Tuesday, 10 July 2007

Uongo ktk mahusiano ya Kimapenzi!

Kuna hili swala la kuwaita wanaume wadanganyifu (waongo) na wanapenda kulaghau ili kupata kile wanachokitaka na cha kusikitisha hapa sio baadhi yao bali wote.

Wanawake pia ni wadanganyifu lakini haionekani kama tunadanganya kwa vile sio wote ni baadhi na uongo wetu sio wa mara kwa mara, uongo wa mwanamke unategemea zaidi malezi na hatimae kubadilika pale unapokua na kuwa tabia, kwa wenzetu wanaume uongo kwao ni sehemu ya UANAUME.

Nakumbuka wakati Fulani nilikuwa kwenye uhusiano na jamaa Fulani hivi, kule alikokuwa akiishi kulikuwa kuna bidhaa Fulani hivi nzuri na nilikuwa nazihitaji sana. Sasa kwa kurahisisha mambo nikaomba huyo mchumba aninunulie (kwa kumtumia senti) kisha anitumie huku niliko.

Yeye akakataa kupokea “senti” zangu akidai kuwa ni kitu kidogo atashughulikia kwa senti zake sio. Nikawa nasubiri mzigo wangu uje lakini kila nikikumbushia napewa hadithi, nikaona tuaache tu kwani ktk siku chache nitakuwa huko (kumtembelea) na hivyo nitavichukua mwenyewe.

Nilipofika huko hakukuwa na mazungumzo yoyote kuhusu vifurushi vyangu bali wakati najiandaa kuondoka ndio akaja “clean” kuwa hakunua kwa vile mambo yaliingiliana na akaomba msamaha. Sasa huyu jamaa aliongopa ili kuulinda “Uanaume wake”.


Uongo ninaozungumzia hapa sio ule wa kikazi, kisiasa au kibiashara bali uongo katika mahusiano yetu ya kimapenzi. Uongo huo wanaotuambia mara kwa mara huwa kuna sababu yake, sio kwamba wanadanganya kwa vile wanapenda bali inawabidi au niseme kuna kuwa na ulazima unaopelekea wafanye hivyo.

Haya ni baadhi ya mambo yanayopelekea tudanganywe!

*Aibu kutokana na utoto wake, magonjwa asilia ktk ukoo wake au magonjwa aliyougua alipokuwa “kinda” na kuachia alama ya kudumu mwilini, ulongo hapo unakuja ili usijue matiatizo yake ya awali ambayo kwake ni aibu. Vilevile kama alikuwa “bozo” yaani wale watu wanaonewa na kila mtu na hawajui kujitetea zaidi ya kukimbilia kwa mama.

*Kutojiamini kwake, kwamba anakufikiria wewe ni “mtu wa hali Fulani” kutokana na zungumza yako au mavazi na wakati mwingine mahali unapofanyia shughuli zako sasa ili a-“fit” na yeye anajifanya kuwa yuko kwenye daraja hilo la juu kumbe masikini mtu mwenyewe ni msaka nyoka tu(mtu wa kawaida).

*Kutojiamini kwako, huenda wewe hupendi jinsi ulivyo(mnene kupita kiasi au mkondefu) na hali hiyo inapelekea yeye kutofaidi mwili wako kikamilifu kwani kila ukichojoa lazima uzime taa kisha unajikubika kwenye shuka na hakuoni ulivyoumbika bali anahisi tu kwa mikono (hey hiyo sio nzuri). Sasa ili aweze kuwa huru inabidi aongope kwa kukupa misifa lukuki ambayo huna ila anajua ungependa kuwa hivyo.

*Kuogopa kukuumiza au kuepuka kununiwa, mwanaume akifanya kosa kubwa siku zote huongopa ili asikuumize lakini baada ya muda Fulani huwa wanasema ukweli na kutoa maelezo ya kwanini walidanganya wakati ule…..ukinuna hapo utakuwa mjinga kwa vile swala lilitokea mwaka au miwili iliyopita, kwa wanawake walioendelea hushukuru lakini kwa mwafrika halisi sidhani mambo yataisha kirahisi hivyo na vikao vitaitishwa aisee!

*Kuepuka mzozo, mwanaume hulazimika kusema uongo ambao yeye anatambua wazi kuwa ndio unataka kusikia kwa wakati huo. Inafikia wakati anakubali kufanya kila kitu (hata vile ambavyo huwa hafanyi) ili tu usimsumbue akili yake na maneno yako kama umemeza kaseti vile.

*Kupumzisha akili na kuepuka maswali mwanaume atadanganya kuwa kazini kila kitu kilikuwa salama na mambo yamekwenda vema kabisa kama alivyotaka,lakini ukweli hapo ni kuwa yaliyojili kule hataki kuyahamishia nyumbani akijua wazi hutomsaidia kitu san asana utamzidishia maumivu ya kichwa tu.

Sina maana kuwa wanawake sio “smart” na michango yetu haiwasaidii wapenzi wetu la hasha! Kumbuka kila mwanaume anajua anaishi au yuko na mwanamke wa aina gani “akilin”, natumaini umenielewa hapo.

*Mwisho kabisa ni ule uongo usiokaribia ukweli na unatokea karibu kila siku hata kwa vitu vidogo na vya kawaida tu, yaani kwa kifupi ni wehu bin ujinga. Ikiwa wako yuko hivyo tafuta ustaarabu mpya.

Pole kwa maelezo marefu ila natumaini yatakusaidia nakufumbua akili yako kwanini hawa viumbe wanapenda kutumia uongo ili kuweka mambo sawa japokuwa wakati mwingine wanaharibu mambo.

Nakaribisha maswali, maoni na nyongeza ya uogo wa wanaume.
Ty.

7 comments:

Anonymous said...

Wee Binti inaelekea unatujua sana wanaume? Haya wanawake jifunzeni kupitia mwanamke mwenzenu.

Big up D.

Aisha said...

mmmm watu hapa kimyaaaa, kwahiyo mmekubali kudanganywa?

Dinah said...

Hahaha labda haijawatokea!

Dinah said...

Anony pale juu, sio kwamba nawajua sana bali natumia muda mwingi kukaa na wanaume, yaani wanaume ndio marafiki zangu wa karibu hivyo najua mawili matatu kutoka kwao.

Asante kwa ushirikiano wako.

Anonymous said...

Dada I just visited your blog hapa...ila wanaume..you seem ulituchukulia course maalumu. You know us kiundani...nani alikufundisha weye...Big up and keep the fire burning.

Nice blog!

Dinah said...

Anony wa saa kumi na moja na dk 51, nimejibu hili hapo juu. Sijachukua kozi wala nini bali ni kurafikiana na wanaume ndio kunanifanya nijifunze mambo yenu ambayo wanawake hatuyajui.

Asante sana kwa ushirikiano wako.

Hassan Kimweri said...

imeonekana kuwa ni kawaida kwa wanaume kuongopa sababu et nimoja kukamilika kwa uwanaume lakini la hasha sivyo hivyo lakini pia hapohapo wanawake pia wamekua ni waongo kuliko hata wnaume kwa sasa na sababu haijulikani ninini na uongo wa wanaume ni kutaka2 jambo fulani liiishe na kuepusha mzozo mwanamke hafikiliii hivyo