Nenda taratibu lakini changamka!



Mara nyingi mwanawake huwa anapenda au kutaka kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na kila kitu kiende sawia kabisa bila matatizo, hii ni kutokana na sababu nyingi tofauti kama vile kuwa mpweke kwa muda mrefu, kuwa na "foleni"ndefu ya mahusiano mafupi na sasa anahisi kuwa wakatiumefika wa kukaa na kutulia na mtu mmoja, uoga wa kuachwa/kuumizwa, kuhisi ameachwa(left out) kwa vile rafiki zake wanawapenzi, kuhisi umri umekwenda n.k.


Haijalishi unauzoefu mbaya au mzuri ktk mahusiano yakimapenzi…unachotakiwa kufanya ni kutuliza akili na kucheza taratibu. Ukichukulia mambo taratibu itakusaidia sana kujua hisia zako juu ya mwenzio na pia kumjua/fahamu huyo mpenzi kabla mambo hayajawa “makini” hali itakayokusaidia kutoumia sana ikiwa atagundua kuwa humfai au wewe kutambua kuwa hayuko vile ulivyotegemea n.k.


Vilevile kwenda kwako taratibu kutamfanya huyo “mpenzi mpya” kuwa “comfortable” na wewe, kwa vile hautokuwa mtu wa kulazimisha mambo yatokee vile unavyotaka……..wanaume wengi hawapendi kuwa “pushed” kwa vile uhisi hawapendwi bali unapenda kufanikisha jambo fulani kama ktk maisha yako na sio kwenye maisha yenu “as a couple”.


Kumbuka kuwa wanaume hutumia uongo mwingi ili “washinde” na wakupate, hivyo kuwa mwangalifu najifunze “kuchuja” maneno/mistari yao wanapokushawishi/tongoza uwe nao, mara nyingi hutoa ahadi nyingi ambazo hu-“sound” kama wanaji-“commite” kwako kabla hata hujawajua vema.


Wewe kama mwanamke unatakiwa kuwa makini, msikivu, mwelevu na mwepesi kuhoji ikiwa utahisi unayoambiwa ni “too much….too soon”, sio macho chini na kila kitu….Ok, haya, sawa, ai wewe……ndio…..wasema kweli mjuba…hihihihi..n.k.……changamka!


Kumbuka kitakacho kufanya umdondokee mtu kimapenzi kabla hata ya kungonoana sio muonekano wake tu (au pesa kwa wengine wazembe-wazembe) bali kumjua kiundani baada ya kuzungumza nae……unapomhoji mwenzio ni rahisi kujua uta-offer nini kwenye uhisiano ili uwe bora na yeye atachangia vipi ili mtoke “pea” nzuri na ya muda mrefu.


Maelezo yake kutokana na maswali yako yatakuwezesha wewe utafakari na kufanya uamuzi wa busara hali kadhalika maswali yako yatamfanya yeye afikiri zaidi ikiwa ni myeyushaji/muongo lakini “anakutaka” basi anaweza kubadili yote aliyosema/ahidi jana kwani kagundua kuwa wewe sio wa kudanganyika…..na akiendelea hamtofika mabli….hii yote nitakuwa imetokana na kuchangamka kwako kwenye kuhoji pale ulipohisi jamaa natoa ahadi kamavile ninyi ni “couple” tayari kumbe ndio kwanza mna-date.


Kumbuka mtu anapoku-“date” haina maana kuwa mko kwenye uhusiano na mara nyingi hushauriwi kufanya ngono ktk kipindi hicho……”date” inaweza kuchukua siku tatu mpaka miezi 4 kabla hujajitolea mwili wako.

Unaswali?

Comments

Anonymous said…
Sasa nina swali kwako dina mfano mimi na mpz wangu mara ya kwanza kabisa kukutana akaanza kutuma vijikadi,mara baada ya wiki moja tukakutana tukaongea kidogo within a month tukangonoana ila kwa mimi ndo alikuwa bf wa kwanza, tupo pamoja mpaka leo tuna miaka 5 pamoja na pia sasa tupo kwenye mipango ya harusi je nilikosea kungonoana naye mapema.??najuta saa nyingine kufanya naye mapema.
Anonymous said…
shosti unajua ukisema date wengine hatuelewi maana huku Bongo mambo ya kudate Mh! please tufafanulie specifically mimi binafsi ukisema unamdate mtu fulani ni nini haswaa maana yake!
Simon Kitururu said…
DI!Mara nyingi wanaume tunadanganya pale tunapolazimika kudanganya ili kupata kitumbua. Hii inatoke kutokana na wanawake kutuwekea ugumu kuanza tu kumueleza ukweli kutokea ulipostukia matamanio. Lakini pia wanabinti mkumbuke kuwa hata kama mwanamme anampenda mwanabinti, date ya mpaka miezi minne inatakiwa iende kinamna ambayo haimtesi mwanauume. Kwa sababu , pamoja nayote , unaweza ukatengeneza hali ambayo ikafanya mtu asubirie na akionja tu akate tamaa ya kuendelea na muonjo kutokana na hisia alizojenga kutokana na kipindi cha msubirio.Nenda taratibu, lakini kuwa makini na jinsi gani na mtu gani unamlenga katika utaratibu. Kumbuka watu huachana hata kama wamekutana katika taratibu zilizoandikwa katika vitabu takatifu kutokana na na ubinadamu binadamu alionao. Kumbuka wote hatuko sawa.
KKMie said…
Anony wa 4:45am, nafikiri ulienda vizuri na hakuna ulichokosea.

Kwa vile alikuwa wa kwanza ikiwa namaana ulikuwa bikira nadhani ungesubiri zaidi ya mwezi mmoja....nadhani ndio mana unapata hisia za kujua kumpa "kidude" mapema......lakini kama mnapendana it's all good.

Kila lililo jema ktk maandalizi ya kufunda ndoa na maisha marefu ya ndoa.

Asante kwa ushirikiano wako.
KKMie said…
Simon wa Kitururu mwenyewe.....where have u bn? I've bn searching eveywhere....

Asante sana kwa maelezo yako.
KKMie said…
Anony wa 4:04PM, "date" ni kutoka na mtu anaekuvutia/unaemtaka lakini bila ya kuwa nae kwenye uhusiano.....akiridhika na wewe au wewe kuridhika na yeye na mkawa tayari basi ndio hapo huamua kuanzisha uhusiano wa kimapenzi....kwa Bongo nadhani itakuwa ile "stage" ya kutongozana na kualikana kwa ajili ya kinywaji/matembezi n.k. sina kiswahili kizuri cha malezo yangu.

Ni matumaini yangu wasomaji wengine watakinyooshakiswahili ili uelewe vema.
Simon Kitururu said…
Di!Nipo . Au niseme nimerudi:-)