Friday, 2 May 2008

Hatubadiliki bali tunakua/pevuka

Sote huwa tunasikia kama sio wewe unauzoefu tayari wa kulalamikiwa na mpenzi kuwa tumebadilika. Utasikia mkizozana kidogo mwenza wako anasema "siku hizi umebadilika sana, zamani hukuwa hivi" anaweza hata akakupa mifano hai lakini wewe unaweza ukabisha kwa nguvu zote na kushangaa au kujiuliza umebadilika nini? Mbona uko vilevile tu kitabia na kimuonekanao.


Lakini katk hali halisi huwa kuna kuwa na mabadiliko makubwa sana(ukuaji), wewe huyaoni kwavile ni sehemu ya ukuaji wako hivyo unabadilika automatically bila wewe kutambua. Ukiangalia nyuma ulipokuwa teen ni tofauti na sasa ambapo uko kwenye early 20s na unapofikia late 20s utakuwa na tabia tofauti na hapo awali hali kadhalika unapofikia miaka 30, 40 na kuendelea.


Wenza wengi hugombana na kutofautiana kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa vile huwa wanategemea wapenzi wao waendelee kuwa vilevile walivyo kutana nao miaka 6 au 15 iliyopita. Hawajui kuwa inategemea zaidi umekutana nae akiwa na umri gani, ukikutana na mpenzi yuko kwenye late 20s au early 30s huwa hakuna mabadiliko......lakini kama ulioa/olewa nyote mkiwa watoto au mmoja wenu ni chini ya miaka 27 basi mimi hapo wala sina la kuongeza!

Huu ndio ukweli wa Ijumaa ya leo? Unanyongeza? basi nafasi ni yako.....

Mwisho mzuri wa wiki. XXX

4 comments:

Jay Jay said...

Sikuwahi kufikiria swala la kukua ndani ya uhusiano, huwa nasikia tu watu wakisema nakupenda, nataka kuwa na wewe masiha yangu yote tuzeeke pamoja. hapa huwa nafikiria swala la kuota mvi zaidi na kunyanzi na sio mabadiliko ya kitabia ambayo umesema kwenye topic yako. Umenifumbua macho zaidi nashukuru mama.

Anonymous said...

Ama kweli hapo umenena vyema dada Dinah, hasa kuhusu kujigundua kuwa kutokana na umri kuna mabadiliko, ambayo huenda kibindamu tusigundue, ila mwenza anaweza akahisi. Tuchukulie mfano wa umri, siku zinavyokwenda utajikuta unaitwa `mzee’, kuna wengine wanakuja juu kabisa, `mimi sio mzee wako’. Hii pia ni hali halisi hata katika mapenzi, na mahusiano yetu kwa ujumla au katika mashirikiano yetu ya kila siku.
Tunatakiwa tukubali kuwa yapo mabadiliko, na sio rahisi tukawa hivyo miaka nenda rudi. Tukitaka ushahidi hasa kwa mwanaume, utajigundua katika nguvu zako za `kudinda’ ambazo awali zilikuwa haraka lakini baada ya miaka kadhaa hasa 40’s utajikuta inachukua muda, kutegemeana na afya yako. Pia katika uharaka wa `kumwaga’ na vitu kama hivyo.
Ukiacha maumbile, hata tabia za ndani mnapokaa kwa muda mrefu mnakuwa kama ndugu, na hali ile ya `u-darling’ inamomonyoka. Inawezekana kama mlijenga tabia ya `kupetianapetiana’ mkawa mnaendelea hivyohivyo, lakini sio kwa ukasi wa mwanzo. Hii inachangiwa na `majukumu’ ya kimaisha, kuchoka kwa mwili, na `stress’ za hapa na pale. Tunatakiwa tukubali haya.
Watu wa busara wanasema umri 40’s ndipo hekima ilipo. Tulitegemea kila mtu akifikia hapo angeweza kufanya mambo yake ki-hekima zaidi. Kama ni mapenzi, basi unayafanya kitaalama, `slow’ na kwa upendo zaidi.Lakini kwa sababu hii na ile huenda katika umri wa chini hukupata muda wa kupeta/kuruka majoka, na sasa huenda umejaliwa vijisenti. Hapa wengine huwehuka na kuwatelekeza wenzao ili wapate ule mwanya wa kustarehe na dogodogo. Kwa vyovyote vile mabadiliko yatakuwepo ndani ya nyumba. Na hapo ugomvi utakuwa haushi. Kazi kwako, wewe uliyetelekezwa, kama huna utalaamu wa kumrudisha mwenzako kimapenzi utaishia kupata vidonda vya tumbo, au kulalamika na hata kuomba muachene.
Kwa ushauri wangu, mimi nafikiri kama kweli tunataka kudumisha mapenzi ya dhati, licha ya `kuaminiana’ lakini pia tujifunze `mitindo na mienendo’ na namna gani ya kuendeleza mapenzi yetu kutegemeana na umri. Usijichoshe na kukata tama haraka. ‘Aaah, umri sasa umeshaenda hayo sasa ni ya vijana. Kwa mume hapo utakuwa umemkosa kwani `uume hauzeeki. Kama dada Dinah inawezekaa ingefaa utoe darasa la ‘mahusiano’ kutegemeana na umri’. Huenda umeshalitoa, lakini kutokana na wapenzi wengi kulalamika kuwa `kwanini mwenzake amebadilika hivi baada ya kuishi naye miaka 10,20 etc.
Nahisi huenda kuna walakini katika `kutayarishana, na kushibishana’ kutokana na uchovu wa kimaisha, au kupiga bora liende. Tusifanye makosa katika mambo kama haya, eti kwasababu umri umeenda hutaki hata kujikwatu, hutaki hata kuonyesha mahaba, hupendi hata kuyaongelea masuala ya kuboresha pendo. Tutaishia kuuana, kutokuelewana na kuwaumiza watoto wetu bure. Kumbe ipo hekima yake. Pendo halina umri jamani, ila matendo yake yanabadilika tu.Pendaneni hadi mmoja wenu anapoingia kaburini.
Mimi
emu-three

Anonymous said...

hallo dina mambo vipi? mie ninatatizo langu tofauti na hii mada,unyayo wangu mgumu nifanyeje niwe na nyayo laini na mie nifurahie maisha

Dinah said...

Anony @2:02:00 PM ni rahisi sana, loweka miguu yako kwenye maji ya jito yaliyochanganywa na mafuta yeyote mzito kwa muda wa nusu saa (fanya hivyo kila jioni kabla ya kwenda kulala).

Baada ya nusu saa chukua jiwe na aanza kusungua nyayo zako zikiwa ndani ya maji (beseni/karai), alafu ikaushe na paka mafuta mazito au unaweza ukapala Lotion maalum kwa ajili ya nyayo nakisha vaa sokesi/soksi zenye "material" ya satin au nailoni kisha lala.

Hakikisha unavaa raba au viatu vya kutumbukiza zaidi kuliko vile vya wazi.

Kila la kheri.