Thursday, 26 July 2007

Je unatumia au umewahi kutumia?


Madawa ya kuzuia mimba! Nimeombwa kutoa maelezo kuhusu hili jambo na mimi sina uzoefu nalo, hivyo tafadhali naomba ushirikiano wako mahali hapa.


Toa ushuhuda kuhusiana na swala zima la madawa hayo na mabadiliko, mafanikio n.k.


Kubaki na jambo bila kuchangia na wenzio ni uchoyo sio, haya karibu sana.


N:B Pamoja na maelezo yatakayo tolewa hapa wewe mwanamke hakikisha unamuona Dakitari kwa ushauri wa kitibabu kabla hujajikitakwenye hii kitu.


Nimebanwa kiaina na shughuli wiki hii.....unakumbuka nilizungumzia mikao ya kimazoezi, mikao inayosaidia ufike haraka sasa nikirudi naibuka na mikao ya kimahaba ambayo ni bab-kubwa sultani ka kipepeo ndani ya Dinahicious

Saturday, 21 July 2007

Maalumu kwa bikira!


Tafadhali, ikiwa wewe ni bikira usithubutu kupunguza siku zako za hedhi kama nilivyoeleza hapo chini nabadala yake subiri mpaka hapo utakapo kuwa mkubwa na tayari kujiingiza kwenye maswala ya mahusiano ya kimapenzi.


Ikiwa unaswali lolote wewe manamke mdogo, usisite kuniuliza naahidi kukusaidia kadili ya uwezo wangu ili uweze kuvuka kipindi hiki kigumu ambacho hata mimi nilipitia, hakika nitakupa mbinu mbili tatu ili uvute muda mpaka utakapo kuwa at least una miaka 21 na kuendelea.


Usiogope nipo hapa kwa ajili yako.


Asante kwa uelevu wako.

Thursday, 19 July 2007

Punguza siku zako za hedhi!


Ktk makala moja iliyopita nilielezea swala la kujiswafi ili kuondoa utoko nakupunguza harufu/shombo ya uke, vilevile nilisema kuwa kwa kufanya hivyo (kujisafisha huko chini) kunapunguza siku zako za hedhi ikiwa utaendelea kujiswafi wakati uko hedhini.


Sote tunatambua karaha ya hii kitu na baadhi hutunyima raha ikiwa wapenzi wetu hawezi kumudu kufanya ngono wakati uko huko mwezini japokuwa wewe unataka kuliko siku zote.


Sasa ni hivi; kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa siku zako ni kati ya 3-7 lakini wewe unakwenda siku 8-12 na huelewi kwanini wewe wakati wengine wanapiga siku tatu tu?


Unapokuwa hedhini damu huchirizika taratibu lakini si damu yote inayotoka nje ya uke na kujaa kwenye "Tampax" au "pads", sasa ili damu hiyo yote itoke yenyewe inamaana itakubidi uisubiri kutegemeana na uwingi wake.


Hivyo, ili kupukuza swala la kusubiri isaidie kwa kidole chako cha kati kuitoa huko iliko kama ambavyo nilielezea awali kwenye swala la kutoa utoko. Endelea kujiswafi mpaka uone maji yanachuruzika bila damu.....kwenye hedhi utahisi uterezi usihofu au kutafuta jitihada za kuumaliza, haumaliziki kwani wakati huo uke unakuwa laini ili kusaidia mabonge ya damu kupenya kwa urahisi (natambua sio wote lakini Mungu ndio alivyoumba hivyo).


Mara baada ya kujiswafi vaa kifaa chako kama kawaida na endelea na shughuli zako, kumbuka kujiswafi kila unapokwenda kuoga na hakika utajikuta unakwenda siku chache zaidi kuliko ilivyo awali.


Pssssss!Awali nilikuwa nakwenda siku sita (nilikuwa bikira so huruhusiwi kujisafisha) lakini tangu nilipoingia kwenye ulimwengu wa ulimwengu (mahusiano yakimapenzi) nikaanza kujiswafi napiga siku 3 tu na damu sio nyingi sana kama ilivyokuwa awali.....


Nakutamia siku njema na kila la kheri katika kupunguza siku zako za damu.


Ciao!


Tuesday, 10 July 2007

Uongo ktk mahusiano ya Kimapenzi!

Kuna hili swala la kuwaita wanaume wadanganyifu (waongo) na wanapenda kulaghau ili kupata kile wanachokitaka na cha kusikitisha hapa sio baadhi yao bali wote.

Wanawake pia ni wadanganyifu lakini haionekani kama tunadanganya kwa vile sio wote ni baadhi na uongo wetu sio wa mara kwa mara, uongo wa mwanamke unategemea zaidi malezi na hatimae kubadilika pale unapokua na kuwa tabia, kwa wenzetu wanaume uongo kwao ni sehemu ya UANAUME.

Nakumbuka wakati Fulani nilikuwa kwenye uhusiano na jamaa Fulani hivi, kule alikokuwa akiishi kulikuwa kuna bidhaa Fulani hivi nzuri na nilikuwa nazihitaji sana. Sasa kwa kurahisisha mambo nikaomba huyo mchumba aninunulie (kwa kumtumia senti) kisha anitumie huku niliko.

Yeye akakataa kupokea “senti” zangu akidai kuwa ni kitu kidogo atashughulikia kwa senti zake sio. Nikawa nasubiri mzigo wangu uje lakini kila nikikumbushia napewa hadithi, nikaona tuaache tu kwani ktk siku chache nitakuwa huko (kumtembelea) na hivyo nitavichukua mwenyewe.

Nilipofika huko hakukuwa na mazungumzo yoyote kuhusu vifurushi vyangu bali wakati najiandaa kuondoka ndio akaja “clean” kuwa hakunua kwa vile mambo yaliingiliana na akaomba msamaha. Sasa huyu jamaa aliongopa ili kuulinda “Uanaume wake”.


Uongo ninaozungumzia hapa sio ule wa kikazi, kisiasa au kibiashara bali uongo katika mahusiano yetu ya kimapenzi. Uongo huo wanaotuambia mara kwa mara huwa kuna sababu yake, sio kwamba wanadanganya kwa vile wanapenda bali inawabidi au niseme kuna kuwa na ulazima unaopelekea wafanye hivyo.

Haya ni baadhi ya mambo yanayopelekea tudanganywe!

*Aibu kutokana na utoto wake, magonjwa asilia ktk ukoo wake au magonjwa aliyougua alipokuwa “kinda” na kuachia alama ya kudumu mwilini, ulongo hapo unakuja ili usijue matiatizo yake ya awali ambayo kwake ni aibu. Vilevile kama alikuwa “bozo” yaani wale watu wanaonewa na kila mtu na hawajui kujitetea zaidi ya kukimbilia kwa mama.

*Kutojiamini kwake, kwamba anakufikiria wewe ni “mtu wa hali Fulani” kutokana na zungumza yako au mavazi na wakati mwingine mahali unapofanyia shughuli zako sasa ili a-“fit” na yeye anajifanya kuwa yuko kwenye daraja hilo la juu kumbe masikini mtu mwenyewe ni msaka nyoka tu(mtu wa kawaida).

*Kutojiamini kwako, huenda wewe hupendi jinsi ulivyo(mnene kupita kiasi au mkondefu) na hali hiyo inapelekea yeye kutofaidi mwili wako kikamilifu kwani kila ukichojoa lazima uzime taa kisha unajikubika kwenye shuka na hakuoni ulivyoumbika bali anahisi tu kwa mikono (hey hiyo sio nzuri). Sasa ili aweze kuwa huru inabidi aongope kwa kukupa misifa lukuki ambayo huna ila anajua ungependa kuwa hivyo.

*Kuogopa kukuumiza au kuepuka kununiwa, mwanaume akifanya kosa kubwa siku zote huongopa ili asikuumize lakini baada ya muda Fulani huwa wanasema ukweli na kutoa maelezo ya kwanini walidanganya wakati ule…..ukinuna hapo utakuwa mjinga kwa vile swala lilitokea mwaka au miwili iliyopita, kwa wanawake walioendelea hushukuru lakini kwa mwafrika halisi sidhani mambo yataisha kirahisi hivyo na vikao vitaitishwa aisee!

*Kuepuka mzozo, mwanaume hulazimika kusema uongo ambao yeye anatambua wazi kuwa ndio unataka kusikia kwa wakati huo. Inafikia wakati anakubali kufanya kila kitu (hata vile ambavyo huwa hafanyi) ili tu usimsumbue akili yake na maneno yako kama umemeza kaseti vile.

*Kupumzisha akili na kuepuka maswali mwanaume atadanganya kuwa kazini kila kitu kilikuwa salama na mambo yamekwenda vema kabisa kama alivyotaka,lakini ukweli hapo ni kuwa yaliyojili kule hataki kuyahamishia nyumbani akijua wazi hutomsaidia kitu san asana utamzidishia maumivu ya kichwa tu.

Sina maana kuwa wanawake sio “smart” na michango yetu haiwasaidii wapenzi wetu la hasha! Kumbuka kila mwanaume anajua anaishi au yuko na mwanamke wa aina gani “akilin”, natumaini umenielewa hapo.

*Mwisho kabisa ni ule uongo usiokaribia ukweli na unatokea karibu kila siku hata kwa vitu vidogo na vya kawaida tu, yaani kwa kifupi ni wehu bin ujinga. Ikiwa wako yuko hivyo tafuta ustaarabu mpya.

Pole kwa maelezo marefu ila natumaini yatakusaidia nakufumbua akili yako kwanini hawa viumbe wanapenda kutumia uongo ili kuweka mambo sawa japokuwa wakati mwingine wanaharibu mambo.

Nakaribisha maswali, maoni na nyongeza ya uogo wa wanaume.
Ty.