Thursday, 4 October 2007

Maana ya Penzi!


Penzi halina dawa, penzi halihusiani kabisa na kufanya ngono(hivyo kubinuka aina nyingi za mibinuko haina maana ndio utapendwa au unapendwa zaidi) penzi huja "naturally" huitaji kulazimisha wala kwenda kwa Mganga....Penzi huitaji na huchukua Muda.

Lakini je, penzi ni nini hasa?
Watu wanasema penzi halielezeki au halina tafasiri maalumu kwamba kila mtu anamaelezo yake kuhusu penzi na maelezo hayo hutegemea zaidi na uzoefu wake.

Mimi kama Dinah nadhani penzi ni hisia zenye nguvu ya ajabu za mtu Fulani juu ya mtu Fulani, hisia hizo hazijalishi muonekano(mavazi, sura, umbile n.k), utajiri, umri, Elimu, aina ya maisha au tabia.

Hisia hizo humfanya mtu ashindwe kufanya mambo ya kawaida ambayo huyafanya kila siku kwa vile kichwani anakuwa anamfikiria yule ampendae, hisia hizo zinaweza kupelekea mtu kubadilisha personality na tabia yake hasa pale unapofanikiwa kuwa na huyo umpendae.

Unapofanikiwa kuwa/mpata yule umpendae huwa unapata raha ya ajabu kila unapomuona, inakuwa ngumu sana kuwa mbali nae. Hisia hizo zikikomaa hukufanya uhisi maumivu yake ikiwa anaumwa, umemuudhi au kaudhiwa na mtu mwingine, anapokuwa na huzuni mpenzi wako hakika utahisi huzuni n.k.

Wewe unafikiri Penzi ni nini?

Maelezo yako yatasaidia wasomaji wengine kama wewe kujitambua kama kweli wanapenda,wanatamani au wanafuata mkumbo.

Karibu sana.

9 comments:

Anonymous said...

dada dinah,nashukuru sana,jamani mimi ni mwanamke ambaye navumilia sana ,mpaka naumia ,sasa mume wangu ananiabuse kwa lugha nyingine ,na nitabia yake nimejariu kuongea naye naona habadiliki,kwakweli,yeye ni mtu wa kunitukana na kugomba mbele za watu na mengineyo,sasa dada dinah,mimi nilipata hali ya ajabu sana mpaka naogopa sasa sijui kama kuna watu washawahi kuyatokea,moyo wangu ukampenda mwanaume mwingine ,tena hata sijamzoea ,sijawahi kumkiss wala chochote,ila moyo wangu tu unamuwaza yeye,je dada dinah ,hii ni kawaida kweli ,sijielewi ,kwakweli ,sasa hilo ni penzi gani jamani ,samahani kwa kutoka nje ya mada ,ila nisaidie kwakweli,hiyo ini?
asante sana.

Dinah said...

Mh! Huyo mumeo ni wazi kuwa hakuheshimu na wala hajali hisia zako.

Hisia hizo ni za kawaida kabisa kwa yeyote ambae yuko kwenye uhusiano kwasababu nyingine sio penzi, anasumbuliwa/nyanyaswa na mpenzi wake, hana raha au amani ktk uhuano n.k.

Huenda likawa sio penzi kwa vile uko ndani ya uhusano mbaya kwamba hupati penzi hali inayokufanya utafute "affection", "comfort" na mapenzi kutoka nje.

Mpaka uwe nje ya uhusiano ulionao ndio utajuwa kama ni penzi au la!

Mimi nakushauri uchukue "break" kwamba mtengane (msiachane) bali muwe mbali-mbali kwa muda.....usimwambie kuwa umechoka na dharau zake bali semakuwa unakwenda kumuona mama/baba/bibi.

Ktk kipindi hicho jaribu kutafakari jinsi gani unampenda mwenzio na jinsi yeye anavyokupenda(well unadhani anakupenda kiasi gani) unataka nini kutoka kwa mpenzi wako na je nyote wawili mfanye nini ili kujenga uhusiano mzuri na wenye afya.

Ktk kipindhi hicho utajua kama kweli unampenda mumeo au unamuhitaji kutokanana sababu nyingine kama watoto, uchumi n.k.

Likizo hiyo ni muhimu kwani vitendo ulivyovieleza ni wazi kuwa vinaweza kukusababishia matatizo ya kiakili.

Chochote utakachokifanya wakati huo wa likizo hakikisha hufanyi jambo ambalo litakufanya ujute baadae.

Hakika wasomaji wengine watakupa ushauri zaidi.
Kila la kheri.

Anonymous said...

dada dinah nashukuru kwa ushauri wako,yaani umejuaje ,niliamua kwenda kusoma kidogo ,nilipata unafuu kidogo ,ila niliwamiss watoto sana,na mimi nimetoka kwenye familia ambayo wazazi wako pamoja mpaka sasa hivi,naogopa sana watoto watachanganyikiwa ,wakati mwingine naona bora nivumilie,ila ndio hivyo tena,mimuoga sana ,hata sijui nifanyaje,usiku mwema.

NDAKI GOMBERA said...

Dinah mambo vip?Kwanza nikupe shavu,upo juu ka mfuko wa shati.Nakukubali sana mtu wangu kuanzia DHW,BC,na kwenye blog mbalimbali.

Ushauri uliompatie huyo swahiba laiyokutwa na maswahibu ni mzuri sana.

Mimi binfsi kama ningekuwa na uwezo ningewashauri watu wanapoanza mahusiano wajitahidi kutumia njia za uzazi wa mpango kuepuka kwanza kupata watoto mapema.

Nasema hivi kwa sababu,naona mahusiano mengi yanaanza kuyumba kwa badhi ya watu wasio na mapenzi ya kweli hasa pale wanapopata mtoto.Kuna vidume wengine wanataka kuendelea kwenda ngwasuma hukukamuacha mrembo wake kalala na mtoto.Saaasa hao ndio shida inapoanzia.!

Mimi nashauri wakinadada wajitahidi kubana ili mimba zisiingie(ila sija sema wabane kungonoka)ilo la pili ni hiari yenu maana ndio interview(lugha ya malkia kuonesha msisitizo)Mimi ndio ushauri wangu.

Dinah yaani naipenda sana page yako lazima kila mara nipite hata kama sikunyingine hujaweka chakula.

Weekend njema wasalimie tz

Dinah said...

Ndaki nashukuru sana kwa ushirikiano wako. Hilo swala la kujizuia kuzaa mapema nilishawahi kulizungumzia sana kwenye forums tofauti lakini watu wengi walikuja juu na baadhi kusema kuwa naiga "uzungu".

Hapo umegonga Ikulu, tabia ya wanawake kukimbilia/jiachia kupata mimba ili mwanaume asikuache au aendeleze huduma za kiuchumi uamuzi wa kijinga.

Vilevile tabia ya wanaume kuwasukuma/lazimisha wanawake kuwazalia watoto mara baada ya kufunga ndoa ni uonevu na ubinafsi.

Sote wanaume na wanawake tunatakiwa kushirikiana when it comes kwenye swala la kuleta kiumbe kingine Duniani.

Mwanaume unatakiwa kutambua kuwa mwanamke anapozaa ni wazi kuwa atakabiliana na mabadiliko mengi ya kimwili, kiakili na kisaikolojia hivyo kabla ya kufikia uamuzi wa kuzaa ni vema kujadali na kuwa tayari kukabiliana na mabadiliko hayo.

Kitu kingine kinachonishangaza ni tabia ya wanaume (huenda wa wanawake) kuacha matumizi ya Condoms kwa vile tu wameoana, tumieno condoms ili kuzuia maradhi na mimba.

Tatizo langu nikianzaga kuandika yanakuja tuuu.......ngoja niishie hapa.

Nakutakia siku njema Ndaki!

Anonymous said...

Dinah kama penzi halihusiani na Ngono kwanini watu wakitaka ngono husema naomba penzi au nipe penzi?

Mimi nafikiri maana halisi ya mapenzi ni hivyo ulivyosema + ngono, bila ngono penzi halinogi Dinah.

Keep it up girl.

Anonymous said...

Mambo,
Love is the most beautiful thing in the world ; is felt , perceived is unselfish, understanding, kind and sees with the heart and not with the mind.

Love is the answer that everyone seeks, is the language that every heart speaks.
Yet not seen.

Is born out of passion, excitement and happiness and it's what makes us all to do things together with all the complexities that do exist in the world today. But with love , respect , tolerance and admiration for one another, one will be able to reach out and makes a difference in other people's lives.

There is more you can accomplish if two people pull together rather than one doing it all.
Above all , love is the key to happiness.

I'm still learning kiswahili when I'm done in 3yrs I'll comment in kiswahili.

Nakupenda sana.
JJ.

Dinah said...

Anony wa 3:50, asante kwa ushirikiano wako. Kweli watu wengi wanachanganya mapenzi na ngono ambapo kwa "case" hii tunaita kufanya mapenzi.

Kkt hali halisi huwezi kufanya mapenzi na mtu ambae humpendi na badala yake utafanya ngono au "hit & run" kama ambavyo vijana siku hizi wanasema.

Kufanya mapenzi ni tendo pakee litakalo kufanya wewe na mpenzi wako kuwa karibu zaidi, ku-share vitu ambavyo huwezi ku-share na mtu yeyote kama mate, harufu ya miili yenu, mapigo ya mioyo yenu, majimaji maalumu yanayozalishwa na hisia zenu za kimapenzi, pumzi zenu, raha ya kufika kilele n.k.

Mnapofika kileleni wewe na mpenzi wako ndio pekee mnajua utamu wake, ninyi pekee mnajua mabadiliko ya sura zenu na milio tofauti ya raha mnayoitoa, ni wewe na yeye tu ndio mnajua mirindimo miili yenu n.k. hali hiyo hukufanya uwe karibu zaidi na mwenzio ambae unampenda lakini kufanya hivyo sio penzi.

Nadhani utakuwa umenielewa, kama bado karibu tena.

Dinah said...

Hahahaha JJ in 3yrs? Kiswahili isn't that hard u know.

Thanks for your comment.

Teamo.xx