Wednesday, 30 January 2008

"Atatembea sana lakini at the end atarudi kwangu" Ukweli..

Mpenzi wako iwe ni mwanaume au mwanamke siku zote anakupa wakati mgumu lakini wewe unamvumilia, inafikia wakati anatoka nje ya ndoa/uhusiano wenu na kujakukuomba msamaha wewe unasamehe kwa vile tu labda unampenda, unawatoto nae na usingependa watoto kumpoteza baba/mama yao au kwenda kulelewa na mtu mwingine ikiwa utamtaliki/acha mpenzio.

Umewahi kujiliza kwanini siku zote akikosa (wakati mwingine anakuacha kabisa) lakini baada ya muda anarudi kwako mbio akikulilia na kuomba misamaha yote kwa kuhapia Miungu yote ajuayo na kukupa ahadi lukuki ili uendelee kuwa nae?

Mpenzi/mwenza mume/mke kama kweli anakupenda au nisema anakupenda kwa dhati na kukuthamini hawezi kwenda kulala nje na watu wengine na pengine kukuacha kabisa kisha ya kimshinda anarudi kwako na wewe kama juha unadhani huko ndio kupedwa, kwamba hapati "penzi" kama lako huko nje ndio mana kila wakati anarudi.

Endelea hapa

Ukweli ni kuwa mpenzi huyo anafanya hivyo kwa vile anajua wewe unampenda kwa dhati na huwezi kumuacha au kumkataa hata akuumize vipi, anahisi kuwa-secured (sio penzi) mikononi/ubavuni mwako...kumbuka usemi usemao "mpenzi akijua unampenda sana anakusumbua" hasa akiwa hana mapenzi na wewe bali yuko na wewe kwa sababu zake binafsi japokuwa alitumia au anatumia neno "nakupenda" n.k.


Sote tunatambua kuwa kuna wakati tunahitaji "mapumziko" kutoka kwenye mahusiano yetu ya kimapenzi /wenza wetu kutokana na uzito wa matatizo kikazi au kimaisha, kuna wakati mtu unahisi kwamba unataka kuwa mwenyewe bila kelele za watoto au maswali kutoka kwa mpenzi au hata "kupetiwa-petiwa" (hasa kwa wanaume pale mambo yao kiuchumi hayaendi vema).

Hili likitokea(ni tofauti ) haina maana kuwa hupendwi bali mwenzio yuko ktk wakati mgumu akifikiria jinsi ya kuilinda familia yake ikiwa ni pamoja na wewe mpenzi/mkewe na mara zote mwanaume huyo ambae anakupenda kwa dhati hatolala na mwanamke mwingine yeyote mpaka kipindi cha "mpito" kipite then atarudi kwako na kuomba radhi kwa kujiweka mbali na wewe na hata kwenda kwa kaka/rafiki yake kupumzisha akili na kupata maoni ya "kiuanaume" ambayo wewe mama huwezi kumpatia.

Hivyo wewe kama mwanamke ni vema ukaondoa hiyo kasumba au imani kuwa mumeo/mpenzi wako atatembea kote lakini lazima tarudi kwako, kwa yeye kufanya hivyo sio penzi juu yako bali penzi lako kwake ndio linamrudisha kwa vile anatambua wazi kuwa hakuna mtu atampenda kama unavyompenda wewe.

Kumbuka nia na madhumuni ya kusihi hapa Duniani kumtukuza Mungu na kufurahia maisha, hivyo ni vema kuwa kwenye uhusiano ambao nyote mnapendana na kuthaminiana, ukiona/hisi hupendwi ni vema kujitoa badala ya kuwa "unhuppy na lonely in love".

Tafadhali usisite kuongezea maelezo/uzoefu wako ili sote tujifunze....karibu.

3 comments:

Mama Kadogoo said...

Raha ya kuwa kwenye uhusiano ni kubadilishana penzi, nakupenda unanipenda. Mmoja wenu akiwa na tabia ya kwenda na kurudi kwako kuomba misamaha inamaana hakupendi bali nakutumia kama fanicha, mfano kiti au kochi na huna maana kwakwe kama mwenza au mpenzi. Mapenzi yanachanganya sana na wakati mwingine yanaudhi na ndio maana watuwengine wanaamua kuwa wenyewe tu kufurahia maisha kuliko kuwa nampenzi anakuumiza.

Haruon said...

Haya maelezo ua kamaulivyosema wewe ukweli unafanya mwanamke ajione mjinga kwa sababu wanawake wengi hasa Baongo ndio wanatabia ya kusema kuwa hata akitoka ni mume wangu kanioa mimi na sio hao wengine.Mapenzi haya balaa tupu.

H. M said...

Dinah, mimi ninataka ushauri kwako, nimeolewa mwaka jana sijabahatika kupata mtoto, mume wangu amekuwa ni mvivu sana ktk swala zima la mapenzi analala sana sasa sijuwi kama labda anachoka na mihangaiko ya hapa na pale, wakati mwingine nimekuwa nikimuhisi hata kuwa na mwanamke nje, mwanzo hakuwa hivi sijuwi kapatwa na nini!wakati mwingine tumekuwa tukilala hata wiki nzima bila kufanya chochote anakuwa na dalili za kutaka kufanya akikushika ziwa mara unamsikia akikoroma wakati huo mimi ninakuwa nimeshaanza kupagawa basi ninakereka sana, niambie dada dinah nifanyeje dada yangu,nasubiri jubu zuri dear au kama utaweza naomba unijibie kupitie address yangu kama ilivyo hapo plz ninahitaji ushauri wako,
ahsante na kazi njema