Friday, 23 May 2008

Mke wangu akerwa na Kitumbo......Ushauri!


"Dada Dinah. Naomba niweke swali langu tena hapa.Mimi nina tatizo kidogo nahitaji kusikia ushauri wako na wa wasomaji wote wa ukumbi huu mzuri.

Nina ndoa yangu kwa miaka sita sasa tuna mtoto mmoja na tunategemea mwingine Mungu akijaalia mwaka huu. Baada ya uja uzito wa kwanza tumbo la mke wangu halikurudi katika hali ya mwanzo, yaani alikuwa na kitumbo kinamna fulani. Lilipungua lakini si katika hali ya mwanzo au tuseme ya kawaida.Tumejaribu kutafuta tight ya tumbo lakini haikusaidia, ingawa labda haikuwa nzuri sana.

Sasa tukafikiri na kuona labda kabla hajajifungua safari hii tujaribu kupata utaalamu wa jinsi gani tunaweza kupunguza na ikiwezekana kurudisha tumbo lake katika hali ya kawaida, maana hata yeye mwenyewe inamnyima raha kiaina. Sasa ni njia gani nzuri za kutumia zisizokuwa na madhara kwa afya? Nitafurahi mno kusikia ushauri na kama tutafanikiwa katika hili."
Jibu: Napata matumaini kuona kuwa wewe mwanaume unaungana na tatizo linalo mkera mkeo na kutafuta namna ya kumsaidia ili ajisikie anavutia tena baada ya kujifungua (wanawake wengi hujihisi kuwa hawavutii tena) kitu ambacho ni muhimu ili kumrudishia Mkeo kujiamini kwake akiwa mtupu hali itakayo pelekea ninyi wawili mfurahie miili yenu kwa uhuru zaidi.
Upangiliaji wa mlo (diet) na mazoezi kwa ruhusa ya Dakitari wake ni muhimu kutegemeana na alivyojifungua kwamba amejifungua kwa kawaida (asilia) au kwa upasuaji.
Pamoja na kuwa kufanya mazoezi kuna-sound rahisi mama wengi hushishwa kuyafanya kutokana na uchovu au kuwa na shughuli nyingi zinazohusiana na swala zima la kuwa mama.
Kabla hajaanza mazoezi ya kupunguza na kulikaza tumbo lake baada ya kujifungua atapaswa kulifunga (kiasili au kibongo-bongo) na vilevile kujitahidi kupunguza unene ulioongezeka kutokana na ujauzito na anaweza kufanya hivyo kwa kufanya mazoezi ya kukimbia, kuruka kamba, kutembea haraka-haraka n.k alafu baada ya kupunguza unene ndio afanye mazoezi niliyoyaelezea kwenye topic hii Mazoezi ya tumbo. Kila la kheri ktk kumpokea mtoto mpya.

8 comments:

Anonymous said...

Alichelewa kuligunga mara alipofifungua au hakuwa akiikaza ile khanga au kitambaa kwani inahitaji moyo sana kukaa na mkazo wa tumbo kwa miezi mitatu. Mwambie asirudie tena kosa hilo na mamabo yatakuwa mzuri akijifungua tena.

Mpenzi wa blog said...

Yeye hapenzi au wewe ndio hupendi? Dinah aliwaambiaga mkiamua kuzaa mnatakiwa kuwa tayari kukabiliana na mabadiliko ya kisaikolojia na kimwili na hili ndio la kimwili alilokuwa akimaanisha. Tumsubiri tuone anashauri vipi.

Mimy said...

ndio matunda ya kuwa mama hayo.

Anonymous said...

mawazo yangu ni kwamba atakapo jifungua tuu, afunge tumbo kwa kutumia kanga ama kama anavyakisasa atumie. Muhimu kujua na kukumbuka ni kwamba maziwa ya mtoto yanaletwa na vyakula vya maji maji na sio mlo mwingi wa kujaza tumbo. Hapo ndo tunapokosea. Ikiwezekana aponde vyakula, na ale kidogo dogo, yaani kila atakapo sikia nja anakula ila kiasi. Matunda,Maji kwa wingi, chai na supu sizizo na mafuta mengii. ikiwezekana anatoa ile leyer ya mafuta kabisa. Na tumbo afunge kabla hajala, asubuhi alale naloo tu, akubali kero ya kulala na kanga tumboni. Kial siku unaongea kukaza kufunga tumbo tratibu ukikosea wiki za mwanzoni ndo umejiharibia, vumilia hata kama maumivuuuu. Na kwa mume uwe suppotive kwake, maan process zote zinakera.

Anonymous said...

jamani, ndio maana wazungu wameleta hizi technologia za tummy tuck. Bwana wee, mwanamke akishazaa, hata ufanyeje, mabadiliko ya kimwili huwezi kujarudisha kama kabla haujazaa 100%. Kina mama wako kwenye loosing side kwa sababu, kina baba wao hawabadiliki bali kwa ulaji mzuri au bia lakini kina mama hata kama mtoto ni mmoja tu, basi mabadilizo kwenye matiti, kama amenyonyesha, tumbo (mistari mistari- strech marks) zisizoisha, na hii (kwa upande wangu)ndio sababu haswa ya wanaume kuanza kukodoa kodoa macho nje ya ndoa. Nakuanza kutembea na watoto wa shule etc

Dinah said...

Anony@3:06 nashukuru ila naomba kuongezea ili kutowachanganya watuw engine.

Wanawake wanaofanya tummy tuck ni wavivu na wanataka matokeo ya haraka na wengi wao ni wenye pesa au shughuli zao sinahusisha muonekani zaidi (wanamitindo/wacheza sinema) au watu wa kawaida wanaiga utamaduni wa Celebs.

Kwani mara tu baada ya kuzaa na kuanza mazoezi mazito ili kupunguza unene ulioongezeka baada ya kujifungua na kukaza misuli ya tumbo sio lelemama, yataka moyo kwani kwa upande mwingine ni kama mateso na hapo ndio wamama wengi wanaamua kujiachia tu by the time wanahisi wako na nguvu/nafasi ya kufanya hivyo inakuwa too late.

Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa ukilifunga tumbo lako vema katika kipindi cha wiki sita tangu umejifungua na baada ya Arobaini kufanya mazoezi ya kufa mtu mambo yanakuwa mazuri kabisa.....na ikiwa ulikuwa mtu wa mazoezi tangu ujana wako ndio inakuwa rahisi kabisa.

Asante sana Anony hapo juu kw aushirikiano wako.

Anonymous said...

Ni kweli Dinnah on ur comments on 4.54, lakini mimi naona pia wanaume wanatakiwa kuwa sensitised on the changes za wake zao baada ya kuzaa, maana kwenye maada hii tunapicture mwanamke aliyezaa kwa njia ya kawaida, lakini kama ameingia C section, unakuta sheria ya kwanza kutoka kwa doctor ni 'kutojishughulisha katika mazoezi hata kazi za nyumbani kwa muda fulani' na baada ya kupona mara nyingi operation za kwetu ni mstari uliokatwa kutoka kwenye kituvu kwenda chini, yaani hata kama mama amepona, hilo jeraha - kwa kusema kweli kabisa ' halivutii' and she is a young mum.
Na kwa kina mama waliojifungua kwa njia ya kawaida, matiti yao huwa yanaonekana yamemwea hata kama wanafanya mazoezi na pia mistari(stretch marks) ya matiti,tumbo wakati wa kubeba mimba mara nyingi haiishi hata kama wakitumia cream. Ni kweli huo ni uzazi - YOU GAIN ONE THING AND LOSE ANOTHER - LAKINI KINA BABA WANATAKIWA KUFUNDISHWA NA KUWATAYARI KUHUSU MABADILIKO HAYO -la sivyo hiyo shock ndio kiini cha kuteleza.

Anonymous said...

samahani natoka nje ya mada,ila hiyo picha imenihamasisha natamani nibebe mimba fasta,inaonekana jamaa anajali kweli,wanaume wengine hata muda na kushika shika matumbo ya wake zao hamna.