Naomba niweke sawa hapa naona nimechanganya baadhi ya watu, nimesema “cheating” inaweza kuokoa uhusiano wako na sio kuwa inaokoa uhusiano wako. Hapo nina maana kuwa ikitokea mpenzi wako ame-cheat haina maana ndio mwisho wa dunia, maisha yanaweza kabisa kuendelea na penzi lenu likawa limesimama imara kama mwamba na hakuna wa kuliharibu/angusha.
Huenda kuwa haijakutokea wewe au mimi, lakini kumbuka hapa hakuna wewe na mimi tu bali kuna watu wengi ambao hili limewakuta kama sio kuwatokea, mimi binafsi siku baliana na tabia hii lakini kama mwandishi wa haya mambo ni vema niangalie pande zote na kusaidia yule au huyu ili sote kwa pamoja tuishi kwa amani na furaha.
“Cheating" inapotokea kwenye uhusiano swala muhimu ni kuzungumzia kilichotokea kama unaweza kufanya hivyo siku hiyo vinginevyo unaweza kuomba nafasi (kutengana kwa muda) ili uweze kuwaza na kuwazua hatua gani uchukue na kufanya uamuzi wa busara.
Moja, Jipe muda mbali nae na huko Jiulize je unampenda mpenzi wako? Je unadhani unaweza kumuamini tena? Unafikiri unahitaji maelezo kwanini kafanya alichofanya? Unaweza kuzungumza na marafiki zako ndugu na jamaa kuhusu tukio zima lakini waombe wasikushauru bali wakupoze nakukupa matumaini kwani ushauri wao unaweza kuharibu badala ya kujenga, wakati huu unachohitaji ni kulitafakari hilo wewe kama wewe kwani ndie pekee unaempenda, unaeishi,/uliyeishi na kumjua vema mpenzi wako.
Pili, baada ya kufikiri nakutafakari ukaona mpenzi anastahili kuwa nawe basi nenda na omba maelezo ya kina kwanini kafanya alichokifanya (lazima atakuwa kesha sema mengi by now nakuomba misamaha yote) lakini msamaha kwa tafasiri yangu ni mabadiliko hivyo aliye-cheat atapaswa kuachana kabisa na mwanamke/mwanaume wa nje (unaweza ukamaliza hilo mbele ya mpenzi wako na huyo mtu wa pili), kubadili mawasiliano na kama ikiwezekana basi kazi ubadili kama sio kuhama mtaa.
Mkosaji itabidi atafute namana au njia ya kurudisha umaminifu na mapenzi kwenye ushusiano wenu. Usijilazimishe kufanya mambo amabyo unahisi yanakurudishia kumbu-kumbu ya kilichotokea hata kama hukuona lakini lazima utakuwa na hisia hizo na itakuchukua muda mrefu lakini u'll get over it.
Baadhi huwa wanajilazimishakufanya mapenzi wakihofia kuwa mpenzi ataenda tena nje, ktk hali halisi jambo kubwa kama hili likitokea na ummempa nafasi ya pili mpenzi wako huwa ana-focus kwako tu na si kwingineko.....hivyo jipe muda utakao mpaka utakapo kuwa tayari.
Wewe unaesamehewa (mkosaji) usidhani kuwa mpenzi wako atasahau haraka kama alivyosamehe hivyo unatakiwa kuwa mvumilivu na kufanya kazi ya ziana ili kurudisha uaminifu na mapenzi kwa mkeo/mumeo/mpenzio.
Tatu,Kutokana na maelezo yake ya wazi ya kwanini alifanya alichofanya lazima utahitaji kubadilika. Usibweteke kwa kudhani kuwa kwa vile yeye ni mkosaji basi ni yeye pekee ndie anapaswa kubadilika, hapana kumbuka kwenye uhusiano kunapaswa kuwa na ushirikiano ili kuufanya uhusiano huo kuwa bora (japo kuwa yeye alikuwa mbinafsi na kuchomoka nje hey umesamehe hahahaha sasa move on), wakati yeye anajitahidi ku-re-store uaminifu na mapenzi wewe pia boresha yale ambayo ulikuwa ukizembea au kutoyafanya (inategemea na sababi iliyomfanya achoropoke).
Nne, kama hali ni mbaya na mnahisi hakuna jinsi ya kuendelea na ndoa basi ni vema nyote wawili kama mtaomba msaada kwa Washauri wa ndoa kanisani na popote mnapoamini au mlipofungia ndoa, kama ni ndoa ya kiserikali basi mnaweza kujaribu Therapy ya wanandoa kwa wale ambao hawako ndoani hapa ndio huwa penye uzuri wa kutokufungana pingu za maisha kwani mtu akileta za kuleta na hakieleweki unachukua hamsini zako tu taratiiiibu (sikutumi uwe nje ya ndoa 4 life na wala sipingi ndoa ila nasema ukweli ulio wazi).
PsssT, si wanawake wengi wenye tabia hii ukilinganisha na wanaume, na ikitokea mwanamke ka-cheat mwanaume kusamehe au kuendeleza uhusiano huwa ngumu tofauti na sisi wanawake.
Mada ndefu hii.....nakuja, usichoke kuwa nami.......
Wednesday, 23 April 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



9 Wamechangia Mada, bonyeza hapa kwa mchango wako.:
Hii mada inanigusa sana, maliza kutueleza halafu nikupe kisa kilichonipata, mpaka sasa niko njia panda sijui cha kufanya.
Dina hii mada imekuja wakati muafaka kwangu. Nimekuwa na mpenzi wangu kwa miaka 3 na wala sijawahi kucheat,lakini last month ametokea mtu ambaye hatukuwa tunafahamiana lakini tukajikuta tumezama katika penzi ambalo sijawahi kulipata na linanichanganya haswaa. Lakini hatuna budi kuacha kuendelea kuridhishana maana na yeye pia ana mpenzi wake wa siku nyingi. Kwako naomba ushauri wa namna naweza kumsahau na kusahau mahaba ya muda mfupi tuliyopeana.
hey dinah
hi topic ni nzuri na i agree totally..i wa sin love with a man that i could say he could give me his kidney if i needed one ...love he was a silent killer he lied on my face and sweared through his mom hana affair while i confronted the woman n ha dtheir pics where they were together n even followed him alikataa hakuw ahiyo sehemu i cannever confuse ma man na mtu mwingine......huyo no matter what the betray was tooo much i could never forgive him n till 2day sijamsamehe kunitesa mi na mwanae for a woman katika nchi ya watu dinah unaijua uk vizuri...cheating do make other pple realize u were onthe right relationship na tena baada ya kucheat wanakuwa good husband,wife or lovers i ve seen on friends........love is unique n with its own uniqueness thats LOVE but it hurtsss(why do fools fall in love)jus a joke
good luck
mamiii
Dinah, wengine hapa ilishashindikana kuwabadili wapenzi wetu tabia. Mie nimeamua nimuangalie tu. Nimejitahidi kila ninaloweza, mwanzoni nilikuwa natumia ukali, nikaona haisaidii. Nikaamua kutumia busara ndio kabisaa.. Nimebaki namwangalia tu. Huyu wangu kila anapoenda nje baada ya siku kadhaa atakwambia siku fulani nililala na mwanamke fulani. NIkamwambia tafadhali usiwe unanieleza ujinga wako kwa sababu haunisaidii... lakini wapi! kila akitoka nje atasema nadhani huwa anaona labda nafurahia ujinga wake! hebu nisaidieni mie naona nimekaribia kuachana nae. Manake sioni badiliko, ndo kwanza hali inazidi kuwa mbaya. Akipata mwanamke mpya huwa anadiriki hata kuniambia nimpishe kwa sababu anataka kuongea nae! kwa hiyo nisije kuleta ungomvi! Hebu semeni jameni kama sio kwamba huyu mtu ana pepo!!
Kabla ya yote ningependa kuuliza swali dogo `kwanini watu wanacheat?’ Nafikiri kila mmoja atakuwa na jibu lake na kwasababu zake, wengine yamewakuta na wengine wanasikia tu kupitia kwa watu.
Hebu waulize hawo waliwahi kucheat, sababu za kufanya hivyo ni zipi, na tembelea kimwana wake ambaye labda ni `muungwana’ muulize mahusiano yao yapoje, akikujibu kiukwelikweli, unaweza kupata jibu.
Swali hili nalikumbuka wakati marehemu babu yangu yupo hai. Katika udadisi nilimuuliza kwanini watu wengine wanapenda kwenda nje ya ndoa.
‘Mjukuu wangu nikuulize swali moja, kwanini watoto wengine hupenda kula kwa watu?’ alinikazia macho akisubiri jibu kutoka kwangu. Alipoona nipo kimya aliendeleza lile swali.
‘Kama wewe umekula vizuri nyumbani ukashiba, unaweza kweli kwenda kula kwa watu, hata kama wamepika ubwabwa…’ aliniuliza tena
‘Siwezi kula kwa watu, kama nimeshiba, nitaweka wapi hicho chakula’ nilimjibu kwa haraka.
‘Haya sasa kumbe unajua. Tatizo hatutaki kujifunza kutegemea hali halisi, ubongo wetu unapenda vitu rahisi. Tatizo la kutoka nje ya ndoa ni tatizo la wanandoa wenyewe, hawashibishani’ Alisema babu.
Hatushibishani, hii ina ukweli na ni vigumu tukakubaliana kwa hili. Tutabaki kulaumu, lakini ukweli ndio huo. Wapo wanaosema `hizo ni tama za kimwili, tunaweza kuzishinda…’ Ni sawa, lakini kwanini tuzishinde kwa hisia wakati `tendo’ lipo. Kwanini tuwekani mitegoni wakati tunajua udhaifu wetu. Hili ndilo kosa letu lakusahau wajibu wetu.
Hebu mimi au wewe jiulize ni lini uliwahi kumuuliza mwenzako unataka chakula gani leo? Wote hasa akina mama watasema karibu kila siku namuuliza mwenzangu. Sasa mbona hamuulizani kuhusu hili, leo mpenzi wangu unataka mapenzi ya namna gani? Wapo watasema mimi nampa kila siku. Lakini je anashiba/unashiba, anatosheka/unatosheka, anaridhika/unaridhika au ndio kusindiliana kama gunia linavyojazwa mapumba! Ukweli hatushibishani kinavyotakiwa.
Kila kitu kina mfumo wake au sio, chakula kina mpangilio wake, huwezi kula aina moja ya chakula tu kila siku, na ndivyo ilivyo katika mapenzi/ngono, huwezi kulala kama gogo ukasubiri jamaa apande na kushuka! Ukifanya hivi hata kama mumeapishana kwa viapo vyote, majaribu ya kucheat hamutaweza kuyakwepa.
‘Mbona hakuniambia kuwa hatosheki, hataki, hapendi hivyo!’ Waaah, ulitakiwa umuulize/muulizane/au mchunguzane, mbona kwenye chakula ulimuuliza…!
Narudi lile swali langu la awali `kwanini wapendwa mnacheat?
Mimi
Emu-three
Anony @ 10:55:00 PM, hiyo hutokea mara nyingi unapokuwa kwenye ushiano wa kimapenzi ambao haujui unaenda wapi tofauti na walio kwenye ndoa au kwenye uhusaino ambao ni "commited".
Kutokana na maelezo yako inaonyesha huyu ulie-fling nae unamapenzi nae kuliko yule uliyekuwa nae kwa miaka 3, huenda ikwa ni ile hali ya "honeynoon" kwamaba kitu kipa basi unahisi unapenda kuliko.
Ikiwa unahisi na kujua (ukipenda moyo wako unajua) kuwa unampena yule wa miaka 3 basi njia pekee ya kuua uhusiano wa nje ni kuliweka wazi kwa mpenzi wako kuwa ulikuwa ama una-cheat kisha anzia hapo ku-re-store uaminifu na mapenzi yako kwake na hakikisha unabadilika mara utakaposamehewa na mpenzi wako.
Jaribu kubadilisha kibao, ingekuwa yeye anafanya ufanyavyo ungesijikiaje? Ungechukua hatua gani?
Kila la kheri.
Pole sana mamii huyo nae mpaka unamkuta yeye bado anakataa tu basi hakuwa tarayi kusamehewa na kubadilika(kuacha tabia yake chafu).
Anony @2:00:00 PM, Hiyo yako ni nzito, unasubiri nini mpaka leo? Ukiambukizwa HIV? Hakuna mtu anaweza kumbadilisha mwenzie bali mhusika ndo anabadilika akiamua kufanya hivyo au akiona sababu yakufanya hivyo.
Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa Mpenzi wako hajiamini (insecure) na vilevile anatambua wazi kuwa hata afanye uchafu gani wewe utabaki tu pale kwa vile unampenda na anajua hilo au unamtegemea kiuchumi na analijua hilo hivyo he is taking u 4 granted.
Huyo wako wala haitaji kusamehewa na wala hastahili kuwa na wewe, mimi binafsi nakushauri uanze tu mbele na kama mko kwenye ndoa yakidini na huruhusiwi kumtaliki mumeo basi nenda kiserikali, tembelea mahakama ya wilaya na wao watakusaidia kumtaliki mume wako na Mali zitagawanywa kutokana na urefu wa ndoa yenu.
Ikiwa mmeishi pamoja (kama mke na mume bila ndoa lakini) kwa zaidi ya miaka miwili na mna mtoto/watoto kisheria inahesabika kama ndoa na hivyo unakuwa na haki zote za urithi kama mke.
Usipoteze muda, maisha mafupi achana nae na kisha angalia ustaarabu mwingine. Kwa msaada wa namna ya kurudisha kujiamini kwako ili kupata mpenzi mwingine nitafute nitakusaidia kwa ushauri.
Kila la kheri.
Dinah asante kwa ushauri, mimi ndo yule anony 2:00. Uliyoyasema ni kweli kabisa 101%. huyu mtu wala si mume wangu, ninaishi nae tu huu mwaka wa 4 sasa. Lakini anayonifanyia ndo hayo. Kwanza hata sijui nasubiri nini!!! Ila kiukweli dinah, huyu bwn amenifanya nisimuamini tena mwanaume yoyote, wote nawaona washenzi tu. Nitakutafuta unisaidie ushauri wa kisaikologia ili nirudie kwenye normal.
Asante.
Post a Comment