Thursday, 25 October 2007

Inakuwaje Mkifunga ndoa?


Mnaacha matumizi ya kondom ili kuzuia mimba na magonjwa mengine ya zinaa ambayo sio lazima yatokane na kufanya ngono holela/ovyo na watutofauti bali yanajitokeza kutokana na mkanganyiko wa vimelea (cells) hasa kwa upande wa wanawake?

Tujadili hili.....

Kisha nitakuja na maelezo ya kina ambayo kwa namnamoja au nyingine yatakusaidia au kukupa mwanga ktk maamuzi yako na mwili wako(hasa mwanamke).
ty.

Tuesday, 23 October 2007

Zeze on kuktk

shamim a.k.a Zeze said...
Samahanini ni kazi zilibana tu sasa wacha niwape somo kujifunza kukatika kila siku au kila upatapo muda kaa kitandani lala chali kwa kutumia kiuno chako chora namba 1...2...3....4...5....6 hadi 10 mwanzoni itakuwa ngumu so waweza anza kwa kuchora namba 1-4 baada ya hapo kiuno chenyewe kitakuwa chepesi kiasi kwanza hata ukibeba mzigo juu kitakuwa kinaendatry this then mlete feed back hapahapa kwa mama malavidadavi
2:48:00 PM

Sunday, 21 October 2007

Kukata kiuno...."basic"


Nakumbuka nilipokuwa mdogo kabla hata sijaanza shule kila jioni tulikuwa tukikusanywa nakuimbiwa nyimbo fulani za Mwinamila na kulazimika kukata viuno, usipokata kiuno hakuna kuadithiwa hadithi usiku chini ya mbala mwezi (aah utoto raha sana).

Nilipokuwa binti mkubwa nikawa naambiwa kuwa usipofanya mzoenzi ya kukata kiuno utakuja kupata taabu pale nitakapo olewa ikiwana maana kwamba unazungusha kiuno kwa ajili ya bwana.

Lakani mimi leo nawapa "basic" ya mauno sio kwa ajili ya kuwanufaisha wanaume zenu bali kuwasaidia ninyi kufurahia wakati wa kufanya mapenzi/ngono.


Kwanza anza na kulizoesha tumbolako kabla hujahamia kiunoni au kwenye hips. Sote tunatambua kuwa tumbo ni moja ya sehemu inavutia kama ilivyo makalio, miguu n.k. hasa kama tumbo hilo ni kama langu (dogo )hahahaha.Haya tuanze zoezi basi ili usije shitua utumbona makorokoro mengine pale utakapo kurupuka na kuanza kuzunguusha kiuno chako.1-Simama wima(ukiwa uchi mbele ya kioo ndio it'll work better), weka mikono yako hapo tumboni alafu sukuma tumbo lako mbele (litunishe) baki hivyo kwa muda kisha lirudishe kwa ndani na ubaki tena hivyo kwa muda. Rudia kufanya hivyo mara nyingi uwezavyo na kumbuka kubana pumzi huku mdomo ukiwa wazi (itasaidia kukaza misuli ya tumbo pia), kubadilisha mirindimo (polepole, haraka, chap-chap, kugandisha n.k) mpaka utakapo hizi tumbo lako linatetema/tikisika (yaani vibrating).

Msingi wa kukata kiuno

Kama nilivyosema awali, simama wima najishike kiunoni(kuhu na huku) kisha peleka sehemu ya kiuno ya kulia upande wa kulia, sehemu ya mbele ipeleke mbele uwezavyo(nina maana ile pelvis tu sio tumbo na kila kitu) alafu baada ya hapo peleke sehemu yako ya kiuno ya kushoto-kushoto, kisha peleka seheumu yako ya mbele nyuma hali itakayofanya matako yako yabinuke/jitokeze kwa nyuma.....nyoosha magoti kisha rudi kulia(ulipoanzia).Fuata hatua hizo kwa mara nyingine tena ambazo ni simama wima-kulia-mbele-kushoto-nyuma kulia x 20 na kuendelea inategemea zaidi na bidii yako.Baada ya kuzoea hatua hizo hapo ndio unapotakiwa ku-create movements na mirindimo yako kivyako. Mfano lala chali, kifudifudi(lalia tumbo), ubavu, chutama, piga magoti n.k kisha nenda kulia-mbele-kushoto-nyuma-kulia mpaka kiuno kizoee......hey alafu usisahau ukiwa ndani ya "game" kukilazimisha mpaka kitakapo kubali/zoea.


Kidokezo: Zoezi zuri la kukata kino ni kulala kifudifudi(kulalia tumbo) kisha kukizunguusha (hapa usipokuwa mwangalifu unaweza ku-cum via kisimi kwa vile unatua unakisugua kiaina sio mbaya ni njia moja wapo ya kujipunguzia stress sio hahahahaha).


Haya Zeze endeleza somo bidada.


Nikirudi nitakueleza tofauti za ukati kiuno na faida zake.

Saturday, 20 October 2007

Jinsi ya kukata kiuno!

Zeze aliahidi kisha akaingia mitini, sasa mimi nitawapa "basic" ikiwahuwezi/hujui kukizunguusha a.k.a gogos.

Endelea kuwepo!

Thursday, 11 October 2007

Hivi huwa tunajiandaa tunapoanza familia?Nimeshuhudia sehemu kuwa ya watu hapa Duniani huamua kuwa na familia (kuzaa) kwa kushitukizwa (bila kuwa tayari). Kwa vile mimi ni m-bongo na nina uzoefu au nawajua wabongo basi nitaegemea huko kwa m-bongo halisi.


Sina hakika kama ni ubinafsi au ile kasumba ya kipuuzi kwamba ukiachia mimba basi Mpenzi hakuachi, pia inawezekana kabisa kuwa ni uzembe wa mtoa mbegu (mwanaume).


Kisheria (as far as I remember) umri wa kushiriki ngono/funga ndoa ni 18+ japo kuwa bibi yangu aliolewa akiwa na miaka 15 akaja kuzaa mtoto wa kwanza akiwa na miaka 20 ila kwa karne hiyo kulikuwa na sababu ya kuolewa ktk umri mdogo ambazo sote natumaini tunazijua.

Sasa ndugu zangu mnapo amua kupeana mimba huwa mnakuwa mmejiandaa baada ya kung'amua faida, majukumu, matatizo, mabadiliko ya kiakili na kimwili (mwanamke)?

Je, huwa mnakuwa na uhakika na uamuzi wenu au mmoja anaamua ili kumridhisha mwenzie au jamii inayomzunguuka? au hutokea tu kwa "bahati mbaya"?
Huwa nasikitika sana ninapo ona binti au kijana huyu mdogo ambae katoka kwa wazazi (bado mtoto) kisha akawa mzazi na yeye kwamba hajui tofauti au mabadiliko ya mwili wake kutoka Utoto, Ujana na kufikia Utu uzima na anapofikia umri mkubwa (utu uzima) anakuwa amejichokea(kazeeka).

Kijana/binti huyu hajafaidi ujana wake....sio kufanya ngono ovyo bali kufanya yale mambo ambayo vijana tunapenda kuyafanya bila kuwa na hofu "mtoto" atakula nini kesho, sijui anaumwa, amekua unahitaji vivazi vipya, siku gani ni clinic, je mpenzi wako ana-cheat n.k., kujua tofauti ya kupenda (bila ngono), n.k.


Ongezea basi uonavyo wewe (bila ku-attack mtu) mimi nasikia usingizi, swaumu kali hapa!

Nakuja......

Monday, 8 October 2007

"Jinsi ya kupenda kwa vitendo"

Kama ilivyo mambo mengine kuwa “affection” ni swala la kujifunza, baadhi ya wanaume waliokuzwa/kulia kwenye jamii yenye mfumo Dume (Waafrika kwa ujumla) huwa hawajui kuonyesha hilo hitaji, embu tuliite “kupenda kwa vitendo” hivyo huenda sio kwamba hataki bali hajui.


Kwa maana hiyo sio mbaya ikiwa wewe mwanadada ukamfundisha nini cha kufanya, ikiwa na wewe ulikuwa huji basi jifunzeni wote ili kuwa una uhusiano bora wenye furaha.


Mpaka hapo umeelewa nazungumzia nini sio? Sasa Ili kufupisha maelezo nitaorodhesha mambo machache ambayo wanawake wengi huwa tunapenda kufanyiwa (kiujumla ukiachilia mbali utofauti wetu) ili tujue kweli tunapendwa kihisia na kivitendo.

1-Hakunakitu wanawake tunazimia kama kukumbatiwa nakupigwa busu mara kwa mara.

2-Kabla hujakurupuka kitandani hakikisha umekumbatia na kubusu hata kama kalala(hakuna raha kama kuamshwa na busu au mkumbatio).

3-Mwmabie jinsi gani unampenda na unavyopenda chapati/mayai/viazi alizopika au hata jinsi alivyoandaa mlo wa asubuhi.

4-Wakati unatoka ndani kumbatia chap-chap na busu kiduchu ndio utokomee kazini, hata kama mnatoka wote kwenda kwenye kituo cha daladala unafanya hivyo kabla hujakanyaga vumbi la nje.

5-Onyesha unajali kwa kumjulia hali kwa sms au sauti mara baada ya kufika kwenye mihangaiko yako na vilevile kumbuka kufanya hivyo kabla hujaondoka eneo la shughuli zako pia hakikisha unamueleza utakuwa saa ngapi nyumbani au kama kuna mahali unapitia basi mfahamishe utakuwa huko kwa muda gani n.k.

6-Ufikapo nyumbani kumbatia na busu mdomoni sio shavuni, badala ya kukimbilia kusema yaliyojili huko utokako.

7- Mnunulie vijizawadi mara kwa mara, wazaramo hununuliwa Khanga au hereni na mikifu ya dhahabu, Wazungu hununuliwa maua, kadi au vidani vya madini tofauti, kuna wengine ukipeleka kitoweo (aina ya nyama) basi umemaliza kezi mwana mama anafurahi kweli-kweli sasa wewe fanya kile unachomudu………..hey sio kila siku wala kila mwezi..


8-Msaidie kusafisha mesa/jamvi mara baada ya mlo wa jioni, ikiwa umechoka hata yeye kachoka pia hivyo mkikutana nyumbani mna-share kufanya usafi ili kuokoa muda.


9-Lolote litakalo tokea kila la kheri, lakini hakikisha unabusu na kukumbatia kabla hujaanza kukoroma.

Kila la kheri ktk hili.

Wanaume, tupendeni kwa vitendo!


Wakati wa kunanihii si mara zote huwa penzi......

Kwenye moja ya makala zangu kuna mshirika (Moses) aligusia mahitaji ya wanawake na wanaume ktk mahusiano ya kimapenzi(nitalizungumzia hilo ktk siku zijazo).
Leo napenda kugusia kidogo kuhusu hitaji moja mbalo sote tunahitaji lakini tuna feli (fail) kulitekeleza, hitaji hilo ni “Affection” ukilitekeleza ni kuwa “affectionate” kwa mwenza wako…………Kiswahili chake ndio nini?
Tumeshuhudia mahusiano mengi ya kimapenzi kuanzia baba na mama, ndugu, jamaa na marafiki wakipendana au kuwa pamoja kama wapenzi, lakini ni mara chache sana utawaona hawa wapenzi wakionyeshana kuwa wanapendana kwamba sio “affectionate".
Ni kweli kuwa unampenda mwenzi na unamjulisha unampenda kwa kumwambia, lakini kumbuka kuwa penzi ni hisia ulizo nazo wewe juu yake. Unahisi kabisa bila yeye wewe ni hamna kitu hapa Duniani lakini yeye haoni hilo unless ufanye kwa vitendo yaani uonyeshe unampenda mwenzio.
Huenda ni kutokana na tamaduni au mila na desturi kwamba hupaswi kufanya mambo Fulani ukiwa nje ya chumba/nyumba, lakini kuna baadhi ya watu hata wakiwa mahali peke yao kama wapenzi huwa hakuna kutekeleza hilo hitaji kitu ambacho mwenza wako ataona kama vile humpendi au humjali na uko nae kama msaidizi (ATM,mpishi,usafi n.k) au mtu wa kukuburudisha kwa kutumia mwili wake.

Kuwa “affectionate” kwa mpenzi wako huitaji kumkumbatia na kumlamba/busu mbele ya kadamnasi bali unaweza kumshika mkono,kutembea nae ubavu to ubavu (sio baba mbele mama nyuma na furushi lake kichwani) vilevile unaweza msaidia furushi ukiweza unambebea hata mkoba wake n.k..

Kwa sasa naishia hapa, nitarudi baada ya masaa machache kumalizia, karibu

Thursday, 4 October 2007

Maana ya Penzi!


Penzi halina dawa, penzi halihusiani kabisa na kufanya ngono(hivyo kubinuka aina nyingi za mibinuko haina maana ndio utapendwa au unapendwa zaidi) penzi huja "naturally" huitaji kulazimisha wala kwenda kwa Mganga....Penzi huitaji na huchukua Muda.

Lakini je, penzi ni nini hasa?
Watu wanasema penzi halielezeki au halina tafasiri maalumu kwamba kila mtu anamaelezo yake kuhusu penzi na maelezo hayo hutegemea zaidi na uzoefu wake.

Mimi kama Dinah nadhani penzi ni hisia zenye nguvu ya ajabu za mtu Fulani juu ya mtu Fulani, hisia hizo hazijalishi muonekano(mavazi, sura, umbile n.k), utajiri, umri, Elimu, aina ya maisha au tabia.

Hisia hizo humfanya mtu ashindwe kufanya mambo ya kawaida ambayo huyafanya kila siku kwa vile kichwani anakuwa anamfikiria yule ampendae, hisia hizo zinaweza kupelekea mtu kubadilisha personality na tabia yake hasa pale unapofanikiwa kuwa na huyo umpendae.

Unapofanikiwa kuwa/mpata yule umpendae huwa unapata raha ya ajabu kila unapomuona, inakuwa ngumu sana kuwa mbali nae. Hisia hizo zikikomaa hukufanya uhisi maumivu yake ikiwa anaumwa, umemuudhi au kaudhiwa na mtu mwingine, anapokuwa na huzuni mpenzi wako hakika utahisi huzuni n.k.

Wewe unafikiri Penzi ni nini?

Maelezo yako yatasaidia wasomaji wengine kama wewe kujitambua kama kweli wanapenda,wanatamani au wanafuata mkumbo.

Karibu sana.