Tuesday, 29 January 2008

M'naume M'namke, nani anamuhitaji mwenzie?


Wengi wetu tunazaliwa kisha kukua na kukuta baba na mama pamoja, bibi na babu pamoja, shangazi na mjomba pamoja, baba mdogo/mkubwa na mama mdogo/mkubwa pamoja na kudhani hivyo ndivyo sote tunavyotakiwa kuwa mara tunapokuwa watu wazima n.k.

Tunapoanza au jiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na baadae maisha ya ndoa (milele pamoja) tunakuja kuhisi kuwa hawezi kuishi bila wenza wetu sio kwa vile wanatulisha na kutuvisha bali tunawapenda napengine ni kwavile umri umeenda na unahofia kuwa "nani atanitaka na mikunjo hii".

Sasa wewe kama wewe unafikiri ni nani zaidi anamhitaji mwenzie zaidi?

Endelea hapa.....

Mwanaume ni mwindaji na uwindaji huo sio wa kupata kitoweo tu (pesa) bali kukupata wewe mwanamke pia, inasemekana kuwa wanaume wengi wanaamua kuwa “single” au wagumu ku-commite karne hii kwa vile wanawake hawawindiki tena.

Kwamba wanawake wamekuwa rahisi kupatikana (kukubali kirahisi) na hivyo wanaume hawahisi kama unawafaa kama wapenzi wao wa kudumu kwa vile hawakukuwinda bali ulijitega mwenyewe (kutokana na U-feminist a.k.a Ubeijing wa wanawake wengi wakidhani ni Usawa).

Hali hiyo inasababisha wanawake wengi kukata tamaa na wanaume ambao hawa-commite kwenye mahusiano ya kudumu na hivyo kuamua kuwa ile “jamii mpya ya Bi au Lesbo”, Hey sitaki kukupoteza hapa let me go to the Point.

Mwanaume anamuhitaji mwanamke zaidi kama msaidizi wake kuliko mwanamke anavyomhitaji mwanaume na sema hivyo sio kwa kuegemea swala la ngono bali kwenye maswala mengine mengi ya kimaisha.


Inasemekana kwamba wanawake ambao hawajaolewa (spinsters) wanaishi zaidi ukilinganisha na wale walio ndani ya ndoa na Wanaume waliondani ya ndoa huishi maisha marefu zaidi kuliko wale walio nje ya ndoa(bachelors), umewahi kujiuliza kwanini wataalamu wanadai hivo?

***************************************************
My only man @ Belsize area this is for you. Asante for visiting here daily even though You don’t understand much Kiswahili. I love you to death baby!xx

11 comments:

Askofu said...

Kwa mtazamo wangu kama mwanaume naona kuwa mwanaume ndiye anayemuhitaji zaidi mwanamke ili aweze kumsaidia kazi mbali mbali kama kufua, kupika na nyinginezo nyingi tu ambazo kwa mtazamo wa juu juu huchukuliwa kama shughuli za wanawake.

Huo ni mtazamo wangu tu Dinah naomba unikosoe kama sipo sahihi.

Anonymous said...

Ninani anamuhitaji mwenzake mume au mke?
Sijui dada yetu hapo ulikuwa na maana gani `kumuhitaji’
Sawa, huenda umeweka usemi huu kimtego ili kila mtu aambae kwenye miono yake, na mimi kama kawaida yangu sipendi kulaza damu.
Kwa uoni wangu, wote wanahitajiana, mume anamuhitaji mke na mke anamuhitaji mume, hii ndio asili yetu, toka enzi na enzi.

Kuhitajiana kwa vipi? Kuhitajiana kwa kila hali, lakini hapa mimi nianze kulenga kwenye mahusiano ya kimapenzi, na mapenzi tunayozungumzia hapa ni ujumla wake, kwani jamii yenye raha ni ile yenye mapenzi yanayoanzia kwa baba na mama.

Historia inaeleza, na dini zinaeleza, kuwa Adamu alitafutiwa mwenzake Hawa ili waweze kuishi pamoja. Kwanini Mungu hakumuumba Adamu peke yake, au kwanini Mungu hakuwaumba wanaume peke yao, au wanawake peke yao, kwasabubu wote wanahitajiana.

Kuhitajiana kwa mume na mke ni kwa ajili ya kuboresha mahusiano(ushirikiano),na kujenga upendo. Inakuwa shida kwa mmoja kuishi peke yake hata kama anauwezo wa kila kitu, lazima mmoja atajisikia hali isiyo ya kawaida, kimaumbile na hata kijamii.

Wapo wanaojaribu kuishi kinamna ya kutokuhitaji mahusiano. Yaani kama ni wake hawahitaji waume na kama ni waume hawahitaji wanawake. Kihalihalisi kama ingewezekan kufunua nyoyo zao ungeshuhudia ukweli ulivyo, kwamba, ndio hata kama wanatimiza imani zao lakini ipo nafsi inatamani kama ingewezekana ingempata mwenzake.

Wapo wameshindwa na wakaenda kinyemela kukidhi haja zao. Wapo na wana watoto nje. Hii ni sehemu mojawapo ya kuhitajiana.

Kupo kuhitajiana kwa kiuchumi, na kimaisha ili kujijenga. Hapa wengi tunafikiri kwa vile wanaume ndio wanaowafuata wanawake kuwaoa, basi tunaona kuwa wanaume ndio wanaowahitaji wanawake kwa saana.
La khasha, huu ni utaratibu tu uliojijenga, lakini mke naye kama angepata nafasi hiyo angemwendea mwanaume na akamposa, kwani pia naye nimuhitaji kama alivyo mwanaume.

Watu wanaona pia kwa vile wanawake wengi wanaolewa na kukaa ndani, basi wao ndivyo wanavyohitaji. Ya kwamba mwanamke anamuhitaji mwanaume ili amuhudumie? Sidhani kama ndio lengo la maumbile!! Mimi nafikiri kila mmoja kwa nafasi yake anamuhitaji mwenzake ili wapate kuhudumiana, mengineyo ni mgawanyo wa kazi, wakati mume anafanya kazi za kuajiriwa, biashara au vyovyote, mwanamke anafanya kazi za nyumbani, kama ni mama wa nyumbani, na pia kama yeye ni muajiriwa au mfanyakazi naye anafanya hivyo ili kukamilisha mzunguko huo wa kimaisha.
Huo ndio mchango wangu kwa leo.

Anonymous said...

Dinah,
Ngoja nijaribu kujibu nionavyo mimi na mawazo yangu ni kuwa mwanaume ndio anamuhitaji sana mwanamke kwa nini nasema hivyo? sababu mwanaume anaweza kuona mwanamke barabarani na kumtamani na nyege akapata muda ule ule, kitu ambacho kwangu mimi hata kama nimempenda mwanaume siwezi kumuona na kupata nyege mara moja, mpaka tutapoanza kuwa karibu na kutomasanatomasana na hatimaye tukiwa uchi kabisa. kila mtu ana mawazo yake hii ni katika kuchangia mada napatikana kwenye email: mwenyewe_m@yahoo.com

Agwegwe Mgwegwedo said...

Nakuuliza hivi wewe ukiwa unakuja unamwambia mumeo?

Anonymous said...

anony. wa juu. unamanisha nini kwa 'kuja'? umeniacha kidogo.

Gentleman said...

mimi ninavyojua kila mmoja anamuhitaji mwenza wake , ni chemistry kwa viumbe vyote .

Dinah said...

Natambua wewe mchangiaji walienikosea heshima utapita kuangalia kama nimeweka comment yako.

Napenda kusema kuwa maelezo yako ni mazuri na yangesaidia wasomaji wengine kuhusu taasisi ya ndoa, lakini kwa vile umeyaweka "kihasira" na kuni-attack mimi in a way nimeamua kutoyaweka hapa.

Kama unataka kuwakilisha hoja au kupingana na maelezo yangu unakaribishwa lakini jifunze kuto-attack mtu ili usikike na badala yake tumia maelezo ya kawaida ili sote tujifunze.

Nitaitoa hii post within 48hrs.

Asante kwa ushirikiano wako.

Anonymous said...

Dinah,Kuna dada mmoja anafanya kazi Clouds FM anaitwa Dina. Hivi yule dada ndiye wewe?

Dinah said...

Anony @11:41am, Hapana sio mimi. Yule ni Dina Marios na mimi ni Dinah J Mentor.

Anonymous said...

mayu dellagawiza?
Japokuwa ni mpenzi mkubwa wa kijiji hiki lakini ni mara chache kuchangia naomba wasaa nami nitoto yangu kwa mada hii kama ifuatavyo.

Kuhitajiana kuko kwa pande zote mbili nikimaanisha kuwa mwanaume anamuhitaji mwananamke kama ambavyo mwanamke anavyomuhitaji mwanaume.kivipi? Mwanamke anamuhitaji sana mwanaume hasa katika suala la Usalama ktk uasilia wake kwani Mwanaume ameumbwa katika hali ya kuweza kuhimili mikimiki ya kila siku ndio maana hata msuri wa mwanaume hauwezi kuwa sawa na wa mwanamke hata kama mwanamke afanye mazoezi ya aina gani. hivyo umbile la mwanaume limeumbwa maalum kuwa kama kinga ya Familia ktk nyanja zote uzijuazo ktk familia hasa kwa upande wa nje.Mfano angalia kwa wanyama madume siku zote huwa walinzi.

Tukiangalia kwa upande wa mwanamke ni kuwa ameumbwa ktk umbo au hali ambayo humuwezesha kuwa ni mhimili mkuu ndani ya nyumba ktk nyanja zote ktk familia kuanzia kuzaa kulea na Amani ndani. Japokuwa kwa sasa hivi hali imebadilika kutokana na jamii kutotambua mchango wa mwanamke katika familia zetu.
Hivyo basi kwa ufupi Kila mmoja anamutaji mwenzie hata hao Ma-spinsters na Ma-bacholers maisha yao huwezilinganisha na waliokatika ndoa zenye Upendo wa kila jinsia kujua haki na wajibu wake. Kuishi miaka mingi sio kuwa na furaha duniani unawezaishi miaka michache likini yenye FURAHA NA FARAJA na vinginevyo kinyume chake ambavyo sio lengo la Maisha hapa duniani.

Ba'Watoto

Anonymous said...

Sasa!? Unasema wewe ni Dinah J Mentor. Mbona jina hilo ni geni katika dulu za magazeti ya hapa Dar? You know I would like to know least of you my dear.