Vaa sidiria au vest kadili siku zinavyo kwenda!


Jinsi matiti yanavyokuwa ndio uzito wake huongezeka hivyo kama binti/mwanamke unahitaji kuyasaidia kwa kuvaa kitu ambacho kitayasaidia kubaki pale yanapopaswa kubaki......nina maana vaa sidiria.


Vest ivaliwe wakati ukifanya mazoezi au unaweza kujifunga khanga (nyepezi) chini ya matiti yako hali itakayosaidia matiti yasiume sana wakati unafanya unayasumbua(inategemeana na ukubwa wake).


Wakati nakuwa wanawake wengi walikuwa wakiamini kuwa kuvaa sidiria kunasababisha matiti kuanguka; sio kweli.


Kumbuka kutovaa sidiria wakati wa kulala kwani naweza kusababisha uvimbe (damu kujikusanya pamoja) ktk matiti yako na badala yake lala kifudifudi(lalia matiti yako a.k.a lalia tumbo)


Natumaini nyote mnalijua hili sio? kama mlikuwa hamjui sasa mnajua.


Nawatakia siku njema na karibuni tena nitakapomalizia swala zima la usafishaji na utunzajiwa matiti kwa wanawake waliondani ya mahusiano ya kimapenzi.


C ya!

Comments

Anonymous said…
Dinah naikubali kazi yako, elimu hii tungeipata wakati ule tunakuwa wengine tusingekuwa hivi tulivyo.

Nafurahia sana blog yako.
KakaTrio said…
Dinnah kumbuka kuwaambia wenzio wawe wanajicheki angalau mara moja kwa mwezi huko kwene matiti yao kama kuna viuvumbe uvimbe ivi manake siku izi kansa - saratani ya maziwa nayo iko juu sana. kwa hiyo wakati mnafanyie mazoezi matiti yenyu chunguzeni pia vijiuvimbe, na kama ukihisi kitu muone dakitari bila kusita
KKMie said…
Asante Maricha kwa maelezo yako, hakika somo litazungumziwa kwa kina hapo baadae kwa wale ambao hawajui jinsi ya kuangalia matiti yako (kujipima kama unauvimbe na kuwahi kwa Dakitari).
KKMie said…
Anony wa 5:12 tarehe 21, nashukuru sana kwa ushirikiano wako na kwa kuipenda bolugu yangu.

Karibu kila upatapo wasaa online.