Monday, 8 October 2007

"Jinsi ya kupenda kwa vitendo"

Kama ilivyo mambo mengine kuwa “affection” ni swala la kujifunza, baadhi ya wanaume waliokuzwa/kulia kwenye jamii yenye mfumo Dume (Waafrika kwa ujumla) huwa hawajui kuonyesha hilo hitaji, embu tuliite “kupenda kwa vitendo” hivyo huenda sio kwamba hataki bali hajui.


Kwa maana hiyo sio mbaya ikiwa wewe mwanadada ukamfundisha nini cha kufanya, ikiwa na wewe ulikuwa huji basi jifunzeni wote ili kuwa una uhusiano bora wenye furaha.


Mpaka hapo umeelewa nazungumzia nini sio? Sasa Ili kufupisha maelezo nitaorodhesha mambo machache ambayo wanawake wengi huwa tunapenda kufanyiwa (kiujumla ukiachilia mbali utofauti wetu) ili tujue kweli tunapendwa kihisia na kivitendo.

1-Hakunakitu wanawake tunazimia kama kukumbatiwa nakupigwa busu mara kwa mara.

2-Kabla hujakurupuka kitandani hakikisha umekumbatia na kubusu hata kama kalala(hakuna raha kama kuamshwa na busu au mkumbatio).

3-Mwmabie jinsi gani unampenda na unavyopenda chapati/mayai/viazi alizopika au hata jinsi alivyoandaa mlo wa asubuhi.

4-Wakati unatoka ndani kumbatia chap-chap na busu kiduchu ndio utokomee kazini, hata kama mnatoka wote kwenda kwenye kituo cha daladala unafanya hivyo kabla hujakanyaga vumbi la nje.

5-Onyesha unajali kwa kumjulia hali kwa sms au sauti mara baada ya kufika kwenye mihangaiko yako na vilevile kumbuka kufanya hivyo kabla hujaondoka eneo la shughuli zako pia hakikisha unamueleza utakuwa saa ngapi nyumbani au kama kuna mahali unapitia basi mfahamishe utakuwa huko kwa muda gani n.k.

6-Ufikapo nyumbani kumbatia na busu mdomoni sio shavuni, badala ya kukimbilia kusema yaliyojili huko utokako.

7- Mnunulie vijizawadi mara kwa mara, wazaramo hununuliwa Khanga au hereni na mikifu ya dhahabu, Wazungu hununuliwa maua, kadi au vidani vya madini tofauti, kuna wengine ukipeleka kitoweo (aina ya nyama) basi umemaliza kezi mwana mama anafurahi kweli-kweli sasa wewe fanya kile unachomudu………..hey sio kila siku wala kila mwezi..


8-Msaidie kusafisha mesa/jamvi mara baada ya mlo wa jioni, ikiwa umechoka hata yeye kachoka pia hivyo mkikutana nyumbani mna-share kufanya usafi ili kuokoa muda.


9-Lolote litakalo tokea kila la kheri, lakini hakikisha unabusu na kukumbatia kabla hujaanza kukoroma.

Kila la kheri ktk hili.

14 comments:

NDAKI GOMBERA said...

Ungekuwa wimbi basi nakupa 5 za Daz!

Uliyoyasema hakika ni ya kweli na yanasaidia.

Hapo nimekusoma vema ila naona ushuri wako umekuwa na upande zaidi.Nafikiri ushauri unaweza kuwa sawa ila itabidi ubadili kichwa cha habari.Unaonaje ungeandika "JINSI YA KUMPENDA MWANAMKE KWA VITENDO".Kama ulimaanisha hivyo basi niatkuwa nakubaliana na wewe.Ila kama kichwa cha habari na maelezo yako viko sawa hapo naona kidogo huo UTAKUWA MFUMO JIKE(kumradhi dada,mama zangu sina uhakika kama hiyo sentesi yangu ni sahihi ahaina chembe ya udharirishaji,sina lengo hilo,nawaheshimu sana)

Kama Dinah utaamini ni sahihi kwa hiyo kupenda kwa vitendo inonyeshwe na mwanaume tu hapo bado tutakuwa tunakunywa chai kwa mlenda!

Suala zima la kuwajibika,hapo swadakta.Kwa hakika lazima tukubali kuwa wapenzi wetu sio wafanyakazi wa nyumbani.Lazima kama kusaidiana katika majukumu ya kifamilia MUDA unaporuhusu.Sio lazima kila siku

Dinah said...

Asante ndaki, "jinsi ya kupenda kwa vitendo" ni mwendelezo wa "Wanaume, tupendeni kwa vitendo".

Mimi binafsi nafikiri Wanawake wengi wa Bongo tunawapenda wanaume zetu(wapenzi) kwa vitendo.

Ukiachilia mbali swala la kufundishwa jisni ya kumridhisha mwanaume kimwili pia hufundishwa jinsi ya kumuonyesha penzi unampenda kwakumkogesha/andaa maji ya kuoga yenye manukato, mpikia, mpoza(calm) akiwa na hasira/amehudhika huko atokako, kuweka mzingira ktk hali ya usafi, msikiliza hata kama unafokea bila kosa, kuwa pale kwa ajili yake hata kama ni "cheater" n.k.

Wanawake wa Kibongo uhaha huko na kule ili kujua/jifunza mbinu za jinsi ya kumfurahisha bwana tofauti kabisa na ninyi mwanaume.

Kwa kifupi wanawake tunamsingi mzuri sana wa kuwaonyesha jinsi gani tunawapenda.

Anonymous said...

Mambo vp Dina, natoka nje ya mada kidgo naomba uzungumze kuhusu swala la mapenzi ya mbali(long distance love)maana mimi kha yananisumbua sana,mara ya kwanza tulikuwa na mawasiliano mazuri kweli ila kila mwaka ukipita naona kama yanapungua sasa ni mwaka 5, ila simu tunaongea mara 1 kwa mwezi, naona kama nachoka , je nikitaka kumwambia tuachane nitakuua namuumiza maana ana hamu na mimi ila mimi naona sina tena hamu na mapenzi yake,ila kingine pia sijapata mtu mwingine naona nataka kuwa ppeke yangu kwanza.je unashauri hili.

Anonymous said...

Dinah,

Naona mada umeielekeza kwa wanaume jinsi ya kuwapenda wake zao kwa vitendo.

Yote uliyosema ni sahii kabisa ila na mimi napenda niongezee yafuatayo:
1. Tabasamu kila wakati unapokuwa unamwangalia mkeo usoni na kumueleza jinsi anavyopendeza maana wanaume wengine kwa kweli kumwambia tu mkewe kuwa anapendeza wanapata kigugumizi.
2. Mkiwa nyumbani sebuleni kwenu fungulia muziki aupendao mkeo kisha muite muuzikilize mkiwa mmekaa wote kwenye makochi yenu. Haiitaji kuzungumza hiyo tu inatosha.
3. Usisite kumuulizia mkeo siku yake imeishaje, ameshindaje ni pilika zipi amekumbana nazo, nk.
4. Usisite kumwambia mbele ya watoto wenu jinsi alivyo mama mzuri.
5. Ni vizuri vile vile kumsifia mkeo mbele ya marafiki zenu maana kuna wanaume wengine hata kumtambulisha mkewe inakuwa shida.
6. tumia lugha ya mahaba unapokuwa unaongea na mkeo na kama mpo peke yenu chumbani unaweza vile vile kutumia lugha inayozidi hiyo ya mahaba!

Nawasilisha,

Moses J.

lilz said...

mmmmh we ANONYMOUS wa 9:53:00 pm!!SASA KAMA UMEMCHOKA SIUMwAMBIE 2!!USIPOMwAMBIA INAKUA KAMA UNAMTUMIA MwENZIO KwASABABU TU UNAOGOPA KUwA MPwEKE!!TABIA MBAYA SANA HIYO!!

ALAFU MAPENZI GANI HAYO YAKUONGEA MARA MOJA KwA MwEZI???NI KwAMBA HAM-AFFORD KUPIGIANA AU TXT ZA MARA KwA MARA AU UBAHILI 2 wAKUONYESHANA MAPENZI????

TUKIRUDI HAPO KwENYE ALIYOSEMA DINAH KUHUSU KUPENDANA KwA VITEBDO...KwA wEwE NI UM-TXT NA KUMCALL MPENZI wAKO KIASI CHAKUMJULIA HALI 2!!MARA KwA MARA!!MUONYESHE UNAMMISS...UNAMPENDA NA UNAMFIKIRIA FROM TIME 2 TIME!!!

MI BINAFSI MPENZI wANGU YUKO MBALI!!ILA KwA SIKU TUNATUMIANA MSG 50-100!!NA BADO HAPO KUNA ATLEAST MASAA MAwILI YA MAONGEZI YA SIMU!!KILA SIKU!!!

AKIFANYA KAZI KIDOGO ANANICHEK....THEN UNAJUA HUYU MTU KANIMISS!!AU ANANIwAZA!!

NIKIMTUMIA MSG 2 INAYOONYESHA SIKO FRESH(ANAwEZA KUTELL NNA MOOD YA AINA GANI KUTOKANA NA NNAVYOONGEA...AU MSG ZANGU!!HATA KAMA SIJASEMA)HATA KAMA YUPO KwENYE MKUTANO ATATOKA ANIPIGIE JUS 2 MAKE SHUR NIKO OKEY!!!

SASA HAPO SIO LAZIMA MLALE NYUMBA MOJA!!UNAYAFEEL MAPENZI YAKE HATA KAMA YUKO MBALI!!AKISEMA KACHUKIA SIJUI MAMBO GANI GANI YA KAZINI UNAMBEMBELEZA....UNAMPA MANENO MATAM UTAONA 2 ANACHANGAMKA TARATIBU!!

Lily

PS. mtanisamehe kwakutumia herufi kubwa!!nimejishtukia karibu nimalize nikaona uvivu kuanza upya!!

Alafu da Dinah naweza kukupa mada sometymzzz kama unataka!!zimenijaa kichwani mpaka nalemewa!!na hongera saaaaaaaaaaaana!!!kazi yako ni baaab kubwa!!

Dinah said...

Anony wa 9:53, nashukuru kwa ushirikiano wako japo umetoka nje ya mada.

Nguzo pekee ya kuendeleza mapenzi ya mbali (LDL) ni mawasiliano ya simu, txt na barua pepe au njia yoyote ya mawasiliano ya internet, mara kwa mara hali hiyo itawafanya muendelee kuwa karibu na kila mmoja kuona mabadiliko ya mwenzie (kukua kwake) hasa kama mtakuwa mkitumiana picha kila baada ya miezi michache.

Mnaweza kuwasiliana kwa barua pepe au room chats kila siku nakuongea kwa sauti(simu)pale unapohitaji(inategemea zaidi na uwezo wako).


Kama alivyoshauri mmoja kati ya wasomaji hapo juu, ikiwa unauhakika ama unajua kuwa umechoka (humpendi tena) kwamba ile hali ya kumpenda mwenzio imeisha basi ni vema kumwambia ukweli tu kuliko kupotezeana muda.

Ataumia sana, lakini atazoea na kusahau haraka kwa vile hauko around.

Tutalijadili hili kwa nafasi siku moja nafasi ikipatikana.

Kila la kheri.

Dinah said...

Moses J na Lilz nashukuru kwa ushiikiano wenu. Ila kwenye maelezo yenu kuna mistari inaelekea kiasi kwenye hitaji lingine ktk mahusiano yakimapenzi ambalo ni "emotionaly secure" kitu ambacho tutakizungumzia siku zijazo.

Napata moyo kuona watu tuko huru kusema mambo kutokana na uzoefu wetu.

Karibuni tena.

NDAKI GOMBERA said...

Dinah!

Mimi nafikiri binti aliyekulia katika mazingira ya kijiji ambako ndio,tunapata malezi halisi ya kiafrika suala la "affection" lipo tofauti sana na nyie wanawake wa mjini.

Mwanamke wangu wa kijiji,nilimtamkia nampenda tangu siku ya kwanza kuanza mahusiano.Hivyo siku zote anajua nampenda ,hata kama sitamwambia nampenda.Ila nyie wa mjini ndio kila siku mnataka tuwaambie tunawapenda ndio muone eti tunajali.

Mwanamke wa kiafrika(mpezi wangu wa kijijini),hana makuu hata kama nitachelewa bila kumtaarifu anajua,babaa alikuwa kwenye mihangaiko ya kutafuta pesa.Na yeye atanipokea kwa tabasamu kubwa kuona nimerejea,hapo ndio nitamwambia kwanini nilichelewa.

Moses unashauri wanaume tutabasamu kila mara tunapokuwa na wapenzi wetu.Binadamu tunatofautiana.Unajua kuna kipindi cha kulia na kucheka.Hapa namaanisha sio kuonyesha uso wa tabasamu kila wakati maana yake unampenda mtu.Moses angali utapigwa changa la macho.Lugha ya malkia inasema"Don't judge a boook...kutokana na tittle yake".Mimi nafikiri ni busara ukiwa na mpenzi wako,kama hujisikii vema unamachungu yako,yaonyeshe.Yeye ndie wa kukuuliza babaa mbona leo nakuona hakuna vema.Kisha ndio umwambie labda nahitaji muda kukuambia linalo nisibu,au nimeshushwa cheo au mgambo wa jiji wamebebe vitu vyangu.

Pia mimi nahitaji kwa kweli msaada wa kuelimishwa."Hivi kweli kuna umuhimu gani WA KUMWAMBIA MPEZI WAKO UNAMPENDA"

Mimi kwa kweli hapo sio kwamba kigugumizi ila sioni mantiki yoyote.Yeye anajua nampenda,sasa nianze kumwabie kila mara nampenda ili iweje?Kwani yeye kahisi simpendi?Haya naona ni mapenzi ya kizungu,mimi mamatumbi kwa kweli naona nikupoteza muda na kaloline zangu(namkumbuka ticha wa Bios)

Naomba sana msaada wenu,hivi kweli kuna umuhimu gani kila siku kumwambia nampenda?au nisipomwambia huo upendo ndio utaisha?Mbona wanaume wakwera wanawapigia simu wapenzi wao nakupenda huku yupo juu ya kifua cha binti mwingine?
Ni hayo tu nafikiri machungu ndio yanayonifanye niende nje ya mada na kutililika bila mpangilio.

Wazalendo nisaidieni ili niweze kupenda kwa vitendo.

Lina said...

Dinah kazi nzuri sana!

Kwako Ndaki , mimi ni mwanamke na kwa upande wangu sidhani kama ni lazima kumwambia kila siku mpenzio kwamba unampenda ila matendo yako yanaonyesha sana penzi lako ..iwe ni jinsi unavyoongea, unavyomuuliza siku yake ilikuwaje au swali au kama ameketi baada ya kutoka kazini iwe utamuuliza anataka maji ya kunywa au kinywaji na mengine mengi Na kwa upande wa kumwambia unampenda hii kwa upande wangu naona ni strong sana pale isipokuwa inasemwa kila siku bali inakuwa kama inakumbushwa na hii inaweza ikawa pale ambapo mmekaa iwe kitandani au tu sebuleni na mwanaume au mwanamke akachukua mkono wa mwenzake na kumwangalia na kusema “ ninakupenda” kwa upande wangu hii inapotokea huwa nanyamaza nikisikiliza sababu huwa inasemwa kwa uzito ikifwatwa na maneno matamu n. k. Au pia unaweza tu acha kadi au barua kwa mpenzio kama surprise juu ya meza/ jikoni etc ikiwa na ujumbe wa kuonyesha mapenzi yako kwake…..nadhani nimechangia walau namna ambayo unaweza kuonyesha penzi na kumwambia mwenzako unavyompenda . Na ni vizuri sana kuwa mbunifu katika kuonyesha mapendo yako

Anonymous said...

Sidhani kama ni mapenzi ya kizungu bali ni mapenzi ya kisasa. Zamani tulikuwa tunawachukulia wanawake 4granted na all we care was ourselves na hamu za kimwili.

Hao wanawake wa kijijini hawajaelimishwa, usikute hawajui hata utamu wa kufanywa ukoje japo kuwa mkifanya anaonyesha kuwa anaupata lakini katika hali halisi anafanya hivyo kwa mujibu wa mafunzo aliyopewa.

Mwanamke wa kijijini hatokuuliza wala kulalamika kwa vile anaamini ukimuacha atakuwa amei-let down familia yake na ukoo wake kwa ujumla, sasa ili kuepuka hilo inambidi ajikalie kimya tu.

Wanawake wengi wa kijijini huwa wanaolewa bila kupendwa kiukweli bali wanaume huwa tunakimbilia kule kwa vile tunajua kuwa hawana wanalolijua na kuwa itakuwa rahisi kuwatawala kuliko wale wa mjini ambao wameshaondoa mavumbi na ukimletea mapepe anakuacha au anakwenda na mwanaume mwingine atake muonyesha anampenda kwa vitendo kama Dinah alivyojisemea.

Mwanamke wa kijijini anajua kupendwa ni kuolewa, kumnunulia chakula na mavazi...hajui mambo ya affection lakini pindi akionyeshwa huko nje ujue sio wako.

Lakini wewe utadai massage ya miguu kutoka kwa mkeo wa kijijini, utataka akupikie n.k hiyo ni affection unadai hapo, sasa kuna ubaya gani na wewe kumuonyesha yako?


Wanaume kila kitu Duniani kina badilika(maendeleo), ikiwa hivi sasa watu tunafanyiwa upasuaji kwakutimia waya badala ya visu, tunawasiliana kwa siku bila miwaya, tunafanya mapenzi kwa kutumia Kondom, tunanyonyana ndimi nakushukiana huko chini kwanini basi Penzi liendelee?

Sote tunapenda na kufurahi pale tunapohisi tunapendwa na wapenzi wetu.

Wanaume wakati umefika, tubadilike.

Eddy

Anonymous said...

Kweli iko kazi!...maana tunarudi pale pale kuwa, wakati Ndaki Gombera anashindwa kuelewa umuhimu wa kumwambia mwenzie kuwa anampenda na kuona kuwa kila kitu kiko sawa tu pale nyumbani maana hata bila ya kusema hivyo mkewe anajua tu kuwa aanapendwa....si ajabu ukimuuliza mwenzie atakiri kuwa ni muhimu Ndaki kufanya hivyo angalau mara moja moja! Hapa ndipo ule utofauti wa mahitaji kati ya mwanamme na mwanamke unapojitokeza!
Inahitaji muda kwa kweli maana hata huyo binti ambaye amekulia na kulelewa kijijini na kwa sasa anaishi mjini ni mambo mengi sana ambayo ameishayaiga hapo mjini ambayo si ya kijijini.

Tutambue kuwa mazingira anamoishi mtu huwa yanaweza kumbadilisha mtu kwa kiasi kikubwa sana na dunia si kusema kwamba imesimama, kwa hiyo hata huyo aliyekulia kijijini ambako alikuwa hata saloon haendi na kaja kweli mjini hivyo hivyo na nywele zake asilia, akifika tu mjini atavumilia kuvuta muda lakini baada ya siku kadhaa utaona na yeye anaingia saloon ili kujiweka katika hali ya ki-mjini mjini!

Mimi vile vile nimekulia kijijini na nakumbuka hata kijinini mtu akiwa na mpenzi wake atajitahidi sana anagalau kumwandikia barua au mashairi yenye maudhui ya kimapenzi na hii ilikuwa inamfasnya mpenzi wake ajisikie kuwa yeye ndiye haswaaaa!

Ndaki, jaribu tu hilo zoezi, najua mwanzoni utapata kigugumizi na si ajabu unajiuliza sasa hivi kuwa mwenzio atakuelewaje maana hukuzoea kumwambia hivyo....ila pale tu utakapoanza na kujizoesha utayaona mabadiliko makubwa mwa mwenzio na utakuja kutoa ushuhuda kwenye blog hii!

Jitahidini kuwapenda wake zenu kwa vitendo!

MJ

Anonymous said...

Naona mlinipata vibaya kuwa labda hatuwasiliani , tunaongea kwa simu labda mara 1 kwamwezi, ila txt tunatumiana sana,ila txt zinatoka kwake hazina mvuto wa mapenzi, inabidi na mimi nijibu the same, yaani hata tukiongea kwa simu hakuna moto kabisa unakuta ananzisha mada kama leo bongo kuna mvua sana,mara jua kali leo sana, mara nimefua nguo hazija kauka,au umesikia habari za zito kabwe, na nyingine nje ya mapenzi kabisa, sasa ndo nikapoteza hamu na mimi,nilikuwa namtumia picha sana, ila yeye anasema muda wa kuingia net unakumwa mdogo nikachoka kutuma hata pic,niliwahi kumuuliza kama ana mtu mwingine najua hatasema hata kwa bunduki.

Anonymous said...

Wewe dada wa "distance love" nakushauri jaribu kuangalia matukio with sobar eyes yaani bila kuwa naive...yaani bila kufikiria kuwa uamuzi utakaofanya utakuwa si wa maana.

Inavyoonekana kwa maelezo yako ni kuwa hauko comfortable kabisa na hilo penzi. Fanya uamuzi before it is too late, mimi nakushauri kama mwanamme ambaye yuko huku ughaibuni. Vijana wengi wakiishafika huku wanazuzukia maisha na hawawakumbuki hao walio bongo maana nawaona wengi tu huku!

Mimi kwa vile ni mtu mzima na nina familia hapo bongo kila siku kabla ya kuanza shughuli yoyote ile ni lazima nifanye mawasiliano na mke wangu na siku nisiposikia sauti yake sijisikii vizuri!

Kama huyo mpenzi wako ni kijana basi nadhani unastahili kuchukua uamuzi. Si kwamba nakutakia mabaya ila ndiyo hali halisi!

NDAKI GOMBERA said...

Kakak Moses na Da Lily na Eddy asante sana kwa ushauri wenu.

Najua ni ngumu ila ngoja nijaribu taratibu kujiongeza katika kumwandikia barua.

Ila pia nakubaliana na zoezi alilosema dada Lily kwamba haina maana sana kila mara nakupenda nakupenda,inabidi hiyo nakupenda uivutetie pumzi na ukiitoa basi imaanishe.

Nitafanya hayo mazoezi ingawa ukweli naon ainakuwa ngumu,lbda simpendi huyo mrembo wangu.Lakini mbona moyo wangu unafarijika sana unapokuwa naye.

Ene wei tutafika tu asanteni kwa muda wenu.