Thursday, 11 October 2007

Hivi huwa tunajiandaa tunapoanza familia?Nimeshuhudia sehemu kuwa ya watu hapa Duniani huamua kuwa na familia (kuzaa) kwa kushitukizwa (bila kuwa tayari). Kwa vile mimi ni m-bongo na nina uzoefu au nawajua wabongo basi nitaegemea huko kwa m-bongo halisi.


Sina hakika kama ni ubinafsi au ile kasumba ya kipuuzi kwamba ukiachia mimba basi Mpenzi hakuachi, pia inawezekana kabisa kuwa ni uzembe wa mtoa mbegu (mwanaume).


Kisheria (as far as I remember) umri wa kushiriki ngono/funga ndoa ni 18+ japo kuwa bibi yangu aliolewa akiwa na miaka 15 akaja kuzaa mtoto wa kwanza akiwa na miaka 20 ila kwa karne hiyo kulikuwa na sababu ya kuolewa ktk umri mdogo ambazo sote natumaini tunazijua.

Sasa ndugu zangu mnapo amua kupeana mimba huwa mnakuwa mmejiandaa baada ya kung'amua faida, majukumu, matatizo, mabadiliko ya kiakili na kimwili (mwanamke)?

Je, huwa mnakuwa na uhakika na uamuzi wenu au mmoja anaamua ili kumridhisha mwenzie au jamii inayomzunguuka? au hutokea tu kwa "bahati mbaya"?
Huwa nasikitika sana ninapo ona binti au kijana huyu mdogo ambae katoka kwa wazazi (bado mtoto) kisha akawa mzazi na yeye kwamba hajui tofauti au mabadiliko ya mwili wake kutoka Utoto, Ujana na kufikia Utu uzima na anapofikia umri mkubwa (utu uzima) anakuwa amejichokea(kazeeka).

Kijana/binti huyu hajafaidi ujana wake....sio kufanya ngono ovyo bali kufanya yale mambo ambayo vijana tunapenda kuyafanya bila kuwa na hofu "mtoto" atakula nini kesho, sijui anaumwa, amekua unahitaji vivazi vipya, siku gani ni clinic, je mpenzi wako ana-cheat n.k., kujua tofauti ya kupenda (bila ngono), n.k.


Ongezea basi uonavyo wewe (bila ku-attack mtu) mimi nasikia usingizi, swaumu kali hapa!

Nakuja......

7 comments:

Ash said...

Dinah si attack lakini natoa ukweli, watu hawajui majukumu ya kuzaa na ya mtoto. Mtoto unapomleta duniani mungu anakuachia wewe majukumu ya kumlea katika mazingira mazuri. so unatakiwa ujue kuwa mtoto wake anahitaji malezi mazuri ili yaje kumnufaisha yeye. lakini sisi hatujui hayo mtoto anazaliwa halafu tunasema kila mtoto anakuja na riziki yake. kweli hatalala njaa lakini kuhusu elimu na mambo mengine ambayo wewe mzazi unatakiwa kutafuta na kumfanyia ili awe kwenye maisha bora je?

Anonymous said...

Wabongo tunahitaji kuelimishwa kuhusu mambo mengi ambayo huwa hatuko makini wakati tunayafanya.Wakatiumefika kwa waandishi wa habari na wasanii kuwa mfano kwenye jamii.

Sanaa ni kioo cha jamii na waandishi wa habari ni wawakilishi wa jamii sasa kwa ushirikiano wanaweza kusaidia binti na kijana huyu kuepuka kufanya ngono mapema, kijana wa kiume kusimama na kuhakikisha haachii mbegu zake kila mtaa pale atakapo amua kujishirikisha na ngono. Mabinti nao wajue kuwa ni jukumu lao kukataa kufanya ngono na kijana bila kutumia kinga.

Vijana walioko kwenye mahusiano yasiyo rasmi wafahamu kuwa kufanya ngono bila kondomu ni uchafu na ni hatari.

Wazazi nao wajaribu kuwa wazi katika kuzungumzia ngono kwa undani na watoto wao badala ya kuwatisha, walimu wasaidie kuelimisha. Ngono ni tamu ukiifanya na yule umpendae, anaekusikiliza, anakuheshumu na kujali utu wako.
ciao

NDAKI GOMBERA said...

Dinah mambo vip?

Ukiitikia na wewe useme Ndaki po! maana kuniitikia kwa jina langu sio tu ni shavu ila ni kuonyesha KUJALI(sms delivery.
Wadau wote naomba msinizodoe,cha msingi mnisaidie.

Binasfi ujanja wote huu nipo hapa mtandaoni shule yangu ni YA KUUNGA UNGA kwa gundi ya karatasi.
Mimi nasikia masela wanaongelea baiolojia(nafikia lugha ya malkia nipo juu)

Mimi ninachofahamu hawa dada zetu au wapenzi wetu (WANAWAKE)wao ndio asilimia kubwa wanasababisha hizi mimba zisizokuwa na mpango.Yaani yeyee inamaana hajui hata ni siku ipi mimba anaweza kupata?

Mi nashangaa,utakutana na binti msomo mzuri tena wa sayansi ya binadamu au Afya au kanakumua PCB au yupo Muhimbili pale eti afahamu siku zake za hatari kupata mimba?

Mimi kwa mtazamo wangu naomba sana hawa mabinti kama kuna njia za asili zaidi ya kondom basi wafundishwe jinsi ya kujizui.

Una sisi wanaume ni sawa na BETRI na wao ni tochi.Sisi peke yetu kama betri hatuwezi kutuo mwanga bila tochi.Sasa nashanga hao wakina dada wanaruhusu betri ziingie na wakijua kabisa tochi ni zima na balbu mpya,sa hapo unategemea mwanga usitoke?

Ukweli ndio maana wanaume wengi wanaaamua kuwapiga chini wanawake wa hivyo maana wanaona wanachanganyia ramani ya maisha.Mimi nina mpango nimalize zangu chuo ndio niwe mdigi leo hii ghala unanileta kibendi.

Au wengine hawajui labda mimi napenda kwanza kujirusha wenyewe wanafikiri nikimzalia mtoto ndio nimempata.Aisee mnajidanganya.

Tena siku hizi,akimbii mtu mimba.Ukisema ni yangu,nakwambia poa...sana sana namchagulia jina...kinachofuata ni mama ulee mtoto wangu au nimpeleke kwa bibi yake anipige tafu nitakuwa narekebisha masuala la Fweza!

Ukikomaa kukaa nae poa ,tunajua mtoto akikua lazima tu amtafute mshua wake.

Sa hiyo nachukua kimwana ambaye sasa namweleza ukweli unajua yule mama yake na mwanangu(sio mke wangu au mpenzi wangu umecheki hiyo introduction yangu) alitegesha kwa lazima ndio nikapata mtoto wa fasta fasta ndio maana nilimpa jian SIKUJUA.

Hivyo naomba TUZAE(sio unizalie) mtoto mama kama upo tayari.Mtoto akizaliwa anapewa jina Brighth,Godbless n.k Mnisamehe kwa mtundika wangu wa leo nahisi nimeandika nikiwa na ka jzba na ukweli labda yalinikuta mimi au mshakaji wangu wa kariiiiiiiiibu.

Asante

SIMON KITURURU said...

Nakubaliana na DI , kuwa kuna asilimia kubwa haijiandai.

Hii sio Bongo tu. Ila , naweza kuelewa bongo, watu wasipojiandaa.
Hasa nikikumbuka enzi zetu.

Enzi zetu, hata kama unania nzuri na mwanadada umpendaye, hata ukikutwa na kaka zake unaongozana naye tu, unaweza kupigwa.Mapenzi mengi yalikuwa magumu kuyakuza kikawaida.

Kwa hiyo, ingawa mimi mwenyewe nilifanikiwa kupigwa buti na demu ,baada ya yeye kupata uhuru, nakubali kuwa hata yule demu alikuwa ananipa penzi kwa sababu tu nilikuwa naaminika kwa kiasi cha kutostukiwa kwa muda mrefu kuwa ni nanihino wake kwao.

Naamini bado watu wengi bongo hawajiandai kutokana nakutokuwa na uhakika na hali halöisi ya maisha.

Bogno , hata kuwa na bajeti ya uhakika , mara nyingi ni lakshari.

Na uhakika kujiandaa kuna hitaji uhakika wa mambo uletao uhuru. Uhuru ukuwezeshao kuwa na uhakika kuwa nanihino ndiye hasa anaye kukuna roho kuliko Alfonso.Uhuru ukuhakikishiao kuwa , kesho na mtondogoo uifikiriayo, itakuwa kama uifikiriavyo au karibu na hivyo uifikiriavyo.Lakini....

Baada ya kukatiza nchi kadhaa , zenye kondom na vidonge vya kuzuia mimba nje nje, bado hili tatizo lakuanza familia lipo. Marekani limezidi sana hasa kwa watu weusi. Ulaya, watu weusi tunajitahidi , lakini hatuchezi mbali na weupe.

Hili linaweza kushangaza hasa katika nchi kama za Ulaya Kaskazini ambazo ukifika tu kituo cha karibu cha treni unaweza kukuta ATM ya kondom, ukifika duka la karibu la madawa unawezakupata vidonge vya kabla au baada ya kumaliza starehe igusanishayo sehemu za faragha.

Sasa fikiria hili swala lilivyo gumu!Mpaka mtu ambaye kwa bahati mbaya akatumbuizwa na anajua anaweza kununua kidonge kabla ya masaa 24 mpaka 48 ambavitasabaisha mtumbuizo usitotoe, bado inakuwa kazi, je ambao hawana hata jinsi ya kuzuia swala itakuaje?

Hiki kitu , nahisi tunakirahisisha tukidai kuwa sababu yake ni kutaka tu kutoachika. Mbona Mifano iko nje nje kuwa; uzae na mtu au usizae, kama penzi limekufa , imetoka hiyo!

Kwanza mnaweza mkazidi tu kuchukiana , kwa sababu ya kulazimika kukutana kwa sababu mna mtoto pamoja.

Pili,
Kuna pressure za jamiii. Najua kabisa , kuna jamii , watu wakioana wanaanza kuhesabu miezi , ili kuona mtoto anakuja au haji. Asipo tokea, mwanamke au mwanamme anaweza kuwekwa kikao , akihisiwa hajui kutumia sehemu za faragha.

DI, hii topiki kubwa, nahisi nitarudi tena!
Seriously, na hamu ya kuanzisha familia!
Kuna ambaye ananipenda hapa sebuleni kwa DI?
:-)

NDAKI GOMBERA said...

Dina nimepita kukusalimia jana usiku ulikuwa umelala.

Leo napita tena saa hizi sijakukuta hapa kwako.Ene wei nimeacha kaujumbe kangu angalia hapo chini ya mlango.

Lakini mwanamke kujishughulisha sio mbaya ila inabidi japo uweke ka"MEMO" nitakuwepo saa ngapi!

Poa ngoja nikamsalimie Kitururu nitapita baadaye basi mtu wangu.

Dinah said...

Nashukuru kwa ushirikiano wenu hapo juu.

Nitarudi kuliendeleza nikimaliza manunuzi ya sikukuu ya Iddi.

Ijumaa njema.

Lina said...

Kwa kweli watu wengi hawajui majukumu ya kuzaa.Ni wachache sana ambao wanapanga.Ukiaangalia swala la walio na ndoa kwa mfano, unakuta baada ya harusi wanajamii wanategemee miezi michache tayari kunatarajiwa mtoto ..tena ukiangalia kwa wasichana japo wana elimu unakuta kamaliza chuo miezi michache tayari kaolewa na mimba nayo njiani…..ni wachache sana ambao wanaolewa tu baada ya masomo na walau kupata muda wa mwaka au walau miaka miwili kujenga kazi – experience ili kuweza kumudu walau majuku ambayo yatakuja mbeleni mtoto atapopatikana ….na kwa wengi ninaowaona wanategemea bado mume kifedha. Ninao marafiki wengi walio katika, hali hii na wengi wanatiahurumu . Mi naomba sana watu kufunguka macho sio maswala ya uzungu wala nini ila ni vizuri mabinti walau kuwa na kazi na kaexeprience kabla ya mtoto….sio vibaya kuolewa mara baaya ya masomo hapana, ila nachosema wanaume wawe more open minded katika kuwatakia mafanikio wake zao katika maswala ya kikazi