Saturday, 21 July 2007

Maalumu kwa bikira!


Tafadhali, ikiwa wewe ni bikira usithubutu kupunguza siku zako za hedhi kama nilivyoeleza hapo chini nabadala yake subiri mpaka hapo utakapo kuwa mkubwa na tayari kujiingiza kwenye maswala ya mahusiano ya kimapenzi.


Ikiwa unaswali lolote wewe manamke mdogo, usisite kuniuliza naahidi kukusaidia kadili ya uwezo wangu ili uweze kuvuka kipindi hiki kigumu ambacho hata mimi nilipitia, hakika nitakupa mbinu mbili tatu ili uvute muda mpaka utakapo kuwa at least una miaka 21 na kuendelea.


Usiogope nipo hapa kwa ajili yako.


Asante kwa uelevu wako.

14 comments:

Anonymous said...

Dina, mimi nina miaka 26 na ni Bikira. Naogopa kweli siku ya kuja kufanya rafiki zangu wananimbia nitaumia sana sababu nimeshakua mtu mzima na sijawahi kutiwa. Je ni kweli?

Dinah said...

Aaah wapi, wengi hudanganyanya hivyo ili ukimbilie kuanza ngono mapema (chini yaumri wa mika 21) ukweli ni kuwa jinsi unavyokuwa ndivyo maumivu ya bikira yanavyopungua kwa vile mifupa yako ya nyonga na misuli ya uke imekomaa na inarainika vema kabisa.

Usiogope kwani hutoumia sana (inategemea zaidi na maandalizi na mapenzi yenu bila kusahau na ukubwa wa uume wa huyo bwana atakae kuanza).

Bikira ikitoka ukubwani ni nzuri kwa vile mwili wako unakuwa tayari umekomaa hivyo maumivu ya uume kuingia yatakuwa ya kawaida.

Usiogope bali subiri utolewe bikira na mtu anaekupenda na wewe unampenda na hapo ndio utapata raha ya siku ya kwanza ya kuanza kufanya mapenzi....litakuwa tukio zuri na la kukumbukwa.

By the pass....unaweza ukatolewa bikira in 10hrs mapaka 3days sio lazima aingie na kumaliza kila kitu siku moja....ndio maana nasisitiza mapenzi na uelevu wa mpenzi wako ni muhimu sio kusokomeza tu.

Karibu sana.

Anonymous said...

Dada Dinah mimi mwanafunzi wa kidato cha nne naombakuuliza, eti ukitunza bikira yako ukijakuolewa mumeo atakuwa akikuheshimu?

Na je niitunze bikira mpaka lini? Nisipokuja kuolewa je?

Naomba msaada wako.

Anonymous said...

Antie Dinah mimi miaka yangu ni 19, huwa nasoma sana masomo yako hapa ila nilikuwa naogopa kuuliza mwaswali kwa vile sioni mahali pahala pa kuulizia kwa sababu sijaanza maswala haya ya wakubwa.

Lakini kuna siku huwa nahamu ya kushikwa-shikwa na sehemu zangu za siri zinapata maji-maji je hiyo inamaana bikira imetoka?

Lilian.

Dinah said...

Anony wa saa tatu na dakika 50, Sio kweli kuwa ukitunza bikira ndio utaheshimika na mumeo ila itamfanya yeye mwanaume ajione wa thamani kwa kuwa hakuna aliyekugusa ila ni yeye (ubinafsi wao tu unless uolewe na mwanaume ambae ni bikira pia).

Mimi kama Dinah nasema hivi; mabinti wote wa kibongo wenye bikira jiheshimuni na mthamini miili yenu kwa faida yenu. Hakikisha mnatunza bikira zenu mapaka mtakapo kuwa watu wazima na tayari kuwa ndani ya uhusiano mzuri wa kimapenzi na yule umpendae iwe uhusiano wa kawaida utakao pelekea ndoa au bila ndoa lakini wa kudumu na mzuri.


Bikira hainakikomo kuituza, unaweza ukabaki bila kukutana na mwanaume kimwili mpaka unafikia miaka 50, ni uamuzi wako tu.

Asante kwa ushirikiano wako.

Dinah said...

Liliani asante kwa ushirikiano wako. Hapana kutokwa na unyevu haina maana bikira imetoka bali ni ute unaosababishwa na hali unayojisikia kwa kiswahili kingine tunaita nyege.

Siku nyingine ukijisikia hivyo jaribu kujamisha mawazo yako au nenda kafanye shughuli yakutumia nguvu kama kuteka/chota maji, kupiga deki, kufagia uwanja au kufanya mazoezi mepesi kama kuruka kamba, kukimbia n.k.

Kufanya hivyo kutakusaidia kukabiliana na hali hiyo ambao inasababishwa na mabadiliko ya ukuaji wako (unakuwa kuelekea uanamke).

Karibu tena mahali hapa.

Anonymous said...

Dada Dinah, mi nina miaka 19, tangu nimevunja ungo nilikua siumwi tumbo la mwezini, lakini kuanzia mwaka jana yaani kila nikiingia mwezini tumbo linauma sana hata darasani siwezi kwenda, wenzangu wananishauri eti nikilala na mwanaume ndio tumbo litaacha kuuma na mimi naogopa kwa vile bado bikira, naomba ushauri wako

Dinah said...

Anony wa 14:59, pole kwa kuumwa na tumbo wakati wa hedhi. Maumivu hayo ni ya kawaida na wanawake wengi tunakumbana nayo kila mwezi.

Kulala na mwanaume sio tiba ya tumbo la hedhi (hakuna tiba), mimi naambiwa litaacha kuuma ikiwa nitazaa, ila sitokimbilia/shawishika kuzaa ili kutibu maumivu yangu ya hedhi.

Hali kadhalika wewe usijaribu wala kushawishika kufanya ngono ktk umri huo kwa kudhania kuwa utapona tumbo la hedhi.

Hey kwa kifupi najaribu kusema kuwa tumbo la hedhi haliponi/acha kuuma kwa kufanya ngono bali maumivu hayo hupungua kwa kutumia dawa za kupunguza maumivu, kujikanda na maji ya moto, kufanya mazoezi kama kukimbia na yale yakunyoosha viungo, na vilevile kunywa maji yaliyotengenezwa kwa kutumia unga wa ndizi ndogo.

Wajua vile vidizi vigogo vitamuu basi tafuta vibichi kimenye, vikaushe kisha twanga/saga alafu changanya na maji nakunywa x3 kwa siku kila unapokuwa na maumivu ya hedhi.

Kamwe usithubutu kuanza ngono sasa, hao wanaokuambia hivyo hawajui lolote wanakudanganya tu.

Piga kitabu, ngono ipo na utaikuta utakapo kuwa tayari....jithamini na jiheshimu kwa sasa.

Egidio Ndabagoye said...

Dinah,
Nimepita hapa.Kazi nzuri

Egidio Ndabagoye said...

Dinah,nimekutag naomba utueleza vitu vinane tusiojua kuhusu wewe.

Anonymous said...

Dada Dinah, mimi ninakuomba unisaidia kwani ni kijana wa umri wa miaka 29 lakini , nina boro ndogo na pia nikitembea na mke wangu uwa inachukua kama dakika tatu au nne,je nifanye nini ili nimtosheleze ila yeye hajaniambia ila ninajua tu na kingine pia ninapenda wamama sana kupita kiasi , naomba unisaidia

Dinah said...

Egidio asante kwa ushirikiano wako wa kupita hapa mida ile ya nane na dk nane.

Ukaja tena mida ya kumi na mbili na dk 3 ukitaka nieleze vitu 8 msivyovijua (unawakili akina nani weye?).

Hapa sio mahala pake, watu watasema na"show off" kuepuka hilo nitafute mahali kwingine..sio.

Karibu tena.

Dinah said...

Mh! Nisingependa kukudanganya sina uzoefu na mwanaume mwenye uume mdogo hivyo sitoweza kueleza jinsi ya kumtosheleza mkeo.

Lakini swala la kumaliza dk 3-4 ni kawaida kwa wanaume karibu wote ila tofauti ni kuwa kila mwanaume anambinu yake yakujizuia kumaliza kabla ya mpenzi/mkewe....tafadhali tafuta makala ya "one minute man" na hapo utapata mbinu mbili tatu za kuanzia.


Unamke na wakati huo-huo unapenda wamama....sasa kitu gani kilikufanya ufunge nae ndoa?

Mama Q said...

Shamim mbona haleti vituuu?tunamsubir kwa hamu jamani,au tukufuate huko 8020?