Sunday, 9 September 2007

Tekinolojia na mapenzi inaendelea hapa.....

Sote tunatambua kuwa mahusiano yamekuwa yakivunjika mara kwa mara, ndoa hazidumu kama ilivyokuwa miaka 40 iliyopita na kama ndoa/uhisiano huo umedumu basi ujue asilimia kubwa ni uvumilivu wa mmoja wao kwa vile kuna watoto ndani ya uhusiano huo na mara zote mvumilivu huyo huwa na uhusiano mwingine nje.

Uhusiano huo unaweza ukawa wa kimwili (mambo ya kimada, nyumba ndogo na vipoozeo), uhusiano wa kihisia tu ambao mara nyingi huitaji kuonana na mwenza wako na huu ni ule wa kimtandao a.k.a internet, uhusiano wa kimapenzi wa simu kwa kutumia sms na ule wa kuongea kwa sauti.

Nitazungumzia mahusiano ya kimapenzi ambayo ni matunda ya Teknolojia kila uhusiano kwa nafasi ili kukusaidia wewe kuelewa na kutoa maoni au kuongezea yale niliyoyaelezea.

Mtandao a.k.a Internet.
Mtandao umekuwa sehemu kuwa ya maisha yetu hivi sasa, wengi wetu tunatumia muda mwingi kukaa mbele ya Komputa kuliko ule mda tunaotumia kukaa na wapenzi wetu.

Kwa baadhi ya wenza (couple) hujitahidi kujigawa ili mwenza wake asijisikie vibaya au kuhisi anatengwa au kutojaliwa na hivyo wapenzi hao huamua kutembelea tovuti tofauti usiku wa manene wakati wapenzi wao wamelala au ilemida ambayo wanamaliza kazi au wako kazini nakisingizio ni kuwa kuna kazi au Data wanapaswa kuzimalizia na zinahitaji uchunguzi "online".

Hapa inaweza ikawa muhusika (mwenza) akawa anatembelea chat rooms, Forums, Emails(sio zote za kikazi), kutembelea Tovuti za Porno au kama sio zile za kutafuta jamaa mliosoma pamoja, marafiki n.k.

Simu za mkononi.....sms!
Mpenzi hapa anatumia muda mwingi kutuma na kusoma sms kutoka kwa watu tofauti na baadhi huwa ni wapenzi ambapo hubandikwa majina yakiume ikiwa muhusiaka na mwanaume na kupewa majina ya kike ikiwa mhusika ni mwanaume.

Simu za mkononi-kuongea!
Mpenzi anatumia muda mwingi kuongea kwenye simu kuliko muda anaotumia kuongea au kufanya mambo mengine yanayohusiasha uhusiano wenu wa kimapenzi.

Tekinolojia hii pia inahusisha swala la kutembelea Gym, Salon......zamani hakukua na haya mambo sio, ila siku hizi utakuta bwana au bibi atumia muda mwingi kwenye kona hizo kuliko ule anaotumia na mwenza wake.

Natambua nimegusa wengi hapa.............karibu tujadili kuhusu hili, tufanye nini ili kuokoa mahusiano yetu ya kimapenzi na wakati huohuo kufaidi matunda ya Teknolojia?

Karibu sana.........

7 comments:

Baba Monica said...

Makala yako umeiandika katika mtizamo wa kike na kuna mambo mengi sana ya msingi yanatofanya hizi ndoa kuvunjika na wala si mitandao. naomba nichanganye lugha kwa kusema kuwa...Marriage has became a secular institution rather than being devotional institution...and that is where the problem is!

Anonymous said...

Mie naona haya mambo ya technology kuchukua nafasi au muda wa wapendanao ni kweli lakini kama watu wanapendana kweli sidhani kama technology itakuwa chanzo cha migogoro yao.

Technology imekuwa ikilaumiwa kwa mambo mengi lakini bado tunazidi kuikumbatia, technology imelaumiwa makazini pia, watu walizani computer zinachukua nafasi za kazi za watu na kwmaba computer zitatumika badala ya watu. Sasa ivi tena tunafikiri na ni kweli zinavunja hadi ndoa za watu lakini ukiangalia kw aundani zaidi utaona ndoa au uhusiano huo ulikuwa destined kuvunjika tu kwa mmoja wa wapenzi kutorizika na mambo fulani yasiyohusiana na technology sasa techie inakuw ai icing on the cake tu.

Anonymous said...

Bi dada leo naona hii hoja hujaifanyia uchunguzi wa kutosha. kama msemaji aliyepita, umeweka zaidi mtizamo wako wa kike tena wa kizamani sana. Hakuna tofauti kati ya maendeleo ya teknolojia katika vitu na watu. Namaanisha Mapenzi/ngono pia ni lazima yakimbizane na teknolojia yenyewe.

Kuna utafiti unaoendelea kuhusu mifumo mipya ya mapenzi/ngono na imani za dini kimombo "Current trends in sex/sexuality the realm of religion" NA hapa dini zinazochambuliwa ni uislamu na ukristo.

Swali linaloibua mdahalo mkali ni aina gani ya ngono inayopendwa zaidi na wanaume/wanawake sasa hivi? Ikiwa mwanamke/mwanaume anapenda mfumo huo wa ngono katika ndoa isiyoruhusu nini kinatokea?

Matokeo ya awali yanaonyesha wazi teknolojia uliyoitaja kama simu na kompyuta zinachangia kurahisisha/ kukwaza mahusiano ya ngono/mapenzi, zinapunguza/ zinaleta misongo ya mawazo nk

Tunatakiwa kufahamu kuwa ukiona ubunifu/fasheni za nguo, magari, simu na hata chakula zinabadilika kwa kasi usitegemee ngono/mapenzi yatakuwa hayabadiliki. Ubunifu uko katika VITU na WATU. Kitu cha msingi ni kuhakikisha tunatumia teknolojia vizuri ili itusaidie kuboresha maisha na wala tusiilaumu kwani hatuwezi kuisimamaisha.

Dinah said...

Baba Monica na anony 2 hapo juu nashukuru sana kwa ushirikiano wenu.

Ila napenda kuweka wazi ninapozungumzia issue na-base kwa wanawake kwani blog hii ni maalum kwa wanawake wa Kibongo sio jamii ya kibongo kwa ujumla ambayo ni Wanaume, wanawake, Watoto,Wazee na Mashoga.

Ikiwa ni mwanaume na umevutia na issue yoyote nakaribisha uzoefu wako ambao utawasaidia wanawake katika "nyanja" ya ngono, mapenzi na mahusiano.....karibu mno!

Anonymous said...

Mimi ni mwanaume; huwa napenda kutembelea hapa kwa vile najifunza machache kuhusu wanawake.

Msemaji hapo juu naona umeelewa tofauti na kile ambacho msemaji wa blog hii anasema.

Yeye habishi au kupingana na maendeleo au nisema Teknolojia bali anasema kuwa Teknolojia hii ya simu na internet imekuwa ikichukua muda wetu mwingi kuliko ule tunao utumia kukaa na wapenzi wetu.

Muda huo mwingi tunao utumia kwenye PC unaweza ni kwa nia njema kabisa kama vile kujifunza au kupata Info muhimu kuhusiana na kazi zako, taarifa za nyumbani ikiwa uko nje, burudani n.k. Lakini wengi wetu tunajisahau kuwa kuna wenza wanapenda au wanastahili ku-share angalau half ya muda tunaotumia kwenye PC au kuongea kwenye simu na washikaji au wafanya kazi wenzetu.

Swala la kujadili hapa ni wenza tukabiliane vipi na wakati huohuo kufurahia matunda ya maendeleo Teknolojia?

Dinah unanifurahisha jinsi unavyoongea kwa undani na kulenga watu wa kawaida walio ndani ya Bongo.

Ni hayo tu kwa sasa.

Anonymous said...

Baba Monica,nakubaliana na unachokisema lakini Dinah kazungumzia mahusiano ya kimapenzi kwa ujumla ikiwemo ndoa kuwa hayadumu.

Kweli kuna mambo mengi yanayosababisha kuvunjika kwa ndoa, ikiwa ni pamoja na kubadilika kitabia, kutovutiwa tena kimapenzi na mkeo/mmeo, kukumbana na binti/bwana ambae unahisi kumpenda kuliko mwenza wako hasa kama ulioa kwa kuridhisha jamii yako au kuondoa mkosi, kutovumilia ikiwa mke/mpenzi kashuka kiuchumi na mengine mengi.

Nafikiri Dinah hapa anachojaribu kusema ni kuwa Teknolojia imekuwa sababu mpya ya kuvunjika kwa mahusiano yetu ya kimapenzi kwa vile binadamu tunashawishika kirahisi kujieleza ikiwa hatuonani au hatujuani na mwishowe unajikuta uko inlove na mtu ambae umekutana nae kwenye forum, chatrooms etc.

Dinah I'm feeling you gal. Keep it up.

Dinah said...

Nashukuru sana kwa ushirikiano wenu. Karibuni sana na msichoke kuja hapa ili tuelimishane.