Monday, 10 December 2007

Mwanamke ni "Victim" bila kujijua!
Leo na-promote Uanamke….

Wiki iliyopita nilikuwa kwenye sherehe za kamuagano (Sendoff) na Kesho yake nikaenda kwenye sherehe za ndoa..….kama mjuavyo penye wengi ndio mahali pa kupata mengi sio?

Nilikuwa nimekaa na wamama Fulani wenye uzoefu mzuri tu ktk maswala ya ndoa, wakitoa ushauri, nasaha, maonyo n.k kwa binti aliyekuwa akienda kuanza maisha mapya ya ndoa ili akawe mke mzuri.

Kama kawaida yangu mimi ni mtu wa kudadisi na kuhoji mambo mengi ila ngono ndio hunivutia zaidi, hivyo nilitaka kujua ngono ikoje kwa wanawake hasa kwenye maisha ya ndoa au niseme ndani ya ndoa.

Wachache walikuwa sio wazi sana kama kawaida ya wabongo wengi hasa watu wazima (nadhani waliona mimi katoto Fulani hivi kumbe ni kamwili tu haka)……nilivyoona wanadengua nikahamia kwa kwa wanawake vijana lakini walio kwenye ndoa na kuuliza tena “wao kama wanawake ngono ikoje ktk maisha ya ndoa?”.


Kila mtu akatoka na majibu yake kutokana na uzoefu wake lakini nilivutiwa na maelezo ya wale ambao waliolewa wakiwa bikira, wale wanaotumia madawa ya kuzuia mimba na wale wanaosukumwa/lazimishwa kufunga kizazi baada ya kupata watoto fulani…….

Nikapata jawabu kuwa wanawake wengi ni “victim” ndani ya ndoa/uhusiano wa kimapenzi bila wenyewe kujijua…..nasema hivyo kwa sababu zifuatazo:-

Akizaliwa ni binti wa mzee Fulani……..Akiolewa anakuwa mke wa Fulani…….Akizaa anakuwa mama Fulani…….alafu akijaaliwa nakuwa bibi fulani anamalizia na swala zima la kukabiliana na kukoma hedhi…..Kila hatua ya maisha yake mwanamke anakabiliana na majukumu lukuki……mwanamke huyu hajawa na nafasi ya kuwa yeye na kufurahia maisha kama yeye bali siku zote za maisha yake amekuwa akiishi kwa ajili ya watu wengine.


*Hebu tumuangalie mwanamke huyu anapofunga ndoa/ingia kwenye uhusiano…..

1)-Mimba usiku wa harusi (usiku wa kutolewa bikira).
-Mwanamke kafunga ndoa akiwa bikira na kwa bahati mbaya au nzuri wanashika mimba usiku huo au wakati wa fungate…….binti huyu hajui lolote kuhusu ngono wala utamu wake….usiku huo anafanywa kwa mara ya kwanza na mume wake anajisikia safi kuwa mkewe hakuguswa na mtu mwingine bali yeye….


Hisia za kumiliki zina mjia na bila kujali maumivu ya binti yule, haki yake ya kupata utamu au kufurahia tendo la ndoa….mume anajimalizia ndani kwa vile tu ni mke wake.

Baada ya miezi 9 mwanamke anajifungua anaanza kukuru kakara za malezi na kukabiliana na mabadiliko kutoka msichana kuwa mama…..mabadiliko haya huwa ni magumu sana as u can imagine.

Kwa vile mwanamke huyu hajui lolote kuhusu ngono na hakuwahi kufundishwa au ambiwa lolote hukusu maswala yamwili yeye anachukulia au kuamini kuwa kilichofanyika au kinachofanyika ni kawaida……binti anahisi kuwa labda anakasoro kwani akikumbuka huko nyuma aliwahi kusoma, sikia, kuambiwa kuwa ukifanya mapenzi unasikia utamu au raha…..au anaona mumewe anavyofurahia….lakini masikini yeye haijui na wala hajawahi pupate utamu huo.

Mwanamke anashindwa ku-share na watu wengine kwa vile anadhani hiyo issue ni nyeti sana na ni kinyume na maadili ya kitanzania au mila na destru za kwao…..hivyo maisha yanaendelea na watoto wanaongezeka hali inayoongeza mabadiliko ktk mwili wake na sasa kila unapofanya mapenzi yeye ni kilio tu kutokana na maumivu (kwa vile hapati hamu ya kungonoana wala utamu wake) hali hiyo inamfanya mwanamke huyu amkwepe mumewe kwa kutafuta sababu nyingine……..


Mwanamke anaenda kulalamika kwa Daktari wake wa Magonjwa ya kike na anafanyiwa vipimo inagundulika kuwa mwanamke huyu anaelekea kwenye kukoma hedhi au kikomo cha hedhi (Menopause) kwa mwanamke huyu wa kibongo aliye ndani ya bongo kupata hamu au utamu wa kungonoana ndio inakuwa basi tena……na she is only 40yrs old.


*Ofcoz huwezi kutegemea binti wa watu bikira awe akitumia madawa ya kuzuia mimba au akujie na Condom ili azuie mimba…….wewe kama mwanaume chukua jukumu la kujizuia ili usimtie mimba binti wa watu ambe hajui chochote kuhusu unachokifanya……


Hili halitokei kwa Bikira tu bali kuna wale wanawake ambo walibakwa hivyo kisha wakaja funga ndoa, wapo walijiingiza kwenye maswala ya ngono wote wakiwa bikira hivyo hawakujifunza kitu, vilevile wapo waliokuwa kwenye uhusiano na wanaume ambao hawajali hisia za mwanamke bali tama zao za mwili….nakadhalika!***********************************************
Waendesha "Kitchen party"......tumieni wasaa huo kuwa wazi zaidi na kuwaeleza/andaa hao watarajiwa watarajie nini ktk maisha yao ya ndoa, jinsi ya kukabiliana baada ya kujifungua......sio mnashupalia jinsi ya kumfurahisha, heshimu, pika mahanjumati, kuwa sexy (pendeza na kuvutia @all times) na kum-keep mume......there are more than hayo in any relationship.....kumbukeni kuwa mwanamke anabadilika jinsi miaka inavyokwenda.....huyo binti anahitaji kulijua hilo kwa undani zaidi.


Wapenzi wanaume.......jaribuni kuvuta muda na mshirikishe mwanamke umpendae kwenye swala zima la kuzaa…..pangeni na muelewane mzae baada ya muda gani…..ondoa “umilikikaji” kumbuka huyo ni mkeo lakini pia ni mpenzi wako……mpe nafasi ya kuujua mwili wake kabla haujabadilika.


Kaka zangu hebu chukua jukumu la kuzuia mimba badala ya kumuachia mwanamke, kumbuka kuwa yeye mayai yake hayatoki lakini mbegu zako zinatoka na kumuingia kwenda kujenga kiumbe hivyo wewe ndio mwenye ku-control hilo na sio yeye.

Ni vema kujadiliana au kujua kama mkeo/mpenzi wako yuko tayari kukabiliana na mabadiliko yanayohusisha uzazi, kumbuka kuwa kuoa au kuwa na mpenzi sio tiketi ya kum-mimba mwenzio (cum inside).


Wanawake.......ambao mnaamini kuwa kupata mimba au kuzaa na Fulani basi ndio utapendwa zaidi au kutoachwa…… nakushauri uache huo Ujinga na Ushamba…..


Only Kubali kushika mimba ikiwa unadhani kuwa ndio kitu unachokitaka, hakikisha unajua faida, hasara, matatizo ya mimba mpaka kujifungua na baada ya kujifungua, kuwa na uhakika kuwa utakuwa tayari kukabiliana na yote hayo.


Epuka kukimbilia kuzaa/achia mimba kwa vile jamii inakukandamiza/sukuma, mtaani kwenu kila binti anamtoto, unahofia jamii kukudhania kuwa wewe ni tasa, ili wakwe wakupende zaidi, ili mwanaume/mume asikuache au aendeleze huduma kiuchumi n.k.....


Sikutishi….bali nakwambia ukweli kuwa kushika mimba maana yake ni mabadiliko…….je unauhakika uko tayari?


Tuende na wakati sio ktk mikao na mitindo ya kufanya ngono tu bali kila kitu kinachoendana na ngono na matokeo yake......tujaribu kuwa Taifa lenye vijana wajanja ei!.....sio tunapelekwa pelekwa na kasumba za kizembe.


Endelea kuwepo ili nimalizie vipingele 2 vilivyobaki….

11 comments:

Anonymous said...

Hi Dinah!
hivi,ina maanisha kuwa bikira ya mwanamke hutoka tu baada ya kufanya ngono?kama kuna mambo mengine yanayoweza sababisha hilo,ni yepi?
aksante

Dinah said...

Bikira as "utandu" pale juu ya uke inaweza kutoka kwa sababu nyingi kama vile kuugua kwa muda mrefu(kuwa na afya mbaya), kuwa mwana michezo/mazoezi,lishe yako (diet), shughuli ufanyazo kila siku kama vile kupanda milima(zoezi hilo), kubeba vitu vizito n.k.

Bikira as "hujawahi kuguswa na mwanaume" inatoka siku utakayofanya mapenzi/ngono.

Hivyo unaweza usiwe na utandu lakini ukabaki kuwa bikira kwa vile hakuna uume/mwanaume aliingia/fanya ngono na wewe.

Asante kwa ushirikiano wako na karibu tena.

Anonymous said...

This is still confusing for most of men.because the only way(at least known to be) they can believe they have met a virgin,is the difficulties one might face while having sex with a virgin girl!during penetration.
is this the same for two cases?thats for one who lost her virginity through sex,and the other one because of daily activities!
thax

Dinah said...

Kupata shinda kuingia/muingilia mwanamke sio lazima awe bikira...ukiwa nauume mkubwa ukakutana na binti mwenye uke mdogo bado utaingia kwa shida nakusababisha maumivu.

Bikira mwenye utandu na yule asie nautandu wote ni bikira kwa vile hawajaguswa/fanya ngono kabisa.....ni wapya sio?

Wote watapata matokeo ya aina moja.....ila utokaji wa damu unaweza ukawa tofauti kutokana na ufanyaji wa mwanaume husika pia ukubwa wa uume wake wakati wa kufanya hivyo.

Tujaribu kubaki kwenye swala la u-"victim"....ninyi kama wanaume mnawasaidia vipi wanawake as wapenzi wenu?

Ty.

Shyguy said...

Salaam dada Dinah,mi ni mwanaume na mpenzi mkubwa wa hii blog,leo umenishtua kidogo na `article` yako ya kuwa mwanamke ni `victim`na kuwaandika sisi wanaume kama wanyanyasaji wa hao mabinti.
Kwanza,Wote tukizaliwa mwanamke au mwaname tunakuwa ni watoto wa fulani,tukiowa baba fulani, tukijukuu babu fulani tunakua na hayo majina mpaka m/mungu akituchukua.Wote tunakuwa na majukumu sio wanawake peke yao nakataa kwa nguvu,kumbuka ukitoka kwenye famlia za ki-maskini ukiwa mwanamme peke yako uwe na kazi nzuri au mbaya ,ujuwe family nzima inategea uilee wewe na kama umeowa maskini mwenzako ujue unafamili mbili za ku -support,wanawake wangapi wanakutana na hayo???.kuhusu kuzaa ni makubaliano ya wenye ndoa ni kweli kunakuwa na`pressure` kutoka upande wa kiume,lakini kumbuka mwanamke akizaa mwanaume ndio anakabiliwa na majukumu ya kumtunza huyo mtoto, kwa hiyo hatupati `easy ride`na huyo mtoto atataka kula,kuvaa,kwenda shule nawale waliooa wenye makuu,mwaka ukipita mwanamke atataka¬birthday, na kama ndio mtoto wa kwanza mwanaume utataka kumridhisha mkeo na kufanya uwezavyo kuifanya hiyo sheree,kama huna hela ndio mkopo unakuhusu!.
Kuhusu usiku wa kwanza kutolewa bikra,sioni point yako kama ina nguvu,una`assume` kila mwanamke anaolewa bikra!sio kweli,wakati mwengine wanawake ndio wa juzi wa mambo yakitandani kuliko waume waliooa,hivyo wanaume wankuwa kwenye hali ya kujiona labda watadharaulika pia kuna wengine wenye uume mdogo ambao wasiwasi wao unaweza kuwafanya hat wasiwezekufanya mapenzi na wake zaoSIKU YA KWANZA!!,hapa umesahau kushahuri madada wengine jinsi ya kuwasaidia wanaume wenye matatizo haya,baadae umewafanya wanawake wajione kuwa wao ndio wanaopata dhahama! usiku wa ndoa!!.
Kuhusu kubakwa kwa mwamke ni kweli wanaume inabidi kuwa waelevu kam wake zetu wamepatwa na hayo,lakini huwezi kulaumu manamme kwa suala hilo inabiidimwanamke awe shupavu kumwelezea mme wake matatizo kama hayo na kama mwanamme kampenda mpaka kumuoa basi atamliwaza mpaka afarajike.
Ndoa sio njia ya kumfanya mwanamke awe victim ni watu wawili waweze kuishi pamoja kwa furaha,kuna wanaume wanaadhilika sana kwenye ndoa na watemi wao ni wanawake ambao wewe unawaita `victims`,wanaume wanapoteza nyumba,haki ya kuwaona watoto na hata kazi kwa sababu ya wanawake,naelewa labda mazingira mengine kama huko bongo wanawake bado mnabanwa lakini kuna mazingira mengi,hasa kama hapa ughaibuni,tumewaleta wanawake zetu kutoka nyumbani ,yanatutokea puaniiii!!.Lakini bado nna hakika maisha yetu watanzania wengi si ya kutaka kutesana! ni wachache wako hivyo bado nina mategemeo hik siku nitakutana na mmbongo mwenzangu ambae tutaishi maisha ya upendo na kuheshimiana hapa ughaibuni au uko bongo!!.

Hassan said...

nimewasoma wote lakini naona mchangiaji hapo juu hujamuelewa mama. Nilivyomuelewa ni kuwa wanawake wengi wanakuwa kama vile wanaonewa kutokana na mfumo dume tulionao wanaume na kasumba zilizojengeka miongoni mwa jamii ya Kitanzania ambazo wanawake wenyewe wanaziendekeza.

Kasumba na imani hizo zinamkandamiza mwanamke hasa linapokuja swala la kufurahi ngono kama mwenyewe dinah alivyoeleza.Mwanamke ni victim kwenye swala la ngono sio maisha kwa ujumla.

Anonymous said...

Dinah asante kwa mada hii, wewe ni mwanamama unaeangalia mambo kwa undani sana na ninakupa heko kwa hilo.

Shyguy nakubaliana na sehemu kidogo ya maelezo yako. Mwanaume akimtia mimba mwanamke hakabiliani na mabadiliko tunayokabiliana nayo sisi wanawake. Wanaume huwa mabaki kama mlivyo na sisi tukisha zaa basi ndio inakuwa shauri yetu.


Mimi ni mama wa watoto wawili naninapenda kuwa wazi kwa wanawake wengine kusem akuwa kuzaa kunakubadilisha vibaya mno kama mwanamke na wakati mwingine mumeo anakuwa kama vile havutiwi tena na wewe kimapenzi na anakuwa pale kwa vile ni mkewe na umemzalia au pia kwasababu akitaka kidude anapewa lakini utaona kabisa haenjoy kama zamani kabla hujazaa.

Nilipozaa mtoto wa kwanza sikuweza kufanya mapenzi na mume wangu kwa mwaka mzima kwa sababu nilikuwa sijisikii. Wakati mwingine nilikuwa najilazimisha tu ili asiende kutafunta nje.Ningejua wala nisingezaa mapema naninakubaliana na dada dinah kuwa ni jambo la muhimu kuwa na uhakika kuwa kuzaa ndio unataka na uko tayari kuface changes.

Anonymous said...

Hivi wenzangu yameshawakuta kuwa mpenzi wako anaangalia wanawake wengine nyuma sana mpaka anakukera?maana wangu yaani mipita mahala au mkiwa mmekaa mahala wakipita wasichana anageuka sana mpaka naona sasa sijui nifanyaje nimeongea anasema niache wivu.

Anonymous said...

Dinah tusaidie kuhusu hilo swala la waaume kutolea macho wanawake wengine hata kama uko nao. Hata mimi mume wangu anatabia hiyo ambayo hunifanya nijisikie vibaya.Asante

Anonymous said...

dada hapo juu 11.17pm,tell ur man to respect u .he cant be looking at other women while u re there ,raise ur eye bro ,confront him ....

Dinah said...

Anony wa 3 wa mwisho, napenda mtambue kuwa mwanaume kukupenda au kuwa na wewe haina maana hawezi kuvutiwa na mwanamke mwingine aliye mzuri kukuzidi au mbaya kukuzidi, mwenye umbo zuri kukuzidi au baya kukuzidi....kutamani sio kuchukua...wewe ndie uko nae wasiwasi wa nini?

Kuna wanawake wanatabia hiyo pia tena mbaya zaidi husifia wanaume wengine mbele ya wapenzi wao.

Swala muhimu ni kuwa wazi kwa mpenzi wako na kumwambia kuwa haufurahishwi na tabia yake ya kukodolea macho wanawake wengine akiwa na wewe.

Asipojirekbisha basi ujue ni hulka yake(ndivyo alivyo) na haiwezi kubadilika au kujizuia hivyo unachotakiwa kufanya ni kuungana nae ktk kushangaa na utoe comments pia...kama binti ni bomba mpe sifa yake, kama ni kikaragozi ponda kama kawaida na utakuwa Okay.

Kila la kheri.