Vishawishi vinavyosababishwa na Teknolojia......

Hapo chini nimezungumzia Teknolojia inavyoweza kuchukua muda mwingi kuliko ule unaotumia kuwa na mpenzi wako, na nimetaja simu na Mtandao (internet )na vilevile swala la kutembelea Salon na Gym.

Sasa leo nazungumzia ni jinsi gani vitu hivi vinashawishi na hata kupelekea baadhi ya wapenzi wetu kutumia muda mwingi katika "kona" hizo kuliko ule wanatumia kuwa na sisi.

Simu za mkoni;
Ni wazi kuwa simu inarahisisha mawasiliano yakikazi, biashara na inatufanya tuwe karibu na wapedwa wetu kila siku bila kupoteza kiasi kikubwa cha pesa kwenda kumtembea ndugu jamaa na marafiki.

Lakini simu hizi pia zimekuwa ni kishawishi kikubwa kwetu kufanya mahusiano ya kimapenzi ya kihisia na mtu yeyote ambae anajua namba yako au wewe unajua namba yake.

Hii inaweza kutokea ikiwa mhusika mwenye jinsia tofauti na wewe anajisikia mpweke siku hiyo, amechukizwa na mpenzi wake, amesongwa na mambo mengi yanayomfanya ajisikie hana raha n.k. na hivyo akaamua kuwasiliana na wewe kwa kukutumia "text" na kila kitu kikaanzia hapo.

Vilele mpenzi wako au wewe unaweza ukapokea "text" yenye mrindimo wa kimapenzi kutoka kwa mfanya kazi mwenzio au mfanya biashara mwenzako au hata rafiki wa mpenzi wako kimakosa, lakini kwa bahati mbaya ukavutiwa nayo (ukidhani ni yako na mhusika kakuzimia) hivyo ukaijibu vema kabisa na mpekeaji akavutiwa na ulichojibu na hapo ndio unakuwa mwanzo wa.......

Hayo yote niliyoyasema na mengine unayoyajua kuhusiana na mawasiliano ya simu yakonoga huwa yanasababisha wenza wetu ku-set pin # ili usiweze kufungua simu yake(ikiwa una tabia hiyo), hata siku moja huwezi ukakuta simu yake imezagaa juu ya meza.........siku zote itabaki ndani ya bagi ambalo linafunguo, wakati wa kulala itawekwa uchagoni (chini yamto), akiwa anaongeza nguvu simuni basi hatocheza mbali na mahali hapo n.k.

Unaweza kuongezea kuhusu hili kwa faida ya watu wengine na hasa walengwa ambao ni wanawake.

Karibu sana.

Comments

Anonymous said…
Tatizo la watu wengi ni kuingia kwenye ndoa wakiwa na ajenda zao za siri. Kama tunakuwa wakweli wakati tuunanza urafiki kabla ya ndoa na baada ya ndoa sidhani kama vijiujumbe vya kwenye simu vitakubabaisha hata uandike kwa utamu gani. Mfano ni mimi, nimeoa mwanamke ambaye tumependana kwa miaka zaidi ya 7 kabla ya ndoa na sasa tumemeoana maisha ni ya raha kuliko yalivyokuwa kabla ya ndoa. Hata uandike email au utume picha zako ulizokuwa umekaa uchi hutapata kitu hapa kwani hizo ni fahari ya nusu dakika na haiwezi kabisa kuharibu penzi langu la miaka 10+. Kama kweli kuna penzi la dhati hakuna kitu kitakachoweza kulivunja.
"for the record, if a man or a woman left his/her significant other for you he/she will most likely leave your for someone else"
KKMie said…
Asante sana kwa ushirikiano wako, hakika maelezo yako yatasaidia wasomaji wengine ambao huyumba-yumba.

Karibu tena.
Simon Kitururu said…
This comment has been removed by the author.
HI DINAH,
Nakwambia unamchango mkubwa katika jamii keep it up! Hata siye hapa ughaibuni tumekuelewa kabisa. Nakubaliana na wewe kwamba technologia imechangia katika kuvunja ndoa na mahusiano ya karibu
Lakini nasema hii ni kwa wale wenye mioyo ya vipepeo.Kama kweli wewe ni lijali au unatoka katika jamii staarabu,huwezi ukaacha yule ambaye anakuwanawe katika shida na raha ukamwendea yule part time eti umekosana na bibi yako au mme wako.
projestus
KKMie said…
Proje asante sana kwa ushirikiano wako. Karibu sana kila upatamo wasaa!