Penzi linapobadilika na kuwa Heshima!


Hili swala la penzi kwisha mimi huwa nalisikia tu kutoka kwa watu tofauti kuwa kuna wakati mtu unajikuta humpeni tena mpenzi wako na unatafuta namna ya kujitoa kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi.

Kwa wale waliko kwenye ndoa huwa ni ngumu kidogo kutokana na "dini" kuwabana au anabaki ndani ya ndoa uhusiano kwa vile anakuheshimu kwa kuwa ni mama wa watoto wenu hasa kama umemzalia watoto 2-3 hivi lakini ktk hali halisi anakuwa na mtu mwingine ampendae nje ya ndoa (part time lover a.k.a Kimada a.k.a nyumba ndogo).

Mwanamke unatakiwa kuwa makini na mjanja kutambua mabadiliko hayo(penzi au heshima), kwani mtu anapokuheshimu na kukuthamini kwa vile umemfanyia jambo fulani kubwa hakuna tofauti kubwa sana na kupendwa.

Hivyo ikiwa kila usiku analala kitanda kimoja na wewe nakukamilisha mambo mengine ya kifamilia na kuambiwa "nakupenda mama nanihii" haina maana kweli anakupenda bali anakuheshimu na vilevile anajaribu kuepuka malalamiko au maswali.

Mimi binafsi naamini kuwa unapompenda mtu kwa maana halisi ya mapenzi huwezi kuchoshwa au penzi lako kwake kupungua kama sio kwisha kabisa.

Pamoja na mambo mengine kuna sababu zinazochangia mabadiliko hayo ambayo ni kujisahau kwako mwanamke, kuwa na tabia ya "ndio bwana", kukubali usemi kuwa "mumeo akiwa ndani akiwa nje si wako bali wa wote", kukimbilia kuzaa siku chache baada ya kuwa ndani ya uhusiano au ndoa kwa vile unahofia usipompa mtoto basi ataenda zaa nje n.k.

Nakaribisha nyongeza kuhusu hili, maswali, maoni na ushauri.

Karibuni sana na kila kheri ktk mfungo mtukufu.

Comments

Anonymous said…
Hi Dinah,

je wakati ukimpenda mtu hustahili kumpa heshima pia? Mi nadhani nikimwambia mwenzi wangu nakupenda fulani si lazima iwe namwambia ivo kumheshimu tu ila pia kumpenda au siyo?

Na vile vile kwa vile umeelekeza kwa wakina daa hili suala, je na sisi wanaume tuangalie mabadiliko gani ama tutajuaje kama mwenzetu naye ana kiserengeti boy mnavoita vijana wa siku hizi?
KKMie said…
Asante kwa ushirikiano wako,hakika unatakiwa kumheshimu mpenzi wako. Lakini ninachokizungumzia hapa ni ile hali ya mpenzi wako kutokuwa na mapenzi na wewe (na anajua kabisa kuwa hakupendi kimapenzi kama awali) lakini still ataendelea kuwa/kuishi na wewe kama kawaida na hata kufanya mambo mengine ya kifamilia/maendeleo lakini anafanya hivyo kwa vile ya heshima kuwa wewe ni mama wa watoto wake sio kwamba anakupenda kwa vile wewe ni mpenzi na mama wa watoto wake.

Nitaelezea hili kwa undani zaidi siku zijazo. Kuhusu swala la wanaume watafahamu vipi nitalizungumzia hilo pia....usijali.

Karibu tena.
Anonymous said…
Asante Dinah kwa hii mada, nakubalina na wewe kuwa kuna wakati penzi huwa halipo namtu unabaki ndani ya ndoa kwa ajili ya watoto na heshima mkeo na vilevile kuogopa kufikiriwa vibaya na jamii yako.

Mabadiliko hayo kamaulivyosema yanaweza kusababishwa na mambo mengi sana na moja ninaloweza kulifikiria harahara hapa ni swala la kujiingiza kwenye ndoa kwa sababu zako binafsi na sio mapenzi japo uta-act kama vile unapenda ili kupata unachotaka kwa wakati huo kama vile watoto, heshima (wale wanaoamni kuwa kuoa/olewa ni heshima), kutodhaniwa kuwa wewe sio rijali au kuondoa mkosi kama wanavyofanya wanawake wengi siku hizi.

Ili kuepuka hayo yote ni vema kufunga ndoa kwa vile mnapendana sio kwa sabau nyingine kama uchumi, kuzaa na kuhofia jamii.

Ni hayo tu dada yangu.

Nafurahia kazi yako.
Anonymous said…
Dinah nimesoma maelezo na kuelewa unazungumzia nini hasa labda kwa vile mimi ni mwanaume.

Swala lingine linalofanya wapenzi wetu wapoteze mapenzi na kuja ile kitu inaitwa upendo ambao ni wa kawaida kwamba unapendwa kama mama fulani na sio kama "wewe" mwajuma au Grace etc.

Nitabia ya wanawake kuiga tabia za watu wengine ambazo awali hawakuwa nazo.

Mfano ulipokuwa nae kabla hujaoa au kuzaa nae aliku mwema, mwenye heshima, mnawasiliana vizuri kabisa na kujali lakini mara baada ya kufunga ndoa yote yanawekwa kando na unakuwa na mke ambae si yule ulikuwa nae awali na hali hiyo it's a turn off to most men.

Sasa kama mmesha zaa inakuwa ngumu kumuacha/kubadili kwa vile kuna another life u created so you just stay in a relationship for the sick of that kid or two sio penzi.

Sote tunahitaji mapenzi jamani, huenda ninyi wanawake mnadhani kuwa ndio mnahitaji kupendwa kuliko sisi lakini ukweli ni kuwa sote tunahitaji MAPENZI.

Ciao Dinah, kazi bomba sana.
KKMie said…
Anony hapo juu, Nashukuru sana kwa ushirikiano wenu na nyongeza kuhusu swala hili.

Ni matumaini yangu kuwa wanawake watajisaili nakuona mabadiliko yao yanayopelekea wapenzi wao kupungukiwa na penzi juu yao na hivyo kubadili na kuwa wao kama wao.

Kwa wale wanaoamua kufunga ndoa au kujiingiza kwenye uhusiano kwa vile wanaogopa jamii itawaona hawana bahati n.k. ni vema kubadilika na kufanya japo kwa ajili yako sio kwa ajili yakufurahisha jamii.

Unapokuwa mtu mzima unatakiwa kufanya uamuzi wako kama wewe, hakika utahitaji ushauri lakini sio lazima ufuate ushuri bali tumia ushauri huo kufanya uamuzi wa busara.

SWALA LA KUBADILIKA KITABIA:
Lakini mimi kama Dinah nafikiri ni vema kuwa wazi na ku-communicate na mama watoto ikiwa unahisi anaiga/kabadilika kitabia, kwani mawasiliano ni moja ya nguzo muhimu sana ktk kuimarisha mahusiano yetu ya kimapenzi.

Si vema na sio UANAUME kukimbia tatizo bali kukabiliana na kulitatua tatizo nina maana kuwa usiende tafuta kimada na badala yake rekebisha uhusiano wako ili uishi kwa amani bila kuhofia mtu wa nje.

Naona wahusika (wanawake) wametuliza boli sijui nimewagusa kumtima, hahahahha.

Karibuni tena.