Tuesday, 11 December 2007

Mwanamke ni "Victim" 2 & 3!


2-Tumuone mwanamke huyu ktk kuzuia mimba.

Mwanamke siku zote ndie anaeachiwa swala la kuzuia mimba, sote tunafahamu wazi kabisa kuwa matumizi ya madawa haya ya nabadili afya ya mwanamke, yanabadili utaratibu mzima wa kupata damu ya mwezi (hedhi) kwamba kuna baadhi ya wanawake huenda mara mbili hadi tatu kwa mwezi.


Wengine hawaedi kabisa (jiulize damu hiyo inakwenda wapi wakati ni lazima itoke ikiwa yai halijarutubishwa) hali hiyo husababisha mkanganyiko wa chembechembe asilia na hivyo kusababisha SARATANI ndani ya mwili au kutopata mtoto/watoto tena….kila ukipata mimba inachoropoka (inatoka sio kwa kudhamilia) n.k.


Linapokuja swala la kumalizia ndani mwanaume hujitoa kabisa na kusukuma jukumu lakuzuia mimba kwa mwanamke. Natambua kuwa hakuna madawa ya muda mfupi yakuzuia mimba kwa wanaume lakini kuna bidhaa ambayo ikitumiwa vilivyo mimba itazuilika, sasa kwanini bidhaa hii (Condom) isitumike kwa nyote wawili badala ya “kusakizia” mwanamke jukumu hilo as if yeye ndio mhusiaka mkuu wa kupata ujauzito?


Ile tabia au niseme kasumba ya “situmii condom kwa vile inapunguza ukaribu wangu na mke/mpenzi wangu” haina ukweli wowote, kuwa karibu na mpenzi/mkeo wako sio lazima umalizie ndani au ugusanishe ngozi yako ya uume na ngozi yake ya uke kwa ndani!Kitendo cha wewe kufanya nae mambo mazuri na kwa ufundi yatakayowafikisha kwenye hatua hiyo tayari ni ukaribu, jinsi unavyo zungumza nae, jinsi uanvyomshika, unavyomheshimu, mthamini, unavyo onyesha mapenzi,msikiliza n.k. wakati mnafanya tendo hilo takatifu ndio mambo yatakayo kufanya uwe karibu nae a.k.a “Intimately” na sio kupiga bao ndani.


Mwanaume jaribu kuwa mbunifu na mtundu ktk anga nyingine ili kuwa “Intimate” na mkeo/mpenzi wako zaidi ya nyama 2 nyama ili kuepuka mimba na wakati huo huo kumsaidia huyu mama kulinda afya yake ili asiendelee kuwa “victim” ktk uhusiano wenu.3-Tumuangalie mwanamke huyu ktk Ufungaji wa kizazi.

Baada yakujipatia watoto Fulani ambao mnadhani kuwa wanawatosha au ndio manaweza kuwamudu na hivyo kufanya uamuzi wa kufunga kizai 4 good ili muweze kufanya mapenzi bila kuhofia mimba/mtoto tena, kama kawaida Mwanamke husukumwa akafunge kizazi.


Mwanamke huyu sina uhakika kama ni kasumba, ujinga, kutokujua, kuwa tegemezi au? Habishi “in good way” wala haulizi/hoji kwanini yeye ndiye anaepaswa kufanya hivyo na sio mumewe/mpenzi wake au wote....waende mguu kwa mguu kwenda kufunga kizazi?.


Mara nyingi (nimeshuhudia kwa masikio yangu) mwanaume anakuja na sababu kama “watoto wakifa kwa ajili au magonjwa na nikataka kuzaa tena nitafanyaje?”…..Ukifa (mke) na nikaoa/kutana na mwanamke mwingine na akataka kuzaa na mimi nitamwambiaje?”…..ikitokea tumeachana (peana talaka) na nikaoa tena nakutaka kuzaa na huyo mwanamke nitafanyaje?”……

Sasa huoni kuwa sababu zako za “kibinafsi” zinamhusu pia mwanake huyo? Hayo yote yakitokea kwake yeye atafanyaje?

Nitashukuru kama nitapata maoni, mawazo, maelezo tofauti kuhusu hili au ukiweza ushauri zaidi kutokana na uzoefu wako……sote tunajifunza na nivema tukiweka mambo wazi ili tujifunze kwa kina zaidi.

Asante sana kwa ushirikiano.

4 comments:

Anonymous said...

dinah
mimi ni single mom na nina mtoto mmoja im on early twenties.nilibadilika sana kuw ana mtoto i have a very low sexual appertite,i used to take contraception pills i had put on more than 2 stones ,its ovious he wasnt attracted to me anymore im couple of pound lighter ,my litle girl amekuwa shes very happy ,i ve someone i deeply love n who loves me thinking of taking our relationship futher(marriage)i was single for 2 yrs before i met him and after i met my daughters dad.wanawake wote plz dont let a man make u feel u worth nothing we re sexy,make ur self look as hot as ever u know what i mean??????i have been strong for my child and im happy i did right decision pills do ur body wrong alot
good luck

MAMA Q said...

Mambo dear!!
Duu nilimiss hiki kijiwe kwa sana tu,Yaani hapa dinah umenigusa sana mana nachanganyikiwa nifanjeje kuhusu uzazi wa mpango,mana pills naskia si nzuri as ukisahau kumeza umeibeba,sindano nazo siwezi tumia as nanyonyesha ,T nayo mara naskie ina kansa,condom nazo naskia zinaleta uke kuwa na majimaji ajili yamsuguano,kalenda nayo ilishanishinda as mzunguko wangu si systematic,kufunga naogopa as ya Mungu mengi...yeleuwiiiiiiiiiiiii kichwa inaniuma as sijui nifanyeje.
Naomba ushauri wako my dear.

PapaaK said...

Kwako Dinah, madamu umekaribisha maoni ngoja na mi niseme kidogo

Nitazungumzia kipengele kimoja tu kilichonikuna cha intimacy, condom na uzuiaji mimba. Natofautiana na wewe kwenye maelezo yako kuwa unapotumia condom hupunguzi intimacy na mpenzi wako..kwa hili nipo tofauti kidogo, naamini ni kweli kwa kisi fulani kwa sababu nikiliangalia kiasili maumbo yetu ya uzazi hayajaumbwa kutumia condom, ilimaaanishwa tangu mwanzo kuwa apo ni mwili kwa mwili, nyama kwa nyama na sio nyama kwa mpira...ndio maana kumekuwa na dhana hiyo na nadhani hata ukiwauliza wanawakwe wengine watakwambia kuna tofauti, seuze wanawake.
Suala la kuzuia mimba linapaswa kujadiliwa na wote wawili kabla ya kiyu chochote, na nadhani hili pia kwa watu walio makini lazima wakubaliane lengo la uhusiano wao ni nini na hatari zilizopo. Na asikudanganye mtu kupiga bao ndani kuna raha yake na nadhani hata kwa wanawake wangependa hiyo...na inaongeza sana ukaribu..kwa wale waliokwisha kuexperience hii watakubaliana na mimi...ila kama nilivosema fikiri kwanza huyo mtu uliye naye mna malengo gani kiuhusiano kabla ya kuanza kungonoana.

Dinah said...

mama q, papaak na anony hapo juu asanteni sana kwa maelezo yenu hakika yatawasaidia wasomaji kwa namna moja au nyingine.