Monday, 19 May 2008

Mam'mkwe hanipendi je niolewe?...Ushauri

kelly said..."Habarini za saa hizi wadau wote wa dinah.... mimi jamani nina jambo linanitatiza ningependa dinah na wadau wengine mnisaidie, kama nimetoka nje ya mada basi mnisamehe bure.... mimi nina mchumba uhusiano wetu mpk leo unamiaka minne,mwaka wa tatu nilivalishwa pete sasa tatizo ni kuwa mchumba wangu hataki nionane na mama yake kwa madai mama yake mkorofi ila ndugu wengine wote nawajua nawananijua na wanataka tuoane hata kesho,kwetu pia anajulikana.

Yeye anaishi kwao na mimi naishi kwetu na kila siku tunaonana na weekend tunashinda wote.... ila linapokuja swala la mama yake yupo sehemu fulani basi hatutaenda hiyo sehemu ili tu nisionane na mama yake.... sasa wadau kama jamaa anataka niwe mkewe itakuwaje hapo?


Nilishaambiwa na wifi zangu kuwa mama yake hanipendi,na yeye ndio kipenzi cha mama yake,siku moja nilimwambia kama mama yako akikataa tusioane itakuwaje akasema ooh atake asitake mimi nikishajipanga nakuoa yeye shauri yake.

Kwa upande wangu mimi sitaki kuoana nae kama mzazi wake huyo hatokuwa radhi na pia sikotayari kumpoteza kwa vile nampenda sana..... wadau na dinah naomba msaada wenu wa mawazo kama nitakuwa sijaeleweka niulizeni nitawafafanulia pale ambapo hamjanielewa nawapenda wadau wote wa dinah "

11 comments:

Anonymous said...

Sio kila ndo unazoziona mjini basi unafikiri zote wazazi waliridhia.. hapana. Wakati mwingine inatokea hivyo. Huwezi kumwacha mchumba eti kisa mama hakupendi. (ingawa hujaeleza huyo mama hakupendi kivipi wakati hamjawahi kuonana). Mama sie mnaekwenda kuishi nae, au mkioana pia utaishi ukweni? Anyway nyie kama mnapendana oaeni tu kama kila mmoja ameridhia. Hayo mambo ya mama yatakuja kujisort out mbele ya safari! Ebo...

Anonymous said...

Dada yangu mpendwa, mwenye maamuzi na anayetakiwa kuwa ni msimamo ni huyo mpenzi wako. Yeye ndio anamjua mama yake. Kama mwenywe kaamua muoane hat akama mama yake hakupendi wewe ndio choice yake sio ya mama yake. Ukumbuke kuwa unaolewa na huyo Jamaa sio mama yake, wala isikupe presha maana mama mkwe akiona mwanae ana msimamo na kaamua kukuoa hatakuwa na choice zaidi ya yeye kukukubali. Naamini its just a matter of time mama mkwe atabadilika. Hii nakuambia maana nimepitia huko, na mama mkwe alikuwa hanipendi maana sisi sio kabila moja, lakini baada ya ndoa nakuzaa mtoto mmoja, ndio nimegeuka kuwa kipenzi chake hata watoto wake wakike anawasahau.Usife moyo dada, u need to strong its not easy. I have been there najua jinsi gani inauma.
Good luck!

Anonymous said...

Mimi ushauri wangu kuwa wewe fata yako achananae huyo mama wamama wengine wanakuwa wameshanganyikiwa na maisha kwa hiyo watakuchanganye mpaka ukashindwa kufanya vitu vyako vya muhimu mimi ushauri wangu ni kuwa wewe usijali kabisa kama mdau alivyosema hapo juu kuwa sio ndoa zote zilikubaliwa na wazazi la hasha!! haikuwa hivyo bali inabidi na wewe ujipendekeze kwa huyo mama ndivyo inavyobidi kwenda saa zingine unamnunulia kitu ambacho ataweza kufulahi na pia ningekusaidia kwa undani zaidi ufanyeje ili aweze kukupenda lakini sitoweza kwa sababu umesema kimkato yaani hujasema kwamba hakupendi kwa nini na hajawahi kukuona hilo ndio tatizo kubwa zaidi>>>>ok lakini kama utasema kwa nini hakupendi zaidi naweza kukusaidia zaidi maana hata mimi kwa girlfriend wangu nilikuwa hivyo hivyo wazazi wake hawanipendi lakini ilibidi nimzidi akili zaidi mpaka mambo yakawa sawa kabisa na sasa hivi nakwenda kama nyumbani kwetu hivi kumbe kwa wakwe zangu.

Anonymous said...

DUH HII NIMEIPATA LEO POWER BREAKFAST,ETI UKO KTK MAISHA YA NDOA(umeoa/olewa)halafu MAMA YAKO AKAFALL IN LOVE NA BABA YA MKEO NA WOTE WAKO SINGLE NA WAKAANZA MAPENZI MOTO MOTO JE HII NI SAHIHI?JE UTAFANYAJE?

kelly said...

Nakushukuru dinah kwa ku-post swali langu nimeweza kupata ufumbuzi wa tatizo langu na sasa naweza kuwa na amani upya.

Wadau wote mlio nishauri nawashukuru sana kweli mmenipa nguvu mpya maana nilikuwa sielewi itakuwaje huko mbele ya safari,nawapenda wadau wote wa Dinahicious

Dinah ur the best tuko pamoja galfriend!

Anonymous said...

POLE SANA,DEAR
WEWE FANYA MAAMUZI YAKO.ILA WA MAMA WAKWE WANA TABU SANA.MIE PIA MAMA MKWE WANGU HAKUNIPENDA KABISA.NA ANINISUMBUA SANA KILA ZURI NALOMFANYIA ANAHISI NAJIKOMBA.YANI HATA ZAWADI NIKIMPELEKEA ANAANZA KUIKOSOA MIE HII HUWA SIIPENDI KWA VILE NI ZAWADI TU.
NA MUME WANGU NI MTOTO WA MWISHO.NI KAMA ANANYONYA.
MAMA MKWE AKIJA KUNITEMEBELEA MUME AKIINGIA TOKA MATEMBEZI ANAMKIMBILIA KU HUG, NA CHAI ANATAKA KUMPA YEYE,NA VIATU ANAMVUA. NI MASHINDANO.J2 TUKICHELEWA CHUMBANI TUNAKULA URODA ANAGONGA,JAMANI MWANANGU HAPEWI CHAI?????N.K
C.L.V.

Anonymous said...

Duu anony 12:38 ma mkwe wako kiboko!

Dinah said...

Kelly nafurahi kuwa wasomaji wangu hapa wamekupatia ushauri ambao umekufumbua au kusaidia kufanya uamuzi mzuri.

Mimi binafsi ninegepnda kuongezea kidogo tu kwani mengi yamekwisha semwa na wachangiaji wengine hapo juu.

Mam'mkwe au mawifi kuingilia kati uhusiano wa kimapenzi inatokea kila mahali au niseme kwenye kila uhusiano hapa duniani hasa kama kaka huyo ni wa kwanza au wa mwisho kuzaliwa kwao kama sio mwanaume/mtoto pekee ktk familia husika

Hii inasababishwa nakuwa too protective (mtoto kwa mama hakui) na kutojiamini kwa wanawake ktk failia husika (mama na dada zake) mara nyingi wanahisi kuchukuliwa nafasi zao na wewe (mpenzi) hili linaweza kuwa ni tatizo la Kisaikolojia kwani kwa baadhi inabidi wapatie therapy ili kuondokana na tatizo hilo.

Inafurahisha kuona kuwa Mchumba wako ni mstaarabu na anakujali na wakati huohuo hataki kupoteza ukaribu wake na mama yake kwa kujitahidi kukwepesha swala zima la ninyi wanawake wawili ambao ni muhimu sana katika maisha yake, umuhimu huo unazidiana kama sio kutofautiana.

Swala muhimu kwenye uhusiano wowote ni mapenzi yenu ninyi wawili wengine hawahusiki hapo, yaani nina maana kuwa huitaji kupenda familia ya mpenzi wako bali kuwaheshimu na wakati huohuo huitaji kupendwa na familia yake bali yeye Mchumba wako.

Asante kwa suhsirikiano.

Dinah said...

Anony @7:45am, mimi sioni tatizo mama yako kumdondokea bab'mkwe wako ikiwa wote hawana wenza. Ile hali ya wao kuwa karibu kama kama "wakamwana" (wazazi wako na wa yule uliyefunganae ndoa), utu uzima wao ambao unaweza kuzuia swala zima la kukutana na watu wengine kama wapenzi (kutokana na uzee) limechangia au kurahisisha mambo.

Kupoteza mwenza haina maana basi na ile hali ya kupenda na kuvutiwa inakutoka (inategemea na mtu), lakini mimi naamini kabisa kuwa bibi na babu zetu (wajane) huwa na hisia za kimapenzi kwa watu wengine ila kwa vile wanahofia jamii ya "kibongo" kutowakubali wanaamua kutoendelea au kuweka wazi mahusiano yao ya kimapenzi na wengine wanajizeekea na kufa wakiwa wapweke....

Mama'ko na baba'ke ni ndugu by ndoa na sio kidamu hivyo attraction + chemistry kutokana na kutokuwa na damu ya aina moja inalipua hisia za kimapenzi kama ifuatavyo......

Anonymous said...

Dinah Ubarikiwe na Mungu Jinsi unavyosaidia wamama kulinda ndoa zao.

Nina shida. Miguu yangu ni myembamba sana na ni kitu huwa kinanikosesha amani kuliko. Muda wote navaa suruali ama nguo ndefu ila nikiwa na mpenzi wangu sina jinsi hivyo inanikosesha raha mno. Naombeni ushauri kama kuna jinsi ya kuongeza usafiri (mguu)

Anonymous said...

mpendwa dada yangu mimi napenda kukuchangia mada km ifuatavyo.

kwanza napenda kukueleza "dunia yangu" katika mapenzi imekosa mwelekeo kutoka na kuchukiwa na mm mkwe. hvy hvy niliolewa na mwanaume ambaye ni kipenzi cha mama. alipenda aoe mke wa kabila lake (muarabu)mwanae akanizimia mm (mwafrica). kasheshe niliyoipata baada ya kuolewa na huyo mwanaume ni kwamba alikuja akatoweka nyumbani na kuniacha na mtoto wa mwaka mmoja katikamazingira y akutatanisha (bila kugombana)toka mwaka 96 mpaka hv leo tunaishi bila mawasiliano yyt (c mm waka mtoto wake) juu ya kwamba tunaishi maeneo karibu (jirani). akiniona km kaona jini (anajitahidi kunikwepa).

ikumbukwe tulidumu ktk ufriend miaka 8 kabla ya ndoa. hv ss mtoto ana miaka 13 (beautiful baby girl)
namchomlaumu mama mkwe nilisikia kuwa alimuamuru mwanae aape kwa imani zetu za kiislamu kwamba hatokuja kwangu na mtoto kwa kuwa c radhi yake (mama) kwa kiapo kikubwa cha dini yetu (yamini)
mpaka leo bado cjapata mwanaume ambaye nilimpenda km mume wangu. ht nikifa leo ntakufa na donda kubwa rohoni juu ya mamkwe.

kwa stori hiyo kuchukiwa namama mkwe usikutizame kwa ukaribu. angalia na familia yenyewe ina imani gani, utamaduni gani.

mimmy_muathirika ktk ndoa