Wednesday, 26 September 2007

Nguzo 5 za uhusiano bora wa Kimapenzi!


Nakumbuka zamani nilipokuwa mdogo, kulikuwa na akina mama ambao walikuwa wakijadili mambo yao ya kimapenzi kila wanapokutana pale kibarazani (mbele ya nyumba) mida ya jioni mida ya jioni wakichambua mchele au kumenya viazi tayari kwa mlo wa jioni.
Wamama hao walikuwa wakijadili mambo mengi sana ila moja ninalokumbuka ni kuwa "ili usiachike ni lazima umpe mumeo kila akitaka, umpikie mapocho-pocho, uwe msafi, umuwekee maji bafuni na kumkogesha, umkande miguu na kupenda ndugu zake".

Kutokana na maisha ya sasa kwa wengi wetu ukiachilia mbali kuwahi kuangalia Isidingo (Tv 4 u) kufanya hayo niliyoyataja inakuwa mbinde kidogo kwa vile tunafanya kazi nyingine ili kuchangia kipato ktk familia zetu na unaporudi nyumbani unakuwa umejichokea, sana sana utafanya moja kati ya hayo si unajua tena mambo fulani (mwenzi mtukufu mwee!).

Alafu ndugu wa mpenzi/mumeo huitaji kuwapenda unapaswa kuwaheshimu au kuwaonyesha heshima tu, kumpenda kijana wao isiwe taabu kha!

Tuachane na hayo basi, tuendelee.....Mimi kama Dinah naamini kuwa haijalishi unapesa kiasi gani, "libido" iko juu kiasi gani, Umzuri au Umrembo kiasi gani, "mnato au mdebwedo", unampenda jinsi gani au unatabia njema kiasi gani ktk uhusiano wako wa kimapenzi kama hakuna hizi kitu 5, nenda shule kajifunze!

1-Ushirikiano
2-Masikilizano na Maelewano
3-Heshima
4-Mawasiliano (angalia picha)
5-Kujali

Hayo mambo matano yanavipengele ambavyo vingine viko wazi sana na sitoweza kuviweka hapa kwa vile watu tumefunga.

Nakaribisha mchango, maoni, maswali na nyongeza ktk hili.

Msikilize Dada Stara

Ty.

16 comments:

Anonymous said...

Umenibamba na maelezo yako sasa dinah mimi nina swali kidogo hapa eti kuna mbinu au matendo yatakayo mfanya mpenzi wako mwanaume asikuache?

Kama ndio ni yepi na kama hapana kwanini wanawake wengi hutafuta mbinu za kuwafunga wapenzi wao wasiwaache au kuvunja uhusiano?Asante dada.

Anonymous said...

Hapo Dinah hujachambua, umeweka juu juu halafu unakaribisha mawazo jamani tukueleweje, bora ungesubiri mfungo uishe kisha umwage radhi hapa.....blogu imefunga....

Anonymous said...

Mbona hapa ni kituko! Loh kuna blog na blogs!

SIMON KITURURU said...

Nakubaliana na wewe kwa hayo matano.
Lakini nisikufiche , kwa uzoefu wangu, hayo matano uliyosema yanaweza kukusaidia kuendelea kuishi na mwenzio, lakini si ukweli kuwa utakuwa unamtamani ufanye naye tendo litangazwalo kuwa meanza kufanya siku msherehekeapo ndoa.

Naongea kivyangu, na nisikufiche , nauzoefu, ingawa unaweza kubisha.
DUH!
Mwanadada wa kibongo napata tatizo kumtongoza mpaka nikubaliwe lakinni.
DUH!
Kuishi katika ndoa kwa mtazammo wangu si tatizo, lakini,kukinai maswala kupo.

Sijawahi kuishi katika ndoa , ila najua kutokana na kuwepo katika shughuli na kushuhudia shughuli.

DUH!

Shule ya Mapenzi nzito,
Dinah!

ENDELEZA KUTUPA SHULE!

Mwenzio pamoja na mazoezi na kushuhudia wenzangu naowajua wanaocheza mechi, bado nasita kuingia kwenye ligi ingawa mpaka mama mzazi anafikiri napitiliza miaka ya kujiunga katika timu...
DUH!
Nimejieleza eeh Dinah!
DUH!

LMAO!
Hahahahah

Anonymous said...

Mambo Dina,hiyo mada imenikuna sana,we mtu mi nimekukubali ingawa sio msomaji sana wa vitu hivi lakini katika kuperuzi nimeona blog yako nafikiri kuna vitu vingi sana tunafanana kitabia(sura sijaona) usikute tunafanana teh teh! si duniani wawili wawili,keep it up,I can see a bright future behind you so kaza msuli and if you dont mind i can be your friend

Dinah said...

Anony wa 12:40 nimecheka! Kweli blogu imefunga kiaina na inaniwia vigumu kuwa wazi kama kawaida yangu.

Nimekaribisha mawazo, maswali na mengine nikijuakuwa wengi upeo ni mkubwa hivyo mnaweza kuongeza jamani ei?

Asante kwa ushirikiano na nitajaribu kufafanua zaidi kwa kutumialugha yakuficha ambayo Kitururu atanisaidia mweee!

Dinah said...

Anony wa juukabisa pale nitajibu swali lako kipekee yaani kwa kurasa yake kwani inamaelezo mengi na nadhani wengi watahitaji kufahamu majibu nitakayoyatoa kuhusiana na swali lako.

Dinah said...

Si, kabla hujaamua kuishi namwenzio ni wazi kuwa utahitaji penzi sio. Sasa mapenzi pekee hayatoshi hivyo unahitaji viungo vingine kuwa na uhusiano wenye afya.

Ukipika wali kwakutumia maji na chumvu utalika lakini ili unoge/uwe mtamu utahitaji viungo kama karanga, nazi au mafuta sio?

Dagaa chukuchuku zinalika lakini ukiongeza viungo kama nyanya, kitunguu, mafuta, pilipili zinakufanya utamani kumaliza liugali lako sio?

Ndio hivyo Si.....alafu nakushauri kuwa ingia kwenye timu ukijua wazi ndio kitu unataka, sio kujiingilia kwa vile mama anataka mjukuu au wanakudhania wewe nanihii...u know...hahahaha

Asante kwa ushirikiano wako.

Dinah said...

Hahahahah anony wa 11:43! Poa poa siku moja utaniona na ndio utajuakuwa twafanana kila kitu au la!

Asante kwa ushirikiano wako nakaribu sana buloguni hapa.

Anonymous said...

Dinah mimi profile yako tu ndio imeniacha inaelekea wewe ni binti mmoja matata sana na mchokozi.

Nakubalina na Simon kuwa hayo mambo uliyoyataja yanasaidia kuishi vizuri na mwenza wako lakini hayaongezi mvuto wa kumfanya mtu andelee kufurahia kuwa na wewe kimwili.

Pia nakubaliana na wewe kuwa kabla ya kuongeza viungo huwa kunakuwa na pishi lenyewe ambalo ni penzi. Lakini si wote wanaojiingiza kwenye mahusiano wanamapenzi na hivyo inakuwa rahisi kupoteza hamu/mvuto kutoka kwake.

Wewe kama mwanamke Unafikiri utawasaidi vipi wale wanawake wanaopoteza mvuto au hamu kwa wenza wao.Asante

Luca said...

Dinah naomba tuwasiliane, kuna issue muhimu nataka kuongea na wewe. Email yangu ni

luca@kiduka.com

Asante
Luca

Dinah said...

Hakuna matata Luca, wewe weka issue yako hapa (sitoi-publish) then nitakujibu kwa email au unaweza kuniandikia email kwa kutumia jina lililopo kwenye profile yangu hapa then ongeza @hotmail.com

Looking foward to hear from you.
Karibu sana.

Anonymous said...

bwanaeee ukitaka mwanaume wa kiswahili asikuache ni kumroga tu. Hata umpe mapenzi vipi lazima atembee nje. Limbwata tu anatulia ndani tusitake kudanganyana hapa.

Jose said...

Msemaji wa 11:40 ikiwa wote wawili mnapendana kwa dhati na mnafanyia kazi hayo mambo aliyoyataja Dinah hakutakuwa na swala la kwenda kutafuta nje.

Mwanamke au mwanaume huwa na sababu zake kwanini anakwenda nje na ukifuatilia unagundua kuwa mmoja kati yao hana mapenzi tena na mwenzie na iliyobaki ni heshima tu kama alivyowahi kusema Dinah kuwa Penzi hubadilika na kuwa heshima hasa kama mmefunga ndoa.

Sote ni binaadamu na kuna wakati huwa tunajisahau na hiyo ndio huwa sababu ya wenza wetu kujiona hawapendwi tena na hivyo kwenda kutafuta penzi nje sio ngono japokuwa huishia kufanya tendo hilo kwa vile penzi wanalopeana huwafanya wajisikie kufanya hivyo. Nawakilisha.

Anonymous said...

jamani eti unamfanyaje limbwata mwanume?? mi naskia 2. i need help ni ingizeni mjini. mi dem wakiarab ah amna kutoka toka wen u feel like most di time na2lia home. sijui kinachoendelea uko i need help jamani plz

ntafute kwene: luv2hav2fun@gmail.com

thnx!

Anonymous said...

dah dada huko kubaya bora ukae kama huelewi kuliko kuji2pa pango la limbwata