Thursday, 17 April 2008

Hivi Limbwata kweli Ipo?

"Mimi dada Dinah, leo nataka kuja na mpya, huenda ikawa ni kero au nikuomba msaada. Si mpya kwamba ni jambo ambalo halipo, ni mpya katika uwanja huu wetu. Na huenda si mpya, umeshaligusia, ila hatukulipa kipaumbele kwasababu ni jambo lakukosa `elimu’. Na huenda sio kukosa elimu tu kwani wapo wenye elimu zao wanaliendekeza.


Tuliite ni Imani za watu fulafulani.Yupo jirani yetu ambaye tunaweza kumuita `womenizer’ au mhuni au mume mwenye pepo wa ngono. Jamaa huyu hakikatizi kitu, kila amuonaye kwake ni mzuri, na alivyo na kisimite, huwa akiomba hakosi.


Alikuwa akitamba kuwa wake kwake ni kama shati, hataki wamtawale milele ingawaje kaoa. Na cha ajabu alienda kupima ngoma hana! Mke wake ni mpole, mke toka kijijini, katulia home, kimya (kaziba masikio kwa pamba). Sasa mke wake akawa analalamika, baada ya mambo kumzidi na bahati alikuja hadi kwa my wife kuomba ushauri.


Kabla hajapewa ushauri alishakuwa na nia moja ya kwenda kutafuta `dawa ya mapenzi’-limbwata au love potion, alimwambia mke wangu ana nia hiyo.Hutaamini, kumbe licha ya mke wangu kumshauri vinginevyo, kuwa `ndoa’ ni kuvumiliana na hakuna dawa ya mapenzi inayoweza kusaidia, na huenda ikaharibu kuliko kusaidia.


Alipewa mifano ya watu mbalimbali ambao inasemekana waliwafanyia waume zao na matokeo yake yakawa kinyume chake. Lakini hakuelewa, alienda kwao mikoani na aliporudi, ndipo tulipoona mabadailiko. Hutaamini lakini ndivyo ilivyotokea.

Yule bwana akawa habanduki nyumbani, yule jamaa akawa hazungumzi na watu hasa wanawake. Hata marafiki zake ambao walikuwa wakikesha naye kwenye bar wakaanza kutilia mashaka. Kulikoni mwenzetu huyu vipi! Jamaa hutaamini hata kazi yake ya udereva wa masafa marefu akaamua kuiacha na alinzisha biashara ndogondogo karibu na nyumba yake.


Wengine waliofika kwake wanasema kawa mume-bwege. Jaribu kufikiria mtu alivyokuwa awali na sasa utafikiri ni watu wawili tofauti.Sasa dada Dinah, sio vizuri kuchimba sana undani wa huyu jamaa na mkewe, ila ndio nimekuja na hili swali jipya, huenda kuna watu wana uzoefu nalo. Huenda kuna watu ya mewakuta au jamaa zao.


Huenda hata wewe mwenyewe umeshawahi kuona, kukuta, hatuwezi kupata maoni ya jambo hili ili kuboreshana kimahusiano, kuonya au kupeana ushauri?What is `love potion’ Limbwata au neneo gani jingine sijui. Hiki ni kitu gani hasa, je kipo,? Je kinasaidia, je nini madhara yake kwa wanandoa au wapenzi? Je kinafanywaje kwa wale wanaojua, na wengi wanaoendekeza hili ni akina mama, twaomba msaada jamani." Mimi Emu-three

Jawabu: Well, mimi sina uzoefu na hili ila nimesikia na hata kuulizwa dawa ya mapenzi na nini na siku zote jibu langu ni kuwa mapenzi hayana dawa ni hisia za mtu juu yako, hazilazimishwi.

Limbwata kwa ufahamu wangu ni ushirikina na inafanyakazai kama ambavyo nguvu za giza/ushirikina unavyofanya kazi inategemea zaidi umenuia vipi (nia yako ni nini hasa when doing it).


Sasa unapomwendea mpenzi wako kwa mtoa Limbwata ni wazi kuwa humpendi na unataka kumbadilisha utakavyo wewe kwani atakapofanyiwa Limbwata atakuwa na "characture" nyingine kabisa na hatoonyesha mapenzi kwako bali atakuwa mjinga kwa kutofanya vitu ambavyo "real man does" hachezi mbali na wewe/nyumbani, haishi kukuzungumzia na kukusiafia mbele ya watu wengine, kulia nakuomba msamaha kila manapozozana, kufanya kila unachoamuru afanye n.k.


Hayo sio mapenzi kwa vile sio hisia zake juu yako na anafanya vitu sio kutoka moyoni kutokana na hisia zake ju yako bali kichwani kutoakana na ulivyo/alivochezewa/changanywa/blackmailed.
Mara nyingi hali hii inapomuishia mtu aliye-Limbwatika huwa hana mapenzi kabisa na mpenzi wake, yaani hali inakuwa mbaya kuliko ilivyokuwa awali.


Wanawake wengi wanaofanya hivi ni ama waliolewa kwa vile wanatabia njema kama wake lakini waume zao hawakuwapenda, wanawake ambao hawajiamini kiuchumi au kuendesha maisha bila mume/mwanaume, wanawake wanao Imini kuachika au kuomba Talaka ni aibu kwa jamii hivyo anaamua ku-stick kwenye ndoa yake n.k.


Hili lipo, linafanya kazi kama nguvu nyingine za giza na hufikia muda nguvu hizo zinaisha.Ushauri wangu kwa wanawake wenzangu ni kujiamini na kutolazimisha penzi, kwani hata ukim-limbwata mwenzio atafanya utakavyo lakini wewe unajua moyoni kuwa hakupendi.


Vilevile ni vema kuzingatia msemao wa kale usemao "mpende akupendae na asie kupenda achana nae".Hata kama uko kwenye ndoa na unaona wazi kuwa ndoa yako doesnt work pamoja na kujaribu kwako kote, usilazimishe omba Talaka endelea na maisha yako ukiwa huru.....mambo ya kung'ang'ania penzi wakati unajua hupendwi ni uzamani. Kunafaida gani ya kuwa mpweke ndani ya uhusiano/ndoa?

Wengine wataendelea.....Asante M3

11 comments:

Dinah said...

Well, mimi sina uzoefu na hili ila nimesikia na hata kuulizwa dawa ya mapenzi na nini na siku zote jibu langu ni kuwa mapenzi hayana dawa ni hisia za mtu juu yako, hazilazimishwi.

Limbwata kwa ufahamu wangu ni ushirikina na inafanyakazai kama ambavyo nguvu za giza/ushirikina unavyofanya kazi inategemea zaidi umenuia vipi (nia yako ni nini hasa when doing it).

Sasa unapomwendea mpenzi wako kwa mtoa Limbwata ni wazi kuwa humpendi na unataka kumbadilisha utakavyo wewe kwani atakapofanyiwa Limbwata atakuwa na "characture" nyingine kabisa na hatoonyesha mapenzi kwako bali atakuwa mjinga kwa kutofanya vitu ambavyo "real man does" hachezi mbali na wewe/nyumbani, haishi kukuzungumzia na kukusiafia mbele ya watu wengine, kulia nakuomba msamaha kila manapozozana, kufanya kila unachoamuru afanye n.k.

Hayo sio mapenzi kwa vile sio hisia zake juu yako na anafanya vitu sio kutoka moyoni kutokana na hisia zake ju yako bali kichwani kutoakana na ulivyo/alivochezewa/changanywa/blackmailed.

Mara nyingi hali hii inapomuishia mtu aliye-Limbwatika huwa hana mapenzi kabisa na mpenzi wake, yaani hali inakuwa mbaya kuliko ilivyokuwa awali.

Wanawake wengi wanaofanya hivi ni ama waliolewa kwa vile wanatabia njema kama wake lakini waume zao hawakuwapenda, wanawake ambao hawajiamini kiuchumi au kuendesha maisha bila mume/mwanaume, wanawake wanao Imini kuachika au kuomba Talaka ni aibu kwa jamii hivyo anaamua ku-stick kwenye ndoa yake n.k.

Hili lipo, linafanya kazi kama nguvu nyingine za giza na hufikia muda nguvu hizo zinaisha.

Ushauri wangu kwa wanawake wenzangu ni kujiamini na kutolazimisha penzi, kwani hata ukim-limbwata mwenzio atafanya utakavyo lakini wewe unajua moyoni kuwa hakupendi.

Vilevile ni vema kuzingatia msemao wa kale usemao "mpende akupendae na asie kupenda achana nae".

Hata kama uko kwenye ndoa na unaona wazi kuwa ndoa yako doesnt work pamoja na kujaribu kwako kote, usilazimishe omba Talaka endelea na maisha yako ukiwa huru.....mambo ya kung'ang'ania penzi wakati unajua hupendwi ni uzamani. Kunafaida gani ya kuwa mpweke ndani ya uhusiano/ndoa?

Wengine wataendelea.....Asante M3

1:19:00 AM

Babii said...

Waaapi nyie bakieni kupiga kelele tu limbwata limbwata, mwanamme ataka malezi, sio mambo ya kihuni, jamani hamumsikii Mwanahawa Ally kwenye wimbo wake wa utalijua jiji!

Hapo hakuna mzizi wala hirizi, nyie tu na upeku peku wenu, hizo zote raha tu! Huenda bibie kabla alikuwa anakosea baadhi ya mambo, ila sasa kaenda kwao kupewa mikoba na mashangazi zake na bibi zake, sasa karudi full makamuzi! Nyie hamtujui, sisi wanaume kinachotusumbuwa kitu kidogo tu, sio K wala TIGO tu peke yake, hizo zapatikana zimejaa tele!Wala tusinge hangaika kuowa, Sisi nikama watoto, mutakavyo tu treat ndivyo tutakavyo kuwa! Alokwambia mwanaume hadeki nani? Mwanaume ataka kudekezwa! Ah kinachowapa point watoto wa pwani ni jinsi wanavyo treat, ukiwaangalia figa wala sizakutisha kama watoto wakinyamwezi, wamburu n.k lakini wao wanajuwa kumuenga bwana!
Wanajuwa kuenzi, sasa kama wajuwa kudekeza kwanini nawewe usidekezwe!

Omar kopa ameimba "...na kwanini nisideke nami nadekea changu.."

Kwa hiyo wapambe angalieni yenu, hao yao yanayeya, madhali hawajaja kuwaomba mlo wala kivazi, yanini kuyatia pafuni..eti pili pili iliyoshamba,we yakuwashiani?

Acha wale raha zao, yaani hao hapo walipo hata wakishindia chumvi kwa ugali, wao waona biriani...! Mzee Yussuf kawamaliza anasema "..mtaumwa na dawa hakuna, kwa wenu upeke peke, na litawachoma.....Kwa roho zenu mbaya.."

Nisamehe sana Dinah, coz katika kitu nisichokipenda, basi ni mtu kudiscuss mapenzi ya mwengine, unless amekupa idhini!

Anonymous said...

I wish, huu ushauri wako dada Dinah, ningeliweza kuubandua mzimamzima nakumpelekea yule dada! I wish ushauri kama huu ungeliwafikia wanawake wa majumbani ambao kwa kiasi kikubwa ndio wanaoendekeza `kasumba' hii. I wish wanadamu wote mke na mume tungelielewa kuwa mapenzi hayana dawa, dawa ni wewe na yeye kushirikiana na kutatua kero zilizowazunguka. Ahsante sana.
Lakini pamoja na hayo kuna kitu kidogo ningeliomba tukiangalie, na hili huwa ninamshauri hata my wife wangu, kuwa wenzako wanapokuja kukuomnba ushauri wowote ambao unagusa `ndoa' hakikisha unakwepa kumshauri `kuachana'. Hii iwe jukumu lake mwenyewe.
Najua ndoa ni neema lakini kwa upande mwingine ndoa inaweza kuwa `shubiri' Ndoa inaweza ikawa ni uwanja wa visa, mateso na uhasama hasa pale pendo linapokosekana. Lakini hii tuichukulie kama ni moja ya mitihani. Tusikimbilie haraka kuikwepa hiyo mitihani kwa kuomba `talaka'. Kuachana ni kubaya hasa pale mkiwa mumejaliwa kupata watoto. Mnafikiri hawa `malaika’ wana kosa gani kulingana na `kutoelewana’ kwenu. Kinamna fulani mnawaathiri kiakili.
Huenda ungepambana na hiyo mitihani ungeweza kumsaidia mwenzako kutokana na janga linalomkabili. Tuelewe kuwa kila mmoja ni `mchunga, msaidizi, na mwalimu wa mwenzake' Ndio maana tumeitwa `wanadamu' yaani watoto wa baba mmoja Adamu. Sasa kwa nini huu udugu unageuka kuwa `uadui’
Sasa kwa mfano umeolewa na dume `tungi' au na dume `uzinzi' au na dume `roho' mbaya’. Hizi zote ni tabia zinazojibandika kichwani mwa watu, na zinaweza kuondoka na ukashangaa huyo dume tungi, uzinzi roho mbaya akawa dume `la Azizi'.
Kitu cha muhimu ukipata tatizo kaa na mwezako shaurianeni, ikishindikana tafuta marafiki wema kama dada Dinah, lakini chunga sana `marafiki’ wanafiki, wanaweza kuizamisha ndoa yako ukajajuta baadaye. Ikishindikana waiteni wazazi/wazee, au ombeni ushauri wa viongoz wa dini. Hapo tena kama mambo `moto’ basi huenda `sio ridhiki’ basi `talaka’ inatolewa. Hapa naongelea `wanandoa’ sio marafiki wajameni!
Limbwata sio suluhisho kama tulivyoshauriwa na dada Dinah. Hebu tusome ushauri wake kwa makini, kuna ujumbe maridhawa.
Ahsanteni
Emu-three

Anonymous said...

Hivi wadau,napenda kujua ni mara ngapi mtu unatakiwa utiane kwa mwezi ama kwa wiki.Maana nataka nipange na mpenzi wangu ili siku hizo tuzijue kwa ajili ya kupeana ujinsia.
Hebu nisaidieni kwenye hili na je ukifanya mara nyingi kuna madhara yoyote kwa sasa au hapo baadae?Maana naskia baba wa taifa alipata na mkanda wa jeshi eti kwa kua alikua anapenda sana kusex

Anonymous said...

duuh mi naomba nielimshwe maana nasikiaga tuuh hata sijui inavyo work.i don believe insuch things...but hey the more mtavyonifundisha hapa ndio ntakavyoolewa.but i wouldnt do that ..not worth it!!

kelly said...

mamboz,ni mara yangu ya kwanza kutoa comment hapa ila ni msomaji mzuri wa dina na hufanyia kazi yale nisiyoyajua.. back to the point mimi naungana na dina 1:25:00 kweli kumuwekea mumeo/mkeo/mpenzi wako limbwata ni kutojiamini pia kumbuka hiyo dawa ikiisha mambo yanakuwa mabaya maradufu utajuta utaona bora na ilivyokuwa mwanzo nimeshashuhudia wengi wanaofanya hivyo wanajuta.

Na mara nyingi wengi hukosea matokeo yake badala ya kupendwa na kufanyiwa yale anayotaka yeye ndio kwanza wanaachika wanabaki wanalia.

Ukitaka kuboresha mahusiano ni kuwa na mapenzi ya dhati na sio kutumia mizizi,na kama unaona mwenzi wako anafanya ndivyo sivyo kaa uzungumze nae kwa upole na mahabati ya nguvu natumai hiyo ndio njia bora na atabadilika.

Dinah said...

Anony @ 10:08:00 AM, kufanya ngono/mapenzi kunategemeana na uwezo wako wa kutakakufanya hivyo (sex drive yako au libido) kama iko juu na mpenzi wako iko juu basi mnaweza kufanya mara nyingi muwezavyo kwa siku.

Kwa wale wa ya kawaida basi huenda ikawa mara tatu kwa siku ndani ya wiki lakini ikiwa iko chini/ndogo huenda mara moja kwa mwezi au miezi miwili.

Huitaji kujipangia kufanya mapenzi/ngono bali unafanya kutokana na unavyojisikia (kuwa na nyege), jinsi unavyovutiwa na mpenzi wako bila kusahau jinsi unavyopenda kulifanya tendo lenyewe na kulifurahia.

Kufanya maranyingi na mume/mpenzi mmoja hakuna madhara yeyote sasa wala baadae ila kufanya mara nyingi na wapenzi tofauti kunamadhara mengi ukiachilia mbali kupata maambukizo ya zinaa pia unazeesha ngozi/mwili wako, uke wako unapanuka/tanuka na unakuwa kwenye hatari ya kupata kanza ya K au kizazi wengine wanaita.

D'hicious sio ukumbi wa Siasa hivyo kuwa mwangalifu unapoweka comment zako hakikisha zinahusu Ngono, mahusiano, ndoa, uzazi, usafi n.k.

Asante.

Anonymous said...

Naona mida ndio hiyo tukawanie usafiri, lakini nimeona maoni ya `babie said...'
Kuna hoja moja amesema kuwa hapendi mtu anayezungumzia mapenzi ya mwingine bila idhini yake. Ni kweli sio vizuri kuzungumzia maswala ya wengine bila idhini yao, sio kwa mapenzi peke yake, hata kwa maswala mengine. Lakini nia yetu hapa, au nia yangu ya kulitoa hili dukuduku ni ili liwasaidie wenye matatizo kama hayo. Huenda wewe lisikusaidie lakini wapo ambao katika kusikia hivi , hata kama alikuwa na mtizamo huo huenda akajirekebisha. Ndio maana nikaona nitumie uwanja huu wa Dada dinah, ili atusaidie, pia na wenzangu tuchangiane mawazo. Sio kusengenya....
Sikupingi, wala sikulaumu, ila nilitaka kurekebisha hako kausemi, na huenda huna nia mbaya ila kwa mtizamo wangu niliona nijisahihishe kwa hilo.

Kesho basi, usiku mwema Dinah, na nawashukuruni wote waliochangia hii kero, kwani nimeyapata mengi ambayo hata mimi nitakuwa na uwanja mpana wa kumsaidia jirani yangu, na wale wote waakaoomba msaada wa mawazo. Tusiwe wachoyo kusaidiana. Mawazo yanaweza kuwa dawa kuliko sindano au kidonge.
emu-three

Anonymous said...

Dinah mpenzi, yale mazoezi ya tumbo mbona kama nataka kuchemsha mwenzio? naona kama matokeo ni ya polepole sana. Hebu nipe motivation tena kwa kuniambia ni kwa kufanya kwa muda gani (i mean yaani after 2month) ndio nitapata matokeo mazuri. Dada usichoke kutuhabarisha!!
Natanguliza shukrani na asante kwa ushirikiano.

Dinah said...

Anony @ 5:38:00 PM, kupata matokea haraka inategemea zaidi na ukubwa wa tumbo lako, vilevile kama umekwisha wahi kuzaa (beba mimba) bila kusahau umri ulionao na fat/unene wa mwili wako.

ZOezi ni rahisi kulifikiria lakini "fat" ya eneo latumbo huwa ngumu kuondoka hasa kama umri wako ni zaidi ya miaka 30 lakini kusem ahivyo sina maana kuwa halitopungua, unaweza pia kuongeza mazoezi mengine ya ziada kama vile kukaza/punguza unene wa mikono amabyo husaidia kuondoa "fat" tumboni, unaweza ukawa unapiga Push-ups amazo pia husaidia kukaza misuli ya tumbo na wakati huohuo kuondoa "fat" sehemu ya tumbo lako hasa kule pembeni(wings).

Minimum ni a 2wks na maxmum ni 3mnth.....Kuwa na nia ya kufanya mazoezi kwa moyo wako wote ili kupunguza/kaza misuli ya tumbo sio lini tumbo litapungua.

Kila la kheri.

Anonymous said...

Huyo ndiye bablii utafikiri katiwa kibiriti! Anyway hapa ni kujadili kuhusu dawa ya mapenzi ipo au haipo. Dawa ya mapenzi ipo, yaani kumfanya mtu akupenda hata kama alikuwa hakupendi, kukufanya wewe uwe na mvuto na haiba kwake. Hapo ni kucheza na saikology, na kuna harufu fulani ambayo mwanaume akiisikia atamtaka mwanamke na kumuona anafaa kuliko wanawake wote nasikia wameitengenezea perfume ili watu wawe wanajipulizia! Hayo ni maswala ya mapenzi. Vile vile kufanya mambo ambayo yatamfanya yule unayemkusudia avutiwe nawe, hiyo ndio dawa ya mapenzi, kutafuta mbinu ya kuweza kupendana zaidi na wote hapa kati yetu tumeshafanya vitimbi kibao ili tupendwe.

Lakini hili swala lingine la Limbwata, haya sio mapenzi, huu ni uchafu, ubwana, ukora, kumfanya mtu awe mtwana wako na wewe ni bwana wake hapa ni mahusiano ya bwana na mtwana na si ya bibi na bwana! Hii si dawa ya mapenzi ni kama kumhyptonise mtu akatokwa na akili akawa kama ndondocha na kufanya kile ukitakacho. Haya si mapenzi kabisa ingawa watu wanafanya kwa kisingizio cha mapenzi. Mtu unayempenda haswa kutoka ndani ya moyo wako utataka yeye ndiye awe bwana wewe ndiye uwe mtumwa wake, utamtimizia kila akitakacho, kila alifanyalo kwako wewe ni sawa kwa sababu ya upofu ulionao kutokana na mapenzi uliyonayo kwake, utaroa, utaoza, hutaona wala kusikia, na siku ukihisi tu mapenzi yake kwako yamepungua au huyaoni hutaweza hata kuinuka kitandani, utakuwa mgonjwa, utarowa, utalia na kusaga meno. Utapata wehu fulani, hayo ndio mapenzi ni wehu na wazimu mtupu lakini ukilipata penzi ni wazimu mtamu.