huwa unakuwa nae time 2 time ataku-miss na kushangaa kwanini huonyeshi ule ukaribu wako kwake japokuwa ulimbusu siku ile.....(utakuwa umeshinda hapo),ukimuona msifie alivyopendeza (hata kama hajatoka hehehehe it works) baada ya hapo toka nae kwa matembezi, mfano park hivi na mkae huko mpaka kiza kitakapoingia kisha mpe busu la madaha ila usipitilize tu.

Baada ya hapo njoo uniambie......kila la kheri!

Msomaji mpenzi unaweza kuongeza ushauri wako ambao hakika utamsaidia muulizaji kufanikisha penzi lake jipya, karibuni sana.

3 comments:

Anonymous said...

Mwanaume huogopi kutoswa kwani huwezi kulazimisha penzi kama anakupenda mambo yatakuwa bomba na kama akikukata basi endeleza urafiki mlionao. ndio maisha hayo sometimes unachukua risk tu.

Anonymous said...

Hahahhaha RICHARD usijali hivyo wangu maana hayo mabo ya kutoswa ukifikilia daaa huwezi kutongoza hata siku ukiwa na nia nae ondoa kabisa haibu na uwe serious basi chombo chako siku unazote unaambiwa kwamba mwanamke hata awe na uzuri gani hana akili za kufikiria na wanadanganyika kwa urahisi wewe ingia na gia zote utaona tu atamwagika mwenyewe...

ITEITEI said...

Pamoja na hayo epuka kumtongoza kwa style ya kumwonyesha we bab kubwa,unatoka familia bora ama una fedha.Mwonyeshe unampenda yeye kama yeye na wewe kama wewe sio kwa rasilimali au vyovyote.Kingine mweke karibu yako zaidi kwa kumshirikisha siri au mipango yako ya kimaisha alaf zungumzia suala la ndoa kisha mwombe ushauri usikie atakuambia nini je atakuwa constructive au hatojali?
Ni mimi ITEITEI