Wednesday, 26 September 2007

Nguzo 5 za uhusiano bora wa Kimapenzi!


Nakumbuka zamani nilipokuwa mdogo, kulikuwa na akina mama ambao walikuwa wakijadili mambo yao ya kimapenzi kila wanapokutana pale kibarazani (mbele ya nyumba) mida ya jioni mida ya jioni wakichambua mchele au kumenya viazi tayari kwa mlo wa jioni.
Wamama hao walikuwa wakijadili mambo mengi sana ila moja ninalokumbuka ni kuwa "ili usiachike ni lazima umpe mumeo kila akitaka, umpikie mapocho-pocho, uwe msafi, umuwekee maji bafuni na kumkogesha, umkande miguu na kupenda ndugu zake".

Kutokana na maisha ya sasa kwa wengi wetu ukiachilia mbali kuwahi kuangalia Isidingo (Tv 4 u) kufanya hayo niliyoyataja inakuwa mbinde kidogo kwa vile tunafanya kazi nyingine ili kuchangia kipato ktk familia zetu na unaporudi nyumbani unakuwa umejichokea, sana sana utafanya moja kati ya hayo si unajua tena mambo fulani (mwenzi mtukufu mwee!).

Alafu ndugu wa mpenzi/mumeo huitaji kuwapenda unapaswa kuwaheshimu au kuwaonyesha heshima tu, kumpenda kijana wao isiwe taabu kha!

Tuachane na hayo basi, tuendelee.....Mimi kama Dinah naamini kuwa haijalishi unapesa kiasi gani, "libido" iko juu kiasi gani, Umzuri au Umrembo kiasi gani, "mnato au mdebwedo", unampenda jinsi gani au unatabia njema kiasi gani ktk uhusiano wako wa kimapenzi kama hakuna hizi kitu 5, nenda shule kajifunze!

1-Ushirikiano
2-Masikilizano na Maelewano
3-Heshima
4-Mawasiliano (angalia picha)
5-Kujali

Hayo mambo matano yanavipengele ambavyo vingine viko wazi sana na sitoweza kuviweka hapa kwa vile watu tumefunga.

Nakaribisha mchango, maoni, maswali na nyongeza ktk hili.

Msikilize Dada Stara

Ty.

Thursday, 20 September 2007

Penzi linapobadilika na kuwa Heshima!


Hili swala la penzi kwisha mimi huwa nalisikia tu kutoka kwa watu tofauti kuwa kuna wakati mtu unajikuta humpeni tena mpenzi wako na unatafuta namna ya kujitoa kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi.

Kwa wale waliko kwenye ndoa huwa ni ngumu kidogo kutokana na "dini" kuwabana au anabaki ndani ya ndoa uhusiano kwa vile anakuheshimu kwa kuwa ni mama wa watoto wenu hasa kama umemzalia watoto 2-3 hivi lakini ktk hali halisi anakuwa na mtu mwingine ampendae nje ya ndoa (part time lover a.k.a Kimada a.k.a nyumba ndogo).

Mwanamke unatakiwa kuwa makini na mjanja kutambua mabadiliko hayo(penzi au heshima), kwani mtu anapokuheshimu na kukuthamini kwa vile umemfanyia jambo fulani kubwa hakuna tofauti kubwa sana na kupendwa.

Hivyo ikiwa kila usiku analala kitanda kimoja na wewe nakukamilisha mambo mengine ya kifamilia na kuambiwa "nakupenda mama nanihii" haina maana kweli anakupenda bali anakuheshimu na vilevile anajaribu kuepuka malalamiko au maswali.

Mimi binafsi naamini kuwa unapompenda mtu kwa maana halisi ya mapenzi huwezi kuchoshwa au penzi lako kwake kupungua kama sio kwisha kabisa.

Pamoja na mambo mengine kuna sababu zinazochangia mabadiliko hayo ambayo ni kujisahau kwako mwanamke, kuwa na tabia ya "ndio bwana", kukubali usemi kuwa "mumeo akiwa ndani akiwa nje si wako bali wa wote", kukimbilia kuzaa siku chache baada ya kuwa ndani ya uhusiano au ndoa kwa vile unahofia usipompa mtoto basi ataenda zaa nje n.k.

Nakaribisha nyongeza kuhusu hili, maswali, maoni na ushauri.

Karibuni sana na kila kheri ktk mfungo mtukufu.

Wednesday, 12 September 2007

Vishawishi vinavyosababishwa na Teknolojia......

Hapo chini nimezungumzia Teknolojia inavyoweza kuchukua muda mwingi kuliko ule unaotumia kuwa na mpenzi wako, na nimetaja simu na Mtandao (internet )na vilevile swala la kutembelea Salon na Gym.

Sasa leo nazungumzia ni jinsi gani vitu hivi vinashawishi na hata kupelekea baadhi ya wapenzi wetu kutumia muda mwingi katika "kona" hizo kuliko ule wanatumia kuwa na sisi.

Simu za mkoni;
Ni wazi kuwa simu inarahisisha mawasiliano yakikazi, biashara na inatufanya tuwe karibu na wapedwa wetu kila siku bila kupoteza kiasi kikubwa cha pesa kwenda kumtembea ndugu jamaa na marafiki.

Lakini simu hizi pia zimekuwa ni kishawishi kikubwa kwetu kufanya mahusiano ya kimapenzi ya kihisia na mtu yeyote ambae anajua namba yako au wewe unajua namba yake.

Hii inaweza kutokea ikiwa mhusika mwenye jinsia tofauti na wewe anajisikia mpweke siku hiyo, amechukizwa na mpenzi wake, amesongwa na mambo mengi yanayomfanya ajisikie hana raha n.k. na hivyo akaamua kuwasiliana na wewe kwa kukutumia "text" na kila kitu kikaanzia hapo.

Vilele mpenzi wako au wewe unaweza ukapokea "text" yenye mrindimo wa kimapenzi kutoka kwa mfanya kazi mwenzio au mfanya biashara mwenzako au hata rafiki wa mpenzi wako kimakosa, lakini kwa bahati mbaya ukavutiwa nayo (ukidhani ni yako na mhusika kakuzimia) hivyo ukaijibu vema kabisa na mpekeaji akavutiwa na ulichojibu na hapo ndio unakuwa mwanzo wa.......

Hayo yote niliyoyasema na mengine unayoyajua kuhusiana na mawasiliano ya simu yakonoga huwa yanasababisha wenza wetu ku-set pin # ili usiweze kufungua simu yake(ikiwa una tabia hiyo), hata siku moja huwezi ukakuta simu yake imezagaa juu ya meza.........siku zote itabaki ndani ya bagi ambalo linafunguo, wakati wa kulala itawekwa uchagoni (chini yamto), akiwa anaongeza nguvu simuni basi hatocheza mbali na mahali hapo n.k.

Unaweza kuongezea kuhusu hili kwa faida ya watu wengine na hasa walengwa ambao ni wanawake.

Karibu sana.

Sunday, 9 September 2007

Tekinolojia na mapenzi inaendelea hapa.....

Sote tunatambua kuwa mahusiano yamekuwa yakivunjika mara kwa mara, ndoa hazidumu kama ilivyokuwa miaka 40 iliyopita na kama ndoa/uhisiano huo umedumu basi ujue asilimia kubwa ni uvumilivu wa mmoja wao kwa vile kuna watoto ndani ya uhusiano huo na mara zote mvumilivu huyo huwa na uhusiano mwingine nje.

Uhusiano huo unaweza ukawa wa kimwili (mambo ya kimada, nyumba ndogo na vipoozeo), uhusiano wa kihisia tu ambao mara nyingi huitaji kuonana na mwenza wako na huu ni ule wa kimtandao a.k.a internet, uhusiano wa kimapenzi wa simu kwa kutumia sms na ule wa kuongea kwa sauti.

Nitazungumzia mahusiano ya kimapenzi ambayo ni matunda ya Teknolojia kila uhusiano kwa nafasi ili kukusaidia wewe kuelewa na kutoa maoni au kuongezea yale niliyoyaelezea.

Mtandao a.k.a Internet.
Mtandao umekuwa sehemu kuwa ya maisha yetu hivi sasa, wengi wetu tunatumia muda mwingi kukaa mbele ya Komputa kuliko ule mda tunaotumia kukaa na wapenzi wetu.

Kwa baadhi ya wenza (couple) hujitahidi kujigawa ili mwenza wake asijisikie vibaya au kuhisi anatengwa au kutojaliwa na hivyo wapenzi hao huamua kutembelea tovuti tofauti usiku wa manene wakati wapenzi wao wamelala au ilemida ambayo wanamaliza kazi au wako kazini nakisingizio ni kuwa kuna kazi au Data wanapaswa kuzimalizia na zinahitaji uchunguzi "online".

Hapa inaweza ikawa muhusika (mwenza) akawa anatembelea chat rooms, Forums, Emails(sio zote za kikazi), kutembelea Tovuti za Porno au kama sio zile za kutafuta jamaa mliosoma pamoja, marafiki n.k.

Simu za mkononi.....sms!
Mpenzi hapa anatumia muda mwingi kutuma na kusoma sms kutoka kwa watu tofauti na baadhi huwa ni wapenzi ambapo hubandikwa majina yakiume ikiwa muhusiaka na mwanaume na kupewa majina ya kike ikiwa mhusika ni mwanaume.

Simu za mkononi-kuongea!
Mpenzi anatumia muda mwingi kuongea kwenye simu kuliko muda anaotumia kuongea au kufanya mambo mengine yanayohusiasha uhusiano wenu wa kimapenzi.

Tekinolojia hii pia inahusisha swala la kutembelea Gym, Salon......zamani hakukua na haya mambo sio, ila siku hizi utakuta bwana au bibi atumia muda mwingi kwenye kona hizo kuliko ule anaotumia na mwenza wake.

Natambua nimegusa wengi hapa.............karibu tujadili kuhusu hili, tufanye nini ili kuokoa mahusiano yetu ya kimapenzi na wakati huohuo kufaidi matunda ya Teknolojia?

Karibu sana.........

Thursday, 6 September 2007

Tekinolojia ndani ya mahusiano yetu ya kimapenzi.

Kutokana na kukua kwa tekinolojia watu wengi tumekuwa tukitumia muda mwingi kwenye Komputa (Internet), simu za mikononi, Luninga na vifaa vya umeme (Gadgets) na kutumia muda kidogo na wapenzi wetu hali inayoweza au inayopelekea mtafaruku ambao huatarisha maisha yetu ya kimapenzi na wapenzi wetu.

Sasa basi leo nikirudi kutoka Kariakoo nitaelezea hilo kwa kina ili kutambua nini kinaendelea akilini mwa wapenzi wetu japokuwa wanaonekana hawajali wewe kukeshakwenye Komputa.

Karibu mida-mida tushirikiane ktk kuzungumzia hili.

Ty.

Saturday, 1 September 2007

Matiti sehemu ya mwisho!


Usafishaji

Pole msomaji kwa kusubiri, sina hakika kama sote tunajua jinsi ya kusafisha matiti. Ikiwa wewe unajua basi ujue kunamwingine hajui na kama ilivyo ada mahali hapa tunajifunza sio au kujazia/ongezea yale tunayoyafahamu.


Hakikisha unasafisha eneo zima la matiti hasa sehemu ya chini (ikiwa wameanguka tayari) kama ilivyo sehemu nyingine ya mwili wako, vilevile hakikisha chuchu zimejitokea na usafishe vema chuchu hiyo....hii sio kwa walionyonyesha au wanaonyonyesha tu bali hata wewe ambae hujawahi kuwa na mtoto.


Unatambua kuwa unapokuwa mtu mzima chuchu hutoa kashombo fulani hivi ambako husababishwa na utokwaji wa majimaji fulani unapokaribia hedhi na wakati wa hedhi (hii ni kutokana na matiti hayo kutengeneza maziwa incase utarutubisha yai lako).


Kunyonywa/chezewa matiti yako ili kuzuia yasianguke haraka;


Hakikisha mpenzi wako anayanyonya akiwa ameshikilia au wewe umeyashikilia, vilevile hakikisha anapo yapapasa au kuyatomasa(neno limekaa vibaya hili Kha!) anywho, basi afanye hivyo bila kuyahangaisha....kwamba ahakikishe yametulia.


Unapokuwa kwenye mkao wowote unaosababisha matiti yako yasumbuke basi hakikisha mpenzi kayakamata sawia au kama wewe mwenyewe hujapoteza akili kwa raha basi yashikilie....kwa kufanya hivyo kutasaidia matiti yako yasilegee kabla ya wakati.


Ni wazi kuwa sote matiti yetu yanakwenda kulegea pale tutakapokuwa tunapoza homoni yaani tutakapo zeeka lakini kuzaa au kuwa mdada mkubwa (over 40) sio sababu ya kujiachia.


Nakutakia mwisho mwema wa wiki, karinu tena mahali hapa.


Siku njema.