Vijana wa sasa wanaharaka sana

Tofauti na zamani vijana sasa wamekuwa wakihofia zaidi kukutana na "the one" mapema zaidi ktk maisha yao kuliko kufanya bidii na kuzingatia masomo ili ufike mahali fulani kielimu au kimaisha (kazi/biashara), natambua kufaulu mitihani sio kufaulu maisha na kufeli mitihani sio kufeli maisha ni wewe tu na mipangilio yako si ndio jamani au?


Sina hakika ni nini hasa kinapelekea mfumuko wa hawa Dogo wengi kutaka kufunga ndoa au kuwa na wapenzi ktk umri mdogo badala ya kuzingatia masomo au pengine kufurahia maisha yao kabla ya kuongeza majukumu mengine kabla hata miili na akili zao hazijakomaa.


Sio kwamba na pinga kuwa na mpenzi au kwamba huyo "the one" hayupo au hapatikani hapana, unastahili kuwa nampenzi kutokana na matakwa ya mwili wako lakini sio kwa kumsaka na kupoteza muda mwingi kwenye "sites" za kutafutia wenza, wachumba au mahusiano ya kimapenzi au maeneo ya vilabu vya usiku, hotels kubwa, maeneo mengine ya starehe.


Katika hali halisi penzi huwa halitafutwi bali hujitokeza lenyewe tu ikiwa moyo wako utampenda mhusika, sasa kitendo cha kuanza kwenda kujiandikisha kwenye hizo "sites" kutafuta wenza ktk umri wa miaka 17-24 mimi binafsi nahisi kuwa ni kujipotezea muda na kujiongezea "stress" ambazo sio za msingi kabisa kwenye maisha yako ktk umri huo mdogo.


Baadhi yao wanajitosa kwenye "dating sites" au "maeneo ya starehe ya wanaojiweza" ili kukutana na wanaume/wanawake ambao tayari wamejijenga ili yeye akiingia kwenye uhusiano huo aweze kutumia vile ambavyo mwenzake amevihangaikia na kuvitolea jasho ili mtaani wamkome, sisemi kuwa huna haki ya kutumia mali (nyumba, gari, pesa) ya mume/mke au mpenzi wako kama anakuruhusu kufanya hivyo lakini huitaji ku-focus kwenye kutafuta mpenzi mwenye aina fulani ya maisha kwani kwa kufanya hivyo sio haki.

Sasa imefikia hatua hapa nyumbani (bongo) kuwa na boyfriend au girlfriend ni lazima kama vile kula au kuoga kama sio kuvaa chupi, unakutana na vitoto vidogo ndio kwanza vimemaliza shule ya Sekondari vinahangaishana mtaani na kwenye kumbi za starehe kama sio online kutafuta "the one".

Achana na swala zima la kuhaha huku na kule kutafuta mpenzi ktk umri huo mdogo na badala yake zingatia kitabu au kazi, tunza mapato yako na furahia maisha yako na huyo "the one" muda ukifika utakutana nae tu.


Wewe unasemaje kuhusu hili?......karibu.

Comments

Anonymous said…
Dina mpenzi,
Afadhali umeliona hili nalo. Kwa kweli linatuumiza sana tukiona na tunadhani labda enzi hizo sisi tunakua tulikuwa washamba. Watoto wamechangamka hamna mfano. Wazee wanaishia kusema kuna mmomonyoko wa maadili. Wengine, wazazi, imebidi tu wakubaliane na hali ili kumfanya mtoto asiwaogope.
Tena ukitaka kuudhinana na hawa "watoto" waliochangamkia mapenzi ni kuwashauri, usitaje kitu kuwaambia waache kwanza au wasihangaikie sana hayo ili wakazanie masomo kwanza, hapo wewe ni adui. Mimi mpaka hili naliona kuwa ni pepo fulani ambalo limeingia wka vijana.
Siku hizi hata huwezi kumjua kijana wa kanisani na asiye wa kanisani ni yupi. Hata sielewi. Dini watu wamezining'iniza pembeni na ngono isiyo halali, ya nje ya ndoa ndio imepamba moto. Labda wale wenzangu wa dini, tukeemee tu kama tunavyokemea mapepo mengine. Tuwaombee vijana wetu jamani.
Sijui wengine hili wanalionaje!
Anonymous said…
wataacha tu wenyewe baada ya kugudua walikuwa wanapoteza muda ila nawahurumia ukimwi sasa ndio huo jamani elimu ni nzuri eti
Anonymous said…
Katika kuchangia `topic’ hii ya `uharaka wa vijana’ ninaweza kuilamu jamii yetu, wazazi na vijana wenyewe. Huenda lawama kubwa zikaenda kwa jamii, nikiwa na maana `udhibiti ‘ kutoka Nyanja zinazohusika.
Wanasema ukisika unavutika kuona, ukiona unatamani na hisia za kufanya zinakujia ili ujue kulikoni, sasa ukiguswa ndio hapo, nyege mpaka kwenye meno. Hii nadharia ndio inayowasukuma vijana `wafanye’ ili kuona wenyewe nini kilichopo. Mitandao, video na TVs ndizo chachu zakuwasukuma vijana wafanye hata kile kisicho-hirimu yao. `Tutajuaje kama tusipofanya’ `Damu inachemka, hisia ni kali ajabu…’
Katika nchi za wenzetu, sehemu za watu wazima zinavikwazo, yaani ili upenye uone kilichopo unahitajika kuanisha kwa kaundika namba ya passport yako au kadi zilizokubalika, ambazo zinaonyesha umri wa mlengwa. Kwa hali hiyo unawadhibiti watoto wasione kile kisichowastahili. Hapa kwetu hatuna `mitandao hiyo’!
Nikuambieni ukweli dada Dinah, kuna watu wanaonyesha picha za ngono mitaani, watoto wanaingia na hakuna mtu wa kuwazuia. Nenda `Uswahilini’ utaona haya. Serikali imeweka sheria, lakini watekelezaji ndio sisi, na tunaona haya yanatendeka, hatusemi, hata ukisema haisaidii, kwani serkali za mitaa/balozi zipo na zinajua,… unafikiri itakuwaje? Achilia majumbani kwetu ambapo watoto wana uhuru wa kuangalia kanda za kila namna, wazazi tunashinda kazini mchana kutwa.
Mzazi kama mzazi unaweza ukamjenga mtoto wako kimaadili, lakini akitoka mitaani, au kwenda shule, huko anakutana na akina `haambiwi kitu’ anasikia, anavutika na hatimaye anajaribu, na hali hii inamkomoza haraka. `Amejua lini haya’
Hii ni sababu mojawapo inayowafanya vijana waharakishe katika masuala ya `ngono, ambayo hatimaye yanawasukuma kuoa/kuolewa mapema.
Maadili hasa ya `kidini’ ndiyo yanayoweza `kumlinda’ mtoto aogope! Lakini katika jamii zetu tunazoenda nazo, maadili ya kidini yanachukuliwa kama `kitu cha ziada’ unafikiri huyu mtoto atamuogopa nani kufanya yale yasiyofanywa akiwa peke yake. Kama mtoto angejengewa mazingira ya kidini, `angeogopa’ kufanya baya kwani anajua `Mungu anamuona’ hata kama yupo peke yake.
Katika hali kama hii mazingatio mazima ya watoto katika elimu na kujiandaa kwa maisha ya baadaye yanakuwa magumu na yenye vikwazo. Achia mbali hali za kimaisha ambazo zinawafanya vijana `kutamani’ kile au hiki wakati uwezo hawana. Binti anataka simu, ataipata wapi kama hajatoa ngono kwa wenye uwezo.
Huo ndio mchango wangu kwa leo
emu-three
Anonymous said…
Vitu vidogo kama hivi ndio vinatofautisha blog yako na nyingine. Watu wengine wanafikiri hii ni blog ya porn kumbe hapa watu tunajifunza mambo mengi na siom kutiana tu.Ongeza bidii dada na Mungu akujaalie.
Anonymous said…
Hongera dada Dinah mi kwa kweli nakufagilia hasa kwa mada zako zilizo na ukweli haswa
inasikitisha sana kuona watoto wadogo wako busy na boy/girl friends badala ya kukazania mambo ya maana maishani mwao inauma zaidi watoto wengine wako primary wanafanya mambo ya ajabu sidhani kama ni kweli video,tv,internet ni vya kulaumiwa ktk hilo ila ni jamii zetu kwa kweli wazazi wamebadilika ktk malezi ya watoto wao hata ukifananisha tulivyolelewa sisi ni tofauti na wazazi ni walewale wanawaachia sana watoto mzazi gani asiyejua mwanae yuko wapi mpaka saa za usiku, jamii nayo inalea uchafu na mabaya
tuna jukumu kama jamii na wazazi tulee watoto wetu ipasavyo ni viumbe ambavyo Mungu ametuachia jukumu la kulea siku moja tutaulizwa tulifanya nini ktk kuwaharibu hawa watoto
Anonymous said…
Dada Dina,
Hapa kwa mara nyingine nakupongeza kwamba kama alivyoandika mchangijai mmoja kwamba hiyo ndio tofauti iliyopo kati ya blog yako na blog zingine.Inawezekana kabisa kwamba baadhi ya watu wanafikiri kwamba hii blog ni ya ngono, lakini ukweli ni kwamba hapa ni shule.
Nawaomba kama kuna kijana yoyote anayesoma blog hii atambue kuwa tendo la ndoa nje ya ndoa ni dhambi kwa MUNGU.
Kidunia ni hatari sana kwa maana unaweza kupata UKIMWI,mimba zisizopangiliwa na kujiharibia maisha yako ya siku za mbeleni, kama hauamini jaribu hata utakuja kujuta wakati umeshachelewa na hauna uwezo wa kubadilisha mambo.
Kwa wazazi tujue jinsi ya kuwalea watoto wetu katika misingi ya Dini.Tusiwafundishe/kukemea watoto kwa matusi, kumabako,kichwa kama shipa la shangazi yako,n.k.Kwani hapo hatufundishi ila tunaharibu.
Katika hali hii ambayo tunayo ambapo vijana/watoto wameharibika kuna wachache ambao wako katika mstari sasa jiulize kwanini hawajaharibika, jibu utalipata ukienda nyumbani kwao uone wanahishi vipi.
Tamthilia,tusiruhusu watoto waangalie tamthilia zisizo na maadili, kwa mfano tamthilia kama Isidingo au Generation zimepoteza wapenzi kabisa kwa sababu zenyewe kwa kiasi fulani zinafuata utamaduni wa muafrika.
Wakati mwingine unakuta wazazi wanaongoza kuangalia tamthilia. Kuna siku nilikuta watoto wawili wako na miaka kati ya 3-4, wanagombania kwamba mmoja amemnyonya mwenzake mdomo sasa anakataa asinyonywe na mwenzake,
INASIKITISHA SANA!!
tmajaliwa@yahoo.com