Thursday, 17 April 2008

Unapotengana na mpenzi

Siku hizi watu tunaachana na wapenzi wetu sio kwa kwenda kufanya kazi mjini au kijiji cha pili bali nchi ya mbali bonge la hatua eeh?

Kutokana na maendeleo ya Tekinolojia na ukaribu wetu na familia tumekuwa "relaxed" pale wapenzi wetu wanapokwenda mbali nasi kwa muda mrefu tofauti na miaka hiyo, kwa mujibu wa marehemu bibi yangu (Mungu amrehemu). Zamani mwanamke ukiolewa inakuwa wewe na mumeo tu sasa anapoaga kuwa nakwenda kijiji cha pili kikazi mke anakuwa ktk hali ya huzuni na kutafuta mbinu za kumshawishi mpenzi ama waende wote au asiende kabisa huko alikoagizwa.

Na hiyo huwa nafasi pakee kwa mwanamke kuonyesha kwa mpenzi wake huyo ni jinsi gani hawezi kuishi bila yeye, jinsi nakiasi gani anamhitaji mumewe na kwamba hatoweza kabisa ku-cope na upweke.

Wakati huo mwanamke alikuwa akionyesha "affection" kwa mume wake zaidi ya siku zote pale inapojuliakana lini hasa anapaswa kuondoka na siku chache kabla mpenzi hajaondoka mwanamke akipaswa kumshawishi mume/mpenzi kutokubali kusafiri au waende wote kwa kutishia kujiua (kupanda juu ya mti....sio mrefu sana na kujiachia uanguke), kulia kila siku, kususa kula nakadhalika, lakini yote hayo yakishindikana basi mwanaume anaahidi kufupisha safari yake ili awahi kurudi kuwa na mkewe/mpenzi wake.

Mume anapokuwa mbali (kasafiri) mwanamke anajitenga kwa kutokuoga mara kwa mara, kutojipamba/remba, kutokuvaa vizuri na vilevile kutotembea/toka nje bila sababu ya msingi, yote hayo ilikuwa ni mapenzi juu ya mume wake nakujaribu kuepuka kuvutia wanaume wengine na yeye mwenyewe kushawishika na ku-cheat.

Wakati huo wote mwanamke anakuwa anajifunza mbinu mbali-mbali za kumfurahisha mume/mpenzi wake au mazoezi ya jinsi ya kumpa raha mume atakaporudi, mazoezi hayo sio kukata kiuno ktk mtindo tofauti tu bali, kucheza mbele ya mume wake (strip dance sio Umagharibi ulianza miaka ya zamani Tz),mapishi, kuimba na wakati huohuo mwanamke hutumia muda wake kuomba Dua ili mume wake arudi salama.

Wanawake wa sasa hatujishughulishi sana kwasababu tofauti kama sio wengiw etu hatujui au hatujaambiwa, vilevile ukaribu wetu na familia na maendeleo ya Tekinolojia vinachangia kutufanya tujisahau na kutokuwa wapweke as much as bibi zetu were!

Nitaendelea......

4 comments:

Anonymous said...

Hii topic, dada Dinah, nilikuwa nikiisubiria kwa hamu, lakini naona unachelewa kuimalizia, naona umetingwa na libeneke la maisha, au kale `kapaja' kanasumbua tena.
Labda nikupe dondoo za vitu ambavyo vilikuwa vinanijia kichwani kwa maulizo makubwa.
1.Mahusiano ya ndoa kati ya zamani na sasa ni yepi yaliyo bora ? Na kwanini hasa. Tujaribu kuangalia ndoa na kuvunjika kwake. Hii inasababishwa na kitu gani hasa, ni sababu ya maadili, kushindwa kuvumiliana au ndio maendeleo? Najua Wanabejin, mtasema ni kwasababu ya `kuamuka’ kwa wanawake nakupambana na `mfumo dume’
Lakini je huu ni ushujaa? Kuachana na kuvunjika kwa ndoa ni jambo jema linalothibitisha kuamuka kwa wanawake? Sijui labda tusikie kinachofuata kutoka kwa dada Dinah, naona uanelekea kuidondoa hii hoja.
2.Je katika hali hii ya sasa ambapo mke/mume anaweza akaolewa/akaoa na waume/mke wengi tofauti tofauti, tukichukulia sasa hivi ambapo `kuachana’ kumekuwa kwingi. Je ile maana ya ndoa kwa hivi leo ipo kweli? Wapo ambao wameamua kuishi bila kuoana, na wanazeeka hivihivi, hii hali hatuioni kuwa si sahihi? Je ina maana wanawake wamekosa wa kuwaoa, au wanaume ndio hawataki kuoa. Kidini sio sahihi hii inajulikana, je kiwewe unaonaje? Hebu dada Dinah endeleza topic yako nisikukwaze na maswali mengi

Mimi
emu-three

Anonymous said...

"Kazi yangu inatokanana uzoefu wangu binafsi kama Dinah,.....pamoja na kusema hivyo nakaribisha mchango wako wewe mwanamke iwe ni kwa kuuliza maswali au kwa kuchangia kile ulichojaribu na kufurahia ili na wengine tufurahi katika hili (Ngono). karibuni!."

Unajua kwa nini dada Dinah nimeamua kuyaweka haya maneno yako hadharani , ni hicho kipengele kisemacho:`...nakaribisha mchango wako wewe mwanamke...'

Aaaah, ina maana wanaume tumeingilia uwanja tusiohusika? Je kweli tulipiga hodi? mimi sikumbuki kupiga hodi...
Unajua kuna kitu kinaitwa `kitchen party' wapo wanaume wamependekeza kuwa na wao wahusike, kwasababu yale mke anayoelezewa yanamgusa na yeye pia?
Nafikiri ndio maana tulipokaribia huu uwanja wako, tukaingiwa na hamu ya kuingia ndani!
Sasa mimi ngoja nipige hodi
emu-three

Dinah said...

M3 nilitumia sentensi hiyo ili kuwafanya wanawake kuondoa aibu, wawe huru na wazi zaidi ktk kujieleza, kuuliza na kutoa ushuhuda ili sote tujifunze.

Haikuwa u-feminist. Asante sana.

Anonymous said...

dada dinah i love ua blog sana tu nakusifu kwa kazi nzuri na mungu azidi kukulinda